
Nyeti zimeingia sasa hivi kwamba Kaka Dk. Mwamoyo J. Hamza (kulia akiwa kazini Voice of America) kaongezewa majukumu zaidi hivi karibuni kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa idara ya kiswahili ya sauti ya amerika, yaani VOA.
nyeti hizo zinapasha kwamba huyu bwana, ambaye amekuwa kwenye idhaa hiyo tokea mwaka 1994, amekuwa mhairiri mwandamizi idhaani hapo, na mhariri mkuu mwenza tokea oktoba mwaka jana, ambapo amekuwa na majukumu ya kiutawala na usimamizi.
mwamoyo ni mmbongo mwenzetu ambaye ana nondozzz za M.A na PhD katika mawasiliano kutoka chuo kikuu cha Howard University na pia akisotea diploma ya uandishi chuo cha uandishi cha bongo ama TSJ.
Mwamoyo amekuwa na majukumu mazito kama mhariri mtendaji mwenza wa idhaa hiyo ya kiswahili amabapo pamoja na mambo mengine amekuwa akichonga miundombinu ya vipindi idhaani hapo, ikiwa ni pamoja na kuandaa vipindi muhimu vya idhaa ya kiswahili ya Voice of America. Hongera kaka Dk. Mwamoyo wa kuiwakilisha bongo vyema, ingawa we mwenyewe ulituficha kuhusu majukumu hayoa mapya na mazito....
Mtani,
ReplyDeleteHongera sana juhudi zako hazitapita bila kuonwa. Hongera saaana saaana.
Ni mimi Ehaaaa, Ottawa Canada.
Hongera sana Uncle Mwa Moyo, juhudi zako binafsi na kwa ushirikiano wa wafanyakazi wenzako matunda yameonekana, tunakutakia kila kheri katika majukumu hayo mapya, nasi tutafuata nyayo zako.
ReplyDeleteBintiyo
Zeddy
Reading
Dr .Tunataka ufanye mambo sasa hivi sababu hiyo radio imepoteza umaarufu wake ,naona ilikuwa kama kijiwe cha kuendeshea siku ilimradi mshahara unaingia, sasa tunataka iendeshwe kiushindani .. .Hongera Mwamoyo...
ReplyDeleteAmani, Heshima na Upendo kwenu.
ReplyDeleteKwa yeyote ambaye amefanya kazia ama kuwa karibu na Dr Mwamoyo hatakuwa na shaka na uwezo na ama upeo wake katika mambo mengi yakiwemo ya Habari. Sina shaka kuwa ataendeleza vema kituo na kuendeleza mabadiliko ambayo wameanza kuyafanya kituoni hapo.
Kila la kheri Uncle Mwamoyo katika nafasi yako mpya na nyeti.
Blessings
Hongera sana, jukumu hilo limempata mwenye Moyo wa ubunifu na maendeleo....kumbuka ni VEMA...kusema hongera....ni VEMA....kukupongeza ni VEMA...ni VEMA kusema hongera kutoka Reading, UK
ReplyDeleteWe don't call people kaka Dr ... instead kaka...! acheni urombo wa kukubakia hizo titles. anyway kaka mwa Heart hongera mshaija.
ReplyDeleteWe annon wa april 13, 2008 2.56AM unamaanisha nini unaposema 'acheni 'urombo' wa kubabaikia titles? Unatala jamii ielewe kuwa warombo ndo wababaikiaji wa titles na ambao hawajasoma? heshima kitu cha bure kwa wenzio..u can be better than that!
ReplyDeleteMdau, Germany
We German ni mrombo nini mbona unalia! hapa mdau hakumaanisha kabila , hiyo ni kama kubonyeza kinzenji kwani wazenji ... dodomaa au!
ReplyDeleteEhaaaa!!!
ReplyDeleteHongera na pongezi nyingi kwa majukumu mapya. Kwa wale wanaokufahamu hili jukumu ni kubwa lakini sio la kushangaza...You were born to do this!!!!Keep on blazing bro!
Sasa tutajidai wapi mkubwa? mimi nafikiri twende Zanzibar @ the Waterfront..Na Spring hii tutafurahi tu.
Much Love!!
From the Hagerstown Gang.
Aisee hiri ri jamaa rina pesonariti kweri!!
ReplyDelete