mwenyekiti wa jumjuiya ya wabongo waishio uingereza mh. abubakar faraj akitoa hotuba ya utangulizi
wajasiriamali waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mtaalamu bw. issa omar


balozi wetu uingereza mh. mwanaidi maajar akimkaribisha bw. issa omar atoe mada yake. chini ni bw. omar akihutubia umati wa wajasiriamali wa kibongo

Omar Issa awahamasisha Watanzania walioko Ughaibuni kufanyabishara nyumbani

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Kusaidia Mazingira ya Uwekezaji Afrika (Investment Climate Facility for Africa), Bw. Omar Issa amekutana na Wajasiriamali wa Kitanzania waishio Uingereza na kuwapa changamoto ya kuanzisha biashara nyumbani.

Katika Mkutano uliofanyika jana katika jengo la Ubalozi wa Tanzania, London Uingereza (Tanzania House), Bw. Issa aliainisha fursa nyingi za biashara zilizopo Tanzania baada ya Serikali kufungua milango zaidi ya uwekezaji na kupatikana kwa wawekezaji wakubwa wa Kimataifa.

Akifafanua zaidi mtaalam huyo alisema hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji zaidi biashara za uwezo wa kati (medium enterprises) ili kuziba pengo kubwa kati ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Alisema ili kuendelea zaidi kiuchumi, makampuni makubwa yanahitaji sana makampuni ya kati kwa ajili ya kutengeneza mali ghafi, kuzalisha nguvu kazi na kutoa ushauri wa kitaaluma.

Katika Mkutano huo ulihudhuriwa na watanzania zaidi ya 30, Bw. Issa aliwashauri wajasiriamali hao kubuni miradi mbalimbali itakayowawezesha kupata mikopo kwenye benki za Tanzania ili kuweza kuanzisha biashara huko nyumbani. Aliwapa changamoto kuangalia fursa za biashara za huduma na ushauri wa kitaaluma.

Alisema benki nyingi hivi sasa nchini Tanzania zinawatafuta wenye miradi ya uhakika ili kuwakopesha mitaji ya kufanya biashara nchini humo. Alisema kwa elimu, upeo na uzoefu waliokuwa nao, wajasiriamali hao wanaweza kuanzisha miradi mizuri itakayowezesha kuinua uchumi wa Tanzania.

Kwa mafanikio zaidi, Bw. Issa amewashauri wajasiriamali hao kujiunga katika vikundi ili kuweza kujumuisha utaalam na mitaji ya msingi ya kuanzisha miradi hiyo. Alisema biashara nzuri inahitaji utafiti wa soko, udhibiti na shauku ya maendeleo zaidi.

Katika maswali yao kwa mtoa mada, wajasiriamali hao walipenda kufahamu mipango zaidi ya Serikali kuondoa urasimu. Bw. Issa aliwaambia kwamba wakati Serikali inaendelea na hatua mbalimbali kurekebisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini Tanzania, ni vyema Watanzania hao pia kutimiza wajibu wao badala ya kukaa tu kusubiri Serikali kufanya kila kitu. Alifafanua kwamba Watanzania walioko nje ya nchi wana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha mazingira ya uwekezaji kama watarudi nyumbani na kuingiza utamaduni mpya wa kikazi.

Awali akimkaribisha mtoa mada, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar alisema kwamba Ubalozi hivi sasa unafanya jitihada za kuwaunganisha wajasiriamali wa Kitanzania wa ngazi zote walioko Uingereza ili kuwashirikisha kikamilifu na Baraza la Biashara la Tanzania (Tanzania Business Council).

Bw. Issa yupo London kwa ajili ya Mkutano wa Uwekezaji wa Africa (Africa Business Forum 2008) ulioandaliwa na Commonwealth Business Forum.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2008

    Wezi hao!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2008

    Hongereni London kwa kuonyesha njia, ushirikiano baina ya Watanzania ni muhimu sana unganeni.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2008

    Wewe ulitoa maoni hapo mwanzo kabisa, mwizi mwenyewe...utabakia hivyo hivyo tu kuona kila mtu ni mwizi; umekosa rathi ya Mama Yako.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2008

    Hivi kumbe kubeba box siku hizi ni ujasiliamali eenhee!!!. Hongereni, endeleni kuosha wazee ili mpate mitaji ya kuja kuwekeza bongo maana jua ndiyo linazama hivyo (i.e. umri ndiyo unasogea)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2008

    tatizo la wabongo ndio hilo wao kuponda tu mara wez mara maboksi nafkir hata wazaz wao wanaofanya city pia wanawadharau nyie kaen na dharau zenu watu wanapiga bao ok anyway tunasubir uraia wa nchi 2 tufanye mambo hela iko nyingi tu tunayo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2008

    nyie ponden tu ulaya itabak kuwa ulaya na africa ni africa tu kwanza tunaomba umeme uwe wa uhakika pesa tunayo iko nyingi kama ya wiz ya maboksi kuosha vibib lakin iko nyingi tu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2008

    I logged my application to start business in Tanzania to convert cars to use Natural gas which is abundant in tanzania and would benefit many a year ago, I even suggested to bring a multinational company to invest in distributing and erecting filling stations but no one so far has even beeped me!
    How can you work or even dare to invest in such a place???
    The guy who wrote "wezi hao" could be right and I would add "Liers! they are doing nothing to support their words."

    malisa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2008

    jamani msitake nichekeee mwe! naona bwan shem umeniwekea old school mate G N'taramira.

    kama anafungua blog yako napenda kumkumbusha siku pantoni lilivyo kwama wakasi sisi bado tuko mikadi tuna rudi no pantoni tukajikita kwenye boti kidogo lulu azame tehe tehe tehe wapi bakari bwa shem mwenyewe ulikuwepo na nanihiiiiiiii mh

    sasa leo G ni mjasilia mali hongera sana mmmmm

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2008

    We anon wa 9.42, mie nafikiri, inaonyesha ni jinsi gani, ulivyokua mjasirimali wa upungufu wa akili. We unamjua mama yangu? Ni mmoja kati ya mama bora wa TZ, kama ungemfahamu, na ameitumikia serikali kwa karibu mda wa miaka 30. Nikikuambia kua alipata ajali, akawa anadai mafao yake ya bima ambayo alikua akiilipia yeye mwenyewe. Alipata ajali 1996 mpaka anakuja kufariki 2005 hajalipwa, kila siku anasumbuliwa na mguu wake uliojeruhiwa. Na alikua mmoja wa watumishi bora serikalini, sas kama huo sio wizi ni nini? Mpaka leo hii faili lake halionekani, unataka kuniambia mimi nikawekeze? Tafadhali sana, kama wewe ni mume, unamheshimu mkeo, mama yako au dadako, basi usingethubutu kumwambia mwenzio kuwa kakosa radhi ya mama yake, ukizingatia humjui. Na kama ni mke basi ni aibu kwako, pia, maana mdomoni mwako inaonekana kumejaa matusi, na sidhani kama ni mama mzuri au utakua mama mzuri kwa wanao. Ukweli kwamba, wengi walio magereza ya bongo, makosa yao ni madogo kuliko walio nje, acheni kuwatetea au kujikosha. Wanaofilisi nchi wapo nje, wanatumia mali za wananchi. Kama hao kina Chenge, Mkapa na wengineo, si ndio mwanzo wa vikao hivi? Kubali ukweli, ni plan za wizi, mbona hao viongozi wanaweka pesa zao nje? Kwa nini jiulize? Watz wanaoishi nje sio wadanganyika, mtawapata hao hao watoto wenu. Ujasirimali wa kuokota mafriji, magazeti, flying pan n.k kutoka majalalani na kwenda kuviuza bongo. Wako wapi customs? Nchi inakaribia miaka 50 toka kujitawala, maendeleo hamna. Angalia wanafunzi Dar wanavyopata taabu kwenda mashuleni, mpaka leo watu wanatumia vyoo vya shimo. Kwa taarifa yako, nimekulia Mchikichini na Kinondoni Biafra. Niliondoka bongo mwanzoni mwa 90, nilirudi 2002, aibu. Hamna rami, hakuna maji, michongoma iliyokuwapo kwenye nyumba za Quarters yoote imekufa kwa kukosa maji. Inabidi mafisadi waonyeshe mfano kwanza, sababu huwezi kumwambia mwenzio anawe uso wakati wewe mwenyewe una matongo tongo. Kama kuna jambo muhimu ambalo ninge wish. Basi marehemu Nyerere afufuliwe, maana tusingeyaona haya maajabu ya filauni. Huu ni mtazamo wangu tuu wadau, tuwaheshimu wazazi wetu.

    Mchangiaji.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 04, 2008

    Kuna rafiki yangu mmoja alimshawishi muwekezaji mgeni aje awekeze Bongo. Kwa nia ya kuja kufungua kiwanda kidogo cha vifaa vya Ujenzi na vya umeme. Mgeni akavutiwa na akawa tayari kuanza kuanfaya utafiti. Mtz baada ya kucheki kwenye website za serikali na masharti ya uwekezaji, akaamua kuwatafuta wahusika wenyewe aongee nao kwa simu. Huwezi kuamini, alimpata tena mmoja wa viongozi wa juu serikalini, kupitia kwa jamaa zake wanaoishi Tz. Yule kiongozi alimwambia kuwa, amwambie huyo muwekezaji awasiliana nae yeye direct, sio yule Mtz ambaye alimshawishi muwekezaji na muwekezaji anamuamini huyu mtz aliyemshawishi. Hapo imekuja greedness na wizi. Nakubaliana na anon wa mwanzo kabisa na anon 11.51, Malisa wapo right kabisa. Tukubali viongozi wetu wengi, wana maisha ya kawaida, hivyo wanavyopata uongozi, wanataka kujitajirisha nafsi zao kwanza. Kila binadamu ana tamaa, ni nani asiyekuwa na tamaa? Nchi ina utajiri wa kutosha katika kila sekta, ila ukweli unabaki kuwa viongozi wengi wa Kiafrika hawazipendi kwa dhati nchi zao, cha kupendeza zaidi, amani imetawala nchi nzima, cha kujiuliza ni kwamba. Je tutaweza kuendelea kuwa na amani kwa hali inayoendelea nhini mwetu? Watu wanaonekana wameshaanza kuchoka, na wanajifunza yanayotekea nchi za jirani kila siku, Mungu atujaalie yasije yakatokea kama yalitokea Kenya. Serikali is aware of that?

    Mkulu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 04, 2008

    Sasa wewe malisa 11:51 am unasema umetuma application yako unamsubiri nani akufuatilie huo mradi au akujibu. Suala meku sio mawazo kwa kipindi hiki, Tanzania sasa inahitaji watekelezaji kwani mawazo ni mengi mazuri tu ambayo yapo. build your confidence na uonyeshe watu kuwa unataka na unaweza!!

    Anyway wazo ni zuri sana na ninakutakia kila la kheri....

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 04, 2008

    namuona jenifer hapo pembeni ya uyo mdada mwenye yelow yelow umetoka bomba ile mbaya
    mdau

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2008

    Mbona mafisadi wa bongo wanawekeza nje? Kwanini sisi tushauriwe kuwekeza nyumbani wakati walioko nyumbani wanawekeza nje?

    Jamani tunaumia sana migogno kutafuta hela yetu...Hela yetu hatuipati kwa hongo wala rushwa ni hela ya kupiga masaaa tu...Sasa tena tuilete Bongo muje muimegue si mtatuua wakati kila siku mnatusema huku tunazeeka....Mwee mimi yanguuuuuuu nitakujanayo siku naamua kurudi bongo mambo ya kuitanguliza wala siyaoni mazuri nimeshawashtukia.......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...