WADAU WATUKUFU,
MTUMISHI WENU NAPENDA KUWAARIFU RASMI KWAMBAHIVI SASA www.michuzi-blog.com IPO HEWANI KAMA GLOBU HII YA JAMII ILIVYOAHIDI, NA UTAKUTA KWAMBA ZAIDI YA ANUANI KUBADILIKA KILA KITU KIKO VILE VILE.
NAWASHUKURU SANA KWA KUNIVUMILIA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MPITO NA SASA NAJIANDAA KUENDELEZA LIBENEKE KAMA ILIVYO KAWAIDA. UWANJA WA MAONI, SALAMU KWA NDUGU NA JAMAA, MSAADA TUTANI NA PICHA VINAKARIBISHWA TOKA KILE SEHEMU DUNIANI.
HIVYO BASI NATANGAZA RASMI KWAMBA ANUANI YA issamichuzi.blogspot.com HAITOTUMIKA TENA NA BADALA YAKE ITATUMIKA HII YA www.michuzi-blog.com KUANZIA USIKU HUU.
HIVI SASA NIKO KATIKA KUJIPANGA UPYA KWA AWAMU YA PILI YA GLOBU HII YA JAMII NA NATEGEMEA TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA KAMA ILIVYOKUWA AWALI
AIDHA, www.bongotyube.com NAYO INAENDELEA NA LIBENEKE NA NASHUKURU KWA MAPOKEZI YA KUTIA MOYO ILIYOYAPATA. NAKARIBISHA WADAU MJISAJILI NA KUANZAA KU-POST VIDEO ZENU AMBAZO ZITAPOKELEWA KWA MIKONO MIWILI ENDAPO KAMA HAZITOKUWA ZA UCHAFUZI WA HALI YA HEWA NA ZENYE KUKIUKA MIIKO YA WAVUTI HIYO MPYA.
NACHUKUA FURSA HII KUWASHUKURU WANAKIJIJI WOTE MLIOJITOKEZA KUNISAIDIA KATIKA KUTANGAZA ANUANI HII MPYA YA GLOBU YA JAMII. SI RAHISI KUWATAJA MMOJA MMOJA KWA JINA, HIVYO NAWASIHI MCHUKUE SHUKRANI HIZI KAMA ISHARA YA KUMSHUKURU KILA MMOJA WENU KWA MOYO WA USHIRIKIANO MLIOUONESHA.
KIPEKEE NAMSHUKURU SANA MDAU WA MK GROUP KUPITIA PALE KIJININI PAKE http://www.mkgroupltd.com/ KWA KUFANIKISHA ZOEZI HILI KWA UFANISI WSA HALI YA JUU NA KWA MUDA ULIOTAKIWA. MKUU ASANTE KWA HILO, NA BWANA AWE NAWE...
WENU MNYENYEKEVU
MICHUZI


Pongezi zako nyingi kaka "Michuzi" kwa kufungua Blog nyingine mpya kama hii na ile nyingine. Nakupongeza kwa kutuendeleza katika upashanaji habari na kutuletea burudani zote tuzipendazo. Tupo pamoja na wewe ndugu yetu.
ReplyDeleteBLACKMANNEN
hafungua blog mpya wewe ila kabadili jina tu au kaondoa lile la issa na kuweka blog.com lakini kila kitu ni kile kile
ReplyDeleteHongera sana.
ReplyDeleteHongera tena Mhe. wa Tegeta,
ReplyDeleteBismillahi naanza, kwaye mwingi wa kudura,
Subihana ni wa kwanza, mmiliki wa ishara,
Maliki alo mjuza, mwenye kutunza ahera,
Hongera Ndugu Michuzi, sasa umefanya kweli.
Barua pepe yafika, Michuzi kafanya kweli,
Kwa haraka nikatoka, niichunguze habari,
Kwa upole naandika, tovuti nimekubali,
Hongera Ndugu Michuzi, Sasa Umefanya kweli.
Bulogu kaifungua, Kafanya kweli Michuzi,
Supu ameiipua, bila kufanya ajizi,
Ni ua limechanua, lapendeza waziwazi,
Hongera ndugu Michuzi, sasa umefanya kweli!
Nikabonyeza tovuti, kutafuta ya zamani,
Kumbe ya kwake tamati, iliishia jioni,
Kumbe kaongeza chati, ya kwake mtandaoni,
Hongera ndugu Michuzi, sasa umefanya kweli.
Naweka chini kalamu, beti zangu zinatama,
Kama vile niko zamu, tovuti naitazama,
Hakika wewe Mwalimu, wengine tunachutama,
Hongera ndugu Michuzi, Sasa umefanya kweli.
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
hongera sana mkuu!
ReplyDeleteOH KUMBE HUWA MNAHARIRI! BASI NENDA TAASISI YA TAALUMA ZA KISWAHILI UDSM ILI UPATE MTAALAMU WA KUWEKA MASUALA YA LUGHA SAWA. NAFIKIRI WAKO TAY. KUJITOLEA. LAKINI HONGERA SANA
ReplyDelete