Dfunk RP: Naweza kujua album mpya inaitwaje


Fid: Inaitwa “DARWIN’S NIGHTMARE”, hili jina lilitumiwa na mtu mmoja ambaye ilifanya documentary iliyofanywa na mtu akaelezea mambo ya Mwanza kuhusu samaki n.k ilileta gumzo sana, Mtu akisema “Darwins nightmare” utajua tu ni kuhusu Mwanza, na nataka kuelimisha watu zaidi.maana katika nyimbo ya Mwanza Mwanza sikuelezea kuhusu Mwanza , nilitaka kujitambulisha tu mimi ni nani, nimetoka wapi na itikadi zangu ni hizi.


Maana kuna baadhi ya watu walipata fursa ya kusikia hiyo nyimbo hawakunielewa kwamba walitegemea wangekuta mambo ya samaki ndani ya nyimbo hiyo,lakini kwa upande wangu haikuwa hivyo,Vile vile Kwenye traki hii(mwanza mwanza) nilijaribu kumkumbuka mtu muhimu sana katika maisha yangu ya muziki marehemu mtoto wa Dandu,kama umewahi kusikia, wakati nyimbo inaanza hivi “nilianza rap kabla mtoto wa Dandu hajafa” God bless his soul.


Fid Q yupo katika safari ya kuleta mabadiliko ya mtazamo wa hip hop kwa watu wa rika zote. Uwe kijana wa jana, leo hata kesho kwa Tanzania na Nchi zingine pia.


“Safari ilianza Mwanza hadi Dar es salaam, ikapita Tanzania nzima na sasa Afrika mashariki na bado tuna lengo la kupeleka nchi za mbaaali zaidi, hatimaye siku tutakuja sema ndoto zimetimia”.


Dereva wa safari yetu hii, ya kuitangaza Nchi hii, na kuleta mabadiliko ya kizazi hiki, kwa manufaa yetu sisi, si mwingine zaidi ya Fid Q, ambaye pia anajulikana kama “Mwanza Mwanza”.


Unanipata hapo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michuzi. Mbona unatupiga chenga za mwili? Hatukuoni kwenye michuzi-blog.com. Tueleze tupitishe mchango kama uchache umepungua.

    ReplyDelete
  2. Hii album cover imefanana saaana na album cover ya mwanamuziki fulani wa hip hop nchini marekani. Big up though.

    ReplyDelete
  3. kwa kupata full story ya uyu mshkaji FID Q pita www.defunkadelic.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...