UKWELI ULIOSABABISHA VIJANA WA MWAKA WA LUGHA(2007-2008) CHUO KIKUU CHA URAFIKI LUMUMBA NCHINI URUSI KUWASILISHA KILIO CHAO UBALOZINI KWA MUDA WA SIKU NNE MFULULIZO. KAMA INAVYOELEZWA NA MWENYEKITI WA UMOJA WA WANAFUNZI HAO
Mimi, mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wa kitanzania wapatao 148 wanaosoma Chuo Kikuu cha Urafiki (Lumumba )nchini Urusi, nimesikitishwa sana na hatua ya ubalozi wetu pamoja na wizara yetu ya elimu kuamua kuubadilisha ukweli ili waweze kufanikisha matakwa yao.
Ninasema hivyo kutokana na ukweli kuwa mimi pamoja na wenzangu tuliomaliza mwaka wa pili tuliletwa kwa mkataba huo huo ulio waleta vijana hawa. Matatizo haya yanayo wapata vijana hawa wa mwaka wa maandalizi ya lugha hata sisi yalitupata miaka miwili iliyopita, kwani tulifika Urusi tarehe 31/11/2005 badala ya tarehe 1/9/2005, hii ikimaanisha kuwa tulichelewa miezi mitatu.
Hali hii ya ucheleweshwaji wa wanafunzi kufika urusi huchangia matatizo mengi sana mojawapo ikiwa ni baadhi ya wanafunzi kurudia mwaka wa masomo kutokana na kucheleweshwa kufika nchini urusi, kwa mujibu wa wizara ya elimu tulipaswa kulipwa fedha za miezi tisa,wakati huo balozi wetu aliyekuwepo Patrick Chokala alidai kuwa fedha za mwezi wa kumi na moja 2005 alituombea kwa serikali kama huruma tu ingawa ilikuwa ni haki yetu.
Mimi niliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa wanafunzi wa kitanzania chuoni kwetu wakati huo,pamoja na viongozi wenzangu hatukukubaliana na swala hilo kwani kwa utaratibu wa serikali yetu (wizara-bodi ya mikopo), mwanachuo hulipwa fedha kulingana na mwaka wa masomo yaani (September-august) kila mwaka, pia ukizingatia kuwa wakati tunakuja Urusi tulisaini fomu za mikopo kwa ajili ya mwaka mzima wa masomo, kitu kingine kinachoonyesha ukweli huo ni kuwa pamoja na kuchelewa kufika chuoni, serikali yetu hulipa ada zetu za kozi ya lugha kwa kipindi cha mwaka mzima ,sio hilo tu ila hata bima ya afya serikali yetu hulipa na inaendelea kulipa kuanzia(septemba-august).
Vile vile wakati matokeo yanatoka kwamba tumechaguliwa kuja kusoma urusi kuna wengine kati yetu walikuwa wameanza masomo katika vyuo vikuu mbali mbali nchini, lakini baadaye wakapata nafasi ya kuja kusoma urusi hali hiyo ilipelekea wanachuo hao kuandika barua ya kuomba mikopo yao kuhamishiwa Urusi kama walivyo agizwa na wizara kuandika barua hizo, na walitekeleza agizo hilo la wizara.
Hivyo basi wizara iliwahakikishia wanachuo hao kupata fedha zao za mwaka wa masomo(2007-2008) watakapofika nchini urusi. Ukizingatia hayo yote pamoja na ukweli kuwa mwanafunzi anayekuja kusoma Urusi ni mgeni wa mazingira ya urusi na anakuja kuanza maisha upya, hii ikiandamana na gharama za lazima za awali ambazo wizara yetu ya elimu pamoja na ubalozi wetu hautaki kuzikubali mfano nguo za baridi kwani ukicheza na baridi ya Urusi unaweza kuathirika kiafya.
Vilevile tunahitaji viatu vya kujikinga na baridi, pamoja na vyombo vya kutuwezesha kujipikia wenyewe kwani wanafunzi walio wengi huwalazimu kujipikia wenyewe kutokana na ukweli kuwa, kiwango cha fedha za kujikimu kinachotolewa na serikali yetu humwezesha tu mwanafunzi kujipikia mwenyewe kwani ukila katika migahawa ,kiasi hicho cha fedha hakiwezi kukufikisha hata nusu ya mwezi.
Kutokana na sababu hizo nilizozitoa za msingi tuliamua mwaka 2006 kuzifuatilia fedha za miezi miwili yaani (September na Oktober) ambayo hatukupewa kwa madai kuwa hatukuwa tumefika Urusi, lakini kila tulipowasiliana na ubalozi tulipigwa danadana mpaka tukakata tamaa lakini tulijitahidi kuwaonyesha na kuwaelezea sababu za msingi kuwa fedha hizo zilikuwa ni halali yetu na haki yetu pamoja na hayo waliendelea kushikilia msimamo wao, cha ajabu tulipokaribia kumaliza mwaka wa lugha tulipewa kwa ghafla fedha hizo na tulipohitaji maelezo tuliambiwa tusiulize zitokako, pamoja na hilo tulielewa ni zile zile tulizokuwa tukizidai.
Sasa ndugu zangu watanzania naomba niwahakikishie kuwa huo mkataba uliotuleta sisi 2005 ndio uliwaleta ndugu zetu 2007 katika chuo hicho hicho, na hawa nduguzetu ndio leo wapo katika maisha magumu na yakukatisha tamaa, kufuatia ukweli kwamba walipewa fedha za miezi kumi na moja tu (September 2007-July 2008) badala ya miezi kumi na miwili, yaani mwaka mzima wa masomo (September 2007-August 2008).
Mimi kama rais wa umoja wa wanafunzi hao, nimejaribu pamoja na viongozi wenzangu kuwasilisha matatizo haya pamoja na mengine mengi , yakiwemo ya fedha za malazi, fedha za mafunzo kwa vitendo (practicals), fedha za vifaa vya shule (stationeries) pamoja na fedha za madawa ubalozini, lakini hakukuwa na majibu yoyote ya kuridhisha,kutokana na hilo na ukweli kuwa vijana waliishiwa fedha kutokana na ugumu wa maisha waliamua kupiga hodi ubalozini ili kujua mustakabali wao kwani walishindwa kuishi bila fedha hizo ambazo wanaamini kivyovyote ni haki yao kama ilivyo kuwa haki yetu 2006, kwani naamini isingelikuwa ni haki yetu mwaka 2006 tusingelipwa fedha hizo, kumbukeni kuwa maisha ya Moscow yamepanda kuliko kawaida (Moscow ni mji wa kwanza wenye maisha ghali duniani), sasa kwanini ukweli huu unabatilishwa?
Niukweli kuwa vijana hawa wanaosoma mwaka wa lugha 2007-2008 wanastahili malipo haya. Kama mlivyosikia sikuzote ukweli kuwa Urusi ni nchi ambayo kazi kwa wasio raia wa Urusi kupatikana ni ndoto na ukibahatika kuzipata japo za kuosha vyombo ukitoka au ukienda kazini unarudi hostel na manundu kwani skin haters (wabaguzi wa rangi) wakikupata amazako ama zao.
Ninaamini kabisa kuwa serikali yetu inamalengo mazuri kabisa na sisi lakini kuna watendaji wachache Serikalini, wanaojaribu kuupindisha ukweli na kuipaka matope Serikali kwa manufaa yao binafsi. Naomba tuondoe ubinafsi kwani itakuwa hasara kwa taifa langu nikifa kwasababu nilikuwa natafuta fedha za kujikimu.
Kwa kuwa Serikali yetu ilituleta Urusi kusoma na kupata ujuzi ili tukalitumikie Taifa letu, basi ninaomba ituhudumie ili tumalize masomo yetu na turudi nyumbani salama.
Ninamnukuu aliyekuwa balozi wetu Patrick chokala mwaka 2006 alituambia “kila mmoja aishi kwa urefu wa kamba yake”, tulipokuwa na madai ya fedha zetu kama waliyonayo hawa vijana wa mwaka walugha (2007-2008).
Ndugu zangu machozi yalinilenga lenga niliposikia hayo maneno ya aliyekuwa muwakilishi wa Rais wa Tanzania nchini Urusi, yaani Mh. Balozi, kwani ikumbukwe kuwa familia zetu ni duni pia huku Urusi ni mbali na nyumbani na hatuna kaka,mjomba, mama mdogo wala shangazi.
Inamaana mimi kama ni mtoto wa maskini niendelee kunyanyasika tu kwasababu wazazi wangu kamba zao ni fupi? Hatuwezi tukalijenga taifa letu kwa misingi hii ya matabaka.
Kama serikali yetu inashindwa kutuhudumia basi isingetuleta ughaibuni ili tuje tuteseke. Ingetuacha nyumbani ili maisha yakiwa magumu turudi majumbani tukale mlenda pamoja na wazazi wetu kwa sababu kamba zetu ni fupi..
Baada ya maisha kuwawia vigumu vijana hawa wa mwaka wa lugha (2007-2008) kama nilivyo elezea awali waliamua kwenda ubalozini kujua mustakabali wao lakini walifungiwa katika chumba kidogo cha mapokezi nje kukiwa kumetanda askari zaidi ya 30 na bila hata nafasi ya kwenda kujisaidia walikaa siku mbili mfululizo bila maji wala mkate , siku ya tatu wawakilishi kutoka wizara ya mambo ya nje ya Urusi walifika ubalozini na kushangazwa sana na kufungiwa kwa vijana hawa.
Wakamwamuru Balozi mlango ufunguliwe na vijana wapewe chakula ndipo hayo yakatendeka. Jamani watanzania, hii hainiingii akilini, kwamba warusi ambao mtaani wanatutemea mate na kututia manundu wanatuonea huruma ilhali ubalozi pamoja na wizara yetu wanaamua kutoa adhabu za jeshini ili kuwafunga wanyonge midomo?
Na baada ya hapo wanatoa taarifa za uongo kuwa wanafunzi wameuteka ubalozi, huo ni uongo wa kupindukia na sio ubinadamu wala uongozi wa sheria (rule of law). Kama serikali yetu inavyosema, kumnyima mtu chakula, maji , pamoja na kumfungia mlango asitoke hata kwenda chooni ni ukiukwaji wa utawala bora na haki za binadamu.
Naomba tulielewe hilo , sasa kuvamia na kuuteka ubalozi kuko wapi? Mimi kama rais wa wanafunzi ninasema madai ya vijana ni yakweli na ni haki yao, nitasimamia upande wao kwani penye ukweli uongo hujitenga , ninaiomba wizara yetu ya Elimu iangalie upya msimamo wake kuhusu madai haya kwani utaratibu wa wizara hauwezi kubadilishwa mwaka hadi mwaka kwa ajili ya kuwakandamiza wanyonge huku mafisadi wakiendelea kuzitumbua kodi za walala hoi.
Bado tunamatatizo mengi sana ambayo yanahitaji kuungwa mkono na watanzania wote wanaoijali na kuipenda nchi yao kama sisi.
Watanzania wenzangu, naomba niwaeleze kuwa fedha za kujikimu ambazo tunapewa kwa mwezi kiasi cha 292 US dollors , ni kidogo sana kutokana na ukweli kuwa hizo fedha matumizi yake ni
1.kulipia gharama za hostel(malazi) kiasi cha 840 us dollors kwa mwaka
2.fedha za chakula kwa kipindi chote cha mwaka mzima
3.fedha za vifaa vya masomo(stationery allowance)
4. fedha za practicals na field works kwa baadhi ya kozi.
5.fedha za kununulia madawa kwani bima ya afya hailipii madawa
6. fedha za usafiri kwamfano wengi wa wanafunzi husoma eneo lililopo mbali na hostels hii inamaanisha wanatumia usafiri wa basi na baadaye treni za umeme(metro) kwenda na kurudi kilasiku.
7. fedha za usajili(registration)
Ikumbukwe kuwa dola imeshuka thamani na inazidi kushuka thamani mwaka hadi mwaka kwani tulivyofika 2005 dola 1 ilikuwa sawa sawa na rouble ya Urusi 30 lakini kwa sasa dola 1 ni rouble ya urusi 22.45.
Hii inamaanisha kuwa, unapozibadili dola kwenda katika Roubles, thamani ya fedha inashuka. Naomba niwape mfano rahisi sana wa kupanda kwa gharama za maisha , mfano wakati tumefika mwaka 2005, mkate ulikuwa ukiuzwa rouble za urusi 10 lakini kwa sasa mkate unauzwa rouble za urusi 20.
ni ongezeko la asilimia 100 , nikisema tunapewa dola 292 unaweza ukafikiri ni fedha nyingi sana lakini mchanganuo nilioutoa hapo juu unaonyesha ni fedha ndogo sana kwa maisha ya kilasiku, ninauliza nani atatuokoa na kutunasua kutoka katika balaa hili?
Kama Serikali yetu ina nia thabiti ya kuwasomesha wanafunzi wengi nchini Urusi, Kwa nini isiwapeleke katika miji mingine tofauti na Moscow ambako gharama za maisha ziko chini?
Ninawaomba watanzania wenzetu mtusaidie katika mapambano haya magumu kwani bila msaada wenu mafanikio kwetu wanyonge wa Urusi pamoja na wanyonge wa nyumbani ni ndoto. Ninaahidi kusema ,kuzungumza,na kusimamia ukweli mpaka mwisho wa maisha yangu, kwani naamini ipo siku ukweli utafaamika na watanzania watatutetea na kutunasua kutoka katika janga hili kwani taifa imara la kesho lazima tuliandae leo.
Ni mimi
BONIPHACE –ELPHACE-MAGINA ,
RAIS wa umoja wa wanafunzi wa kitanzania
CHUO KIKUU CHA URAFIKI(PATRICE-LUMUMBA) MOSCOW
URUSI.
kijana umeeleza mambo mengi sana katika waraka wako mrefu sana lakini mimi naona kama wewe unajifunza porojo za kisiasa za bongo ndiyo ninyi tunaowakataa hata kina kikwete na kina lowassa wametoka katika mfano wa watu wa aina yako siasa nyingi kuliko ukweli,nani alikuambia Urusi kuna maisha mazuri na mlifuata nini huko ,kama mnaona maisha magumu rudini nyumbani kuliko kutuleza porojo zisizo kuwa namiguu wala kichwa ,mbona wenzenu waliopo kwenye nchi nyingine za ulaya wanachachalika kama mnaona mnatolewa manundu rudini nyumbani kuna vyuo vya kumwaga sasa hivi mtapata nafasi na mtasoma,watu tuacha kuhangaikia mambo ya nauli zinapanda manataka kutuumiza vichwa ili mpate pesa ya kwenda kunywa vodka na malaya wa kirusi ,pumbavu zenu
ReplyDeletemh Rais wa wanachuo ,
ReplyDeleteinawezekana kabisa kilio chako na cha wenzako ni kweli kabisa ,maana serikali kwa kweli inakabiliwa na matatizo ya wanafunzi vyuo vikuu,
LKN POINT OF CORRECTION,MOSCOW SIO MJI WA KWANZA DUNIA WENYE MAISHA YA JUU noooooo,
UK -sababu ya PAUND
JAPAN--sababu ya DOLLA
GENEVA
....
,....
,...
KILA LA HERI KTK KUTATUA MATATIZO YA WANACHUO,
nashindwa kuelewa kwa nini wanafunzi wanataka kulipwa wakati hawakuwepo urussi kipindi hicho!
ReplyDeletena huko ubalozi mlienda mkaambiwa muingie kwenye chumba kisa mkafungiwa mlango na mkakatazwa kutoka au mlienda mkafikia reception na mkakatazwa kuingia ndani zaidi ya hapo na mkakosa cha kula na pa kulala kwa kuwa hamkuenda nacho hiho chakula?
Ndugu zanguni hayo mambo ni ya kifisadi tu hakuna lolote.
ReplyDeletesikutegemea mimi kama huyu balozi mpya aliyeletwa huko Moscow anamambo ya kishenzi namna hiyo,,,naamini Patric Chokala ( Balozi aliyemaliza muda wake) asingefanya upuuzi kama huo.
wewe utafungiaje wanafunzi tena ughaibuni??hili swala ni kubwa mno, ndugu zanguni wala msiishie hapa kwa anko Michuzi, vyombo vya habari ni vingi mno pelekeni kila kona ya dunia waone ushenzi unaofanywa na serikali yetu.
Mwaka jana tulishuhudia wenzetu kutoka Ukraine wakirudishwa kwa mambo ya dizaini hii hii.
jamani serikali yetu tunaenda wapi???????
si ni bora basi msipeleke vijana nje??
na nyie wawakilishi Ubalozini kuweni na utu, na akili za kiutawala pamoja na utaifa, huwezi kumfungia mtanzania mwenzako ugenini.
kumbuka wewe bwana balozi ni wa kupita tuu kama wenzio, ofisi utaiiacha tu hiyo, hivyo jari vijana wako sio ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Mdau-India.
Ah!! ni muendelezo uleule wa mfumo wetu mbovu wa utawala unaojali saana siasa na ubinafsi kuliko taaluma zingine ndio maana hata hiyo nafasi ya ubalozi huko amepewa mtu ambaye siamini sana kama kweli ni mwana diplomasia thabiti zaidi ya kupewa fadhila za kisiasa tu . Poleni sana vijana kwasis tunaoelewa tunajua nini kinachowakuta lakini kwa utamaduni wa kitanzania hatuna tunachoweza kuwasaidia zaidi ya kuwaombea mafanikio katika mapambano yenu kama ambavyo juzi imetokea kwa madaktari wanafunzi , Kazeni moyo ' YANA MWISHO ' Rashidi alisema .
ReplyDeleteNYERERE,TUNAOMBA UFUFUKE
ReplyDeleteKwanza poleni kwa usumbufu na taabu.
ReplyDeletePili mjue hizo si taabu kama wanazopata ndugu na jamaa waliopo Tanzania ambao hawana uwezo wa hata mlo mmoja kwa siku.
Tatu, serikali iangalie jinsi gani ya kutumia rasilimali ndogo tulizonazo;kwani si ajabu kukuta kuna wanafunzi wanakwenda nje ya nchi kujifunza masomo ambayo hata nyumbani kuna vyuo vinafundisha; kwa maelezo ya mtoa ujumbe kuwa watu wengine walikuwa wanasoma Tanzania wakaacha na kwenda nchi za nje...huu ni wenda wazimu.Ni afadhali kupeleka watu wakasome Postgraduate na masomo yenye uhitaji maalum nchini.
nne ni lazima nasi wanafunzi tukue sio siku zote kutoa breaking news nchi za nje kuonyesha serikali haijali watu wake....Hii nasema nikiwa sikungamanani na serikali,chama wala upande wowote. waliopo nje na wanaobeba mabox ni mashahidi wangu...hata nchi yenye maendeleo kama UK,USA wana wanafunzi wenye matatizo lakini huwatua kwa busara sio kupigana kelele!! Je mzazi wako asipokuletea pesa shule ya borading utaandika barua na kutuma kwa Michuzi!!Tufanye vitu kama professional...vinginevyo tutakuwa na kizazi cha kisaniiiiiiiii!!
La mwisho...ambalo nimeliona hata kwa serengeti boys walioletwa na serikali hapa ughaibuni!!
wanapewa pesa ya mwaka mzima badala ya kupewa pesa ya kujikimu kila BAADA YA MWEZI AU ANGALAU KWA MIEZI MITATU MITATU!!! UNAWEZA ULIZA KWANINI NASEMA HIVYO!!!^#^^^^#%#*&%
SABABU KUU NI KWAMBA HAWA VIJANA WENGINE NI MALIMBUKENI BAADA YA KUPEWA PESA HUISHIA KUFANYA MATUMIZI YASIVYO TAKIWA(kama kwenda kuanzisha miradi Tanzania,kukaa na ndoa zisizo rasmi n.k) NA KUISHIWA BAADA YA MUDA MFUPI NA KUANZA KUPIGANA MAKELELE..usikute na hao wa Urusi wapo kundi hiii...
na kuna hatari baada ya kumaliza shule badala ya kwenda kutumikia taifa nyumbani kwa kufanya kazi;serikali itabidi ianze kutibu wagonjwa wa UKIMWI!!kwani vijana wanajirusha mnooooooooooooooo bila taadhaliiiiiiiiiii
Samahani kama hoja hazina AKILI...vinginevyo ukipewa nafasi ya kusoma kweli soma sio kuanza kutunisha misuli na serkali;kwani elimu ndio silaha pekee itakayotufanya siku moja tuchukue nchi na kuipeleka huko tunakoona ni kuzuri otherwise mafisadi watazidi kututesa!
poleni vijana!!!!!!!!!!
ReplyDeletehakuna kurudi nyuma mwendo ni huo huo.Urusi sasa ipo juu sana katika taaluma zote.Hivyo vijana wanao soma huko hata kama kuna vyuo vyetu vinafundisha taaluma hizo lakini si kwa kiwango cha Urusi.Urusi wameanza kupeleka vyombo mwezini kabla Tanganyika haijapata uhuru,wanajitegemea kwa kila kitu.Hivyo waacheni vijana wasome sio kuwambia kuna taaluma wanasomea hata vyuo vyetu vinafundisha.
Vijana hizo ni changamoto zikabilini ipasavyo,na mkirudi nyumbani muendelee hivyo hivyo.
Nawatakia masomo mema.
NIMEMUELEWA RAIS WA WANAFUNZI LUMUMBA,
ReplyDeleteWAKUMBUSHE WENZIO HUKO,SIO KILA LINALOFANYWA NA WENGI LIPO SAHIHI.MSITAFUTE HAKI ZENU HALAFU BAADAE WENGINE WAKATAFSIRI NI FUJO AU KUVURUGA AMANI.WASHAURI WENGINE SIKU ZA USONI WAKITAKA KUTAFUTA HAKI, WATUMIE NJIA MBADALA YA USALAMA ZAIDI SIO WOTE KWENDA UBALOZINI.HIVI NA SISI WATANZANIA HUKU TUNAOKABILIWA NA MAJANGA YA KIMAISHA KAMA MFUMUKO WA BEI, WOTE TUKIAMUA KWENDA IKULU PALE KIVUKONI KWA MUHESHIMIWA ITAKUWAJE.
NAFIKIRI JIBU UMESHALIJUA ITAKUWAJE.
SOMENI KWA BIDII TUNAWAITAJI HUKU MJE KUKOMESHA UFISADI.
Poleni bwana hayo yalitukuta sie hiyo ni kawaida ya serikali ya Tanzania .Utamlipaje mwanafunzi dolar 300 wakati kiwango cha chini kwa maisha Moscow ni dollar 2000 kwa mwezi hao vijana wanaishije mie siwezi kujua? Na nani alifanya estimation za kipato hicho walifuta vigezi gani?as result vijana inabidi wajishughurishe na mambo ya maovu..
ReplyDeleteKuhusu maisha sijuhi mtu anajaribu kufanya ulinganifu eti London Expensive kwasababu ya Pound.. Tokyo sababu ya Yeni hao watu sijuhi wanaishi dunia gani..Moscow wakati wa fainali za UEFA wapenzi wa mpira wengi walishindwa hata ku spend night moscow kwa sababu ya ughari wa maisha.. mfano kwa wasio jua square metre nyumba moscow ni kuanzia dollar 6000 na kupanda wakati London ni equivalent ya 3500 usd..angalia mambo hayo ...usipenda kutoa hoja bila ya kuwa na details...
Sasa kwa vijana msiwe waoga Urusi ni nchi ya kibabe jaribu ku-adapt situation skin- head wapo lakini watu wasio warusi ndiyo wanaofanya kazi Moscow data za karibuni almost 5 million foreigners wanafanya kazi moscow jichanganye muwe among of them...mbona wanafunzi wa nchi nyingine wanapiga mzigo nakupata hela poa tu wala hakuna haja ya kwenda kugoma ubalozini ...ingia mtaani kazi urusi ni za kumwaga ndiyo nchi pekee Europe ambayo haina unemployment problems kila siku wanatangaza deficit of manpower... kama una makaratasi ya shule officially kazi utapata hasikudanganye mtu ila kama mzamiaji hapo urusi hakukaliki siku hizi ...
Na kwa wale wenye kasumba za kizamani U.K. /U.S.A kazi siku hizi hakuna wamarekani wenyewe wanahamia urusi na makampuni yao eti mtu unawashauri vijana eti kwanini hamkwenda Ulaya ..siku hizi hakuna deal huko fungua macho mambo yako Russia /China basi.Mwisho ujumbe kwa.......
mtu akiongea na wewe lugha unayo ijua basi maneno yote uingia kichwani.. ila mtu akiongea na wewe your mother tongue language basi maneno yote uingia moyoni..For...our dear diplomats jaribuni kufanya uamuzi kutoka moyoni siyo kichwani...
USHAURI WA BURE KUTOKA KWA...
MDAU WA KARAGWE
Rudini nyumbani.
ReplyDeleteMnalalamika sana bila maana yoyote kabisa. Nyinyi mnalipwa fedha na kuna wanafunzi wakitanzania wako nje wanajisomesha wenyewe.
Rudini nyumbani.
we anon 7.52 hauna akili INAONYESHA::::mi ni mmoja wa wanfunzi nje (sio urusi) na nafanya kazi na napata msaada kutoka kwa wazazi nikikwama.. nikishindwa maisha ya hapa basi ntarudi nyumbani kwani ni mimi mwenyewe nilitaka kuja huku kwa gharama zangu. sasa basi hao vijana WAMECHAGULIWA NA KUAHIDIWA MIKOPO,NA NDIO MAANA WANAENDA KUDAI HIZO HAKI ZAO,ufikirie kabla ya kuandika.
ReplyDeletekwa wenzangu nawapa pole kazeni buti na mtafute tuajira.
POLENI VIJANA WA PREPARATORY FACULTY-patrick Lumumba.
ReplyDeletematatizo ya fedha toka serikalini yamekuwepo kwa muda mrefu tu hapa urusi,na mtaondoka mtayaacha watakaokuja nao watayakuta pia watayaacha. because THAT IS THE WAY IT IS& I SEE NO CHANGES!
mimi mwenyewe na wenzangu 9 kunamchezo mchafu tulifanyiwa mwaka 2005/06 accademic year japo hatukuwa mwaka walugha. ALIYEHUSIKA HADI LEO HII HATUMJUI KAMA NI WIZARANI,BODI,AU whatever lakini tulipigwa panga USD 830 kilamoja wetu,hadi leo hii hizopesa zimekuwa ndoto!!!!
mwenzetu mmoja ambaye ndugu yake anafanya kazi pale wizara ya sayansi yeye aliletewa baada ya mwezi 1. wengine tulifuatilia tulipigwa danadana mara ubalozi wanasema wanawasiliana na bodi,bodi wanasema mhasibu wa wizara [mr.RUTA] ndiye anashughlikia hizopesa zetu tutapewa. HADI HIVI SASA TULISHA KATA TAMAA & LIFE GOES ON!!!
Tena mlaji alitumia tekniki kali sana,maana :-
1.alihakikisha kuwa kila mji aliathirika mtu mmoja tu[logic:to weaken the fpllowup efforts as acollective of people]
2.alihusisha watu wenye tabia ya upole wa muonekano kitabia,wasiopenda jazba na wepesi wa ku-give up![logic:not to pause constant pressure on him/her]
TULIFUATILIA LAKIZI HADI LEO HII HUU NI MWAKA WA NNE BILA JIBU LENYE MATUNDA. BALOZI aliye pita na timu ya utendaji ukiwauliza watakwambia maana wanalijua hili na naamini walilishughlikia walivyoweza ila MCHAWI WETU HAELEWEKI YUKO WAPI.
USHAURI: YOU SHOULD DO WHAT YOU HAVE TO DO,SO THAT TO GET TO DO WHAT YOU WANT TO DO.
WE ARE LIVING IN THE CRAZY WORLD IN WHICH NO BODY CARES WHAT YOU FEEL SO LONG AS IT DOESN'T TOUCH OR AFFECT HIS/HER LIFE! so as they told you 'your feet is your only carriage,but when you are gone everything is gonna be alright!
wenzetu walituchangia mkopo tukasukuma siku,tulipoishiwa ubalozi walitukopesha kwa muda,tulipo pata za2006/07 tukalipa deni la ubalozi, and problems &life all together goes on!so don't worry ma young brothers!!it will come to pass,even though slowly and painfully!!!
nani alikuambia urusi ndiyo jiji ghali kuliko yote duniani acha porojo zako we bwana mdogo hizo psa mnazolipa kwa mwaka kwa ajili yha nyumba huku scandinavia ni psea ya miezi miwili tu kwa kodi tena ni nje ya miji siyo kwenye miji mikubwa kama stockholm au helsinki au copanhagen na mengineyo sasa huo ughali unatoka wapi nyiehangaikieni hivyo visenti vyenu mkikosa rudini nyumbani kwani mmefukuzwa mambo mengine huwa mnajitakia nyie wenyewe bona wenzenu tunafagia na kubeba box huku kwa watu acheni kuleta ubishoo vijanakazi urusi zipo nyingi tu me nilikaa finland miaka kumi na nilikuwa nafanya ziara mara kwa mara urusi nimekutana na watanzia wengi tu wanaofanya kazi kama ubaguzi upo popote palee duniani .acheni kusumbua watu fanyeni kazi kama mmeshindwa kukimbizana na ulaya njia ya kurudi nyumbani nyeupe huna hata haja ya kuomba viza wala permit
ReplyDeletenyie madogo tulizeni mizuka,serikali inawafundisha namna ya kuwa wajeshi[ma hardcore] ili nanyie mkishika madaraka enzi zenu unakuwa husikilizi kilio cha mlalahoi wala nini unakula kodi kifisadi kulipiza taabu ulizo pata huko. so msikonde kaza viuno tu na nyie mkashike chance faster muendeleze kula kifisadi.
ReplyDeletemie mwenyewe taabu niliyopata wakati nasoma sasahivi naombea tu nipate ofisi nikuonyesheni shughuli,atakaye leta zakezipi kufuatilia mitikasi yangu huyo nazaa nae hata kwa bastola kimafia mafia!maana wengine hatukuzaliwa kuteseka tu na wengine ku-enjoy life,sasa ni zamu yao na yako pia itafika. kwa sasa wee uchune tu teseka ule shule ukimaliza zama ulenao sahani moja!!
vijana mswala yenu ni yamsingi watu walio urusi na walio pita urusi wanayafahamu.
ReplyDeleteanon uliyesema umekaafinland na umekuta watanzania wanafanyakazi urusi na kurudi nyumbani wala huhitaji viza wala permit wewe ni limbukeni maana hata unachokisema hukijui na kwa maneno yako unajishitaki mwenyewe kuwa hujawahi kufika urusi,maana ungekuwa umefika ungejua kuwa kutoka urusi kurudi nchii kwako au kwenda kokote duniani unahitaji exit viza,so usidandie mambo usiyo yajua ukijidai unifahamu urusi. pia unatakiwa uelewe kuwa ukiwa urusi kwa student viza hutakiwi kufanya kazi wala working permit hazitolewi kwa wanafunzi urusi,so kama ulisikia mtu akibangaiza alikuwa anatake risk,maana ukishikwa ni depotation!!safari nyingine ukichangia hoja sema yale tu unayoyafahamu kwa uhakika.
anon uliyesema wanafunzi wanadai pesa ya kununulia vodka na malaya sikulaumu maana inathibitisha uwezo wako mdogo wa uelewa ulionao kichwani,kwani hata hao malaya unao wasema sidhani kama mshahara wako[kama unakazi hapo ulipo] unaweza kutosha kumchukua huyo malaya na kupata unachotaka kwake hata kwa saa1 tu!safari nyingine usiwe limbukeni bali ongea kama binadamu mwenye kushirikisha ubongo kabla ya kutenda.
mwisho mimi vituko vyote nilivyotendewa nikiwa urusi nimevumilia na kuvihifadhi,waliohusika kwa kuwa sio miungu lazima kisasi tutalipizana hapahapa duniani,no one will go down unpunished unless they die early or i do! otherwise hata kwa kununuliana majambazi lazima kitaeleweka tu,nchi hii kunawatu wakishika nyadhifa wanajiona are not reachable!the time is over we wanna see changes now,hakuna mapinduzi ya mtutu wala uvunjaji amani huo hatuutaki,lakini every one will be responsible for avery single action they do to humiliate the right of the other!this method will work since there is no justice unless you demand it. enough is enough beging for our life,is a shame to live beging your right as if is a favour!!
vijana kazeni buti atayerudi ajetuendeleze operation kushirikiana na mimi,lakini yangu ni silent so fanya kivyako namimi kivyangu,but achieving the same results.NO FEAR NO WEAR no WAR!
Anon 5:26 na kuunga mkono kisera.
ReplyDeletena wewe Anon 5:18 kwanza mshamba tu unadandia dandia vitu bwege kweli wewe, kakuambia nani urusi jiji? mpuuzi kweli wewe unaonesha dhahiri kabisa kwamba ulikuwa unampango wa kwenda Russia ila ukabaniwa badi hasira zako zote uwatolee wenzio mimaneno ya kashfa.
pumbavu sana wewe, nenda kaanze Jiografia ya msingi ujue mitaa kama huwezi kwa akili ya kawaida.
Anon 10:06 umeeleza ya maana kwani hata wale ndugu zetu wa Ukraine walikuwa na kilio cha namna kama yenu ( Russia ), serikali yetu imejaa rushwa,ufisadi,udharimu na kila aina ya uibilisi ndani yake.
wee subirininchi tuishike sie vijana, wazee wote vijijini mtarudi....pumbavu na matajiri wote lazima mtaifishwe, shenzi.
Mdau-Paris
first of all, sorry to hear about your struggles. I do not live in Russia and I've never been there but I have friends who went to school there and know how it's like.
ReplyDeleteDo not get discouraged by some of the negative comments here; every person is entitled to their opinion.
I remember a few years ago students in Tanzania were (rightfully) demanding an increase in the daily allowance rate. Some people rebuked them and told them the same things people are saying to you here; asking why should students be given so much money while I am starving. But they do not ask why the government squanders so much money on even less important ventures; not to mention corruption, etc.
Some have said why don't you come back; they are missing the point as it is the government, under an agreement with the Russian government that decided to send the students there with an agreement that they will be receiving subsistence allowance from HSELB; it's not like these guys went and boarded the plane without any prior understanding with the govt as to who will take care of their upkeep during studies. I totally agree with Anony from 3:44 PM. Like him, I am abroad but on a scholarship that has nothing to do with govt of Tanzania. So if things went sour here, I'd pack it and go home. Wouldn't bother anyone at the embassy or the govt because it is not them who brought me here. But your case is different, and the govt is 100% responsible for you.
It is because of this disjointed views amongst the Tanzanian public that the people in power feel they can keep squandering money and do whatever they want without any repacations.
Someone suggested you guys get jobs to help pay bills. It's not a bad idea, and if your status in Russia allows you to work then by all means go for it. However, this does not mean that you should stop fighting for your allowances. it is your right and just because you work (assuming you get a job); doesn't mean the govt should backtrack from it's agreement with you which was to fund your stay there through loans from HSELB.
Moreover, you should not be forced to have to work. You should be given enough money for upkeep so that you can spend your time concentrating on your studies.
I don't understand why some people are spending all this time and effort arguing whether Moscow is the most expensive city in the world? That is just veering off-topic; the main issue here is the sponsorship (or lack thereof) of these students. Does it really matter whether London or Tokyo is more expensive than Moscow? At the end of the day, the point is, life is pretty expensive; and these students aren't getting the money there were promised.
Best of luck in your endeavors.
IoI Upepo wa siberian umewapitia eh! mlifikiri ulaya hela zinaokotwa IoI work hard atii moscow expensive ungekuwa hapa London ungesema nini. acheni politik Ano. wa kwanza u make me laugh point!!!
ReplyDeletewewe anon 10.06 ndiyo nyie wote mliopoteza mwelekeo ona fikra zako zilivyo za kijinga na kipumbavu ,angalia sasa kama kweli wewe msomi utakaaje kukaa na kufikiria kuwa utalipiza kisasi huo ni upumbavu na ujinga na inaonesha ni jinsi gani ulichokipata huk urusi hakijakusaidia thats watu wanaona kuwa mnaenda kupoteza muda na kuchoma pesa za walala hoi kamam yote hayo mliyajua kuwa hakuna kazi na matatizo kwa urusi ni ya kawaida mnaendelea kufuata nini ,wewe na hao wenzako wote hovyo tu na inaonesha ni mmoja kati ya hao wanaohangaika hapo ubalaozini,hakuna atakayewaonea huruma au na sisi mnataka tutme picha tuwaoneshe picha za walalahoi mnaotaka kutafuna kodo zao wanavyolala huko manzese,pumbavu zenu nyie hasa wewe anon 10.06
ReplyDeleteHii ni aibu na masikitiko sana. Kuna vijana wenzetu wanatafuta elimu huko Urusi na hawapati mahitaji yao. Kweli serikali inatakiwa kufanya wajibu wake. Wananchi wengi wa Afrika wanataka kusoma ila serikali zetu (viongozi madarakani) wanaleta shida sana. Hii itakwisha lini? Ukiuliza vijana Tanzania wanataka nini, unajua wanataka kusoma. Ukienda nchi zingine za Ulaya na hata Marekani, wanata video game na kustarehe sana. Mimi nashindwa kuelewa hizi serikali za Afrika, ikiwemo Tanzania wataacha lini kucheza na vizazi vijavyo. Hope yetu kubwa ni kupata kiongozi kama Obama. Tunahitaji Obama wengi Afrika. Serikali ya Tanzania, kila leo scandals za mamilioni ya pesa yameibiwa: Benki kuu, Tanesco, Migodi ya madini, Uuzaji wa viwanda, Corruptions zinazoendelea kila siku, Muhimbili, wizara ya elimu, na mengine mengi. Cha ajabu hawa viongozi na baadhi ya wafanyabiashara wanaiba (wanaita just back door business-deals)na kujenga hapo hapo Dar. Wanafurahi kuishi kwenye Bangaloos na kuendesha magari ya fahari, wakati jirani zao hawana chakula wala dawa za Malaria. Hizi pesa zinazoibiwa, zinaweza kulipia mengi, huduma kwa wananchi. Viongozi wanafanya makosa na hakuna hatua yeyote ile wanachukuliwa, hii itandendelea mpaka Afrika itakuwa na makuburi kila mahali. Kila mtu aliyesoma na mwelevu anajua jinsi gani tunavyojitakia matatizo yetu. Watu wengi wanakufa bila sababu na vizazi vingi vinazidi kupotea bule. Tu Stop All this Now. Stop Crime Against Your People Now. Time is UP
ReplyDeleteTAFUTENI DEAL KWANI HAKUNA WARUSI WANAOTAKA KUOLEWA? OENI KWA DEAL MPATE MAKALATASI MCHAPE KAZI. KWANI HIYO MIKOPO MIDOLLA MTAWEZA KUIRUDISHA? AMA MMESAHAU MSEMO WA KOPA ULIPE? KELELE NA MANENO KIBAO MKIAMBIWA HIYO MIKOPO MLIYO SIGN MRUDISHE DOLLAR 294 KILA MWEZI KWA MIAKA MINNE UTAWEZA KURUDISHA? PUNGUANI WOTE NI KWELI MRUDI BONGO MKALE MRENDA KAMA CHOKALA ALIVYOWAAMBIA KAMBA ZINGINE FUPI. ETI TUNAHITAJI VIATU VYA BARIDI? NANI KWAKWAMBIA USIENDE NA RABA MTONI ULIVYOONDOKA DAR? KILA SEHEMU KUNA UBAGUZI HATA BONGO WAHAYA WANABAGUA WACHAGA SASA NINI BADO HUJAELEWA.. KAMA WANAWAPIGA FIGHT BACK HUNA MIKONO? ULIPOKUWA UNA SIGHN MIKOPO SIULIAMBIWA HAKUTAKUWA NA VIATU VYA BARIDI? YOU SHOULD KNOW BETTER THAT SOMETIMES CURRENCY WILL DEVALUE! UNALETA MCHEZO MKISIKIA WATU WANA BEBA BOX KICHEKO UNADHANI WANAPENDA.MICHUZI MIMI NASHAURI HAO VIJANA WARUDI TU NYUMBANI KWA SABABU SIONI NI JINSI GANI SERIKALI ITAWASAIDIA VIATU VYA BARIDI AMA KUSHUKA THAMANI YA DOLLAR HIYO HAIKUWEPO WAKATI WANA SIGN HIYO MIKOPO AMBAYO WAKIMALIZA SHULE HATA KURUDISHA HAWATAKI......
ReplyDeleteJAMANI, KWA KWELI NDIYO MAANA TANZANIA TU MASKINI HIVI - TUNA WATU WENGI WA AJABU. UKISOMA MJADALA MZIMA UTAONA JINSI WATU WALIVYO NA AKILI ZA AJABU. POINTI NI MOJA TU: SERIKALI IMEWAPELEKA WANAFUNZI WETU NJE YA NCHI, HIVYO INAPASWA KUWATENDEA HAKI KUANZIA NA KUWALIPA FEDHA ZINAZOTOSHA HADI KUWAFANYIA UTU. HUWEZI KUMLAUMU MWANAFUNZI KWA SHIDA ANAZOPATA KUTOKANA NA UTENDAJI MBOVU WA SERIKALI. NDIVYO ILIVYO KWA WALIMU, MADAKTARI, WAKULIMA, MANESI, WASTAAFU WA AFRIKA MASHARIKI, POLISI, WANAJESHI, N.K. WATANZANIA TUAMKE JAMANI, TUSIONE SIFA MWANASIASA AU MTUMISHI WA SERIKALI ANAPOJENGA JUMBA KUBWA WAKATI VITU VYA MSINGI VINAISHIA KWA ANAYEPATA SHIDA KUTUKANWA. KAMA WEWE HUKUSOMA KIASI CHA KUPELEKWA RUSSIA, BASI KAA KIMYA. NIMALIZE TU KWA KUSEMA KUWA KWA MUJIBU WA TAKWIMU ZA SASA HIVI NI KWELI MOSCOW NDIYO MJI WENYE GHARAMA KUBWA ZA MAISHA. WANAOBISHA HAWAJUI TU! NA TUSIJIDANGANYE KUWA ETI TANZANIA TUNA VYUO VYA MAANA, SI KWELI. MIMI KWA UZALENDO WANGU NIMEJARIBU KUTAKA KUCHUKUA PH.D NYUMBANI NA USUMBUFU NINAOUPATA KWA AJILI YA KUPATA MAELEZO TU, NI WA AJABU. HAPA NILIPO KILA KITU KIPO KWENYE TOVUTI, LAKINI SISI NI AIBU. TANZANIA BADO HATUJAFIKA POPOTE NA NDIYO MAANA WALIOSOMA NJE WANA UWEZO MKUBWA ZAIDI WA KAZI. ASANTENI.
ReplyDeleteMadogo eeeh...ni hivi....nyinyi rudini nyumbani. Ni kweli serekali inaufisadi lakini na nyinyi msitupigie makelele hapa.Kuna wenzenu huku hata form one wanakwama kuipata....nyie mmebebwa mpaka huko tena kwa kupata hizo nafasi KIFISADI wote nyie.....kwa kujuana then mnatuletea upuuzi wa kutaka hela ambayo hata mlikuwa hamjafika Russia.
ReplyDeleteTumechoka......mtuache. kuna mambo ya msingi bado yanatuumiza Vichwa sasa na nyinyi tena... RUDINI NYUMBANI KUNA MTU ALIWAFUKUZA HUKU??? Kuna U-DOM inatafuta wanafunzi......Dodomaaaaa.Karibuni Nyumbani.
Poleni sana.Inatia huruma sana hii watawala wetu huwa kuna wakati nahisi akili zao wameshikiliwa.Sio zao.
ReplyDeleteHawa kwa mujibu wao walipelekwa Russia na serikali kwa mkataba fulani mmoja wapo ukiwa huo wa kuwagharamia muda wote wakiwa masomoni,sasa iweje wakubwa pale maghrofani wanasahau kuweka saini vijana waendelee kuchapa buku kama kawa?
Haya mammbo yanayia hasira kweli.Peter nafikiri hao kwenda ubalozini ni sawa kabisa balozi pale Moscow ndio anasimamia mkataba walioweka na serikali ndio mwakilishi wa bodi ya mikopo na kila kitu.Nikiwa na maana kuwa kila kitu kinapita mikononi mwa balozi.
Ninaweza kushauri kitu hapo vijana komaeni tu mpaka kieleweke serikali yetu imezoea kusukumwa sukumwa.Kurudi nyumbani sio suluhisho maana na nyumbani hali ni kama ya Russia kupata mkopo ni kimbembe.
yeap nakubaliana nawe Egidiyo. Ukisoma vizuri comment yangu nimesema iwapo wangekuwa wameenda huko kivyao like some of us then wasingebother na ubalozi, ila the fact that serikali iliwapeleka huko ina maana kuwa serikali ina jukumu la kuwagharamia hivyo wanapaswa waende ubalozi wakadai haki yao like they did.
ReplyDeletehaha, kuna watu humu inaonekana shule yao ndogo basi inawaume kweli wenzao kwenda kusoma nje na wanafurahia wanavyopata shida.
ReplyDeleteWe umeambiwa wamepata kifisadi; ingekuwa watoto wa mafisadi wangeshindwa kujikimu? Watoto wa kifisadi kwanza waende urusi kufanya nini? Sanasana wao wanaunganishiwa nafasi chache za commonwealth zilizobaki kwenda better places than Russia.
Hao wanafunzi angalia track record yao, form 6 wamechana, sio makapuku kama wewe. S'ship pekee zilizobaki zinazopatikana kihaali ya 1 Japan, hii hata Wizara hawahusiki. Ya 2 Cina, Wizara wanasaidiana na ubalozi ila pepa kusimamia na kusahihisha ni wachina wenyewe, 3 Turkey, semanyingine zinakuwa na restriction ya dini, na 4 ni za Poland, Russia, Ukraine.
Katika hizi hakuna ufisadi. Kama we hukuchana kuweza kuapata s'ship hizi umia kivyako, sio uwaombee mabaya wenzi na kutaka nao wakose
wee anon wa saa 02:55AM huenda unadhani elimu yangu haijanisaidia,lakini kwa haraka tu nachokiona kwako ni ama:-
ReplyDelete1.ndugu zako ni miongoni mwa wanaoshiriki kuwanyima watanzania hakizao za msingi,hivyo ukisikia tamko la kuanzisha operation ya kuwachapa unaona balaa halichezi mbali na mlangoni kwenu!lakini kelele zako hazinizuii kutekeleza niliyo kusudia maana njia pekee ya kuleta discipline ya utendaji ni kuwafanya wahusika wajue kuwa sio ombi bali ni wajibu wao kutenda.
2.ama huenda wewe umesha athiriwa kifikra na umekuwa mnyonge sana hadi unadhani kuelimika ni kukaa kama bubu ukisema yes sir! yes sir! ukidhani huo ndio ustaarab kama walivyofanywa babuzetu na wakoloni. nataka nikuhakikishie kuwa ktk nchi zile ambazo raia wanamiliki silaha haki inafuatwa sana maana watendaji wanajua akileta zakezipi kichapo ni hapohapo,na kabla jambazi hajakuvamia anajiuliza je huenda nawewe unachamoto pia! so don't worry kichapo kipo palepale,that is the only way to bring back discipline ya utendaji bora and feeling of sense of duty! kama wewe ni miongoni wee jiandae kula kichapo tu!kisasi kipo hapahapa duniani,ukisubiri baadae utaishiw kuliwa wewe tu,ila sio mimi!
mwisho nakutakia utafute elimu ya kukuondoa ktk utumwa wa mawazo,maana kama ulikwenda darasani elimu yako ulidesahivyo haikusaidii kukuondoa ktk uduni wa maisha yako ila imekulemaza na kukufanya uwe bwege,maana hata bosi wako aki kwambia anakutaka kimapenzi si ajabu ukakubali kuwa gay ilimradi tu ni umfurahishe bosi au profesa wako kama takuwa yeye ni gay nawewe unataka ufaulu.mimi sio kama wewe! you bet me i bet you !haki mbele kama tai
itifaki inazingatiwa.
ReplyDeletenyie mnalalamika nini tena mnalipiwa shule halaf bado mnapiga kelele.si tuko UK tunapiga box na shule tunalipa wenyewe na hamna mtu anayepiga kelele msituuzi wengine.waone kwanza vifisadi wadogo na scholarship simmepata kwa kujuana pumbaf
ReplyDeleteWaswahili husema "SWALA LA NGOSHA MUACHINE NGOSHA MWENYEWE".Nnachotaka kusema ni kwamba swala kama hili linalohusu uanafunzi waachiwe watu wenye upeo na mada hizi.Haipendezi hata kidogo kuona mtu anachangia pumba ambazo hazina faida yoyote.Wengi wa wasioenda shule hawana la mana pindi mada za shule zinapoletwa.Hawana la heri hata moja katika uchangiaji wao.Na wengi wao ni wale wasioenda shule na wanaopiga box na kuona kuwa kupiga kwao box ni muhimu sana kuliko kusoma.Nisieleweke vibaya wapo vilevile wachache wao ambao hawakwenda shule na wanaopiga box na wakawa na mitazamo mizuri juu ya mada mbalimbali,ila wengi wao vichwa maji na hawala la msindi la kuchangia zaidi ya kuleta ushauri usio na manufaa kwa mtu.Kivupi ni kwamba kama mtu unaona huna uwezo wa kuchangia basi nyamaza,acha wenye upeo na mada wachangie.Kuhusu suala hili ni kwamba matatizo kama haya kweli yanawapata wanafunzi wengi wasomao nje ya tanzania.Si kwa udhamini wa serikali yetu bali hata udhamini wa mashirika,makampuni au organization nyenginezo nazo huwa na matatizo kama hayo.Cha msingi ni kutokata tamaa juu ya kudai haki zenu.Mi ni mwanafunzi nisomae nje ila kwa udhamini wa benki fulani,pia tupo katika tafrani kama hizo zinazowakumba nyie wenzetu.Tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kukabiliana na mazingira yanayotunguka.kila la heri katika kutafuta haki zenu.
ReplyDeletewe utake usitake nyie ndo vifisadi wenyewe mnapata scholarship kwa kujuana.watu tumefaulu vilevile form6 na atukupata scholarship mkiambiwa ukweli mnakasirika.msifikiri wote wanaofanya kazi ulaya hawasomi utakuwa unajidanganya mwenyewe,ulaya sio lelemama kazeni msuli tafuteni kazi msijione mnaakili sana minilipata div 1 na nnapiga box vilevile.cha msingi fees imeshalipwa tafuteni kazi ya kukufanya uishi.ahsante
ReplyDeletenakubaliana na anony wa 1:53 hapa juu. Sisemi kwa dharau au makidai, ila sometime kwakweli kuna watu fulani huwa tunawaita waosha vinywa hapa ukumbini huwa kila topiki wanajisikia waseme tu; haijalishi kama ana maana la kuchangia au la. Ila pia kuna wengine wanafanya makusudi kuchokonoa watu na kuchemsha damu; hao huwa tunawadharau tu.
ReplyDeleteLakini kwenyemada fulanifulani, mathlani hii hapa; nafikiri kuna watu wengine vijiba vya roho vinawasumbua. Kuna watu shule hakuna sasa wakisikia fulani kapelekwa nje kusoma anaona kwanini isiwe mimi. hii kasumba inatusumbua sana ndugu zangu na inachangia kutokwenda mbele kwa kweli
I just wanna say something here; I may be going off topic a bit; but this issue has rose a couple of times in previous comments. I know some of you may disagree with me, and that's fine.
ReplyDeleteThere's a popular belief in Tanzania that you can't get anything unless you know someone; have some sort of connection you know. In a lot of ways that is true; and it pains me and hurts me when I see such trends. For a simple example, just read this documentary from Adam Lusekelo about BoT's dream team.
But at the same time, I feel that most working class Tanzanians have just given up or some use the old-boy-network thing as an excuse. Because I have seen a lot of folks back home capable of doing big things who never even give it a try because they think they won't get it since they are "nobody". I for one can vouch for that. I have had people ask me numerous times in regards to both school and work, "how did you get such and such an opportunity" and my reply is always simple and frank. I just tell them, I tried.
Don't get me wrong; the technical-know-who is very much part and parcel of daily doings in Tanzania; but that is no reason to give up. I give a challenge to my fellow nobodies, do not resort to thinking that everyone that got one opportunity or another is a "Fisadi"; some are just common folks like me and you; who worked hard; tried and thank-God they got it. If we cultivate this mentality of "aah hupati skolaship mpaka umjue fulani" we won't go far. There are still a few places out there which look out for the truly qualified
Nimeona website ya chuo mnachosoma kiko bomba. Kutokana na mahesabu yangu mimi ni kuwa mmepewa $292 kwa mwezi, ukitoa rent ya chuma $70 kwa mwezi mnabaki na $222. Hii ina maana wamewakadiria $8 kwa siku. Kama mkate mzima ni $1 ukila $5 ukaweka $3 mbona inatosha. Plus siku zote kwenye elimu lazima na wewe msomaji uchangie. Kuliko kuitegemea serekali kwa kila kitu omba ndugu jamaa na marafiki wakusaidie hata kama ni $30 tu kwa mwezi. Yes maisha magumu lakini maisha magumu kila sehemu. Nawatakia kila la kheri.
ReplyDeleteJuly 2008: Worldwide Cost of Living Survey 2008: Moscow is the world’s most expensive city for expatriates for the third consecutive year, according to the latest Cost of Living Survey from Mercer. Tokyo is in second position climbing two places since last year, whereas London drops one place to rank third. Oslo climbs six places to 4th place and is followed by Seoul in 5th. Asunción in Paraguay is the least expensive city in the ranking for the sixth year running. Dublin remains the world's 16th most expensive city and Europe's 8th most expensive.,,,,,,,,,,,,,,,,wewe uliesema sio kweli soma hiyo,u have 2 know news
ReplyDelete