Mwanamuziki Alikiba anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa washabiki wake wote na washabiki wa bongo flava waliojitokeza kwa wingi huko Washington DC na Minnesota. Baada ya kufanya mavituzzzz heavy wiki iliyopita mjini Minneapolis iliyowafanya watu wakubali kijana ana talent, Alikiba anaahidi kufanya show ya mwaka mjini Houston Texas jumamosi ijayo 09/13.
This is going to be a sold out event hakikisha haikukosi na unafika mapema.....
kwa maelezo zaidi check flier hapo juu ama nenda
alikibausa.com


Jamani Houston Tumefunga, kwani huyu Ally si Muhisilam? Jamani muogopeni mungu, Ramadhan imefaradhishwa kwa wanawake na wanaume wa kiislam kama walio faradhishiwa walio pita kabla yenu.
ReplyDeletemdau wa Houston
Kijana jali Mola wako, pesa zinakuja na kwenda, hivi wewe una washauri?
ReplyDeleteingawa nakubaliana na watowa maoni wawili wa hapo juu lakini napenda kuwakumbusha waislamu wote kuwa kumtii mola sio kwa mwezi wa ramadhani tu, ni kwa miezi 12 ya kila mwaka. Ni wajibu wa waislamu kukumbushana na kukatazana mabaya. Lakini tutaonekana kama tuna nyuso mbili kama miezi yote 11 hawa vijana wanafanya maonyesho na kuimba sehemu mbali bali na hatusemi kitu wala hatuwaonyi, na inafika ramadhani kila mtu anakuwa mhubiri mkuu. Kwa nini hatukatazi haya miezi mengine 11 iliyobaki? Tukumbuke kumcha mola sio kwa mwezi wa ramadhani ni ni kwa maisha, ramadhani ni kuzidisha ibada.
ReplyDeleteEwe kijana wa kiislam,jaribu hata kumheshimu mungu na keheshimu mwezi wa ramadhani.fanya toba kuna leo na kesho...leo uko hai kesho utakuwa kwenye futi sita.Mimi nakukumbusha tu.
ReplyDeletePengine jamaa sio muislam. Kwa vile waislamu wanafunga ndo watu wengine wasijirushe ??? No way.
ReplyDeleteTutakwenda kumchek na tutapata pombezz pia. Sisi sote sio waislamu.
Nyie vipi ?? Dunia sio yenyu pekee.
Unafiki mtupu kwa hiyo miezi 11 ruksa kutenda maovu? nani kakuambia kwenda kwenye show ni dhambi?
ReplyDeletegood points ananymous wa tatu, mimi ningeliongezea tu labda tumuombe kaka michuzi ambae naamini pia ni muislamu asite kuleta matangazo ya aina hii wakati huu wa ramadhani.
ReplyDeletekwani hiyo shoo ni kwa waislamu tu si kaeni home kungoja msosi sie tukajirushe acheni hizo hapa sio uarabuni libeneke kama kawa ALLY usikondeshwe na hao makamuzi kama kawa.
ReplyDeleteNaona ndiyo maana Hurricane inakuja Houston.
ReplyDeleteNyie waislamu nyie mnatubore sasa. Tukisema sana tutaambiwa tunaleta udini huku kwenye blog...
ReplyDeleteNyie mmeacha kazi zenu mwezi huu mtukufu?
Ina maana nyie baada ya mwezi mtukufu ukiisha basi mnaenda huko kwenye hizo clubs na sio dhambi tena? Hivi hamjui kuna nyimbo zina maadili na sio kila mtu anayekwenda kwenye hizo party basi itakuwa kutenda madhambi tu huko...Au nyie mkiendaga huko mnafanya nini la zaidi ambalo hatulijui na mnaona aibu kulifanya mwezi huu mtukufu?
Jesus alisema anayeonakuwa hana dhambi anyanyue jiwe na ampige yule mwanamke...na wote waliokua hapo hamna hata mmoja aliweza kufanya hivyo...Tusiwe wepesi kuwanyooshea wenzetu vidole na pia kumcha Mungu sio kutoka nje ndani bali ni kutokea ndani nje...na kuwaonyesha watu wengine tu ...
Hao waislamu tunaowaona wanatukakanana kwenye ile blog wao hawaujui mwezi mtukufu au na nyie hamuwaoni mkawaonya?
Kama huyo aliyesema hapo juu uislamu sio mwezi mtukufu tu ni the all year around na sio kufunga tu na kufuata maadili yanayompendeza muumba.
Hv nyie mnaolalamika kwani mmelazimishwa kwenda? Kila mtu ana uhuru wa kuamua jambo analotaka kufanya, wewe kama unaona umefunga sio lazima uende. Kuna washabiki wengine kibao ambao tutakwenda kumuona and as they say, "the show must go on," with or without you. So nyie endeleeni kufunga acheni sisi tukajirushe. Nakubaliana na September 09, 2008 3:02 PM tendeni na semeni haya mambo kila siku ya mwaka na sio kutafuta tu mwezi mmoja wa kujifanya mko serious na dini then miezi mingine mambo yale yale inakuwa haileti maana. Mcha Mungu hana mapumziko Jan had Jan unatakiwa uwe unatembea mstari ulionyooka. Tena unakuta miezi mingine wanawake wanavaa nguo zinazowaacha nusu uchi ila ikifika miezi hii basi baibui kubwa tu hii sio sawa.
ReplyDeleteSISI PIA TUNA KWARESMA MBONA HATUFATANIFATANI, MNATUBOA NA HIYO DINI YENU YEYE YUKO KAZINI NYIE MBONA HAMKAI NYUMBANI MWEZI HUU, WAARABU ORGINAL SIO WABONGO WAKUCHOVYWA WANAPIKA PIZZA MWEZI HUU NA WANCHANGANYA NA NGURUWE MPO HAPOOOOOOOOOO NENDA DENMARK BILA MZEE WA MEZA MZUNGU HALI PIZAA!!!MPO HAPO!!
ReplyDeleteDogo anashindwa kuelewa kwamba IKE is on its way, making its landfall on Saturday Morning. Kuweni makini kwenye maamuzi.
ReplyDeletePili mwezi mtukufu, ila sidhani kama watu hawatojaa, maana jamaa huwa anasababisha.
B.
Acheni Udini humu
ReplyDelete