juu mwana fa akiwa na nancy na nakaaya sumary. chini akiwa na masanja mkandamizaji

HABARI ZIMEENEA MJINI KWAMBA MSANII MAARUFU WA BONGO FLEVA HAMISI MWINJUMA a.k.a MWANA FALSAFA AMESHAVUTA.


UKWELI NI KWAMBA JAMAA BADO YUPO YUPO BADO NA NIMEONGEA NAE SASA HIVI NA KASEMA MBONA YUYEYE YUPO KAZINI NBC MAKAO MAKUU NA BADO ANADUNDA?


AMEELEZEA MASIKITIKO YAKE JUU YA UVUMI HUO USIO SAHIHI, NA KUSHANGAZWA NAO SANA WATU WANAOMZUSHIA MAUTI. ANAMSHUKURU MUNGU KWAMBA YEYE BADO YU HAI NA KWA MAJAALIWA ANAENDELEZA LIBENEKE KAMA KAWA.


RAFIKI YAKE YA KARIBU AMBWENE YESAYA a.k.a AY NAYE AMEELEZEZWA KUISHANGAZWA NA UVUMI HUO, AKISEMA AMEKUWA AKIPOKEA SIMU KIBAO TKA KILE PEMBE YA DUNIA NA AMEKUWA WAKIWAELEZA WADAU KWAMBA MWANA FA BADO YUPO YUPO...


HABARI NDIYO HIYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kama wabunifu walivyo fanya kazi ya kutunga sms hiyo iliyosema Mwana FA katutoka alijua kuna wadau hawasomi sms hadi mwisho ndo madhara hayo yaliyojitokeza. Someni sms hadi mwisho. Ndo Mambo ya XTREME na Jiachie SMS hayo. Ni Kama ile ishu Ya Mkuu wa wilaya ya Tegeta siku ile ya wadau wa.....

    ReplyDelete
  2. Mkuu Michuzi,
    "Yupo yupo" tafsiri yake si sawa na "yupo". Ni vyema ukaweka bayana nini hasa unacholenga katika ujumbe. Maana ujumbe wako unazidi kumwagia petroli kwenye moto.
    Mdau

    ReplyDelete
  3. Pia michuzi kwa nini umetumia pen nyekundu kukanusha habari za msiba?Pen nyekundu huwa inatumiwa na waalimu ama kutangaza habari ya kifo.Mkuu gani wa nanilii umeniangusha.

    ReplyDelete
  4. mara nyingi lisemwalo kama halipo laja, inakuwaje watu wakuzushie kuwa umevuta kama hakuna sababu, tuambie ukweli kwani ukificha maradhi ujue kifo kitakuumbua, au wanamaanisha umekufa kimziki?si unakumbuka watu walesema kuwa kasheba kachoka na kwamba treni iko njia moja kitu ambacho hata yeye mwemyewe alibisha na kutunga mwimbo wa yellow card lakini ukweli ulionekana.Michuzi kadai upo upo inamaanisha umechoka ila iziraeli bado hajafika maeneo

    Mbega

    ReplyDelete
  5. Mdau namba 2 hapo juu,

    Mambo ya jikoni haya weye wa kibarazani (aka mbeba box) utayajulia wapi bwana.

    By the way hivi sasa hapa Bongo MwanaFA anatamba na singo yako ya "Bado nipo nipo" kwa hiyo that phrase has become his trade mark.

    Korasi inakwenda hivi ...

    MwanaFA utaoa lini?
    Bado nipo nipo bwana
    Unasema..??!
    Bado nipo nipo
    MwanaFA utaoa lini?
    Bado nipo nipo bwana.... Kwani wa kwanza kuwa mimi?!

    ReplyDelete
  6. Picha ya juu kulia(kulia kwa anayeangalia picha!),kama mshiriki mmoja wa BBA3?(Jina linahifadhiwa)Au nimeanza kuharibika macho?

    ReplyDelete
  7. salaam bwana michuzi i just want to put a comment on this picture but not only this picture but to all male bongo flavour artists..ma problem is why their can't their wear casual dresses instead of t-shirt and jeans at night!!!this is so lam..

    ReplyDelete
  8. ANONY 6;25pm mbona mi sielewi?

    ReplyDelete
  9. ANONY 6;25pm kwanini na wewe usiandike kiswahili katika hii blog ya watanzania?

    ReplyDelete
  10. Halaf anonym. wa 6.25 ana kingeredha kigumu!!!

    ReplyDelete
  11. Mimi nathani anaumwa ebu mwangalie kwenye picha hiyo ya juu hiyo ndo sura yake ya kawaida? kama siyo ni mgonjwa, pia angali physique yake amekonda si yule nimfahamuyo mimi, lazima kuna jambo ndo maana watu wakazuwa. Kuna tofauti ya THEY na THEIR, watanzania wengi wanachanganya maneno haya:-

    THEY = WAO, NI ZAIDI YA MTU MMOJA
    KWA MFANO: WANAKWENDA =
    THEY ARE GOING NA SI THEIR
    ARE GOING

    THEIR = HII NI POSSESION =
    KUMILIKI KWA WATU
    WENGI KWA MFANO NGUO ZAO
    NI ZA ZAMANI = THEIR
    CLOTHES ARE TOO OLD LUGHA YOYOTE ILE MTU UKITAKA KUWA MAHILI UNATAKIWA KUIFANYIA MAZOEZI HII IKIWA NA KUSOMA MAANDISHI MBAMBALI YA LUGHA HUSIKA MARA KWA MARA NA UNASOMA BETWEEN THE LINES, UNAPOSOMA UWE UNAJIULIZA KWA NINI MWANDISHI KATUMIA NENO HILI NA KALIANDIKA KWA MPANGO HUU. KUSOMA VITABU NI MUHIMU SANA.

    ReplyDelete
  12. Ano. 11:08 PM Sio Mahili ni (Mahiri) where u from bagamoyo kilwa au Kisiju?

    ReplyDelete
  13. Kazi kweli kweli!!
    Maana sasa naona mada ina enda kwengineee, kwenye kukosoana kuhusu lugha.
    mmh mi nampa hongera mwana FA kwa kazi zake nzuri, sasa sijui ntakosolewa nini

    DADA LAO
    lol

    ReplyDelete
  14. watanzania bwana wanamatatizo sana ndio maana hatuendelei yaani nyie ukiona mtu kakonda tuu basiii mgonjwa jamani maisha kuna kupanda na kushuka ati siyo kila siku ijumaa bwana. nyie mtabaki ooh mgonjwa eeeh karibu atakufaa je nyie wazimaaaaaa je mmepima kuona uzima wenu acheni mambo yenu bwana, uzushi tuu.
    mwanaFA piga mzigo kaka wanaozusha ahawana kazi na wala hakuna mtu aliyefanya vizuri akasifiwa. mwama songi nalikubali tena BADO UPO UPO KWANZA ... BY flojoma

    ReplyDelete
  15. Mimi na mabinti damu damu

    ReplyDelete
  16. huku walizusha dolly patron kesha ukata...akatoka kuwashangaa watu akiwa kapendeza kweli na alishangaa hizo hadthi zimetoka wapi?

    ila bongo wasikuone umekonda basi wnakununulia ticket

    ReplyDelete
  17. Sio MAHIRI ni MAHILI, usimkosoe bure, MAHIRI wewe ni Msukuma nini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...