Kaka Michuzi,
Pole na kazi. Naomba niwekee ujumbe wangu kwenye website yako. Nina uchungu sana na wizi unaokithiri wa wafanyakazi wa posta za nyumbani Tanzania.Wiki mbili zilizopita nimemtumia mama yangu frame za miwani kwa kukutumia registered mail.
Wafanyakazi wa posta wamefungua bahasha na kuchukua miwani halafu wakaweka peni na kufunga bahasha. Bahati mbaya nilisahau kuandika juu kwenye bahasha kuwa kuna miwani ndani, labda ingesaidia.
Uaminifu hakuna kabisa kwa wafanyakazi wa Posta nyumbani! Yaani mama amepokea bahasha ikiwa na peni kwenye kiboksi cha miwani! nimeumia sana moyo kwani niligharamika nikiwa kama mwanafunzi kumridhisha mzazi wangu halafu mtu anaiba mzigo usio wake.
Hii ni tabia mbaya sana.Jamani wafanyakazi wa posta acheni wizi.Mmeniumiza sana roho kwa mlichonitendea. Mdau,
Helsinki, Finland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Na mimi naunga mkono huyo mwenzangu. Mwezi mmoja uliyopita nilituma zawadi za mtoto kama kawaida mtu akijifungua unampa hongera na zawadi za mtoto.Lakini mpaka sasa bado havijafika au vimefika mtu kachukua. Kweli sio ustaarabu na sio ubinadamu. Lakini kuna msemo usemao za mwizi ni Arobaini! Na mali ya wizi haijengi bali ..... Hata mimi nilidhani wizi umekwisha posta kumbe bado? Kweli inauma na inasikitisha sana sana. Je wahusika wakuu au management ya Posta mko wapi na kwa nini mnaruhusu hali hii iendelee kutuaibisha na kutokuwa na Imani na WaTanzania?
    Mdau UK

    ReplyDelete
  2. aibu aibu aibu tupu. Mimi nilimtumia ndungu yangu kitabu cha nyimbo za dini. Ndugu yangu kanitumia ujumbe kuwa hakupata. Sasa jamani hata kitabu cha dini mtu anaiba hivi kweli hii inakaaje. Yaani sasa hivi afadhali kuwaagizia watu wanaoenda nyumbani wakupelekee kuliko kutuma kwa kutumia posta, kwani havita fika.

    Najua maisha nimagumu kwa kila mtu lakini du, watu watumavyo vitu sio matajiri, bali wanataka kuwasaidia ndugu na jamaa ambao wamewaacha nyumbani.

    aibu nyingine ni kwamba nikatuma pesa kwa njia ya western union. Hela ilifika lakini tatizo ndugu yangu alipofika kuchukua pesa, aliambiwa asubiri yaani kama masaa kadhaa kabla hela hajapewa na vile kwa kusumbuliwa.
    Hivi hii imekaaje jamani? aibu aibu tupu.
    Mdau Lon, UK

    ReplyDelete
  3. Pole Mdau mimi pia nilituma parcel ilikuwa registered na kuona muda unakwenda nilituma email kwa customer service kuhuliza kulikoni
    siku hiyo hiyo wakanijibu kuwa mzigo umefika tangu tarehe hiyo....
    kwa hiyo nawaombeni kama mizigo yenu mlituma kwa registered wasiliana na email hii customer.care@posta.co.tz wapeni namba ya parcel mngoje watasema nini maana huyo mtu ambae amepokea hiyo parcel lazima aende na kitambulisho kwahiyo mwizi atajulikana tu

    ReplyDelete
  4. Hii inaonesha watanzania MAFISADI TANZANIA NI WENGI. Tofauti ni kiwango au labda wengi wao hawajapata upenyo wa kuchota kwa nguvu. INASIKITISHA.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  5. I DONT AGREE WITH YOU SIR!

    MIMI SIUNGI MKONO KABISA HII KAULI YAKO SI KWELI KABISA WAFANYA KAZI WA POSTA NI WADOKOZI MIMI NAHISI WEWE ULIWEKA PEN NA UKADANGANYA KWAMBA UMETUMA FRAME ZA MIWANI SASA MAMA ALIVYO POKEA PEN NA SI FRAME ZA MIWANI KAMA ULIVYO MWAHIDI UKAJA NA MBINU YA DARASA LA KWANZA ETI WAMEKUIBIA HAPO POSTA. KWELI KABISA NEXT TIME ANDIKA ULICHOTUMA KWANI HII MBINU HAITAWEZEKANA TENA MAANA UKIANDIKA WATAFUNGUA HUKO HUKO WATAONA UNACHOTAKA KUTUMA KUMBE JANJA YAKO YA NYANI KULA INDI BICHI ITAJULIKANA. HAYA BASI NA MIMI NILIMTUMIA MCHUMBA WANGU HUKO FINLAND PETE YA ALIMASI ALIPOFUNGUA MCHUMBA WANGU AKAKUTA NI KIPANDE CHA CHUPA TU WAMEWEKA NASIKITIKA KWA SABABU KAMA NINGEANDIKA KWENYE BAHASHA NIMETUMA ALIMASI LABDA WASINGECHUKUA.BABU NEXT TIME REMEMBER TO INSURE YOUR STUFF BEFORE YOU SEND ANY MZIGO THAT MEANS YOU WILL BE REFUNDED. WHAT IN THE WORLD ARE YOU DOING THERE IN FINLAND YOU CAN`T EVEN THINK LIKE EDUCATED PERSON.WAFANYAKAZI WA POSTA NI WAADILIFU NA WACHAPAKAZI WE ARE ALL PROUD OF THEIR SERVICES AND COMITMENT TO SERVE FOR TANZANIAN PEOPLE. NI MIMI YULE YULE MSEMA KWELI NA MTOTO ALIYEKUWA NA AKILI NYINGI CHUO KIKUU CHA MUZUMBE UNIVERSITY MUROGOGORO NA PIA KULE SANTA ANTONY MBAGALA PETER WA NALITOLELA!

    ReplyDelete
  6. Kitu ambacho hawawezi kuiba ni vitabu tu. Wanaogopa sana kusoma.

    ReplyDelete
  7. MIE BINAFSI NILITUMA BOX MWAKA JANA, LILIKOPOTELEA HATA SIJUI, HADI LEO HALIJAFIKA. SASA SUBIRINI BOX NITAKALOTUMA NEXT TIME LIFUNGUENI LAKINI MSINILAUMU. YAANI SIKU HIZI NIMEACHA HATA KUTUMA KADI ZA BIRTHDAY AU XMASS. WATANZANIA MLIOKO ABROAD NAWASHAURI MKITUMA VITU POSTA WEKENI INSURANCE, KIKIPOTEA HIYO INVESTIGATION INAYOFANYWA SIYO MCHEZO MAANA INABIDI WANA-TRACK MZIGO NA UKIONEKANA ULIFIKA HADI POSTA FULANI BASI POSTA HAINA JINSI BALI KUKULIPA, FOR THAT CASE HAKUNA ATAKAYEFUNGUA.

    ReplyDelete
  8. yaani mie wafanyakazi wa posta wamenikaa kooni kama niwatukane, but najua Michu ataibania comment yangu. eti bongo tambarare, tambarare my a****mmmyuuuuu (msonyo)

    ReplyDelete
  9. acheni malalamiko mengi yasiyokua na maana..TUMIENI DHL!

    ReplyDelete
  10. ILA SIO SIRI MI MWENYEWE NILIWAHI KUTUMA KADI,ALIYEIPOKEA ALIKUTA IMEFUNGULIWA,AFU JUU IMEFUNGWA NA SOLO TEP..WALIDHANI LABDA NIMEWEKA HELA KATIKATI..DAH!..DHIKI HIZI

    ReplyDelete
  11. Nyie wote hapo juu hamna hela. Tumieni FedEx au DHL, unapewa na track number.

    Kwa posta wafungu camera nyingi za kuwachunguza wafanyakazi.

    Mama yangu aliwahi kutumiwa dhahabu toka uarabuni miaka ya sabini mwishoni posta waliiba. Alitumiwa na mwanafunzi wake aliyemfundisha. Mama mpaka leo hasahau.SHAME

    ReplyDelete
  12. Wizara inayohusika fanyeni haraka muibinafsishe Posta kwani hiyo ni moja ya kero ambazo wakubwa wa kampuni hiyo hawazioni, sasa ikiuzwa hao wamiliki wapya hawatapenda wakimbiwe na wateja kwa vitabia vya wizi wizi namna hiyo...yaani huo ni upuuzi... mtu anaiba vichupi vya katoto kachanga!! au anaiba miwani pea moja tena ya kizee!!! Ni aibu kubwa.

    ReplyDelete
  13. HUU NI UJINGA MTUPU, NINYI WABEBA MABOKSI MMEKAA MNALAUMU POSTA, HOW DO YOU KNOW SIO WABEBA MABOX NDIO WAMEFUNGUA NA KUCHUKUA MIZIGO YENU? UNLESS MSEME KUWA NI NYINYI WENYEWE MNAFANYA KAZI KWENYE MASHIRIKA YA HUKO YA POSTA NA MNA HAKIKA MIZIGO YENU IMEONDOKA SALAMA SALMINI, SIO KUKAA TU MNASEMA OVYO WAKATI WE ARE ALL HUMAN BEINGS.. HAO WAFANYAO KAZI POSTA ZA HUKO HOW FAR ARE YOU SURE WAMETOSHA MAISHA YAO... THINK FIRST PEOPLE, KAMA NINYI NDIO WAIZI MSIFIKIRI WOTE.. STUPID

    ReplyDelete
  14. Acheni kuwatetea watu wa posta kwa kifupi ni wezi wakubwa. Kisa cha kufungua mizigo ya watu mnatafuta nini? Na nyie mnaosema DHL ina maana hata vichupi vya mtoto tutumie DHL? Sie tunabangaiza huku hatuna mipesa tuliyoiba benki. Maana yake nini kutoamini wahudumuwenu? Ina maana basi ukienda Hsipitali nako usiwaamini wauguzi maana badala ya PPF wataweka maji? Jamani lazima tuaminiane. Ulipoomba kazi post hukuandika kwenye CV (Bingwa wa kuiba) So tafadhali acheni udokozi wa mizigo ya watu.

    ReplyDelete
  15. nyie mnaosema watu wa huku ndio wanaiba hamjui mnachosema. Waibe miwani???????? Watu wa post huku ni federal employees na wanalipwa kishenzi na kzi wanaijua

    Sasa mbona tukitumiwa huku vitu vinafika bila hata kuguswa lakini ni huko tu havifiki?

    Inakatisha tamaa sana na kama aliyesema hapo juu sio kuwa siye ni matajiri. Tunajitahidi kuwatumia ndugu zetu japo kidogo tulichonacho basi nao wanachukua

    SHAME ON POST OFFICE WORKERS

    ReplyDelete
  16. Hakika hii inasikitisha sana ingawa si wafanyakazi wote wa Posta wenye hulka hiyo.

    ReplyDelete
  17. Yani hii kitu imenikuna sana, kweli kabisa POSTA TZ ni wezi wakubwa, wakiona bahasha imetuna tu kosa, we fikiria mpaka kadi wakiona kubwa lazima ipigwe wembe wakague ndani, wasione bahasha nzito kwao ni kosa lazima ichanwe, mimi nilitumiwaga kadi ya bday kubwa ndani kukawa na chocolate wakachukuwa then wakachukuwa bahasha zao flan wakadumbukiza huko ile bahasha yangu ya kadi juu wakaandika hivi" MZIGO WAKO UMEFIKA UKIWA WAZI" kwa hiyo ili mzigo wako usiendelee kuharibika tumeweka hiyo bahasha, yani niliumia sana, ukiangalia wale wahudumuwenyewe ni njaa tupu, na wizi mtupu!!!

    ReplyDelete
  18. Inauma sana na kusikitisha sana. Wizara husika iko wapi na kwanini imelala? Wenzetu huku wanathamini Posta sisi .... Nani atakuwa mwokozi wa wanyonge? Bila kujenga imani ya posta sidhani kama kunauwezekano. Rudisheni Imani na Uaminifu ktk Posta. Kudokoa hakutokufikisha popote!!!

    ReplyDelete
  19. Huyo Peter Nalitolela ni mfanyakazi wa Posta kwahiyo lazima atete uozo. POSTA Tanzania imeoza nani assiyejua ukweli huo! Halafu mnataka mpandishiwe mishahara wakati hamtoi huduma bora? SHIRIKA likiuzwa kwa wawekezaji mnaanza kulalama eti serikali haiwajali. sasa nani asiyejali nani? Jali ajira yako na tuone serikali itaanzia wapi kubinafsisha shirika lenu. LAKINI ninachojua mwisho wao umefika. Mtazunguka mtaani bila kazi XXXXXXXXXXXXX nyie. Na mwizi hufa akiwa maskini wa moyo, akili, mwili na mali.

    ReplyDelete
  20. Wizi wa posta Tanzania umetukuka..

    Mwaka jana nilimtumia binamu yangu zawadi ya Birthday, ilikuwa ipod. Kitu kilichofanyika Posta Dar ni kwamba walimpa receipt kwenda kulipia ushuru, wakati wanakagua wakakuta ni box tupu, Acha Aibu iwatoke...
    Bahati nzuri nilikuwa nimelipia Bima, na ilibidi hao hao posta Dar wailipie.. I pod ya £100 ikawagharimu £780. Ndivyo wapendavyo kuyatia hasara makapuni wayafanyiayo kazi bila kujua kwamba Ufisadi ni kurudisha nyumba Tija na maendeleo ya wafanyazi

    ReplyDelete
  21. mimi sikubaliani na hao wanaolalamika kuwa wafanyakazi wa posta kuwa ni wezi jibu ni hapana siyo kweli kwamba wote ni wezi ila kuna wenye tabia kama hiyo maana katika wengi wazuri wabaya pia hawakosekani,mimi binafsi nilishamtumia mke weangu simu mbili kwa njia hiyohiyo ya register toka hapohapo finland ni kweli sikuwa na imani kama kweli zitafikia nilikuwa kama nacheza kamali vilie lakini nashukuru mungu zilifika salama na haraka pia toka siku hiyo nimekuwa natuma vitu mbalimbali kwa njia hiyo maana nimegundua ni njia salama ,kwa hiyo kusema wafanyakazi wote wa posta ni wezi si kweli jibu ni kwamba kuna baadhi tu ambao siyo waaminifu

    ReplyDelete
  22. Tatizo la state services hizo. Mimi nilishasahau mambo ya posta kabisa. Kwenda posta...kudadadeki!
    Hili ni tatizo la kupewa maendeleo kabla ya kufikia wakati wake. Fikra bado zipo nyuma sana...kazi kuwaza kuiba na kumwaribia mwenzako. Sijui watu wataelimika lini bongo kufanya kazi kwa haki na professionalism.
    Wewe fanya kazi yako...ukimaliza ondoka. Sasa wataka kushiba mara mbili kazini...pumbafu!
    Hao wanaotetea Posta na kusema watu watumie DHL ni wajinga...narudia tena WAJINGA

    mtoto

    ReplyDelete
  23. Huyo mdau hapo juu aliyejiita Peter Nalitolela sio kweli,mimi namfahamu Peter siku nyingi sana hawezi kuandika huo uppuzi ulioandika..kwahiyo koma kumchafulia jina kijana wa watu..thanks..

    ReplyDelete
  24. Hiyo miwani kama ni miwani ya macho sasa sijui huyo mwizi ataivaaje, kwa sababu macho hupimwa na kukadiliwa ni miwani gani ivaliwe. Mijizi mingine kweli haina akili.

    ReplyDelete
  25. WATU WANAOPINGANA NA MALALAMIKO HAYA AIDHA WAKO NYUMBANI AU HAWAJAWAHI KUISHI NJE NCHI NA KUTUMA KITU.

    MIMI NIKO NJE YA NCHI MIAKA KARIBU KUMI SASA, HUKU KWA WENZETU MFANYAKAZI AKIPOTEZA HATA KADI YA SALAM ZA MWAKA MPYA AMBAYO INA UJUMBE TU, HAINA HATA SENTI NDANI YAKE, NA ABAKAINIKA KUWA NI YEYE ALIYEPOTEZA - KWANZA KIBARUA KINAOTA NYASI HAPO-HAPO NA ANAKABIDHIWA KWA POLISI MOJA KWA MOJA.

    TUMA CHO CHOTE KILE, BARUA, KADI WAKE HATA PESA NDANI YAKE, HATA KAMA SIYO REGISTERED, ZITAFIKA. HIVI JAMANI TUNAWEZA KUFIKIA KIWANGO HIKI?

    NADHANI UKWELI HUU UNATHIBITISHWA NA TAKWIMU ZA PARCELS ZINAZOKUWA ZIKITUMWA MWAKA HADI MWAKA KUPITIA POSTA ZETU HUKO NYUMBANI.

    WATANZANIA WENGI WAISHIO NJE WALISHA-KATA TAMAA YA KUTUMA VITU.
    BORA UTAFUTE MTU ANAYEKUJA NYUMBANI UMKABIDHI. JAPO HUWEZI KUKABIDHI VITU VINGI KWA SABABU YA RESTRICTION ZA UZITO WA MIZIGO.

    BINAFSI NAAMINI KUWA HUJUMA HIZI AU UFISADI HUU UNAFANYWA NA WATU WACHACHE TU. LAKINI KAMA MIMI NI KIONGOZI WA POSTA HUSIKA, AU KIONGOZI WA POSTA NZIMA NA KUNA MALALAMIKO YA MARA KWA MARA YA AINA HII, NI KWELI NITASHINDWA KUJUA IDARA HUSIKA NA KUFANYA UCHUNGUZI KUJUA NANI MWIZI?!!

    IMEFIKA HATUA HATA KWENYE BAADHI YA POSTA ZA NJE UKIWAAMBIA UNATUMA KITU/ MZIGO TANZANIA WANAJUA KWAMBA UWEZEKANO WA KUFIKA HUKO UENDAKO NI MDOGO.

    MIMI NADHANI HAPA PANATAKIWA DHANA YA UWAJIBIKAJI. BADALA YA KUHANGAIKA NA WATU WA NGAZI ZA CHINI HUKO POSTA, KWA NINI KIONGOZI MKUU ASITAKIWE KUWAJIBIKA. AKIONDOKA HUYU... ATAKAYEKUJA ATAJUA ANATAKIWA AFANYE NINI.

    UAMINIFU KATIKA POSTA ZETU NI SUALA LA KUTUPIWA MACHO. NI AIBU.

    MDAU
    UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  26. Dawa yao kuwatumia boksi la mavi hao

    ReplyDelete
  27. Sijui hata mnalalamika nini mlio nje, kinachowafanya mdhanie mizigo inaibwa Tz ni nini? kwani kama posta za hapa wanaiba mzigo uliotoka nje, kwa nini wasiibe mzigo unaotumwa nje? tofauti ni nini hapo? mizigo inayokuja toka nje inapita nchi nyingi mpaka ifike Tz, inaweza kupita pia katika nchi nyingine za Africa kutegemea na ndege iliyopakiwa. huko kote possibility ni kubwa tu mzigo kuibiwa, si lazima uibwe hapa. Na nyie watumaji pia acheni ubahili, mkituma mzigo lipieni pesa za kutosha mzigo uje kwa ndege, hai cost pesa nyingi kiasi hicho, ukitumwa kwa posta mzigo utakuja na meli maana obvious gharama uliyotumia ni ndogo. I am speaking through experience. nimeshatuma mizigo nikiwa NL, kwa meli itachukua miezi kufika bongo,japo sijawahi kuibiwa mzigo kwa njia hii, na nimeshatuma kwa ndege pia, gharama huzidi kidogo tu, mzigo unachukua less than 5 days, na ukifika mhusika anapigiwa simu anakwenda airport kuchukua mzigo wake ulio salama. Naomba mtumie njia hizi zilizokwenda shule. Huyo alotuma vichupi vya mtoto sijui katuma vya nini wakati Tz kuna kila kitu siku hizi, ni bora angetuma hizo pesa chupi zikanunuliwa huku maana cheap is always expensive.

    ReplyDelete
  28. Kwanza tatizo sio Fedex wala DHL, kuna watanzania wanakaa vijijini we acha tu na wanamshukuru nyerere kwani aliweza kuwawekea Posta hadi vijijini kama sio hivyo poasta yenyewe iko wilayani, we unasema DHL wanakujua kijijini huko?
    Pili kwa mnaowatetea Posta hata hapahapa bongo ukituma mzigo kwenda mkoa mwingine tabu tupu ndo maana ukiangalia siku hizi watu wengi bongo hutumia mabasi ya abiria kusafirisha mizigo yao, kwani unafikiri kisa ni nini? Ni baada ya kuchoka na wizi wa Posta.
    JAMANI POSTA BADILIKENIIIIIIIIII!!!!! AAAAAAAAAAAGGHHHH!!!

    ReplyDelete
  29. hahahahaaaaa,sina mbavu aisee
    njaa mbaya wadau

    ReplyDelete
  30. Posta inabidi ibinafsishwe Perod!!!!!!!!!!!.
    Ni wezi balaa,nilituma chupi za watoto tu wakaiba,yaani njaa yao sijui nisemeje.
    Mdau U.S.A.

    ReplyDelete
  31. ndugu wa helsinki au kuoopio, haya mambo ya posta yanaumiza watu wengi. sasa imagine miwani mtu anaiba, hajui size au ubovu wake wa macho ukoje ili mradi bahasha ilikuwa kubwa yeye kaiba. na nimfanyakazi, sasa maendeleo lini? in short it's not only glasses even stamps. mtu unaweka kwenye barua stamps za Tsh2000/= ukitoka mfanyakazi anabandua na kuuzia mtu mwingie! it's very embassing! hata wakati mwingine hazifiki kwa sababu tu ya mpuuzi mmoja. Ebu meneja wa posta fuatilia suala hilo ni aibu kwa taifa letu.

    ReplyDelete
  32. ndugu wa helsinki au kuoopio, haya mambo ya posta yanaumiza watu wengi. sasa imagine miwani mtu anaiba, hajui size au ubovu wake wa macho ukoje ili mradi bahasha ilikuwa kubwa yeye kaiba. na nimfanyakazi, sasa maendeleo lini? in short it's not only glasses even stamps. mtu unaweka kwenye barua stamps za Tsh2000/= ukitoka mfanyakazi anabandua na kuuzia mtu mwingie! it's very embassing! hata wakati mwingine hazifiki kwa sababu tu ya mpuuzi mmoja. Ebu meneja wa posta fuatilia suala hilo ni aibu kwa taifa letu.

    ReplyDelete
  33. posta wizi umekubuu. mi post kad tatu zimeibiwa. juzi nimemtumia boyfriend wangu kad ya birthday na picha zangu shaaaa tokea mwanzoni mwa october mpaka leo hazijafika, na posta niliahidiwa wiki moja itakuwa imefika. honey umeona malalamiko ya wenzangu?? bongo uaminifu noooooooo.

    daw wangu maskini ngoja nikupe happybirthday to u yako leo.

    4 ever and 4 always. Shukuru

    ReplyDelete
  34. Nyie wote mnaosema hawa ndugu zetu walioko nje watumie DHL na FED EX, hivi wote wakitumia hayo makampuni hawa watu wa posta watakuwa na kazi kweli? Ina maana wengi wao watapunguzwa kazi, hivi sasa utumaji wa barua toka nje umepungua sana kwani watu wanatuma emails. Hebu fikirie mnapochangia.
    Mie nikiwa Dar niliwahi tuma kifurushi kipelekwe Urambo Tabora, cha ajabu kifurushi kilifika kimefunguliwa na ndani wamechukua torch na na radio ya mkononi niliyomtumia babu toka Dar. Posta wanaiba sio mizigo toka nje peka yake hata ya humu humu ndani.

    ReplyDelete
  35. Michuzi heshima yako,Hii huwa inanikera na kuniumiza kichwa kwa wale wasiojua matumizi ya herufi kubwa na ndogo.Mnaotuma maoni tafadhalini tumieni herufi ndogo,unapotumia kubwa unamaanisha unasema kwa ukali na sauti ya juu(shouting).Tumia sarufi inavyopasa.Hivi humu ndani hamna wataalamu wa lugha?
    Michuzi usibanie tafadhali iwe somo kwa wengi.

    ReplyDelete
  36. afadhali wameiba miwani labda watavaa. Picha zikiwa kwenye bahasha ya brown hazifiki. Sijui wanafikiri ni hela.

    Kumbuka watu tunaishi nchi tofauti na destination ni bongo. kama hawa walalamikaji wangekua wanatoka nchi moja kweli ningeelewa.

    Sijui mishahara ni midogo au wao ni mafisadi wadogo tu tamaa imewajaa

    Halafu kama kitu kikijaliwa kufika {Kuna wakati nilikosea nikaandika thamani ya vitu nilivyotuma lakini nilikua nimeinsure ili vikiibiwa nilipwe hela yangu}

    Bwana wangu custom duty wakaambiwa ni shs laki moja lakini cha kushangaza ni kuwa mara wakiambiwa watoe shs 50,000 halafu wakapewa receipt ya shs 25,000. Yaani ni uizi au rushwa ya kimachomacho

    ReplyDelete
  37. POSTA NI WEZI BWANA SI EMS SI NINI!! Mimi nimetuma documents za shule kwa EMS narudia tena EMS yenye tracking # mara mbili zote hazikufika mwaka jana. Uki-track parcel imefika hadi Dar, lakini EMS wanasema hawajapata. Na posta ya huku haiwezi kuingilia mambo within Tz.process ni ndefu sana kufuatilia. Hivyo nyie wajinga mnaotetea badala ya kusaidia kutatua uozo fungeni mabakuli yenu mfanye ya maendeleo.

    Na wanaosema ati DHL, FEDEX,etc. hivi mnajua bei zao zilivyo kubwa? Sasa kama posta yetu ingekuwa safe, kwa nini hiyo hela ya DHL nisiweke ndani ya parcel ndugu yangu aongeze siku za kuishi japo? Hivyo ndivyo wenzetu walioendelea wanavyo-save na kutajirika. Ukitaka kufanya mambo ili kuonyesha una hela na wa maana wakati huna hata hiyo ya kuweka ndani ya parcel huna maana hata nusu. TUMIA HILO BICHWA LAKO SIYO DOMO.

    ReplyDelete
  38. Hivi Michu huwa unawatumia wahusika jumla ya malalamiko ya watanzania? hawataki kukubali na kuanza kubadilika. Hakuna ubishi ya kwamba kuna malalamiko mengi ya kupotea kwa vifurushi vinavyotumwa toka nje kwenda Tz. Haijalishi kama mwizi ni mmoja au wote, ni jukumu la shirika. Sisi hatumjui huyo mwizi ndani ya Posta, kwa hivyo Posta kwetu ni uozo tu. Nilituma mzigo wa ngu mwaka juzi mpaka leo hakuna kitu, halafu ukifuatilia hiyo customer service utachoka. Eti wanadai wanakusaidia.... Badilikeni kama Royal Mail ilivyowatimua wasiokuwa waaminifu (wakiwemo watanzania wengi) hasa kwenye ku-sort parcels. Mbadilike, YES YOU CAN sio kilema hicho!

    ReplyDelete
  39. Nakubaliana na anonymous wa November 25, 2008 3:49 PM,

    Nilipokuwa naishi USA mizigo yote kwa posta ilifika, ila nilipokuwa naishi Uholanzi.... Duuh, ni mara chache sana mizigo inafika. Kwa hiyo sidhani kama ni wafanyakazi wa posta TZ pekee yao, lazima kunasehemu hivi vitu hupitia na kupotea kwani haijalishi kama umetuma kwa priority mail au lah.... Mizigo hupotea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...