Home
Unlabelled
adha ya ukosefu wa mahali pa kupumzikia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
HAKUNA UBAYA WOWOTE ULE KWENDA KUPUMZIKA UFUKWENI KWANI KWANI PANA HEWA FRESHI. CHAMAANA NI KWAMBA WAMILIKI WA MAENEO KAMA HILO WANATAKIWA WASIMAMIE VIZURI USAFI WA MAZINGIRA. HUO NDIO UTAJIRI WETU WA ASILI TULIONAO INJOIIIII.
ReplyDeleteKWANI MWANAINJI WA KAWAIDA AENDE WAPI? HIVI HAPO COCOO BICHI PANAKUWA HIVYO KILA SIKU? HIO INAMAANA MWANANCHI AMECHOKA KUKAA NYUMBANI KWAKE NA ANATAKA AKABARIZI NA UPEPO MWANANA WA KUTOKEA BAHARINI! FIKIRIA WAKAAZI WA MORO, IDODOMIYA NA KWINGINEKO SI WANATAMANI WANGEPATA HIO BAHARI WAKAPATA KAUPEPO. SIJAELEWA UNAMAANA GANI ULIPOSEMA HIVYO. KUMBUKA PIA KUMBI ZA STAREHE NA VILE VI_PUB VILIVYOMEA KILA KONA YA MITAA YETU VILIKUWA VIMEFULIKA WATU WANAJIVINJARI.
ReplyDeleteni pakujiuliza kodi wanazokatwa wafanyakazi huwa zinanda wapi na zinatumika vipi,na watoto umuhim gani hasa kwenye holiday kama hizi
ReplyDeleteMichuzi Michuzi,
ReplyDeleteSehemu zakuishi zenyewe ni shida ukilinganisha kwamba nyumba moja ina familia zipatazo kama sita [wapangaji]
Wewe unaongelea mambo ya sehemu zakupumzika?
Kama unaliona ni la muhimu basi serikali ijenge mji mkubwa wenye facility zote.
Kwa wakati huu acha wabanane hapohapo.
Pamoja na kwamba pana hewa freshz!!
ReplyDeletebado mazingira haya yanabidi kutunzwa vizuri na kuboreshwa. nimekuwa nikipita mitaa hii kwa miaka mingi na kweli recreation place kwa sisi walala hoi ni kasheshez pamoja na sisi walala hoi kuwa na mchango mkubwaz, hali ya coco inazidi kudorora pamoja na ahadi nyingi za madiwani!
Fukwe kama za bahari beach na kunduch beach ziwe free pia, maana mahoteli makubwa huwa wanajifanya wanamiliki fukwe hizo. Wanaweka vibanda na vitanda ufukweni na kuweka askari kuzuia 'non residents' wa hoeli hizo kubarizi pale. Vile vile, kuwe na utaratibu wa usafiri wa uhakika wa kwenda na kurudi fukwe za mbali, pamoja na kuzikarabati/kuziwekea fukwe hizo kama kigamboni nk miundombinu ya kuvutia watu.
ReplyDeletepojo
KWANZA FUKWE ZA DAR ZIBORESHWE, ZIWE NA MANDHARI MAZURI,MITI NA MAUA YALIYOPANDWA KWA MPANGILIO NA BENCHI ZA KUDUMU,AMINI KUNA FUKWE NZURI TANZANIA,UBUNIFU TU,
ReplyDeletePILI, ENEO LA JANGWANI, KUANZIA SUKITA KULE HADI MAKUTANO NA SURRENDER BURIJI, LIBINAFSISHWE KWA AJIRI YA KUTENGENEZA BUSTANI ZA JIJI NA SEHEMU ZA MAPUMZIKO. UKIJA ULAYA UTAONA WALIVYOBADILI MAENEO YAO MABAYA KUWA MAPUMZIKO NA BUSTZNI NZURI.
LABDA KIKWETE KASIKIKA???????
MBONA DAR KUNA BEACHES NYINGI KWANI NI LAZIMA KILA MTU ARUNDIKANE COCO BEACH?
ReplyDeletewewe uloweka comment ya kwanza, una umri gani? maana naona mtazamo wako ni mdogo sana! umefikiri juu ya suali la usalama wa watu wote hapo na hususan watoto? hebu angalia umati huo mtoto akipotea hapo kuna chance gani ya kumuona haraka? mtu anaweza akamuiba mtoto kirahisi na akatoweka nae kirahisi, kila mtu akimuona kamshika mtoto na mtoto analia si atadhani ni baba/mama na mwana kumbe wala! pia ikitokea mtu kuzama baharini unadhani itachukua muda gani kugundulikana kama amezama seuze kuweza kutafutwa? tena kuna suali zima la vibaka. tena kuna issue kama pakitokea panic ndogo tu na watu kuanza kukimbia ovyo ovyo unadhani wangapi watafariki? (imagine atokee mtu apige kelele kaona bomu, unadhani patakuwaje hapo?) sijui hata kama askari wanafika hapo wakati kama huu, na hata kama wanafika angalia umati huo askari hawana control ya crowd.wewe unasema usafi wa mazingira. unadhani hilo ndio big issue hapa?
ReplyDeleteTatizo tuna viongozi wengi wasio na maono au vision of so to speak.
ReplyDeleteWanashindwa kuona kuwa sehemu iliyojengwa maalumu itasaidia serikali na jamii kwa ujumla.
Kwa haraka haraka tu, sehemu ikijengwa maalumu itasaidia kiusalama,na hata kukusanya watu wengi zaidi.Kutakuwa na wafanyakzi ambao wataongeza ajira kati ya watu wetu.Vilevile serikali itweza kukusanya ushuru kwa shughuli zote za kibiashara zitakazofanyika hapo.
Haya kwa viongozi wetu ni mambo yatokanayo tu kwao.Wala hawana habari kabisa kuwa inatakiwa mipango mizuri ili kufikia malengo hayo.
Iliyobaki ni kuomba Mungu tu atusaidie, hatuna cha kufanya. Halafu viongozi wa dini wakituambia ni walevi na wazinzi tutalalamika ?
Hapa ndio inavyoonyesha kuwa sasahivi mmeishiwa biti na nyimbo pia. Hivi ulitegemea watu wakitaka kula raha waende wapi? Sio wote nanapendelea kwenda Baa au gesti, wacha watu wajimwage ..... kibaya kwako wa mwenzio dili...
ReplyDeleteMhh mimi naona hiyo sio tena starehe ya beach bali sasa imekuwa ni balaa tu. Naona haina tofauti yoyote na kariakoo. Kama beach ndiyo hivyo basi haifai tena.
ReplyDeleteMdauzzzzz
Naunga mkono kabisa maneno ya mdau wa January 02, 2009 5:24 PM, KWakweli kabla ya kuanza kufikiria anasa na sehemu za kupumzika, fikirieni kwanza wananchi wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku, nakumbuka wakati nakua kwetu tulikuwa tunakaa kwa bibi mzaa mama, yeye ndio mwenye nyumba, sisi wajukuu, mama na baba na watoto zao,tulikuwa na wapangaji wanne wenye familia zao, wameoa na wana watoto, yaani kifupi ngumba ya vyumba sita ilikuwa na watu zaidi ya thelathini, sijui mpaka leo tuliishi vipi, sasa hivi nipo ulaya naona watoto wa miaka 16 wanapewa nyumba za kupanga wakae pekeyao kama wanataka kuhama kwa wazazi nashangaa sana, najiuliza hivi nikuwa katika mazingira gani? na wale waliopanga kwetu walikuwa na haligani, hapo sisi ndio tulikuwa tunaonekana mazungu mtaani(uswahilini) tunamiliki nyumba na kuna watu wanatulipa kodi, wakati ukweli ni kwamba sisi wenyewe tulikuwa choka mbaya. Maeneo ya kupumzika, wakapumzike kina nani wakati raia wamechoka kwa kazi ngumu na masaa mengo ya kujituma huku wengine wakifukuzwa na askari wa jiji, maeneo hayo yawekezwe kiasi gani wakati pesa hizo zingesaidia kuboresha huduma katika zahanati na hospitali za miji mbalimbali.... nakerwa sana na wabongo tunavyojiona tuko safi kama vile africa kusini, wabongo tunapenda sana starehe na niwabinafsi mno, haya DAR iboreshwe kwani nchi ina mkoa mmoja tu, vipi mikoani ambako watoto wanaenda shule maili kibao kutafuta elimu wakati hata kifungua mdomo hawajapata? Nchi sio Dar peke yake, na watu wa kigoma na mpanda na mikoa mingine ni raia wa nchi hiyo hiyo mnayotaka iwekezwe fukwe na mabustani jangwani sijui na sehemu gani..! Nchi yetu maskini tena maskini mno,takwimu za dunia zinairank between bottom ten duniani... acheni kujishebedua na msiwe wabinafsi kujifikiria mlio dar tu na mnaoweza kutoa comment kwenye internet wakati kuna wabongo kibao hata hela ya kwendainternet cafe dili, no bora wanunue mihogo wale...
ReplyDeleteNakumbuka mwishoni mwa 2005 nilikuja likizo nikakuta katika vituo vya mabasi kuna meza zinauza mihogo mibichi iliyowekwa kwenye maji na Raia wanakula hivyo hivyo, yaani machozi yalinitoka na nikawaonea huruma sana raia hao ambao wakisikia hela wanazokatwa na tra na serekali kwa ujumla zinataka kujengewa fukwe..... Mungu Ibariki Africa.
Mdau.
Ukweli utabaki kuwa Ukweli. Mlalahaoi hapaswi kutafutiwa sehemu ya kuenjoy. Katika utafiti wangu shida nyingi zinasababishwa na maskini. Asilimia kubwa ya maskini ndio wanaozaa watoto wengi wakati wanajua kabisa hawawezi kuwatunza. ukiwapa hao watu vitu vya bure watatuletea shida. Ninashauri serikali ifanye kila kitu kulipia ili walahoi waelewe hasara ya kuzaa sana. Pia serikali ingeweka kodi kwa kila mzazi anayezaa zaidi ya watoto wawili ili watu watakao zaa watoto wengi wawe wale wenye pesa ambao wanaweza kuwatunza. DAWA YA JIPU NI KULIPASUA NA NIMESHALIPASUA.
ReplyDeleteCha kufanya
ReplyDelete1. Kujenga nyoo vya kudumu
2. Kuwe na police
3. Life guards muhimu
4. Office ya emergency medical service iwe hapo
5. Mapipa ya kuweka takataka
6. Waweke maduka ya kuuza vitu
Then they are good to go.
Na hii iwe kwa kila beach sio hapo coco beach tu. Ndio maana watu wamejazana kama nini, Utazania Corney Island wakati wa summer. Tofauti ni vivutio, police, wauguzi na life guards huwaoni hapo.
Mh. Balozi
ReplyDeleteHapo ndipo Copacabana, Cancun na Ibiza yetu. Pia ni karibu kwa hao wakazi wanaobarizi upepo mwanana wa bahari.
Suala ni kupaboresha kama wadau wengine walivyosema.
maeneo makubwa ya jiji la dar hayatumiki kama inavyotakiwa,mfano pale jangwani palipaswa kujengwa vizuri na kuwa na michezo na maeneo mazuri ya kupumzika na viduka vya ice cream chips na watu wangeweza kwenda huko kirahisi bila kujazana hapo coco beach tu,cha ajabu hakuna maofisa wenye kufikiria jambo hilo ila kujaza mitumbo yao tu na kuacha wananchi wakiangaika kila wakati,bongo tambarare
ReplyDeleteWafuate nyayo zetu sisi Wachagga. Nakuakikishia hapo hakuna mchagga hata mmoja wote wako milimani.
ReplyDeletehahahahaaaaaaa teh teh
ReplyDeleteyan apa ikitokea mtu kazama no uokoaji ata kidogo,au shark weee
ila mbanano wooote huu raha iko wapi???khaaaa,wangeenda kigamboni,bagamoyo,nk
JAMAANI KAKA MICHUZI KAULIZA NINI KIFANYIKE HAJATAKA MALALAMIKO ...NINI KIFANYIKE MAANAYAKE ITASAIDIA KWANJIA MOJA AU NYINGINE HATA KAMA KUNA WAFANYABIASHARA WANAWEZA KUCHUKUA MAONIYENU WAKAYAFANYIA KAZI KWAFAIDA YA WATANZANIA WOTE HASA ...SISI WALALAHOI...MIMI NADHANI HAPO COCO VINGEFANYIKA VITU VIFWATAVYO..
ReplyDelete1.ULINZI WA POLISI...
2.VIJENGWE VIBANDA VIZURI VYENYE MVUTO VYAKUUZA SNACKS NA SOFT DRINKS
3.LIFE GURDS
4.BOTI ZA MICHEZO
5.WATAFUTWE WAJASIRIAMALI WAKITANZANIA WATAKAO KUWA NA UWEZO WA KUTAKE UP PROJECT KAMA HIZO..
KITU KINGINE KINACHO WEZA KUFANYIKA
ReplyDelete1.ZIJENGWE BUSTANI NZURI ZA KUPUMZIKA
HILI SWALA SERIKALI YETU HAIJA LIFIKIRIA KABISAA....BUSTANI NISEHEMU NZURISANA YA KUPUMZIKA...PIA KUMBIZA CINEMA JAMANI ZIJENGWEE NA ZIWE NA BEI YAKAWAIDAJAMAANI MLALA HOI ATAPATA WAPI 5000/- SHILLING..MAJUMBA YA CINEMA YENYE BEI NAFU YANAWEZA KUWA KIVUTIO CHA WATU WENGI SANA NA MKUSANYIKO UKAPUNGUA HAPO COCO BEACH.
WATU WANAJAZANA HAPO COZ HAWANA PAKWENDA JAMANI STAREHE NIPART OF TIME JAMANI SIO KITU CHAKUPUUZA NDIOMAANA WATU WANAAMUA KUWA WALEVI TU ....