Jeneza la Marehemu Fanuel Sedekia wakati wa kutoa heshima za mwisho leo ambapo maelfu ya watu walimiminika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Arusha kumuaga.
Jeneza la marehemu likiwasili uwanjani
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulifurika waombolezaji

Wadau wa Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Makumira Arusha wanaungana na waombolezaji wote kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na wafiwa wote wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Ndugu Fanueli Sedika ambaye leo Maelfu ya wakazi wa mji wa Arusha wamejitojitokeza kuuaga mwili wake.
Hakika Sedekia alikuwa mtu wa watu.
MOLA AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA PEPONI
AMINA
--
Picha kwa hisani ya Meshack c.Maganga
Tumaini university
Makumira University college
Faculty of Humanities and social science
+255 713 486 636
ARUSHA
TANZANIA
www.meshackmaganga.t4.com
http://www.makumira.ac.tz
meshackmaganga@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. RIP my dear Fanuel!!!

    That's all i can say!! the rest God knows....!!!

    ReplyDelete
  2. RIP Fanuel, ntakukosa. Nimebarikiwa kupitia nimbo zako.

    ReplyDelete
  3. Hakika Mungu apokee sifa na utukufu wote kwa jinsi ambavyo amelitukuza Jina lake kwenye mazishi ya mtumishi wake Fanuel Sedekia.
    Bwana Yesu azidi kuifariji familia ya marehemu,amina.

    ReplyDelete
  4. Mungu awape faraja kubwa wote hasa familia ya Fanuel Sedekia na wote ambao Mungu amekuwa akiwabariki kwa nyimbo za marehemu Fanuel.
    For about 10 years I have been always inspired by his annointed songs and forever I will.
    RIP Fanuel. Loo kama ndoto.
    Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la bwana libarikiwe.
    (asante kwa picha ndugu wa Makumira)
    Mdau, NL

    ReplyDelete
  5. Ndugu Sedekia alipendwa na watu sana ,uwanja ulijaa watu amabao sijauona kwa miaka ya karibuni hasa hapa Arusha kweli ameacha Historia ambayo inaishi.Mungu ametwaa jina lake libarikiwe.
    Meshack Maganga
    Tumaini ARUSHA

    ReplyDelete
  6. Hakika Sedekia alikuwa ni mtumishi wa Mungu kila kona ya Tanzania ilipata habari ila kwetu sisi ni somo je kesho utakuwa wapo na umefanya ninikatika kazi ya Bwana Bwana alito na bwana alitwaa Jina lake libarikiwe

    ReplyDelete
  7. Tunamshukuru Mungu kwa maisha yako Fanuel,mwisho wako umetudhihirishia wazi kuwa kweli ulikuwa mtumishi wa Mungu aliye hai. Umetuachia pengo kubwa sana ambalo kamwe halitazibika. Japo umetuacha lakini Sauti yako ingali ikahubiri pamoja nasi. Tunaumia sana ila najua Bwana atafanya njia, HAKUNA JARIBU LISILO NA MLANGO WA KUTOKEA.
    BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE. AMEEN!
    Tutakukumbuka daima kwani tunakumbuka jinsi gani tulivyoianza kazi ya uimbaji na galaton lako pale Mazengo Sec Dodoma,
    Unakumbukwa sana na Kimaro, Baraka, Nehemia, Tina, Tuli, Flora na Bite,
    Tunakaza Mwendo ili nasi tufike huko uliko tuendeleze ile Fellowship yetu.
    R.I.P Fanuel

    ReplyDelete
  8. Kweli pengo ulilotuachia aliwezi kuzibika.Tutakukumbuka daima,nyimbo zako zinatufundisha na kutufariji sana
    POLE KWA WANAFAMILIA WOTE NA WATANZANIA KWA UJUMLA,
    BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE,
    REST IN PEACE.

    ReplyDelete
  9. Ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu amelala, lakini Fauel Sedekia bado anahubiri! Jina la Bwana Lihimidiwe!

    ReplyDelete
  10. Ni zaidi ya miaka 12 sasa lakini bado ni kama ndoto kuamini kwamba Fanuel hatuko naye tena. nyimbo zako zimeendelea kunibariki siku baada ya nyengine na nakuombea upumzike kwa amani mtumishi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...