MPIRA UMEISHA NA KILIMANJARO STARS IMEFUNGWA BAO 2-1 NA HARAMBEE STARS YA KENYA KATIKA NUSU FAINALI YA KWANZA YA KOMBE LA CHALENJI UWANJA WA NELSON MANDELA.
KUFUNGWA TUMEFUNGWA LAKINI CHENGA TUMEWALA....
KILI STARS SASA WATAWANIA NAFASI YA TATU KWA KUCHEZA NA MSHINDI KATI YA UGANDA NA BURUNDI KATIKA NUSU FAINALI YA PILI INAYOANZA SAA 9 UNUSU UWANJANI HAPO HAPO
Jamani kwa wenzetu mliopata nafasi ya kuungalia mchezo je mnaweza kutupa tathmini ya haja juu ya maamuzi haya, kwani inaelekea maamuzi mengi yamekuwa ni yakubabaisha na je kiuchezaji timu ilikosea wapi na je kulikuwa na umuhimu wa kuwa na mwalimu tofauti kwenye Kilimanjaro stars zaidi ya Maximo? Labda kwa kuwa mashindano ni wachezaji wa ndani, labda na mwalimu wa Timu angekuwa pia wa Nyumbani!
ReplyDeleteSasa tunahamia wanja la Old Trafford jijini Manchester kwa pambano 'fungua mwaka' kati ya wenyeji ManUntd wakiwakaribisha Chelsea.
ReplyDeletePambano litaanza saa moja jioni saa za afrika mashariki(16:00 hrs UK time).
Wasifu wa Chelsea ni kuwa imecheza ktk mechi sita za mwisho mfululizo ugenini na kushinda au kutoka sare, hivyo inateremka Old Traffod na mentality hiyo.
ManUtd wao wanajua wakishinda mechi hii ya leo na mbili zinazofuata watakuwa wakuwa juu ya Liverpool FC na hivyo ni mwanzo wa changamoto kuzipiku Chelsea na Liverpool Fc ktk premier league.
Jamani huo ndiyo mchezo lazima kuna kushinda na kushindwa. Tuangalie makosa yalikuwa wapi na next time tujitahidi kuyarekebisha na kushinda. Sioni wakulaumiwa.
ReplyDeleteMdau
Aibu tupu, ubabaishaji wa Maximo kuweka makipa wabovu. Kipa namba wa tatu wa Simba na kipa wa JKT Ruvu wasimame mbele ya madume, wapiiii? Ngojeni Kodivaa tutafungwa kama watoto. Hii ni dalili mbaya. Tumefungwa hadi na Somalia?
ReplyDeleteUpuuuuuuuzi, aibu sana kufungwa na Wakenya, aibu kubwa mno. Kenya wao alishawahi kutucheka kwa kuwa na Maximo, kumbe yuko sahihi. Halafu inaelekea timu zote zimetujulia kwamba zinatufunga dakika za mwanzo halafu tunarisha bao moja, tunapigwa kadi nyekundu, mambo kwisha. Pumbafu kabisa.
Leo uwanjani Old Trafford atakuwepo Jose Marinhno kama mtazamaji, hii italeta mashamushamu ya kumbukumbu wakati Jose akiwa meneja wa Chelsea.
ReplyDeletePia data zinaonyesha kuwa katika kitimutimu cha ManUtd kukutana na Chelsea mara 16 hapo Old Trafford ManUtd imeweza kuibuka mshindi mara mbili tu.
Diego Maradona pia atakuwepo uwanjani akiwafuatilia wachezaji wa Argentina, jana alikuwa wanja la Britania kumtizama Mascherano wa Liverpool na leo atakuwa anamfuatilia Tevez, Diego Maradona ni kocha wa timu ya taifa la Argentina.
Leo asubuhi jijini Manchester wachezaji wa Chelsea ilibidi watoke nje ya hoteli yao baada ya 'alarm' ya moto kulia na hivyo kukaa ktk baridi kwa dakika 50 kabla ya kuruhusiwa kurejea tena ndani hoteli baada ya fire brigade kufanya ukaguzi na kukuta hakuna hatari ya moto.
Ikumbukwe kuwa mechi ya mwisho kati ya ManUtd na Chelsea ya premier league kule London Stamford Bridge timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Timu yenye rekodi nzuri ya kuzifunga 'big four' ni Arsenal lakini mpaka sasa data zinaonyesha hicho sicho kigezo cha kuongoza ligi au kunyakua ubingwa.
HARAMBEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!SIMBA WA AFRIKA MASHARIKI ANGURUMA...FISI AROROMAAAAAAAAAAAAAAA!!!
ReplyDeleteMichezo hii ya kombe la chalenji imetufunza nini hasa sie mashabiki wa Kilimanjaro stars(Taifa stars)?
ReplyDeleteKuwa ktk michezo kuna kushinda na kushindwa. Timu ya Zambia ambayo nayo ni mshiriki wa CHAN kule Ivory Coast pia imetolewa mapema ktk michuano ya chalenji.
Kwa wachezaji wa taifa stars kuwa oh walikuwa wanatuogopa sana, sasa ni wakati wa kuzidisha mikakati ya kufanya vizuri. Pia hata wachezaji wetu professional ngambo kule si pakujivunia, bali waongeze bidii Ivory coast wafanye vizuri ili wakapate mikakati bora zaidi ya kimchezo wakiwa professional ulaya.
Mwisho tushukuru tumepata dawa ya kujipanga vizuri zaidi ingawa hii dawa tulionyeshwa chalenji ni chungu kama shubiri.
Naamini tutatoka Kampala na ari mpya ya kufanya vizuri Ivory coast, wakati wa malumbano haupo.
hii mechi ilikuwa ngumu ikichukuliwa Kenya wana wafahamu wachezaji wa Yanga na timu zingine za ligi kuu ya bara.
ReplyDeleteMfano beki wa Yanga na Harambee stars anamfahamu vizuri Mrisho Ngassa, bado kuna kina Shikokoti na Mike Baraza.
Timu ya Kilimanjaro ina wachezaji zaidi ya saba waliocheza chalenji DSM 2007 na kuitoa Kenya ktk hatua za mwanzo.
Kikosi cha Harambee kilikuwa na sura ngeni mpya ambazo Kilimanjaro hawazijui kwa muda mrefu.
Hii ni somo kwa Kili stars kujipanga upya na kuwa wabunifu uwanjani baada ya maelekezo toka kwa kocha, maana dakika 90 huchezwa na wachezaji wabunifu wa kupambana na mapya kila dakika ya mchezo. Hivyo wachezaji wa Kili na Zanzibar watatumia funzo hilo Taifa stars kule Cote d'Ivore kwa kusikiliza vizuri maelekezo ya waalimu na kuzalisha matunda ndani ya dakika 90.
Timu haina kipa, hilo ndo tatizo kubwa na limetokana na kichwa ngumu cha Maximo. Kipa namba moja wa bongo Kaseja aishaomba msamaha lakini Maximo hataki kusamehe. Matokeo yake timu inakwenda kwenye mashindano na kipa namna 3 wa timu ya 5 kwenye msimamo wa ligi na yule wa JKT sijui ni ya ngapi?
ReplyDeleteKimsimamo wa ligi timu zilizotakiwa kutoa kipa wa timu ya taifa ni Yanga, Kagera Sugar au Mtibwa Sugar, maana ngo makipa wake wamefungwa magolli machache kwenye ligi.
Na huko Ivory Coast tukienda nao makipa aibu yake mtaisikia!
Kisiju
ReplyDeleteJamani kufungwa pia ni mchezo ama sivyo Mdau wa Maximo na TFF? Ahh nimesahau wachezaji walikua wamechoka kwa kucheza mechi mia mwaka huu!!
Kama mashindano haya tunakua wa tatu ama wa nne, je huko Ivery cost itakauje??
Ukweli mtume Maximo vipi tena?? Mjomba huyu mtu hatufai. Kama kawalisha limbwata ni nyinyi hapa kwangu zilo.
Tusubili Aibu huko Ivory Coast. Wadau amkeni jamani.
Kipa toka timu iliyojuu ktk ligi ya nchi siyo kigezo pekee cha kuchaguliwa timu ya Taifa.
ReplyDeleteMfano makipa wa timu ya Taifa Uingereza wanatoka ktk timu ambazo zinasuasua ktk msimamo wa ligi ya Uingereza.
Makipa hao mmoja ni David James wa Portsmouth ambae ni kipa nambari moja wa timu ya Taifa ya Uingereza. Ktk michezo ya ligi David James na timu yake Portsmouth hufungwa mpaka mabao 6 bila majibu.
Lakini kocha wa Timu ya Uingereza Capello anaangalia masuala mengi, je kipa ana nidhamu ya kitimu, ana ushirikiano na wachezaji wenzie, Je kipa huyo akipatiwa wachezaji safu ya ulinzi anaweza kuwapanga na wakamsikiliza? Je umbo la kipa linakwenda na sayansi ya mpira wa kisasa? n,k n.k
Timu siku zote inashinda pamoja na kuanguka pamoja, hakuna timu ya mtu mmoja, kama ingekuwepo basi nyota Robinhno wa Manchester City angeifanya timu yake iongoze ligi ya premier Uingereza au David Beckam angeibeba timu yake ya Los Angeles iwe mabingwa.
Kituo kimoja cha TV(siyo TBC1) kiliurusha mpira huo jana.Tumefungwa magoli halali ya kizembe huko kwenye beki na hasa goli la pili.Tuna matatizo ya mbinu za uwanjani bado kama alivyosema jamaa mmoja hapo juu.
ReplyDeleteSALUM SUEDI:Huku akifahamu kabisa kwamba ana kadi ya njano tayari,hakuna Nsajigwa uwanjani bado alidirki kufanya faulu ya kijinga na kutolewa.
Maximo aache kuwafundisha vijana ubabe,timu imekosa nidhamu kabisa,wachezaji hawana nidhamu,wana faulo zisizo za muhimu.Tujipange kwa ajili ya CHAN.
REFA:Kituo kilikuwa hakionyeshi slow motion,lakini penati anayodai mgosi haikuwa na utata sana.Mgosi baada ya kumtoka beki alisimama akisubiri aguswe ili aanguke.hakuwa kwenye motion ya kwenda kufunga.Halafu timu yetu isitegemee marefa,you simply keep scoring hata goli 5 au sita.
Full support kwa anony 12,Jan2009, kwa kuongezea data za makipa wa England national Team:
ReplyDeleteDavid James- Portsmouths
Paul Robison-Blackburn
Scott Carson- West Brom
Chris Kirkland- Wigan athletic
Robert Green- West Ham
Joe Hart -Man city
Joe Lewis- Peterborough United
Kocha mkuu Capello anatizama uwezo ndo maana hata Peterborough United imetoa kipa wa Taifa England.
Kitu kizuri hakijikuzi kitaonekana tu kikiwa bora.
Hapa kwa Kaseja inaelekea kuna watu walikuwa wanategemea kumuuza nje ya TZ Kaseja, wakaona Simba haifanyi vizuri na kwa vile hayumo ktk Taifa Stars labda wamuuze Yanga ili wajenge hoja zao kuwa ni kipa bora zaidi.
Sasa kwa vile yuko kwa mabingwa Yanga na hachaguliwi Taifa wanaendeleza kampeni aingizwe Taifa stars ili waweze kumuuza ngambo ingawa hana vigezo vyote muhimu vya kuwa Stars.
lakini bahati mbaya Kaseja Stars hayumo ndo wanaona wamekosa ulaji wa US Dollar, kila Taifa stars ikishindwa kihalali, angekuwepo Kaseja tungeshinda.
Mawakala wa Kaseja jifunzeni kutoka England team, timu ya Taifa Stars hata Mbagala Market wanaweza kutoa mchezaji bora.
Nilijua Kisiju hautoacha kutoa maoni..tulipowafunga Rwanda na Zanzibar ulitoa pongezi na nikakwambia kuwa hizo pongezi zako ni za kinafiki..na leo umethibitisha kuwa wewe ni mnafiki kwa sababu umezionyesha rangi zako halisi!!..mara ya mwisho tulitwaa challenge mwaka 1994 ..inakaribia miaka 15..maximo kaja nchi hii 2006..kati ya 1994 mpaka 2006 kuna miaka 12..kwanini katika kipindi hicho cha miaka 12 tulishindwa kulitwaa hilo kombe?..huyo Kaseja anaepigiwa kelele alishawahi kufungwa na Enyimba magoli 7 katika mechi mbili tu za mwaka jana..sijazungumzia mechi nyingi sana alizokuwa akichezea stars siku za nyuma..wenye mapenzi ya dhati kwa timu yao ya taifa wanaonekana sasa...na wanafiki wanaovaa sura za bandia kama vile Kisiju pia wanaonekana sasa.
ReplyDeleteUnajaribu kukejeli pointi ya Fatigue lakini ina ukweli ndani yake..wachezaji hawa wamecheza ligi kuu mzunguko wa kwanza wote..wamecheza mechi sita za kutafuta nafasi ya kwenda Ivory Coast waliporudi wakacheza kombe la Tusker , halafu tena wamecheza mechi za challenge..halafu ukumbuke kuwa katika challenge timu zilikuwa zinacheza mechi kila baada ya siku moja!!..hata ligi kuu ya England haiko hivyo!!..kama uliangalia mechi ya juzi dhidi ya kenya utakuwa umejionea ni jinsi gani wachezaji wetu walivyo kuwa hoi haswa kipindi cha pili..ilifikia wakati athumani idi alishindwa hata kukimbia uwanjani..rafu aliyoicheza salum swedi kipindi cha pili ilitokana na akili kuchoka..ndio maana hata wakati anatoka nje alikuwa hajutii makosa kwa sababu mwili ulikuwa hoi..wachezaji wetu ni wa ridhaa sio wakulipwa na wamecheza nyingi sana na ngumu sana kwa hiyo kwa wao kutolewa sioni kama ni dhambi na wala siwezi kumpiga mtu jiwe la kichwa eti kwa sababu tumelikosa kombe la challenge..tangu lianzishwe ni mara ngapi tumeshalitwaa kulinganisha na Kenya au Uganda? na kwa miaka yote hiyo maximo alikuwepo hapa Tanzania?..Kisiju acha majungu hayakusaidii..fitina zipeleke kwenye simba na yanga kwa sababu huko ndiko mahali kwake.
Kilichonishangaza mimi ni kwa viongozi wa TFF kulalamikia waamuzi wakati waamuzi wao pia ni wa aina hiyo hiyo wanasahau kwamba tuliwafunga Uganda , Kenya , Sudani kwenye kufuzu kwa CHAN na waamuzi wa kutoka ukanda huu huu nadhani hii ni mara ya kwanza kutokea
ReplyDeleteBadala ya kuwajenga wachezaji kisaikolojia kucheza katika mazingira hayo magumu wakaanza kuandaa sababu za kujitetea