
IT'S ALL ABOUT PARTY IN HOUSTON, TEXAS.
TETEMESHA SOUNDS & ALL STAR DJZ
brings you
AFRO BONANZA FRIDAY @ CLUB SAFARI,
ON THE 9TH OF JANUARY, 2009
HUU NI USIKU WA LADHA ZA KIAFRIKA AMBAO UNAANZA IJUMAA HII NDANI YA UKUMBI WA SAFARI MAENEO YA BISSONET, NDANI YA HOUSTON.
HIYO NDI O ITAKUWA SEHEMU YA KUJIDAI NA KUFURAHIA UTAMADUNI NA MUZIKI WA KIAFRIKA, KUANZIA ZOUK, LINGALA, QUITO, GENGE,WESTERN AFRICA MUSIC, NA BILA KUSAHAU REGGAE&OLD SKULL EXCLUSIVE KUTOKA DUNIANI KOTE IKIWA NI OMBI MAALUMU KUTOKA KWA WAPENZI WA MUZIKI.
SHOW HIYO ITAANZA SAA 10 ZA USIKU MPAKA SAA 10 ZA USIKU. KAMA KAWAIDA ALL STADJ'S WATAWACHEZESHA WATU MPAKA MAJOGOO DJ KAYCEE & DJ REX ON 1'S N' 2'S.
ONESHO HILI LINALETWA KWA HISANI KUBWA YA SAFARI ENTERTAINMENT 09


kuanzia saa 10 usiku mpaka saa10 usiku? yani 24 hrs?
ReplyDeletepia mbona list ya miziki mingi? itapigwa yote kweli au polojo tu! mbona mda mdogo ukizingatia watu wa huston wanaenda madisco au out saa nane za usiku ndo wanatoka majumbani kwao,yani night club zinaanza kuchanganya saa tisa usiku lakini clubu au party za watz wa Huoston tu sielewi kwanini wanachelewa kutoka makwao
kasumba ya zamani ya eti" nichelewe watu waone nguo yangu"
basi wote wanachelewa.ha ha ha haaaa ha.
Karamagi apata pigo jipya
ReplyDelete2009-01-07 12:53:06
Na Mashaka Mgeta
Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) imetupilia mbali rufaa ya kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS), iliyokata dhidi ya uamuzi wa Mamlaka ya Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra) wa kukataa maombi ya kuongezwa kwa gharama za kuhifadhi kontena bandarini.
Rufani ya TICTS kampuni ambayo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi anamiliki hisa asilimia 30, iliwasilishwa katika Baraza hilo na mwanasheria wake, aliyetambulika kuwa ni C. Rwechungura wa kampuni ya uwakili ya Rex Attorneys. Sumatra iliwakilishwa na H. Songoro.
Karamagi pia aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kabla ya kuhamishiwa Nishati, pia alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TICTS kabla ya kuondolewa wakati sakata la Richmond lilipopamba moto mwaka jana. Sakata hilo lilimwondoa katika nafasi ya uwaziri.
TICTS ilikata rufaa hiyo dhidi ya uamuzi uliofikiwa na Sumatra wa kukataa mapendekezo yake (TICTS) ya kuongeza gharama za kuhifadhi makontena bandari kwa madai kwamba ongezeko hilo lingepunguza mrundikano wa kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Uamuzi wa kuitupa rufaa hiyo, iliyopinga uamuzi wa Sumatra namba SMTRA/06/2008, ulitolewa Desemba 29, mwaka jana na kusainiwa na Msajili wa Mahakama hiyo, Edson Mkasimongwa.
Aprili 18 mwaka jana, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kwa niaba ya TICTS, iliwasilisha kwa Sumatra ombi la kutaka kupitiwa upya gharama za kuhifadhi na kuondoa kontena bandarini hapo.
Mbali na kupunguza mrundikano wa kontena, sababu nyingine iliyotolewa na TICTS ni kuwadhibiti wasafirishaji kwa njia ya meli ambao wanadiwa kuifanya bandari hiyo kuwa eneo lao la kuhifadhi makontena yao.
Hata hivyo, baada ya kutathmini ombi hilo na kuitisha mkutano wa wadau, Sumatra ilitoa uamuzi kuwa ongezeko lililopendekezwa, lilikuwa kubwa na lisilokidhi ushindani wa soko.
Sumatra kupitia tamko lake la Juni 11, mwaka jana, ilitoa maelekezo kuhusu ongezeko linalostahili, likiwa chini ya kiwango kilichopendekezwa na TPA kwa niaba ya TICTS.
Hata hivyo, Julai 25, mwaka jana, TICTS ilikata rufaa kwa Baraza hilo, ikidai kuwa, kamati ya mapitio ya Sumatra, ilikosea katika maeneo kadhaa katika kupitia pendekezo la kuongeza gharama hizo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotupilia mbali rufaa hiyo, TICTS ilitaja mapungufu hayo kuwa ni pamoja na kamati hiyo kutokidhi kifungu namba 26 (2) cha sheria ya Sumatra, kwa kutojitosheleza kushawishika na mazingira yaliyothibitisha haja ya kupanda gharama hizo.
Pia TICTS ilidai kuwa kamati hiyo haikutoa fursa ya kujibu hoja zilizotolewa na wadau kuhusu ongezeko hilo.
Hivyo, miongoni mwa maamuzi yaliofikiwa na Sumatra, ni hifadhi ya kontena kuwepo kwa muda wa siku 21, ambapo kuanzia siku inayofuata gharama itapanda kutoka Dola 20 za Marekani hadi 40, badala ya Dola 50 kwa kontena yenye urefu wa sawa na futi 20 (TEU) iliyopendekezwa na TICTS kutozwa kuanzia siku ya 16.
Aidha, Sumatra iliamuru gharama za kuondoa kontena ziongezeke mara dufu kutoka Dola 36 hadi 72 kwa kontena za urefu wa futi 20 na kutoka Dola 72 hadi 144 kwa kontena zenye urefu wa futi 40 (FEU), badala ya Dola 122 na 150 zilizopendekezwa kwa kontena za TEU na FEU.
Aidha, Sumatra iliamuru punguzo kwa wateja watakaofanikisha kuondoa kontena ndani ya saa 72, linapaswa kubaki kutoka Dola 10 hadi 20 kwa TEU na Dola 20 hadi 40 kwa FEU, badala ya kiwango cha Dola 15 na 25 kwa TEU na FEU kama ilivyopendekezwa.
Katika rufani yake, TICTS kupitia kwa mwanasheria wake, C. Rwechungura, ilidai marekebisho ya gharama hizo, yalilenga kupunguza muda wa kontena kuwepo kwenye bandari ya Dar es Salaam, kutoka siku 21 hadi saba.
Kuhusu ushindani, TICTS ilidai kuwa Sumatra `ilijichanganya` kwa kufikiri kuwa asilimia 15 pekee ya kontena zilizopo bandarini, zinamilikiwa na wateja waliokamilisha taratibu muhimu kwa ajili ya kuondoa mizigo yao.
Pia, TICTS ilidai kuwa Sumatra ilitumia takwimu zisizo sahihi katika uhakiki wake, haikutumia viwango vya sasa vya hifadhi na uondoaji mizigo bandarini, badala yake ilitoa kipaumbele kwa viwango vinavyotozwa katika bandari ya Mombasa katika mtazamo wa ushindani wa kimataifa.
Kwa upande wake, Sumatra ilieleza kuwa uamuzi uliofikiwa, ulikidhi mamlaka, kazi na wajibu ulioanishwa katika sheria yake, hususan vifungu vya 5 na 16 (2).
Aidha, ilielezwa kuwa katika kufikia uamuzi wake, Sumatra ilijikita katika ombi na mapendekezo ya TPA kuhusu ongezeko la gharama husika, sababu zilizotolewa na matokeo ya mkutano wa wadau uliofanyika Mei 18, mwaka jana.
Sumatra ilisema kuna sababu nyingi zinazochangia msongamano wa kontena bandarini, ni ufanisi duni katika mchakato wa utoaji mizigo.
Pia ilieleza kuwa viwango vilivyopendekezwa na TPA, havikukidhi ushindani wa soko ikilinganishwa na hali ilivyo katika bandari ya Mombasa, hivyo ingeweza kusababisha bandari ya Dar es Salaam isiwe kivutio kwa wateja.
Kuhusu TICTS kutohusishwa kujibu hoja za wadau, Sumatra kupitia kwa Songoro ilikanusha, na kusema TICTS ilishiriki na kuwa licha ya kupewa fursa ya kujibu hoja za wadau, haikufanya hivyo.
``Ni dhahiri kwamba Sumatra ilifuata taratibu kufikia uamuzi wake na mkutano wa wadau uliitishwa kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 18 (2) cha sheria ya Sumatra,`` ilisema taarifa ya Baraza hilo.
Baraza hilo lilisema kuna ushahidi kupitia ripoti ya Sumatra kwamba kuna sababu nyingi zinazochangia mrundikano wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, Mahakama hiyo ilikubali kuwepo tofauti kati ya takwimu zilizotumiwa na Sumatra na zile zilizoanishwa katika ripoti ya mwisho TICTS kwa miaka 2004, 2005, 2006 na 2007.
Miongoni mwa tofauti hizo ni idadi ya kontena kwa mwaka 2004 kwenye bandari ya Dar es Salaam ilikuwa 227,114, wakati ripoti ya TICTS ilikuwa 259,369.
Aidha kwa mujibu wa uhakiki wa Sumatra, kontena zilizohudumiwa bandarini hapo kwa mwaka 2005, zilikuwa 258,389 wakati kwa mujibu wa TICTS ni 293,919.
``Kwa kuwa Sumatra walifuata taratibu husika ikiwemo kuitisha mkutano wa maoni ya wadau, kabla ya kufikia uamuzi, tumeridhishwa kwamba uamuzi uliofikiwa hauwezi kubatilishwa, rufani haina msingi, tumeitupilia mbali na mrufani atawajibika kulipia gharama zilizotumika,`` ilisema sehemu ya uamuzi wa Baraza hilo.
SOURCE: Nipashe
duuuuuuuuuuuu debe masaa 24 jamaa watakula box saa ngapi na saa ngapi wata kuja huko si unajua wabongo bado wanazile za long time kama alivyosema jamaa hapo juu yaani kwa kuchelewa wanaongoza
ReplyDeletemdau wa jan 8,8:11 asante kwa habari uliyotuletea manake nilikuwa naisubiria kwa hamu sana. ila mpaka leo nashindwa kuelewa hao TICTS wapo kwa ajili ya kusaidia watanzania au kwa manifaa yao binafsi. haingii akilini kuona wanang'ang'ania kupandisha gharama mara 4 ya za mwanzo(mfano kontena futi 20 wanataka dola 122 kutoka dola 36) na siku za kugomboa ziwe 16,hii si ni balaa!!! mi nafikiri huu ni mradi wa mtu na wote tunamjua,kwanini serikali wasimfanyie fitna kama wanaumia na jinsi wananchi wake tunavyotaabika!! inakeraaa! asante!!!
ReplyDeletewatu wa houston kwa mchezo hamjambo
ReplyDeleteNi vizuri kuwa na shughuli za kujifurahisha lakini mngetumia moyo huo huo kuwa na vikao vya maendeleo mngefika mbali
ReplyDelete