Wadau hivi nani hajawahi kusikia kuhusu kubemenda mtoto huko majumbani na mitaani kwetu.
Ila mimi pamoja na kupekua huku na kule wakati wa ujauzito na hadi leo sijawahi kuona kubemenda kwa nchi zilizoendelea.
Hivi kweli kuna kitu kama kubemenda mtoto?
Ni nini hasa? na inasababisha na nini?
-Mdau Jiang Alipo
Mada hii iko hewani kule
mamanamwana.blogspot.com
na mdau unakaribishwa kuchangia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hiyo ni moja ya zile dhana za Afrika tambarare yaani zisizo na kichwa wala mguu. Kama watu wanaamini ukifanya mapenzi na mama wakati mtoto ananyonya kutamwathiri mtoto wakati wanasahau ni matatizo ya mlo ndiyo yanamwathiri mtoto.

    ReplyDelete
  2. hakuna suala kama hilo katika maisha ya ndoa bwana,hapo wanandoa wanajisahau kumpa mtoto malezi bora kisaikolojia,kumnyonyesha kwa wakati unaotakiwa au kila wakati mtoto anapohitaji kunyonya then mtoto ananza kupata madhara kiafya watu wanaanza kusema oh kabemendwa mara oh mama ameanza mapenzi mume wake wakati mtoto mdogo,na hii ni dhana mbaya sana kwa wanaume ndo wanapopata nafasi ya kuanza mahusiano mengine na wanawake wengine kisingizio mke analea na nikimwingilia kimwili mtoto ataharibika, WIZIIIII MTUPUUUUUUUUU. Ni Mr Solomon wa Dar

    ReplyDelete
  3. KUMBUKA NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA HAWANYONYESHI WATOTOT LANGU JICHO

    ReplyDelete
  4. Ila mambo mengine ya ajabu sana Kwa mara ya kwanza naingia kusoma blog ya jamii nakutuna na mada inayonigusa sana, au huyu mdau anafahamu nini kinaendelea ndani ya nyumba yangu? hivi karibuni nimepatwa na tatizo kubwa kwa mke wangu, mimi nilikuwa najitahidi nisimuingilie mke wangu kuogopa nisije nika m-bemenda mtoto, yeye(wife)akawa ananinunia akidai mahudhurio yangu sio mazuri kwake hivyo akanihisi huenda nina kanyumba kadogo, Sasa nafanyeje kama hiyo dhana ni ya kweli?

    Mzee X

    ReplyDelete
  5. Hakuna kitu kama kubemenda mtoto katika sayansi. Hii ni njia ya kijadi ya kuwafanya watu kupanga uzazi kabla ya kuja njia za kisasa kuwepo. Hii ilikuwa inawafanya wababa kuwa mbali na wake zao hivyo mama kupata nafasi nzuri ya kumlea mtoto angalao miezi sita ya mwanzo. Ukweli ni kuwa watoto wengi wameonyesha kuathirika kiafya wakati mama anaposhika ujauzito mapema. Hii inatokana na ukweli kuwa mama akishika ujauzito mapema uangalizi wa mtoto hupungua na wengine huacha kunyonyesha hivyo watoto hudhoofika. Ushauri wa kitaalamu ni kuwa kama mama kukutana na mama kimwili wakati wa kulea hakuna madhara yoyote kwa mtoto. Inashauriwa njia za kupanga uzazi zitumike ili kuzia mimba. Mwaweza kuanza kujamiiana baada ya ukavu kutokea au baada ya arobaini. Kama mama akipata ujauzito aendelee kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita ya mwanzo(mimba ikifika miezi sita). baada ya hapo anashauriwa kuacha kunyonyesha ili maziwa yenye kinga(colostrum) yatengenezwe kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa na wala si kwamba yana madhara. Dr. Primus, Muhimbili

    ReplyDelete
  6. Ndiyo Dr. , ushauri wako ni wa maana sana. Pamoja na hayo naomba watu wanaokebehi hii falsafa kwa kisingizio kwamba haipo kwa wazungu waache kudharau falsafa za kiafrika. kwa wakati huo hii falsafa ilifanya kazi sana ukizingatia dawa za uzazi wa mpango hazikuwapo au uhamasishaji wake ulikuwa mdogo lakini pia ukimwi haukuwepo. Mimi nadhani tuwasifu walioanzisha hii falsafa kwani walisaidia watu badala ya kuidharau ila kama alivyosema Dr. hapo juu, hivi sasa siyo lazima kuifuata kwa sababu zipo njia zinazoleta matokeo kama ya hii falsafa. Mimi nadhani hivi ni vitu vya kuwekwa kwenye kumbukumbu zetu kama waafrika kwa ajili ya vizazi vijavyo

    ReplyDelete
  7. jamani kubemenda ndio nini?

    ReplyDelete
  8. Mdau wa jan 16, 8:45pm, Nadhani wengi wetu hatuna shida na walioanzisha hii falsala kama ulivyoiita.Kwa wakati wao ilikuwa na mantiki kutokana sababu ambazo zimeshaelezwa. Shida kubwa ni hawa watu ambao bado wanaibeba hii falsafa mpaka sasa, ambapo dhana yake imepoteza maana. Na hatutakuwa tunakosea tukisema kuwa kwa sasa imepitwa na wakati..!Kupitwa na wakati sio kwamba tunawakejeli walioianzisha, hapana bali ni hali inayojitokeza, ukilinganisha na matumizi. Mwenyewe umesema sasa hivi kuna UKIMWI, Kuna mdau hapo juu katatoa angalizo kuwa dhana hii yaweza kuongeza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI(VVU) kwa kinababa kutafuta nyumba ndogo nje ya ndoa wakati akimsubiri mama amalize malezi.Nikiangalia ni muda gani mama anatakiwa awe na ukaribu na mtoto kwa maana ya kunyonyesha ni mwaka hadi miaka miwili( katika hali ya kawaida). Sasa fikiria ndugu yangu uwe benchi kwa kipindi hicho kwa kuogopa kubemenda mtoto ?! Uzalendo waweza kukushinda na ikifikia hivyo ujue utatafuta ajali..!! Sasa tufanyeje ? Tuwe wapole kwa kuwaenzi walioianzisha au tukemee itusaidie kwa wakati huu tulionao...?!

    ReplyDelete
  9. Kubemenda mtoto kupo, ni wakati mama ananyonyesha yeyote kati ya wanandoa akitoka nje na baadae wakakutana ktk tendo na huku mama anaendelea kunyonyesha. mchanganyiko wa damu hapa utajibu kwa kale kachanga kanyonyako. Wawili wazazi wanaweza kuruka watakavyo mradi wana makubaliano na wanajua watakavyoepuka ujauzito usiotarajiwa. Akiingia mgeni indicators zitaonekana. Wazungu wametutangulia ktk mengi wana madawa mengi msiwaangalie. mtaumiza mtoto bure.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...