HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA WATU SITA, WAKIWEMO WANAFUNZI WAWILI WA SHULE ZA ECKENFORD NA MLINGANO, WAMEKUFA NA WENGINE SABA WAKO MAHUTUTI BAADA YA BASI WALILOKUWA WAMEPANDA KUGONGANA NA SEMI TRELA MAENEO YA MUHEZA MKANYAGENI, MKOANI TANGA.
INASEMEKANA BASI HILO, IITWAYO RMETA, LILIKUWA LINAOVATEKI HILO SEMI TRELA NA MBELE LIKATOKEA GARI LINGINE NA DEREVA WA BASI, AMBAYE NAYE NI MIONGONI MWA WALIOPOTEZA MAISHA, AKASHINDWA CHA KUFANYA NA KUPARAMIA HILO TRELA.
HIVI SASA MAITI NA MAJERUHI WAKO KATIKA HOSPITAL TEULE YA MUHEZA NA HALI ZA ABIRIA KADHAA NI MBAYA. MKUU WA MKOA WA TANGA AMESHAWASILI HOSPITALI HAPO HIVI SASA NA MADAKTARI NA WAUGUZI WANAJITAHIDI KUTIBIA MAJERUHI.
GLOBU YA JAMII INATOA POLE KWA WALIPATWA NA AJALI HIYO NA ITAENDELEA KUTOA HABARI ZAIDI KWA KADRI ZITAVYOPATIKANA.
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, Amen
ReplyDeletePoleni wafiwa na majeruhi mpone haraka.Jamani ajali ajali,jamani madereva wa mabasi ya abiria kuweni makini zaidi na sheria za barabarani.Mr.Mwema,Defensive driving courses ndiyo the best option.Madereva wa magari ya abiria walazimishe kuhudhuria hizi course kila mwezi au baada ya miezi miwili.
ReplyDeleteBraza Michuzi, asante kwa kutupasulia habari. Hata hivyo nakushauri utujulishe hilo basi ni kampuni gani na lilikuwa linakwenda wapi.
ReplyDeleteKilamba Mchuzi
Nawapa pole wafiwa na wahanga wa ajali hii ya kizembe.
ReplyDeleteKuna haja ya kufanya mapitio ya mfumo mzima wa usafiri wa abiria na sheria zetu za usalama barabarani.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/
Nafikiri wakati umefika kusema BASI kwenye hizi ajali.
ReplyDeleteKila Kukicha watu wanapoteza maisha na kujeruhiwa vibaya. Nguvu kazi ya taifa inateketea.
Naamini Tanzania kuna 'vichwaa' vyenye uwezo la kusaidia kupunguza hili tatizo la ajali za mara kwa mara kama siyo kuliondoa kabisa hili 'janga'.
Of course, "accidents do happen", lakini naona inabidi kuwe na msisitizo fulani kuwapa all stakeholders awareness and do something to change the situation.
Najua mambo ya 'credic cruch' na uchumi kwa ujumla huwa yanapewa kipaumbele sana na our 'talented' people with such good written English from all parts of the world, lakini hili nalo tusilifumbie macho! Tuwe na moyo kama huo tuokoe maisha ya watu wetu ambayo siku hadi siku yanapotea. Tutazungumzia uchumi wakati tupo SALAMA, lakini tukiwa 'MAJERUHI' au 'WAFU', kuna suala la uchumi?
Nina uhakika, sisi kama wananchi tukiamua kwa kuipa pressure serikali tutaweza kuzipunga hizi ajali.
NINI KIFANYIKE?
Jua Kali
Jameni, imetosha sasa. Labda na mwenye gari pia awajibike kisheria kwa kuajiri madereva feki. Pia dereva wa semi trailer, iwapo unaona dereva mjinga analeta panga kwenye koo la abiria wake, kwa nini usipunguze speed ili apite na uokoe maisha ya watu?
ReplyDeleteRIP wote
Blackmpingo
....wakati umefika sasa abiria kuchukua tahadhari wanapoona dereva anakiuka taratibu za usalama barabarani ikiwemo mwendo wa kasi, kuongea na simu wakati anaendesha gari n.k Ajali nyingi zinaepukika...
ReplyDeleteMungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu Ameni.
******JOOMEK********
pole sana wafiwa inasikitisha sana wakati nawalikuwa kuja kuliokoa taifa letu la Tanzania
ReplyDeleteR Y
TUNAOMBA RAIS NA WAZIRI WETU MLIINGILIE KATI SULA HILI LA USALAMA BARABARANI THIS IS WAY TOOOOOOOOOOOOOOOOO MUCH.Mpaka tunaogopa kwenda kusalimia ndugu zetu. PLEASE DO SOMETHING..
ReplyDeletemichuzi umeibania ile comment ee?fisadi chipukizi wee
ReplyDeleteJamani eeeeh!! Hizi ajali za barabarani too much.. hivi kweli hakuna mtu anayeweza kufanya lolote juu ya hili tatizo? Mtatumaliza jamani.
ReplyDeleteMdau, Boston, US