HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA WATU SITA, WAKIWEMO WANAFUNZI WAWILI WA SHULE ZA ECKENFORD NA MLINGANO, WAMEKUFA NA WENGINE SABA WAKO MAHUTUTI BAADA YA BASI WALILOKUWA WAMEPANDA KUGONGANA NA SEMI TRELA MAENEO YA MUHEZA MKANYAGENI, MKOANI TANGA.
INASEMEKANA BASI HILO, IITWAYO RMETA, LILIKUWA LINAOVATEKI HILO SEMI TRELA NA MBELE LIKATOKEA GARI LINGINE NA DEREVA WA BASI, AMBAYE NAYE NI MIONGONI MWA WALIOPOTEZA MAISHA, AKASHINDWA CHA KUFANYA NA KUPARAMIA HILO TRELA.
HIVI SASA MAITI NA MAJERUHI WAKO KATIKA HOSPITAL TEULE YA MUHEZA NA HALI ZA ABIRIA KADHAA NI MBAYA. MKUU WA MKOA WA TANGA AMESHAWASILI HOSPITALI HAPO HIVI SASA NA MADAKTARI NA WAUGUZI WANAJITAHIDI KUTIBIA MAJERUHI.
GLOBU YA JAMII INATOA POLE KWA WALIPATWA NA AJALI HIYO NA ITAENDELEA KUTOA HABARI ZAIDI KWA KADRI ZITAVYOPATIKANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, Amen

    ReplyDelete
  2. Poleni wafiwa na majeruhi mpone haraka.Jamani ajali ajali,jamani madereva wa mabasi ya abiria kuweni makini zaidi na sheria za barabarani.Mr.Mwema,Defensive driving courses ndiyo the best option.Madereva wa magari ya abiria walazimishe kuhudhuria hizi course kila mwezi au baada ya miezi miwili.

    ReplyDelete
  3. Braza Michuzi, asante kwa kutupasulia habari. Hata hivyo nakushauri utujulishe hilo basi ni kampuni gani na lilikuwa linakwenda wapi.
    Kilamba Mchuzi

    ReplyDelete
  4. Nawapa pole wafiwa na wahanga wa ajali hii ya kizembe.
    Kuna haja ya kufanya mapitio ya mfumo mzima wa usafiri wa abiria na sheria zetu za usalama barabarani.
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  5. Nafikiri wakati umefika kusema BASI kwenye hizi ajali.

    Kila Kukicha watu wanapoteza maisha na kujeruhiwa vibaya. Nguvu kazi ya taifa inateketea.

    Naamini Tanzania kuna 'vichwaa' vyenye uwezo la kusaidia kupunguza hili tatizo la ajali za mara kwa mara kama siyo kuliondoa kabisa hili 'janga'.

    Of course, "accidents do happen", lakini naona inabidi kuwe na msisitizo fulani kuwapa all stakeholders awareness and do something to change the situation.

    Najua mambo ya 'credic cruch' na uchumi kwa ujumla huwa yanapewa kipaumbele sana na our 'talented' people with such good written English from all parts of the world, lakini hili nalo tusilifumbie macho! Tuwe na moyo kama huo tuokoe maisha ya watu wetu ambayo siku hadi siku yanapotea. Tutazungumzia uchumi wakati tupo SALAMA, lakini tukiwa 'MAJERUHI' au 'WAFU', kuna suala la uchumi?

    Nina uhakika, sisi kama wananchi tukiamua kwa kuipa pressure serikali tutaweza kuzipunga hizi ajali.


    NINI KIFANYIKE?

    Jua Kali

    ReplyDelete
  6. Jameni, imetosha sasa. Labda na mwenye gari pia awajibike kisheria kwa kuajiri madereva feki. Pia dereva wa semi trailer, iwapo unaona dereva mjinga analeta panga kwenye koo la abiria wake, kwa nini usipunguze speed ili apite na uokoe maisha ya watu?
    RIP wote
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  7. ....wakati umefika sasa abiria kuchukua tahadhari wanapoona dereva anakiuka taratibu za usalama barabarani ikiwemo mwendo wa kasi, kuongea na simu wakati anaendesha gari n.k Ajali nyingi zinaepukika...
    Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu Ameni.

    ******JOOMEK********

    ReplyDelete
  8. pole sana wafiwa inasikitisha sana wakati nawalikuwa kuja kuliokoa taifa letu la Tanzania

    R Y

    ReplyDelete
  9. TUNAOMBA RAIS NA WAZIRI WETU MLIINGILIE KATI SULA HILI LA USALAMA BARABARANI THIS IS WAY TOOOOOOOOOOOOOOOOO MUCH.Mpaka tunaogopa kwenda kusalimia ndugu zetu. PLEASE DO SOMETHING..

    ReplyDelete
  10. michuzi umeibania ile comment ee?fisadi chipukizi wee

    ReplyDelete
  11. Jamani eeeeh!! Hizi ajali za barabarani too much.. hivi kweli hakuna mtu anayeweza kufanya lolote juu ya hili tatizo? Mtatumaliza jamani.

    Mdau, Boston, US

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...