Edwin Van se Sar
wazee wa 'bwawa la maini' na 'wazee wa darajani' sie mashetani wekundu tunazidi kuweka rekodi UK kama kawaida yetu. ni rekodi nzuri tu si za kufukuza makocha!!
Edwin Van de Sar ameshafikisha dakika 1302 za ligi bila kuruhusu bao katika mechi 14 mfululizo za ligi baada ya jana kumnyuka Fulham 3-0. Bado dakika 89 tu avunje rekodi ya Dany Verlinden (si wa ligi ya UK) ya dakika 1390 ya mwaka 1990.
Mdau Geofrey Mbata
----------------------------
jamani, si mngoje mshinde ubingwa kwanza? mbona mna kimuhemuhe? hapo mnajiona kama mmeshachukua kombe, dah! na tunawaamnbia kabisa hicho kiti mlichokalia kwa muda kwa magoli ya mbeleko kina wenyewe, msikichafue....
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. NNYIE MAN U KENGE KABISA KAZI KUPENDA MISIFA WAKATI UWEZO MDOGO ETI 'TUNAWEKA REKODI KAMA KAWAIDA YETU..WAZEE WA REKODI NI BWAWAZ TU..BWAWAZ NDO TIMU ILIYOCHUKUA UBINGWA WA CHAMPIONS LEAGUE MARA NYINGI KULIKO TIMU ZOTE UK, BWAWAZ NDO TIMUMILIYOCHUKUA UBINGWA WA UK MARA NYINGI KULIKO ZOTE..ASA NYIE MAFALA REKODI GANI MNAYO? KIPA WETU JOSE MANUEL PEPE REINA NDIYE KIPA ALIYETWAA 'GOLDEN GLOVE' MARA YA 3 MFULULIZO KWA KUWA KIPA MWENYE KUKEEP CLEANSHEETS NYINGI UK KULIKO YOYOTE!!
    TAREHE 14/03 KIAMA CHENU MAANA J4 MOURIHNO NDO ATANZAKUWAPELEKA JANDON PALE SAN SIRO KISHA SISI TUNAMALIZA KAZI. mKUMBUKE HATA DEMU AKIWA MGUMU, AKIANZA KUGAWA TU BASI NDO KILA SIKU MCHEZO WAKO UNAKUWA NDO HUO HUO SASA VAN DE SAR AKIFNGWA TU NA INTER NDO YATAANZA KUINGIA KAMA MVUA.

    MZEE WA LIVA..CHAMA DUME!!

    ReplyDelete
  2. Watu wa liverfools bwana, yaani nyie mnaongelea historia mliyoweka miaka ambayo wengi wenu mlikua hamjazaliwa. Man Utd tunatengeneza historia yetu sasa hivi, tunachukua kombe la premier mwaka huu halafu inakua ngoma droo na nyie, tunavikombe vya FA kuliko timu yoyote, champions league labda barcelona watuekee ngumu mwaka huu, halafu nadhani mnasahau kwamba kwa sasa sisi ni CHAMPIONS OF UK, CHAMPIONS OF EUROPE AND CHAMPIONS OF THE WORLD, beat that!!!

    ReplyDelete
  3. Hold on a second !
    Mzee wa Liva...............
    hail a good perfomance and condem a bad one kisport...
    unakuwa kama unamsuta mtu aliyekuchukulia mkeo ?
    ok hear me out y'all yes liverpool has more silverware in premier and UEFA champ
    but ofcourse Man U has silverwares of every cup and it's done a treble and a double !!
    hang on to your seat ! we are after a quad !
    g'day mates.

    ReplyDelete
  4. HAHAHA INAUMAA EHEEE....
    NAONA IMEKUCHOMA MPAKA KUNAKO. HAHA
    SISI NDIO MABINGWA WA DUNIA SASA. BISHA USIBISHE
    UKWELI UTABAKIA NDO HUO. NAJUA WEWE NI MPENZI WA LIVERPOOL, KAKA TIMU YENU TOKA LINI MALA YA MWISHO KULIONA KOMBE LA UK. HAHA, NA IYO REKODI YENU YA KUCHUKUA MARA NYINGI UBIGWA WA UEFA TUTAWAPOKONYA VILE VILE. HAHA.

    SASA KIAMA CHENU KINAKUJA SI MLIPONYOKEA
    KWENYE TUNDU LA SINDANO MECHI YA MWISHO TULIYOCHEZA. SASA HII TUNAWAFANYA KAMA WENZENU WALE THE BLUEEZZ...

    HAHAHA AM OUT....

    BIGWA WA DUNIA WA SASA... SHETANI JEKUNDU....!!!!!

    ReplyDelete
  5. MICHUZI NAE ANA DONGE LIMEMKABA KOONI
    HAHAHA, BIBI UMEME MSHUSHIE NA MICHUZI NAE AJUI KAMA IYO TOSHA NI REKODI, NA TUKICHUKUA KOMBE ITAKUWA REKODI NYINGINE INAISINDIKIZA IYO. HAHAHA. ANKO MICHUZI NAONA UNATAPASUKA PALE TUTAPOWASHINDILIA GUNIA LA MAGOLI MECHI INAYOKUJA TUKICHEZA NA NYIE.. HAHA

    NTAKUKUMBUSHA TUU MTAONA UWANJA MCHUNGU.HAHAHA

    BIGWA WA DUNIA KWA SASA A.K.A SHETANI JEKUNDU

    ReplyDelete
  6. MICHUZI + BWAWA LA MAINI = ?

    YAANI LIVER MSIONGEE KABISA KWA KUWA MNAPENDA SANA HISTORIA, ANDIKENI VITABU MUUZE MASHULENI ILI WANAFUNZI WAJUE HISTORIA YA LIVER.

    MAN U NI KIBOKO ZAIDI YA LIVER KWA KUWA KACHUKUA KILA KOMBE NA KWA STYLE AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA, POPOTE PALE LABDA PLUTO KAMA WANA LIGI KAMA HUKU DUNIANI
    BUBE-TABATA, MANGUMI

    ReplyDelete
  7. Yeeeeeeeeee! Yebaaaaaaaaaaaaaaaa.

    Liver "poop" mdebwedooooooooooooooo

    ReplyDelete
  8. LIVER FOOLS.....
    Jina linajitambulisha lenyewe.Michuzi bongo TV zilikuja mwaka Gani?na mpira UK kwa bongo ulianza kupamba mota mwaka gani?Kuanzia hapo watu waanze kuongelea hizo historia zao.
    Madrid wana historia ya Ulaya zaidi,lakini ni miaka ipi??
    Zote ni Historia hata kama imewekwa juzi lakini ipi inakuwa na nguvu zaidi?tangu 1990 liver mnarecord gani?kuanzia Community Shield,Carling Cup,FA,Premiership na Champions League?
    KIZURI SIFIA,KIBAYA KOSOA ndio utaendelea maishani

    ReplyDelete
  9. Man u 3-Fulham 0....
    Sio kweli Reina ndio anaweka cleansheet nyingi kwa msimu ndio maana an gloves za gold.Peter Cech aliyeweka record ya mech 11 consecutive bila kuokota mpira wavuni mbona hakupata hiyo gloves??
    Wadau wa Record na kauli za matusi hapo mwanzo busara huna na hutaelewa kwani wenzio wanajivunia record inayowekwa wakati kila mtu anaona na anajua zaid ya za kwako ambazo unabaki kuzisikia kwenye bomba.
    Huwezi kujivunia kuuza ng'ombe kwa kesi ya Kuku.....michuzi upooooo????????

    ReplyDelete
  10. as a LFC fan 4 LIFE,Man Utd wana haki ya kupongezwa.mbona sisi LFC tunasifiwa kuwa hatujafungwa Anfield Road toka msimu huu na tunavimba vichwa??tena hata usukani wenyewe tutashika na kuachia.wadau wenzangu wa "YNWA" be fair.zamu ye2 ikifika nasi tutajiachia.
    so far,kigoda cha ligi ni cha mafahari wawili.Cheski,Gooner..oooppss,Gunners just R.I.P y'all!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. hivi nyinyi watu mmezaliwa uingereza? au kujipendekeza tuu kwenye timu za watu?

    Villa Squad ya migomigo mpaka siku ya kufa.

    ReplyDelete
  12. aaah! hata sijaamini sight na sound za Bradha Mithupu, yaani inaku-uuma saaaanaaaa Man U wanavyofanya mabo eeeh!
    Unashahau kabisa kuwa Man U ndio waflme wa Kandanda Ulaya nzima achilie mpali hapa kwa malkia.
    Ipo siku utalia zaidi kwa kushindwa kuipenda Man U

    Abajalo Orijino aka Man U ya Sinza

    ReplyDelete
  13. Bro mithupu huyo MBATA ni mvivu wa kutafuta info,namfahamu toka Mazengo ni mzembe, hiyo record isha vunjwa na mimi mwenyewe na timu yangu ya VETERAN hapa jijini GEITA.
    Mdau toka Geita
    AMOS.

    ReplyDelete
  14. Eti sisi Man U. Wabongo bwana, si mshabikie timu za kwenu Bongo!!! Mbona mnang'ang'ani timu za watu(Wazungu/Waingereza kwa ujumla). Ohh eti mie Man U, Liverpool, Chelsea, Arsenal sijui. Ebu nendeni mkashabikie Simba na Yanga, au timu zingine za Africa!!!!!

    ReplyDelete
  15. Michuzi, katika maisha ukisubiri mpaka ushinde ndo ushangilie, unaweza usishangilie, inabidi ushangilie hatua ndogo ndogo zote za mafanikio. Lakini kama wanavyosema wenzetu "He who laughs last, lasts best". Na mdau aliyesema tushangilie Simba na Yanga, nani kamwambia hatushangilii??? Mi ni mpenzi mzuri wa simba, lakini si mbaya kushangilia timu nyingine, maana huu ni ulimwengu wa utandawazi na taarifa zipo kila mahali, kwa nini tusizitumie na kushangilia timu nyingine? Kwa kusema hivyo, nahitimisha kuwa MANCHESTER UNITED WANATISHA! Ni hayo tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...