Na Mwandishi Maalum
SERIKALI imeamua kuchukua hatua za kuifufua Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ikiwa ni pamoja na kuipa kampuni hiyo dhamana, ili kuiwezesha TTCL kupata uwezo wa kukopa fedha za kujiendesha kutoka taasisi za fedha nchini.
Aidha, serikali imeamua kuwa itakuwa ni kampuni hiyo itakayosimamia matumizi ya Mkongo (fibre optic cable) wa Taifa ambao unalenga kuboresha matumizi ya teknolojia katika uchumi na maendeleo ya jumla ya Tanzania.
Kama ilivyokuwa kwa TTCL, Serikali pia imekubali kubeba madeni yote ya Shirika la Posta Tanzania, ili kuliwezesha shirika hilo kupata uwezo wa kujiendesha lenyewe kwa kukopa fedha kutoka taasisi za fedha ikiwa ni moja ya hatua za kupambana na changamoto za ushindani katika dunia ya sasa ya teknolojia mpya.
Serikali pia imeazimia kuharakishwa kwa mchakato wa kutungwa kwa sheria ya kusimamia na kudhibiti matumizi ya simu za mkononi na inteneti, na pia kukomesha wizi wa simu hizo za mikononi kwa kutumia teknolojia ya kileo.
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyokubaliwa katika mkutano kati ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na mashirika yaliyoko chini ya wizara hiyo, uliofanyika leo, Jumanne, Februari 17, 2009, Ikulu, Dar Es Salaam.
Mkutano huo chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete ni mfululizo wa mikutano kati ya Rais na wizara mbali mbali na mashirika yaliyoko chini ya wizara hizo inayolenga kutathmini utendaji wa Serikali katika miaka mitatu iliyopita.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano wa leo ni pamoja na Makamu wa Rais Dr Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo, na watendaji wakuu wa TTCL, Shirika la Posta, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam (DIT), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Mbeya (MIST) na Taasisi ya Nguvu za Atomiki (TAE).
Katika zoezi hilo la kutathmini utendaji katika Serikali yake lililoanza mwanzoni mwa mwaka huu, yaani mwezi uliopita, tayari Rais Kikwete amekutana na viongozi wa Wizara ya Miundombinu na mashirika yake, na Wizara ya Fedha na Uchumi na mashirika yake.
Mkutano huo wa leo umekubaliana kuwa upo umuhimu wa kuiimarisha TTCL na njia moja kubwa ya kufanya hivyo ni kwa Serikali kutoa dhamana kwa kampuni hiyo kuweza kukopa fedha za mtaji wa kuendesha shughuli zake.
Nyingie nyingine ya kuiimarisha kampuni hiyo ni kuipa kampuni hiyo jukumu ya kusimamisha shughuli za Mkongo wa Taifa, ambao utajengwa kwa fedha za mkopo kutoka Jamhuri ya Watu wa China, ikiwa moja ya mafanikio ya ziara ya siku tatu ya Rais wa nchi hiyo, Mheshimiwa Hu Jintao, ambaye aliondoka nchini jana, Jumatatu, Februari 16, 2009. Mkongo huo utagharimu dola za Marekani milioni 180.
Kwenye mkutano huo wa leo, Rais Kikwete ameelekeza kuundwa kwa kikosikazi cha kuharakisha ujenzi wa Mkongo huo, kujadili na kutoa mapendekezo jinsi Mkongo huo utakavyotumika kunufaisha uchumi na hivyo kutumika katika maendeleo ya jumla nchini.
“Mkongo huu usiwe tu wa kupunguza gharama za matumizi ya simu za mikononi tu…hili ni jambo zuri lakini ni lazima tuwe na mpango wa jinsi ya kutumia Mkongo huu katika kunufaisha zaidi uchumi wetu na kuwa nyenzo muhimu katika maendeleo ya jumla ya nchi yetu,” ameelekeza Rais Kikwete kwenye mkutano huo.
Kuhusu Shirika la Posta, mkutano umeelezwa jitihada za Serikali katika kulisaidia shirika hilo kwa kusafisha mahesabu yake kwa kuchukua dhamana ya madeni yaliyokuwa yanalikabili shirika hilo. Serikali ndiye mmiliki mkubwa zaidi wa hisa za shirika hilo, kwa kuwa na asilimia 41.
Kuhusu TCRA, mkutano wa leo umekubaliana kuwa ipo haja na hoja ya kuharakisha utungwaji wa sheria ya kusimamia na kudhibiti matumizi ya simu za mikononi na inteneti, na pia kufunga mitambo ya kuweza kukomesha wizi wa simu hizo za mikononi.
Mkutano huo umejadili na kukubaliana kuwa pamoja na mafanikio makubwa ya maendeleo ya simu za mkononi na matumizi ya inteneti katika miaka minane iliyopita, bado yamekuwepo matumizi mabaya ya simu hizo ikiwa ni pamoja na matusi.
“Lazima tujenge nidhamu haraka katika matumizi ya simu na inteneti… siyo huduma hizo kutumika kutukanana… kwamba kila mtu mwenye mtu wa kumtukana, basi kila akiamka asubuhi, kazi yake ni kumtukana mtu huyo kwa kutumia simu ama inteneti..,” amesema Rais wakati wa mkutano huo.
Idadi ya simu za mkononi nchini, kwa maana ya kadi za simu zilizouzwa nchini, imeongezeka kutoka kutoka zaidi kidogo ya laki moja unusu mwaka 2001 hadi milioni 10 kwa sasa. Kodi kwa Serikali kutokana na mawasiliano ya simu imefikia sh bilioni 660 katika miaka hiyo tisa iliyopita.
Kuhusu COSTECH, mkutano umekubaliana kuwa iko haja ya kuongeza bajeti ya kufanya tafiti mbali mbali nchini, bajeti ambayo kwa sasa ni ndogo, asilimia 0.3 ya Bajeti nzima ya Serikali ya kila mwaka.
--------------------------------------
Kwa habari za kutandikwa kwa Mkongo huo wa mawasiliano
NI UPETEVU WA MUDA WAO NA UPOTEVU WA PESA ZETU !! HAWA WATU MPAKA LINI WAENDELEE KULELEWA KAMA WATOTO WADOGO HUKU KILA SIKU HAYA MASHIRIKA YANAVURUNDA NA SERIKALI KUYAKINGIA KIFUA ??
ReplyDeleteKAMA MTAALAMU WA INTERIOR DESIGN NADHANI CARPET YA STATE HOUSE INA WALAKINI.KWA KAWAIDA INATAKIWA KUWA NA RANGI MOJA ISIYOIVA SANA HIYO ILIYOPO IMEIVA SANA NA IMECHORWA KWA RANGI ZILIZO NA MNGA'O MKALI NA HAIJAMECHI NA VITU VILIVYO HAPO NDANI.CARPET KAMA HILO LINGEPENDEZA VIZURI KAMA LIMEWEKWA JUMBANI KWA MTU AU HATA CHUMBANI LAKINI SI KWENYE UKUMBI WA MKUTANO.PIA VITI HIVYO VYA NJANO NI MAHSUSI KWA DINING ROOM NA WALA SI KWA AJILI YA MIKUTANO UKIANGALIA VITI HIVYO HAVINA CHAGA ZA KUEGEMEA KWA PANDE ZOTE MBILI TOFAUTI NA VITI VYA MIKUTANO.NAAMINI KAMA KUNA INTERIOR DESIGNER WA IKULU YA DAR ES SALAAM HAKUZINGATIA COLOUR KABISA NA VIFAA SAHIHI(VITI NA RANGI ZAKE) AU ALITUMIA TU UTASHI WAKE KATIKA KUCHAGUA.HIZO NI RANGI KALI SANA AMBAZO HAZIENDANI NA UKUMBI WENYEWE.
ReplyDeleteNamuunga mkono anon wa pili hapo juu. Mimi nilidhani ni dining room au restaurant kusoma habari nikakuta kumbe ni ukumbi wa mkutano.
ReplyDeleteNa mimi pia nimeona kama hivyo ni viti vya dining. Arm rests ni lazima ziwepo.
ReplyDeleteVile vile ile picha ya katikati haijakaa pima maji. Otherwise, rangi ya ukuta, carpet na lighting nazipa 110%
Naungana na namba moja kwamba huu ni upotevu mwingine wa pesa na muda usiokuwa na sababu. Hivi kwani raisi wetu toka lini amekuwa mtaalamu wa kudeal na issues specific za wizara kiasi hicho? Na huo muda uko wapi jamani? Wataalam si wapo wafanye hiyo watoe reports yeye achukuwe hatua that's all. Na kitu probably ndio inapelekea mawaziri kutofanya kazi zao. I was surprised raisi alipozungumzia issue ya Rates (TRL) aligusa issues ndogo za kizara ambazo mimi ningekuwa waziri ningeresign kwa kweli.
ReplyDeleteHii njia imeonekana kwamba haifai/haina matunda we keep on applying same thing hivi tunatarajia vitu tofauti? Kama ndivyo basi shida ni kubwa kuliko tunavyodhani.
Baada ya kutazama kapeti turudini kwenye mjadala. Ilikuwaje TTCL ikaanguka?
ReplyDeleteMkurugenzi wa mwisho TTCL kabla ya ubinasishwaji Ndugu Adela Mapunda yu hai na anaweza kutueleza nini kilitokea. Wajumbe wa Bodi Ya TTCL wakiwemo aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye sasa ni Makamu wa Mwenyekiti wa chama tawala, waliokuwa mawaziri wakuu Jaji Joseph Warioba na Dr Salim Ahmed Salim wanaweza kuchangia vizuri kwenye mchakato wa kuifufua TTCL.
Hivi nyie kwenda kuosha macho na kutoa ukungu huko MAJUU imekuwa shida kila kitu huku ni kibaya kibaya kila jambo huku kwenu ni baya baya lo1! tumewachoka, KWENDENI ZENU HUKO........!!! PAM BAVU ZENU.......!!!
ReplyDeleteHili wazo la kuyasaidia mashirika ya TTCL na POSTA ili yaweze kumudu ushindani na kurejea tena ulingoni katika biashara ni Wazo Jema na Zuri.Naliunga mkono bila shaka.Kinacho nitia wasiwasi hapa ni jinsi zoezi zima linavyofanyika.Linafanyika kienyeji mno bila ya Ridhaa ya Bunge.Najua sana kwamba hata kama Serikali ikisha pitisha maamuzi yake hapo katika Baraza la Mawaziri,Bunge letu halitakuwa na jingine la kufanya isipokuwa kuridhia tu.Lakini huu sio utaratibu sahihi.Serikali ilitakiwa ifanye Tathmini nzima ya masuala yake yote ambayo yatahitaji msukumo mpya wa pesa ili shughuli ziweze kurejea katika hali yake ya kawaida.Baada ya hapo,kwa pesa za ziada ambazo serikali itaomba(kwasababu serikali yenyewe haina pesa zake yenyewe,pesa zote ni za walipa kodi)serikali italazimika kuliarifu Bunge pesa hizo zitatokana na vyanzo vipi?Je,kodi za bidhaa na mapato zitaongezeka ili kuzipata fedha hizo au vipi?Na kama kodi zitaongezeka ,basi zitaongezeka kwa kiwango gani bila kuathiri maisha ya watu na walipa kodi kwa jumla?Hapo ndipo Bunge litakapo tafakari,iwapo kiwango cha kuondezeka kwa kodi kitakuwa kikubwa mno basi Bunge litashauri kiwango cha fedha kitakacho ombwa na serikali kipunguzwe au utazamwe uwezekano mwingine wa kutafuta mitaji kwa kuuza hisa au kukopa nje na kadhalika.Vile vile kama wenzetu Marekani na Uingereza na hakika duniani kote walivyofanya!Lakini siyo kienyeji namna hiyo kama sisi viongozi wetu walivyo jisahau na kuzoea kufanya.Wala hakuna tatizo lolote,ni utaratibu tu unaofaa na unatumika duniani kote.Tusirudie kosa la kumwamini yeyote yule kupita kiasi kwa ustawi wa maisha yetu,hata akiwa nani katika nchi hii!Lazima taratibu ziheshimiwe.Nitoe rai kwa nia njema kabisa kwamba ni vyema utaratibu huo ungeanza kutumiwa na serikali yetu kuanzia sasa ili kujenga imani na matumaini mema kwa watanzania wote ambao ndio walipa kodi wenyewe.Serikali isijitwishe mzigo wa kujiamulia mambo yenyewe "Kama vile ina pesa zake,na ilhali pesa hizo ni mali ya walipa kodi wenyewe".Huwezi kujiongezea kodi kiholela kama yalivyokuwa mazoea katika nchi yetu hii bila kutafuta ridhaa ya walipa kodi wenyewe.Kwa sababu maendeleo yanayo tafutwa ni yao wenyewe na wala si ya kulazimishwa na mtu mwingine!Nafikiri nime eleweka ndugu zanguni!papperazzi
ReplyDeleteHofu yangu, ni kuwa itafika 2015 watu bado wanatathmini tu! Sijui vitendo lini!
ReplyDeleteSi ajabu michuzi ukabana...
Huwa najiuliza wasomi waliosomeshwa na serikali na wenye elimu za juu bila kulipa hata senti moja wako wapi?
ReplyDeleteMaana haya mashirika ya umma kila siku yana matatizo lakini ukiangalia viongozi wake wamesoma elimu za juu na hata wengine wamesomeshwa ktk nchi za dunia ya kwanza(kila kukicha nondoziii)
Hivi roho zao haziwasuti na kuona angalau watumie elimu yao kuleta maendeleo ya makampuni na taifa kwa ujumla badala ya kuwaza kujinufaisha wao na familia zao tu.
Hivi kweli ndio usomi huo au wa kuuwa na kuuziana makampuni ya serikali.
Anon wa 18 Feb, 3.35pm nakuunga mkono.
ReplyDeleteNinahojiuliza na pengine wadau na pia Bwana Michuzi ni kuwa Bw JMK alisomea uchumi pale UD sasa sijui yeye ni wa mlengo upi Kynesian or Adam Smith??!!
Hii inaweza kutusaidia kuelewa misingi yake ya kifikra.
Mwalimu aliamini kwa nia nzuri tu kuwa Serikali imiliki na kuendesha njia kuu za uchumi mwishoni akakubali amefeli.
Alhaji Mwinyi na Bwana Mkapa walipokuja wakaona hapana tuuze makampuni yote kwa watu binafsi wakiamini Serikali isimiliki wala kufanya biashara. Nayo ilikuwa na nia nzuri lakini japo kumekuwa na mafanikio kidogo pia imelitia Taifa hasara kubwa kutokana na uuzaji holela, utathmini holela ambao haukujali kabisa maslahi ya Taifa.
Sasa Bwana JMK amekuja nae inaonekana yuko kati kuwa Serikali isimamie na kuendesha baadhi ya njia kuu za uchumi. Na tunakubali Nia ni nzuri tu, Lakini nae naamini atafeli kama wenzake.
Nasema atafeli kwa sababu kinachofanana kwa wote Wakuu wetu wanne ni kuwa kama waliomtangulia anafanya maamuzi kwa imani bila kuzingatia hulka na tabia halisi ya wanyama na pia misingi ya biashara.
Binadamu na wanyama wengine ni wabinafsi kabla ya yote. Tabia yao kuu ni uhai na usalama wao wenyewe, familia zao na mali zao. Ndio maana huwa ni wakali kujilinda kwa lolote ambalo linaweza kuathiri hayo.
Ukizingatia hilo basi unaweza kuelewa ni kwa nini Tamko La Rais toka Ikulu haliwezi kumfanya mkurugenzi wa kampuni fulani aache kujinufaisha yeye na familia yake eti akijali mlipa kodi aliyeko Nachingwea!! Nyerere na Ukali wake kama pilipili hilo lilimshinda sembuse Sembuse JMK!! Tamko la Rais sio kama "NA IWE USIKU NA MCHANA NA IKAWA HIVYO"
Baada ya muda mfupi ATC, TRL, NIC(ambayo nasikia imefungwa ikisubiri kufunguliwa upya???? sijui wateja nao wamefungwa!!)), POSTA, TTCL, BANDARI, NHC zote zitarudi tu serikalini na kikombe kuomba zisaidiwebaada ya muda si mrefu.
Jambo ambalo JMK na wenzake wanasahau ni kuwa pesa hizi zinazomwagwa huku si za SERIKALI bali ni zetu "WALIPA KODI".
Nia nzuri si msingi wa mafanikio.
Mtanzania
mhhhhh ivi mimi ninashindwa kuelewa kwamba hii TTCL SI IMEBINAFISISHWA KWA SASKATEL ,JE HAWA VIONGOZI WA SASKATEL WANAFANYA NINI HAPA NCHINI KWANI MPAKA KAMPUNI INAFADHILIWA NA KODI ZA WANANCHI,JE KWELI MUHESHIMIWA RAISI HUWA HAWA MAWAZIRI WAKO WANASOMA KWELI HII MIKATABA KABALA YA KUISAINI,MUHESHIMIWA JARIBU KUFILIA KUPANDISHA ,MAISHA YA WATANZANIA SIOO KUWABEBA WAZUNGU KWA KUWAPA MITAJI
ReplyDelete