
MWIMBAJI MAHIRI WA MSONDO NGOMA MUSIC BAND JOSEPH MAINA AMETUTOKA.
KIONGOZI WA BENDI HIYO MUHIDIN MAALIM GURUMO AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA MEREHEMU MAINA AMEFARIKI MILANGO YA SAA MBILI UNUSU ASUBUHI AKIWA NDANI YA DALADALA SEHEMU ZA TEMEKE MIKOROSHINI.
GURUMO ANASEMA MAINA ALIKUWA NJIANI KUELEKEA STUDIO SEHEMU ZA OSTABEI AMBAKO MSONDO NGOMA INAREKODI ALBAMU MPYA. NYIMBO NNE ZIKO TAYARI NA MBILI ZIMESALIA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDA KUTIA SAUTI.
GURUMO AMESEMA MIPANGO YA MAZISHI ITAJULIKANA BAADA YA NDUGU WA KARIBU WA MAREHEMU KUWASILI DAR. HIVI SASA MAITI YUKO HOSPITALI YA TEMEKE ALIKOPELEKWA MARA TU BAADA YA UMAITI KUMKUTA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
AMINA
Du, hakika nimesikitishwa sana na kifo cha Joseph Maina. Poleni sana wana-Msondo!
ReplyDeleteE! mola iweke roho a marehemu mahali pema peponi. Mwanadamu unajua utokako hujui uendako, laiti angelijua wala asingesubiri aingie ndani ya daladala, labda angekaa na familia yake nyumbani, ila binadamu hatujui hatma yetu. Ndio maana kuna umuhimu wa kujua kuna siku ya mwisho na inatokea wakati wowote na popote. Binadamu tukifikiria hayo hatutokuwa na chuki baina yetu na upendo ungezidi. Mungu amuweke mahala pema inshallah.
ReplyDeleteMdau Netherlands
poleni ndugu wa marehemu,ila hii habari ni ya aibu,eti mwanamziki amefika kwenye daladala.
ReplyDeleteSalm zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kwa wapenzi wote wa Msondo.tutamkumbuka marehemu kwa sauti yake maridhawa......
ReplyDeletemdau
Ugiriki
poleni sana familiya ya marehemu kwani ni kifo cha ghafla sana amefia kwenye basi akielekea kurekodi poleni sana bendi ya msondo kwa mstuko mliyoupata.
ReplyDeleteMungu ailaza roho ya marehemu mahali pema Ameni.
sweet
Arusha.
Mungu amuweke mahala pema peponi, Amina.
ReplyDeletemungu amlaze mahala pema peponi
ReplyDeletemwenyezi mungu ailaze roho yake pema peponi. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. POLENI WAFIWA
ReplyDeletemwenyezi mungu ailaze roho yake pema peponi. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. POLENI WAFIWA
ReplyDeletemwenyezi mungu ailaze roho yake pema peponi. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. POLENI WAFIWA
ReplyDeleteMungu amlaze mahala pema peponi,inasikitisha sana,kufia kwenye daladala!
ReplyDeleteWakongwe "Msondo Ngoma"na ndugu wa marehem Poleni sana kwa msiba huu mkubwa,tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko na majonzi makubwa,mwenyezi amlaze mahala pema peponi marehemu Mahina.
ReplyDeleteTumempenda lakini Mwenyezi mungu kampenda zaidi.
Poleni sana.
Kutoka
The Ngoma Africa band,Ujerumani
wee mdau kuna aibu gani mwanamuziki kufia kwenye daladala??ulitaka akafie wapi?ulaya???halafu tuanze kusumbuana michango huku...muone vile kichwa kidogoooo utasema mdoli...RIP JOHN MAINA MGOSI WA NDIMA
ReplyDeleteMwanga wa milele muangazie ee bwana..!
ReplyDeleteR.I.P. Maina. Pole kwa wasanii watanzania na wapenzi wote wa msondo ngoma.-
ReplyDeleteSozigwa, Espoo.
poleni sana watanzania wenzangu kumpoteza mtu muhimu sana katika fani ya mziki wenye usia mahili sana kwakweli itachukua sana muda kuziba pengo hili mie banafsi nipo ukerewe lakini hizi nyimbo sinanipa simazi kubwa sana l will miss msondo ngoma baba wa muziki roho ya marehemu iwekwe mahala pema peponi AMINA
ReplyDeletewe anon wa saa 4.05pm ndugu yangu unahitaji msaada wa kitaalam,kifo kina aibu,kwani kapanga afie wapi.....poleni wafiwa, mungu amlaze pema peponi...amin
ReplyDeleteNi habari za kusikitisha sana za kifo cha Jose. Ni mwanamuziki mahiri na hodari sana. Mimi binafsi ninatoa pole sana kwa wafiwa, Msondo Ngoma na wapenzi wote wa Msondo, hakika Jose atakumbukwa siku zote.
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya marehemu Joseph Maina mahala pema peponi, Amina.
Tatizo la Watanzania tunaulimbukeni kwamba kufanikiwa ni kutopanda daladala, mawazo ya anony-4.05 yanaeleza fikra zetu duni. Sehemu nyingine daladala ni usafiri unaoheshimika na wakati mwingine Maprofessor na viongozi wa siasa wanautumia. Watanzania tuna kasumba kiasi tumeshindwa kuboresha usafiri wa jamii kwa viongozi kukimbilia mashangingi na kila mwananchi sasa anaona kumiliki gari ndio mafanikio. Tubadilike la sivyo nchi inaangamia. RIP Joseph Maina, Mungu akulaze pema peponi Amina.
ReplyDeletePoleni sana Msondo,
ReplyDeleteNimestushwa sana na taarifa za kifo cha kaka Joseph Maina!Mungu awape amani chama lote la Msondo na mashabiki wake...mzee Gurumo pole sana.
Lakini nikiwa kama msanii ninayetegemea muziki kwa maisha yangu pia,inaniuma kusikia kwa msanii wa hadhi ya Maina na utumishi wake wa muda mrefu kwenye muziki na ukiangalia mazingira ambayo mauti yamemkuta no matter what...ni wazi inaonekana kuna haja ya serikali kusikiliza kilio cha wasanii na kuangalia haki zaidi na kuwawekea mikakati mingine ya 'welfare' kwa wasanii Tanzania.
Sio kama wasanii wote ni watu wa kuendekeza starehe na hawana mipango...wasichojua watu wengi hapa ni kuwa kisheria muziki sio kazi rasmi nchini Tanzania...na hii maana yake hatumo kwenye mfumo wa kiuchumi wa serikali!
Yaani maana yake hata kama mimi kama msanii kipato changu ni,let say laki tano kwa mwezi,still siwezi kupewa mkopo wa mabati kama anaopewa mwalimu au wafanyakazi wengine wanaopokea chini ya laki mbili kwa mwezi.na benki pia ni hivyo hivyo hatuwezi kupewa mkopo hata wa shilingi laki moja kwa mwaka,kwa sababu kazi yetu sio rasmi...haijarasmishwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania bado!
JAMANI NIMESIKITIKA SANA ILA NINA UCHUNGU SANA KWANI HUYU BABA NIMEANZA KUMJUA TOKA NIKIWA MTOTO KWELI AMAFIA KWENYE DALADALA? NIMEANZA KUMSIKIA NIKO KARUME
ReplyDeletePRIMARY MIAKA YA 90.NIMEENDA SECONDARI ZANAKI FORM 1,ANGWANI FORM 5,CHUO CHA BIASHARA C.B.E,MWAKA 2OO4 NIKAOLEWA, NIKAANZA KAZI SHIRIKA MOJA LA SERIKALI NIMEJENGA NYUMBA NINA WATOTO 2 NINA GARI KILIO CHANGU KWELI HUYU MTU MAINA ALIYENITANGULIA MAISHA ANAFIA KWENYE HIACE? OOOOOOOOOOOOOOO MOLA WEEEEEEEEEE hiiiii ni niniiiiiiii HEBU TUIMBE WIMBO HUU
kiliooo kilio
kiloooo kilio
kiliooo kilio
utamlilia nani
ebaba tusamehe
tumefanay makosaaa
tulizania muda bado
wakuja kutubuuuu
wazo kutubu kwa kujuta kuzaliwa
tanzania kweli hata kibajaji mtu unashindwa kumiliki? jk tusaidie
Nawapa pole sana familia ya marehemu Maina, bendi nzima ya msondo bila kuwasahau wapenzi wote wa msondo ngoma dunia nzima. R.I.P. Maina; - Ben wa Segerea
ReplyDeleteR.I.P Maina
ReplyDeleteMchango wako na kazi yako nzuri itakumbukwa daima, ulikuwa mstari wa mbele kuliendeleza jahazi la na muziki Tanzania utakumbukwa kwa umahiri wako ktk kuimba, uchangamfu na nyimbo zenye maadili na mafundisho kwa kila rika Mungu aiweke roho yako mahali pema
kwani jamani ni vibaya kufia kwenye daladala? mlitaka afie kweney RANGE ROVER
ReplyDeleteWatanzania tumezidi fikira potofu eti kafia kwenye daladala ni aibu. Kifo kina aibu kwani kufa kwenye gari yako kwa ajali au kwenye daladala mwisho wake ni nini? siku ikifika hatu gesti unaweza kufa au hata kwenye choo cha kulipia na umepaki shangingi lako nje. Unachotakiwa ni kujiandaa muda wowote na kila mtu anakipaumbele chake wengine hawanunui gari kwenye nyumba za kupanga hadi ajenge na gari ni kitu cha mwisho. Mwingine hata kama kapanda tandale kwa tumbo ana RAV 4 new model au mnadharau madaladala kwa ajili mna vimikopo vya magari ofisini kwenu. Tuache dharau na tumuombee marehemu apumzike kwa amani.
ReplyDeleteYaani juzi jumapili nimemuona akiimba kwenye TV nikawa naulizia hivi huyu yupo hai au kafa?? Nikajibiwa na mdogo wangu kwamba ye yupo hai - basi nikamwambia mdogo wangu kuwa jumapili ijayo ntaenda kuwaangalia hapo AfriCentre. Jana mchana nasoma taarifa kwenye blog kafa uwiiiiiiiiiiiii. Kwa kweli inasikitisha mno na ni kifo cha ghafla - Wapenzi wa Msondo POLENI SANA - na pia wasanii wenzake haswa wa msondo Mungu awape nguvu maana ni ngumu kuamini kwa kweli. Ukiona hivi - kwa kweli unatakiwa kujiandaa kabisa - wote njia hio ila hatujui siku wala saa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
ReplyDeletenyie acheni uongo bwana mtu unazaliwa,unaenda shule, baada ya yote hayo unafanya shuhuli yoyote ya halali inayo kupatia riziki iwe ajira ya kudumu au binafsi.ok nini matokeo ya kazi ni maisha bora.maisha bora ki vipi? ni pamoja na malazi nk hata gari liko included mimi naona uniambie MUZIKI WA BONGO HAULIPI.mbona michuzi nimemjua toka nikiwa zanaki sec alikuwa akija kupiga picha umiseta lakini siwezi kumfikia kiwango cha maisha bora because aliisha anza maisha longtime swali huyu maina hadi kufia kwenye daladala MUZIKI ULIKUWA HAULIPI?
ReplyDeleteMaskini katika pitapita za mitandaoni nimeona picha picha ya marehemu ndani ya daladala watu wanamwangalia, kutokana na maelezo yaliyomo ni kwamba marehemu alikaa ndani ya daladala hilo alilofia kwa takribani ya lisaa limoja. Yani nashindwa kuelewa kwanini watu walishindwa hata kufunika uso wake. Walimwacha wazi saa zima watu wanamwangalia anavyoningĂnia upande mmoja. Yani inasikitisha sana. Yuko kule kwa mzee wa sumo. Innalillah wainnailaih rajiuun
ReplyDeleteMdau Netherlands
Na wewe anon wa February 18, 2009 8:14 AM; unajitia umefanikiwa sana kwa kuwa una nyumba na gari.Kwanza aliyekwambia Jose hakuwa na nyumba ninani? au aliyekwambia kupanda daladala maana yake ni kutokuwa na gari au kutofanikiwa maisha ni nani?.Huo ni ulimbukeni tu.Kwanza hiyogari yenyewe uliyonayo inanuka rushwa tu.Ndio maana waswahili husema "masikini akipata matako hulia mbwata..mbwata". Sasa kama kweli wewe unathamini maisha ya wasanii wetu, tangu uanze kumsikia Maina umeshanunua cd au walau cassetes ngapi za msondo? au hata msanii yeyote wa Tanzania? kama sio kujifaragua na kujishebedua huko huko, haluuu....lioneni kwanza macho yake,kama kingwendu amekwamwa na tonge la ugari wa moto vile!!.kazi ku-dowload nyimbo za watu kwenye internet tu.Ndio maana jike dume we!!.Pole kama nimekutusi. RIP Joseph Maina, tutakukumbuka kwa Uimbaji wako.
ReplyDeleteMdau
mwenye hasira
Kuna NUTA ndani ya Msondo?
ReplyDeletePoleni sana tena sana Wana Msondo!Rambirambi ziwafikie ndugu,jamaa na marafiki wote wa marehemu mkoani Tanga na popote pale walipo.Tuko nanyi kwa majonzi makubwa katika kipindi hichi kigumu cha msiba.Kazi ya Mungu japo ina machungu!Mchango wa Maina utakumbukwa na wapenzi wote wa muziki wa dansi nchini Tanzania daima milele.Uhai hauwezi kulinganishwa na thamani yeyote ile ya pesa!Kututoka kwako wewe Maina,ndugu yetu,bila ya kwaheri,imetuacha wakiwa vilivyo!Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,amina!
ReplyDeletewabongo bwana kweli vichekesho,ukienda bongo hata ni week2 wanakuuliza mbona umetoka majuu hujaja hata na gari ya kutanulia??wengine watakusema umechoka baadae miongoni mwao haohao watakuja kukupiga mzinga kisa umetoka majuu,hivi tukisema walioko majuu na walioko bongo tusiwe tunaombana hela ni wapi watakaoumia???mtu anakwambia anatesa ana gari ya kutanulia bongo choo anachojisaidia kimejaa umeme wake wa luku kaichokonoa mita iende polepole,joto lile la bongo bado anajipulizia pafyum feki za china basi si kikwapa hicho hehehe kama huyo dada hapo anaedai kayapatia maisha mi nikifika bongo hao ndio nawageuza vimada wng kwa kunibabaikia kwao natumia hivyo vigari vyao vya mtumba dubai kwavile wanataka kuwakoga wenzao wana bwana katoka majuu kumbe na mie nawakomesha siku zng zikikaribia hata siwaagi nakula pipa lng shaaaaaa kwenye kona nalala na speed 120
ReplyDelete