Ndugu,Jamaa na Marafiki, Tunasikitika kuwajulisha ya kuwa Mzee Leonard NJ Merere ambaye pia ni baba mzazi wa ndugu zetu Naomi na Jacob[JJ] Merere wa Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumanne [Feb 10th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.
Marehemu alikuwa na umri wa miaka 73, ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu wanne.
Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa watoto wake huko Boston-Masachusetts.
Kila mmoja wetu anaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi. Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili, Jeneza pamoja na ticket ya atakayekwenda pamoja na mwili ni dola elfu ishirini[$.20,000].
Ni mzigo mkubwa sana ambao kila mmoja wetu anombwa kusadia ili kukamilisha shughuli hii hasa ukizingatia ya kuwa kwa kadri mwili unavyokaa funeral-home ndio gharama zinavyozidi kuongezeka.Mwili utasafirishwa punde zitakapopatikana fedha za kulipia gharama.
Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:
NAOMI MERERE
BANK OF AMERICA,
ROUTE NUMBER :011000138
ACCOUNT NUMBER:009441233628
Au kwa adress hii:
Jacob & Anna Merere
510 Skylinedrive suite # 11Dracut,
MA 01826.
Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:
Jacob & Anna Merere [JJ]-978-726-2227 au 978-957-2153.
Naomi Merere-978-413-3722 au 978-632-9823.
Juma Malika-781-244-7353
Saimon Twalipo-978-423-1192
Pastor Abisalom Nasua-214-554-7381
Email-Adress:- RambiRambi@Yahoo.com
Tafadhali chukua muda kuwafariji wafiwa na kuwaombea
Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa kuwasaidia familia Merere !
Mbarikiwe,
Mch.Abisalum Nasua,
Mollel,
Jackson
Kwa Niaba ya Marafiki wa Familia ya Merere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani familia ya mzee merere poleni sana. Mungu awe nawe wakati huu mgumi, na awasaidie kwenye mipango ya kumsafirisha mzee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...