Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana , Profesa Manorisi Meshack (kulia Kwake) kutembelea Chuo hicho Mjini Dodoma leo. Shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Ooh Lovely Mazengo (complex)! Naona wanapita juu ya mto (wa masika tu) unaotenganisha mabweni na madarasa 9 a.k.a ng'ambo, kwa nyuma naona jengo maarafu la maabara, 3rd floor Physics, 2nd floor Biology, ground floor Chemistry. Hapo wanaelekea pale Sick bay (zahanati ya shule), then Kulia kutakua na Azimio (kwa Kameme) kushoto Mwenge (kwa Mdushi), watakuta uwazi then kulia tena Muongozo (kwa Sichone) Kushoto Muungano (kwa ishengoma)na mbele kabisa Ujamaa a.k.a soweto (kwa Mwamfupe a.k.a Unyamaunyuma). baada ya Ujamaa ni Toilets (a.k.a beach) , basket ball court, mabwawa manne , mabanda ya nguruwe na ng'ombe. Na pembeni ya Azimio na Muongozo ni Bwalo, jiko, mashine, mabafu.

    Naikumbuka shule yangu ;

    Ngoja niimbe kidogo,

    Complex complex, mazengo pressure!

    Maazengo! shule yetu,
    twaipenda sana,
    twaitakia barakaa!
    fanaka na heri,uzima amani,
    maisha mema, maanayo yafuraha,

    Tuijende shule yetu kwa juhudi nyingi,
    Tuinue shule yetu kwa maarifa tele,
    twende mbele kwa pamoja kwa umoja wetu elimu ni mwanga!

    Mdau Kiwoso UK

    ReplyDelete
  2. Hahahahahha..... Duuuuuu, Ebwana Kiwoso umenifurahisha sana....Yaani umenikumbusha vitu ambavyo sikutegemea kabisa....

    Sema umesahau kidogo, walikotokea kushoto kidogo mwa maabara, kuna church, then nyuma tena ya church kuna ukumbi maalum, ambao ndo tulikuwa tunawavuta watoto wa msalato, unakumbuka hiyo?

    Halafu kingine sasa umesahau maticha walivyokuwa wanawakurupusha watu monie monie, ma usafi na vitu kama hivyo, tena unyama ndo alikuwa na kiherehere sana cha kukurupusha watu '5'oclock in the morning' na fimbo, utafikiri nguruwe bwana!!!

    Umenikumbusha mbali sana kunikumbusha jina la Beach 'kule msalani'...sema tatizo tena ukasahau SUDAN, wazeiya walipokuwa wanaenda kufanya mapumziko kama siku hiyo wanaona class miyayusho, na kula nyasi, ila MSASA akiwakuta sasa 'HeadMaster wa kipindi hicho' ndo balaa...

    Ebwana Wu-zengo complex haitakaa itokee tena...nadhani wajanja wote wa east zoo wanalitambua hilo.

    Ni hayo tu, ila shukrani kwa kukumbushia tathmini..

    Mdau SAMCHOM In the Mixx

    ReplyDelete
  3. Hiyo inanikumbusha da'COMPLEX CAMP na hapo wanatokea ng'ambo enzi za Mr. Makunja, Mr. Mgalula, Kipatiko na wengineo...
    Mshkaji wa UK wewe ni Hanania?
    MN

    ReplyDelete
  4. kiwoso....
    duh..sikukumbuki ila umenikumbusha mbali sana ..haswa unyama unyama..au undava undava..
    duh..complex ya chitinde..complex ya professor muna ..complex ya netanyahu...unamkumbuka yule second master kipindi cha Mnasa??

    Duh..kweli siku zinapita! michuzi kweli hii blog kiboko!
    mdau -uk

    ReplyDelete
  5. hivi yule mzungu wa hesabu mr.pierce nasikia alirudi kwao.

    mzee alikua anazijua namba kiasi kwamba ukimpa tan anakupa arc tan.

    lakini mazengo ilikuwa shule mbaya sana. chakula kibaya, mbu ndiyo usiseme, maji hakuna, magonjwa kibao.

    mazengo kuna msimu wa malaria, halafu kuna msimu wa kuhara damu ambapo ukienda chooni unakuta baadhi ya vyoo vimetapakaa damu.

    i was planning kutengeza documentary ya vyoo vya mazengo.

    ReplyDelete
  6. I really hate Kaunda suit. Yaani piga ua buruza haunivalishi huo upuuzi.

    ReplyDelete
  7. lol...Kiwoso, 2nd Master wa kipindi cha msasa alikuwa Magere, umemsahau? full unoko jamaa.. Inanikumbusha jamaa alikuwa anaitwa Bissa Masoud, jamaa alikuwa anapenda sana kumuigiza Magere...

    Chomolla, Amerika

    ReplyDelete
  8. Safi sana kutukumbusha Michuzi. Nilikuwa A Level pale 88-90. Namkumbuka mwalimu wangu wa namba Miss Anna (from US) na mwalimu wa Geography Mr Sanga ("People are going to uniform without town! I need only one of them"). Mwalimu wa Physics alikuwa ni mkali mmoja anaitwa Nyanda (alienda Atomic Commision eventually)

    Ulinzi wa mtu ulikuwa ni mtu mwenyewe... madenti tulikuwa tunapangwa guard kikweli kweli na tulikuwa tunakitu kinaitwa Awamu - mnabaki shule likizo ya mwezi wa sita kulinda. Awamu ilikuwa inafaida zake kwani tulikuwa tunahost Umiseta na kupata fursa ya ku make new friends siyo.

    Lakini top ilikuwa ni ile special relationship kati ya Mazengo na Msalato (aka Six). Huu uhusiano ni kama ule uliopo kati ya US na UK - solid as a rock.

    ReplyDelete
  9. Ile shule ilikuwa nzuri mno. Nilipokuwa nasoma pale mashetani yangu yalikuwa yananiambia kuwa kuna siku tu atatokea mtu aibadilishe kuwa chuo fulani. I was right it seems.

    ReplyDelete
  10. Du ! Mazengo shule yangu, yaani hii picha imenikumbusha mbali sana, hilo ni daraja lililokuwa linatenganisha domitories area na academic area, da safi sana

    ReplyDelete
  11. Duh, wazee hii picha na hizo comments zanikumbusha mbali sana. Nilikuwa pale mwaka 96 hadi 98 A level, nakumbuka enzi hizo Headmaster ni Msasa na Second Magere, walimu wetu kina Makunja, Mgalula na kina Muna.

    Vijiwe vya kina Ngwea na Mez B, enzi hizo na Kina Makalla...duh, ebwana eh, tumetoka mbali.

    Mdau wa PGM 98

    ReplyDelete
  12. Kiwoso tena hapa,

    Wadau sikusahau wala kukosea, lengo langu ilikuwa ni kuchokoza kumbu kumbu zenu. Kuna walioniulizia Headmaster Msasa, huyo simfahamu, mimi nilikuwepo enzi za Mzee Sylivester Mkoba (kati ma-head ninaowakubali school mgt ilikuwa juuu) 2nd master Mkwizu ( mnakumbuka ile so yake),Academic master Mr Mwinuka, waalimu wengine maarufu ni kama Kuntu ( alihamishiwa ukaguzi), Mr Muna (biology a-level), Mr Peter (mu-UK wa Adv Maths, Add Math), Mr & Mrs 'Horoksi'(wa Australia) wa physics n biology, Mr.Takashi Jinguji - Survey o-level, Mr. 'Kifutu' (mu haya) Mr Katunzi, Chaula.

    Pia nawakumbuka viongozi wa wanafunzi kama
    HP Andrew (where r u?) vice wake ni jamaa mmoja Jaluo,
    Kaitaba - mambo ya msosi ( nasikia alienda JWTZ,
    Nzohumpa -kada wa chama (ccm)
    Kisembe -kwa soka beki 5- nasikia alifika ligi daraja la 1
    Andrew Pala -kwa soka winger/striker
    Shimimana Alfred (Shima)- beki 5 - Singida Untd, Sigara, etc
    Otto Maufi - very mascular - nimsikia hivi majuzi kwa kufanya fujo kwenye soka,
    Omari Mumboka - soka na maneno - Moro
    Msudani - huyu ni kati beki bora enzi zetu,

    na wengine wengi bila kumsahau Theobaldi machapati,

    simon Kitururu mbona sikuoni kuchangia? unakumbuka msazengo? na ile soo ya kwenda kuwachukua Kondoa girls? ilikuwa bado kigogo ndoa yetu na msazengo invunjike,

    Mdau Kiwoso UK.

    ReplyDelete
  13. Michuzi, hii photo inanikumbusha wakati nasoma Mazengo A level 2000-2002, hiko kipanda hapo nyuma ya waheshimiwa ni choo, tulikijenga wanafunzi wenyewe tukiongozwa na wenzetu wa civil o level ilikuwa technical school, sitasahau jinsi tulivyokuwa na zamu za kulinda usiku, kuchunga ng'ombe, kukata kuni nakadhalika, kweli ilikuwa complex,

    Nayaona majani kwa chini, msimu wa mvua desemba, hivyo Dodoma ni kijani tupu na mbu wengi sanaaa, lakini baada ya april ni kukavu ile mbala, mafuta ya kupaka inabidi ujipake bafuni kabla ya maji kukauka mwilini kwani ukitoka bafuni tu mwili mkavu na haushiki mafuta.

    Big up michuzi kwa hii photo

    ReplyDelete
  14. Michuzi tundika na picha Pugu Secondary a.k.a Mwakanga Secondary

    Mdau PCM 1985-1987 Houston

    ReplyDelete
  15. aaahhh! Braza Mithupu sorry namaanisha braza Michuzi sasa umefika pabaya, mambo ya kutukumbusha Mazengo kwa mtindo huu inatuumiza sana roho. Wote tuliopita Mazengo hatukutaka kuondoka hapo. Mbona Mazengo ilikuwa ni second home pale Dom,
    Wazeiya Mnamkumbuka Mr Shirima alivyotushindwa watoto wa kiume akataka eti Watoto wa Kike wasome na sisi ili apate unafuu wa kutawala badala ya Kuongoza?
    Mnakumbuka tishio kuuawa la alilopewa Mr Msasa baada ya kuvuka mipaka yake ya uongozi na kuanza kufuatia "non-of-your bussiness"?
    Mnakumbuka Mama Kabota, Mama Muna na half cake za pale mtaani? Namaanisha bajeti ya TZS 200/= Unapata kitafunwa cha wiki mzima?

    Kiwoso, mnakumbuka mambo ya kikuyu?
    Nataka kucheka, machozi tu ndio yanatoka!!!!
    Mazengo tutaukumbuka daima, walimu wako wanoko kina Magere, Msasa, has Tete, Muna , Kabota siwezi Kumsahau unyamaunyama na mke wake bonge la kitu watabaki akilini mwetu kwa kipindi kirefu sana kijacho.

    Wana chemba wa Ujamaa tayari wanateleza moto wa Mazengo.
    Keep it up brothers and sister ya mazengo complex always unit make Unity.
    Woza mazengo now mnaita St nini??
    Mdau-Ex Mazengo May 1997

    ReplyDelete
  16. Jamani nilikuwa Mazengo O-level 1992-1995 nimekaa room 4 up muungano.
    Nawatafuta washikaji kama Bagabuje Joseph, Deogratias Elisha, Musa Joseph, Siwajibu Mwendwa, Bruno Kilatu, Godfrey Kazana, Peter Nkoi, Mlagala Mlungu,Geofrey Mbata, Tumaini Mbano, Mohamed Salehe(Msukuma wa kiarabu)Darasa langu ilikuwa ni electrical mkondo E. Nilikuwa nachukua Auto Electrics
    Jina langu ni Bethuel na contact ni bm_k7@yahoo.co.uk
    Mdau UK

    ReplyDelete
  17. Niungane na wenzangu tuliosoma shule hii kubwa wakati huo tukiita The greatest High School in east and central Africa). Mliosoma hapo A-Level 1979-81 mpo? Mnawakumbuka H/Master Aseri, Second Master Kirimbai (ung'eng'e mpaka asubuhi baadaye alikwenda Baraza la Michezo la Taifa), waalimu wetu Bategereza, Mlaponi, Peeres, Mathew na mpishi wetu Chonya? Wakongwe John SSita, Maduhu Ngalula, Salum Kungulilo, Honest Temu, Frank Raymond mpo wapi? Mbarikiwe
    Mdau Elias

    ReplyDelete
  18. Kamwe siwezi kuruhusu hili, yaani Mazengo Complex ipite bila hata ya ku-comment?? Hii ni kwa wale waliopitia Mazengo miaka ya 1996-1998!!! hasa wale walioishi bweni la Ujamaa "white house" Je mnakumbuka urinals???weekend inspection?? milio ya fisi usiku?? misemo kama kuanika utumbo?? polluter?? kunyukwa??Mang'atio?? wazee wa kiama (Rombo line)wadau kama babu Ema..., marehemu kipanya.., Maganga.. Hums de pum (mzee wa sinsenyo sinsenyo).. Nemes Massawe..(mshkaji!!) joseph mushi, vincent Mwakatobe... ema pompi du.Max..Mayson.. na wengineo wengi, kweli siku hazigandi...
    Ze mdau ..

    ReplyDelete
  19. kweli wana complex mpo..huyo mdau wa 1997 ni nani? mimi maganga...tuwasiliane kaka...

    ReplyDelete
  20. mdau wa UK, kweli umenikumbusha enzi ya Chitindinde na Kumtafutafuna mpiznai wake huko kwao Bahi,aaaiiiiiiiiiissseeee!!! sio mchezo
    memory za mazengo zote ziko tyt sana.
    woza complex,woza mazengo,woozzaa!!
    Mdau ExMazengo May 97

    ReplyDelete
  21. NILIKUWEPO HAPO 1983/84 - 1984/83 A-LEVEL EGM HEAD MASTER MKOBA, SECOND MASTER MSASA, PEARCE MWALIMU WA NAMBA, ALIRUDI KWAO AUSTRALIA ALIFARIKI, KIRIMBAI NI MCHAGGA HUYU ALISOMEA U.S.A. MLAPONI, MWALIMU MMOJA HIVI ALIKUWA NA MABINTI WAKE NJIA YA KUELEKEA MJINI, NI MNYAKYUSA - NDILE (MWAKALINDILE), MWALIMU MWAKYEMBE, BEATLES MMJOA HIVI WA UFUNDI, MWALIMU MMOJA HIVI ALIKUWA MPENDA MPIRA SANA, MISS CHONYA WA GEOGRAPHY, SANGA WA GEOGRAPHY PIA NILIKUTANA NAYE IRINGA ALIKUWA HEAD MASTER WA SHULE MOJA HUKO LUDEWA, MSASA NILIKUTANA NAYE SONGEA ALIKUWA HEADMASTER HUKU MTWARA, MKANGWA WA PHYSICS, NYANDA NAKUMBUKA SANA TAABU YA CHAKULA ENZI ZILE TUNAKULA DONA LA NJANO NA MAHRGE KAMA MAWE, NILIKUWA NAKAA AZIMIO, MNAKUMBUKA KIBARIDI CHA DODOMA NA VUMBI, TULIKUWA TUNAOGOPA KWENDA NG'MBO PREP USIKU KUWA ETI KUA JINI. KAKA MKUU WETU WA SHULE ALIFUKUZWA SHULE KWA KUKUTWA NA BINTI WAKIFANYA VITU VYAO ALIKUWA WA MBEYA AMBYE TULITOKEA WOTE MZUMBE SECONDARY. NAIKUBUKA SANA SHULE YANGU. MR KIWOSO NI KIWOSO GANI ULIKUWA PALE LINI? MKOBA ALISHAFARIKI.
    MNAKUBUKA KULINDA USIKU, NA KUBAKI WENGINE WEKIENDA LIKIZO.

    NI MIMI MDAU WA UNITED KINGDOM

    ReplyDelete
  22. e bwana dah! umenikumbusha enzi zile kitambo, nimesoma pale 97 hadi 2000. nayamisi sana mabwen yetu ya ujamaa kwa tembo, muungano ,mwongozo, azimio kwa baba askofu. masela wa east zoo mpo wapi? form one enzi zile wanaitwa nyoya na palikuwa na mapigo ya chaga, cable, kumwagiwa mkojo uliochanganywa na kinyesi(jina lake limenitoka kidogo) kwa kile kilichoitwa kukatwa mkia! mnakumbuka siku moja tupo paredi tena wakati wa inspection mara kundi la nyuki likapita na cha kushangaza zaid msela wangu Jumbu Msuka(mlemavu anatembelea magongo) akawa wa kwanza kwa kasi ya kukimbia? Masela wangu wa stoo ujamaa chiwanga, chilongan, imani sanga (camera man), obadia, masamalo pamoja na njelekela ngiliule(mzee wa kulala sita kamili na kufufuka sita na dkk 20) bigup ma skul mate wangu, nawamis sana. mi sebastian joseph (katibu wa bweni la ujamaa enzi zileeee! za tembo) tuwasiliane mazee, email yangu ni hii hapa; sebamaige@yahoo.com

    ReplyDelete
  23. jamani! nimesoma msalato looking for Nemes Massawe a very good friend of mine if u read this Neme can u find ur time to email me on nnifer2002@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...