Majeruhi akiwa Hospital kwa matibabu.

Watu zaidi ya 100 wameteketea hadi kufa nchini Kenya baada ya Lori la mafuta lililoanguka kuwaka moto na kulipuka.


Taarifa zinasema moto huo ulizuka baada ya mamia ya watu kukusanyika kuzoa mafuta yaliyomwagika. Watu wapatao 200 pia wamejeruhiwa kwenye moto huo katika mji wa Molo , mkoani Rift Valley, na maafisa wanasema idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.


Ajali kama hii iliwahi kutokea miaka ya 90 huko Kijijini Idweli Mbeya na kupoteza maisha ya watu wengi, Gonga hapa usome zaidi


/2004/06/000000_dirayadunia.shtml

Na Mdau Spotistarehe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Aisee Michuzi naomba nikusahihishe kuhusu mafaa ya Idweli yalitokea mwanzoni mwaka 2000 na sio miaka ya 1990 uliyoandika kwenye blog yetu ya jamii

    ReplyDelete
  2. kwanza kabisa tuwape pole wenzetu.

    pili nimefajaribu kufuatilia habari hiyo, na inaonekana tatizo lilitokea baada ya askari waliofika kwenye eneo la ajali kwa ajili ya kutoa ulinzi kuanza kutoza watu Ksh 50-100 ili wawaruhusu kuchota mafuta. ndipo walipoanza kulaumu na mmoja wa wananchi kuwasha kiberiti na boom! watu 100+ wamekufa....

    tatu, serikali ya kenya imejitahidi katika kutoa msaada na kutibu majeruhi. jeshi (national guard) walienda kuokoa, helikopta zimetumika kusafirisha majeruhi kwenda hospitali mbalimbali na serikali nzima (ambayo inaumwa "political constipation" kwa sasa) imetoa support katika hili swala.

    nne naomba kukumbushwa,idweli tulifanyaje katika hili?

    ReplyDelete
  3. bwana michuzi asante sana kwa kuleta hii habari hapa kwenye blog yako. nina wapa pole sana watu wote walio patwa ni hili janga. ingelikua vizuri magazeti yaweke hii habari kwenye first page za magazeti yao ili watu wengi waweze kujua kwamba kuchota mafuta ya taa au ya gari wakati yamemwagika ni hatari sana. watu wengi wamekua wakikimbilia magari ya mafuta yakipata ajali na kuchota mafuta bila ya kujua kuwa wanaatarisha maisha yao. hata kama kukiwa hakuna mtu anavuta sigara mlipuko unaweza kutokea kwasababu mara nyingi engine ya gari itakua na joto lingi na inaweza kuanzisha moto. pipe zikivunjika na kutoa hot steam inaweza kuanzisha moto. watu wakiwa wamebeba makopo ya chuma yakaanguka kwenye barabara ya lami yakaanzisha spikes na mafuta yakagusa hapo moto unaweza kuanza. jamani hili ni jambo la hatari na inafaa watu waanze kufundishwa madhara yake. tunaweza kuanzia vijijini hata mashuleni. tusipuuze hili jambo linaweza kutokea kwetu. tunaweza kutumia radio ili kuwaelimisha wananchi. tusingojee accident kama hii kutokea ndio tuanze kulaumiana. MICHUZI ASANTE SANA.

    ReplyDelete
  4. Mdau uliyetaka kujua Idweli kulifanyaje?
    Idweli huko Mbeya Lori la mafuta lilianguka na wananchi walikimbilia kuchota mafuta hayo inasemekana wanakijiji walimwaga maji kwenye Vyum=ngu na masufuria hadi Vikombe kuhifadhi mafuta baadaye baada ya kujaza kila chombo mmoja wa vijana alijaribu kiba Battery toka kwenye gari ile na ndipo msuguano wakati wa kukata nyaya za Battery ukatokea cheche za umeme wa BAttery na kuwasha moto na watu kibao walipoteza maisha...
    Mdau Spoti na Starehe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...