mzee mzima habibu jeff
juma choka huwa hachoki
mkongwe wa tumba ali jamwaka
unapotamka mpira kwa bongo ni simba na yanga. kwenye muziki wa dansi ni sikinde na msondo, ambao ndio nguzo ya muziki nchini. hapa niko na super stereo hassan rehani bitchuka. toka shirika la maendeleo la dar (ddc) kuachana na mlimani park orchestra bendi hii hivi sasa imepiga hatua za haraka haraka na kuboresha tija kwa kile wenyewe wanachokiita kuwa na uhuru kamili wa kujiamulia mambo wakiwa bendi inayojitegemea. muziki wao umekomaa sana na wapenzi wanazidi kuipenda nginde nginde
vinara wa sikinde ngoma ya ukae shaaban dede (shoto) na hassan rehani bitchuka 'super stereo'
mkongwe joseph bernard akiendeleza libeneke la sikinde bila matatizo. wapenzi wa marijani rajabu watamkumbuka nguli huyu ambaye alikuwa dar interntional enzi za super bomboka 
wakongwe wa kupuliza midomo ya bata mzee mbaraka (shoto) na hamisi milambo
karama regesu na abdallah hemba hawana mshindani kwenye masauti
safu ya ushambuliaji kuna yasini, sanga na abdallah hemba. 

mtu mzima ramadhani mapesa anakul rizim
bob ngosha anapiga bezi kama hana akili nzuri. hata kanda bongoman anamtumiaga akifanya shoo zake afrika mashariki
anko tony katika bezi. huyu alikuwa mwanzilishi wa bendi ya segere orijino sasa yuko nginde nginde
mjusi shemboza anapiga magitaa yote bila shida. hapa anakula bezi

hivi sasa mlimani park orchestra ni bendi inayojitegemea ikiwa chini ya meneja wake juma mbizo. kwa mawasiliano nao  piga namba +255 715 276 358

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Kiongozi Wa Albino, MbeyaMarch 29, 2009

    MHESHIMIWA HEBU TUWEKE SAWA KUHUSU SUALA LA CHENGE LIMEFIKIA WAPI??
    AU NDIO MAITI HAINA SHERIA???????????

    ReplyDelete
  2. Labda hicho chumba hawajakosea... si choo bali ni tangazo la GENTS wa kukodiwa...

    ReplyDelete
  3. HATA WEWE MWANDISHI UMECHEMKA. "UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE HALL??!!" ACHA KUTUKANGANYA BWANA. HAKUNA ALIYE PERFECT. HAHAAAA

    ReplyDelete
  4. herufi "i" imedondoka

    ReplyDelete
  5. Ah! Wahuni washaiba "I"!

    ReplyDelete
  6. hahaha...hilarious

    ReplyDelete
  7. JON MASHAKA KAZI KWAKO HAPO, ANDIKA ATIKO

    ReplyDelete
  8. Inaonekana hiyo herufi 'I' imedondoka. Maana nafasi yake inaonekana ipo hapo

    ReplyDelete
  9. LUGHA ILIVYOCHAFUKA!
    Lugha yetu Kiswahili, kwa sasa imechafuka,
    Nimefanya usaili, maneno yalofumuka,
    Nitaanza ya awali, ambayo yanatumika,
    Kwa sasa imechafuka, lugha yetu Kiswahili.

    Sasa anaitwa `demu’, msichana kaumbika,
    Nani wa kumlaumu, Kiswahili kufutika?
    Mchawi kumtuhumu, wa `busara’ hutumika,
    Kiswahili chafutika, lugha imekuwa ngumu.

    “Mambo poa mshikaji’, hapo mtu kaitika,
    Ndugu zangu tutaraji, Kiswahili kutoweka,
    Ako mfatiliaji, sawasawa kukiweka,
    Kwa sasa imechafuka, lugha yaenda na maji.

    Na neno `chelae pina’, lingine ni `kushoboka’,
    Wabomoaji vijana, hao ndio wahusika,
    `Kapiga chini’ kimwana, eti ndio kaachika!
    Kwa sasa imechafuka, kwa marefu na mapana.

    Ameisaini `vocha’, anasema `kaanguka’,
    Kiswahili chajificha, lugha sasa kuropoka!
    Wasema muuza `bucha’, mke hasiyetosheka,
    Lugha imeshachafuka, Kiswahili chajificha.


    Malenga Mngoni
    TTPL, Morogoro.

    ReplyDelete
  10. Ann, hapo juu , KUKODI SIO LET WALA LENT NI RENT. Au ulikuwa na maana ye LEASE?..Mhhh lugha za watu hizi.
    Mimi nadhani i imedondoka au kufutika.

    ReplyDelete
  11. NENDA KWENYE KAUNTA YA ANFIELD YA MUCHACHO UKASOME NENO WELCOME LILIVYOANDIKWA.

    ReplyDelete
  12. CHUMBA HIKI NI KWA AJILI YA WANAWAKE WANAOHITAJI KUKODISHA MIDUME BAADA YA KUJIKUTA WAPWEKE UKUMBINI, NI SAWA TU HAKUNA KOSA.

    ReplyDelete
  13. Hapo wahuni wameenda kukojoa toiletini wakaiba ile "I" kwenye TOILET. Hapo si mwandishi aliyechemka mkuu

    ReplyDelete
  14. anony March 30, 2009 7:29 AM, kiingereza kina maneno mengi. mtake radhi deogratias.

    ReplyDelete
  15. Hapo hapajakosewa kitu wala herufi kuibiwa hapo, kwasababu ni tangu walipo-upgrade ADJH(AGAKHAN DIAMOND JUBILEE HALL)hayo maneno yalikuwepo vivyo hivyo, yaelekea aliyeambiwa aandike hana makosa kwasababu pale ukumbi unamilikiwa na wadosi, kama angekuwa amekosea basi pangefutwa mara moja kwasababu hao wadosi ninao wajua mimi ni wale wa dhehebu la Ismailia, ambao ni matajiri na waliosoma..kwa ujumla neno "LET" lina maana ya "to become rented or leased", ni mtazamo tu.

    Mzalendo 101

    ReplyDelete
  16. kiswahili chapanuka,
    maneno yaongezeka,
    lugha haijazeeka,
    na kamwe haitokoma. KISWAHILI ZIDIKUKUA, TANZANIA NA AFRika

    ReplyDelete
  17. Mbona michuzi hapa umechanganya mada,au mimi ndio sielewi, swala la sikinde na yale maandishi ya Kiingilisho.
    M3

    ReplyDelete
  18. Pongezi kwa sana WanaNginde ngoma ya Ukae!The Real Tanzanian Music Brand.Kama kuna muziki wa kisasa au wa dansi ambao umejaribu kwa kiasi kikubwa kuwakilisha midundo ya asili katika makabila mbalimbali Tanzania basi Sikinde wao ni nambari wani!Viva Sikinde!Sasa kumekucha,acheni papara!Tulizeni vichwa vyenu,leteni muziki muzito wa kiwango kile cha Franco Makiadi Luambo au Tabu Ley Rochereau wa KinCongo!Hongereni sana Bitchuka na Shabaan Dede kwa mafanikio hayo makubwa sana!Pongezi nyingi zaidi ziwaendee wanamuziki wote wa bendi ya Sikinde ambao bila ya wao SIKINDE isingefika hapo ilipo sasa!God Bless You!Kuna challenge moja niliwapa Bitchuka na Dede pale Kariakoo DDC Park kuhusu masuala mengi sana ya maendeleo yenu.Naamini kwamba sasa mko na bendi yenu wenyewe basi mambo mdiyo kwanza yameanza!Tuwasiliane basi kwa ushauri wa hapa na pale!Wapenzi wa Sikinde tungependa kuiona Sikinde ikivuka mipaka na kuwa Bendi inayotukuka hata nje ya mipaka yetu.Anzisheni Website yenu.Tangazeni kazi zenu kupitia Mitandao mtapata mialiko mingi sana ulimwenguni kote walipo waafrika na watanzania kwa ujumla na hata kwa wageni walioishi na kuipenda afrika ya mashariki!Kwenye masuala ya kiufundi msisite kuajiri Sound Engineer,Mhasibu na Mwanasheria wenu hata ikiwa ni kwa mikataba tu ya muda mfupi mfupi.Nawatakia mafanikio makubwa sana Sikinde.Tupo Pamoja Wazee wangu!Nyie ndio tegemeo letu.Pongezi zimwendee Ferguson Bitchuka na PDG Shaaaban Dede na Wakongwe wote wote wa Sikinde!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...