Home
Unlabelled
kuperuzi na kudadisi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Michuzi me narudi mwezi wa sita nianze harakati za kuwa mbunge mambo yote hayo!aaaaaaaaaahhhhh jamani ndio maana hawa wabunge hawataki kuacha hii kazi,hebu fikirieni watu wana miaka mingapi bungeni?!ndio maana wanapata hata mitaji ya biashara na hakuna wanachofanya.Huko vijijini kuna watu wanaishi chini ya $1 wengine aaah mambo tambarare,kwa mpango huu hatufiki ng'o labda baada ya century 12.Tujiulize ni wangapi wanaenda majimboni kila mwezi angalau kuangalia kinachoendelea?!.Eeeh Mungu isaidie Tanzania,binafsi sioni kama tunapiga hatua za kuendelea na badala yake tunapiga hatua za kurudi nyuma.Kwani huto Tanzania uchumi haujayumba?!serikali na wizara ya fedha mnafanya nini!?hamuangalii matumizi?!kwa akili zangu fupi nnadiriki kusema hiyo misada inaishia kulipa wabunge tu.Huwezi kumpa mtu hela ya matengenezo ya gari ilhali ni ya kwake,mjomba unafanya nini!?Me siichukii Tanzania naipenda sana ila kwa hili hapana.Wote waliojifanya wanajiuzuru mbona huku nako hawajajiuzuru?!jamani wanajua kuwa uwaziri ni theruthi mambo yote mjengoni.Tanzania tunasafari ndefu sana ya kufika kunapotakiwa.Wenzetu wako chuo mwaka wa 2 sisi tuko chekechea.Rais utaita mikutano mingi ya marais wengi tu lakini nakushauri anza na kwako,badilisha mfumo hizi gharama ni nyingi na hazihitajiki.Wekeza katika elimu,hebu fikirieni haya mahela yangewekezwa kwa wanafunzi,vyuo na sehemu nyingine muhimu si tungepiga hatua?!Hospitali ya Amana iling'aa sana alipokuja yule rais aliyemaliza muda wake,jamani kaingalieni sasa hivi yani hata hutamani kumpeleka mgonjwa.Hospitali haitamaniki,wazazi waliojifungua wanalala chini,aaah jamani hata kama familia zenu zinaenda ulaya,Marekani na India kama si Sauzi kutibiwa angalieni na hawa.Halafu tunaambiwa turudi tuijenge nchi?!jamani tuijenge wenzetu waibomoe?!hiyo si ni hela ya walipa kodi?!.Nioneni mtumwa wa mawazo ila nakubaliana na rafiki yangu mmoja huwa ananiambia achana na biashara ya kusema urudi uijenge nchi.Me naona nikiendelea sitamaliza,Michuzi naomba nisamehe kwa urefu wa maoni yangu ila imenigusa sana.
ReplyDeleteNi bora bunge liendelee na kuongeza bidii kwa kazi nzuri kama bunge hili lilivyofanya, kwa mfano:
ReplyDelete1. Kumulika viongozi na watendaji mafisadi na kuwafanya wajiuzulu (kwa mfano Lowassa, Karamagi).
2. Kuzuia ununuzi wa umma unaokiuka sheria (kama Dowans).
3. Kuangaza mikataba hewa (kama IPTL, Richmond) na kuifanya serikali iiirekebishe au kuachana nayo kabisa.
4. Kuwa bunge lenye meno katika utendaji wake wote kwa ujumla.
Likiendelea kwa mwamko kama huu uliyojitokeza katika bunge hili nadhani gharama za sasa hivi hazitaaangaliwa sana.
Aidha ni vema wabunge wakumbuke wao ni watumishi na wawajibike.Ni vema kwa mfano kwenye swala ya wasiorudisha mikopo- majjina yaanikwe tu bila kubembelezana. Uwe ni utaratibu wa kawaida- majina ya wasiolipa kwa wakati yatangazwe kwenye vyombo vya habari kupitia ofisi ya Spika.
Lakini vile vile inabidi wananchi wawe macho kuwachagua watu wanaostahili kuingia bungeni, siyo watu ambao watakwenda kulala na kusubiri mikopo nafuu, mishahara na allowance tu huku hawatoi mchango wowote. Wananchi waache kukubali kutoa kura zao kwa sababu ya pilau, vitenge na noti za msimbazi. Wananchi wakikubali kutoa kura zao kwa vishawishi hivi basi wasilalamikie utendaji baadae.
mhhh. No comment!
ReplyDeleteHaya mambo ya posho za wabunge hata Uingereza nako yamezua mzozo. Wakati watu wanahangaika na recession wabunge wao wanadai posho tu kila siku tena zaidi toka pesa ya wavuja jasho. Kwa muda wa wiki hizi mbili kumekuwa na scandals za posho... wabunge wanachukua posho na kutumia visivyo.
ReplyDeleteKwenye magazeti ya leo jumapili nchini Uingereza na pia kwenye skynews kuna scandal ya yule mama ambaye ni Home Office secretary (Jack Smith) kudai malipo ya pesa aliyotumia (posho), kumbe pesa hiyo alinunulia filamu ya ngono kuangalia nyumbani kwake. Wapekuzi wamemuumbua kwenye vyombo vya habari na kaomba msamaha na kusema atazirudisha amount ya pesa alizopewa.
Itabidi nami nigombee ubunge kule kwetu Mvumi-Dodoma
Za ukarabati wa gari-1,000,000 kwa mwezi!!! Haya mashangingi si ndio tunaambiwa kwamba serikali inayanunua kwa sababu ya umadhubuti wake? Ina maana kwa miaka mitano ya ubunge walipa kodi tunalipia shangingi la kila mbunge shs milioni 60? Hizo laki nne unusu za jimbo kwa mwezi zinaenda wapi?
ReplyDeleteKudadadeki #$!@%$$@#@%!! Halafu taifa linajifanya kulia kuwa lina uhaba wa wataalamu. Hela yote iko kwenye siasa, nani atasomea udaktari, uhandisi, uuguzi, ualimu nk? !$%$&&!@
SISI TULIO UK NA USA TUMEKUBALI KUWA BONGO NI TAMBARAREEEEEEE.
ReplyDeleteAU NDO WAJINGA NDO WAKLIWAO
Swali kubwa ni kuwa hizo hela zakuwalipa na kulipia vitendea kazi vyao zinatoka wapi?
ReplyDeleteNa je hawa wabunge walipataje huo ubunge?
M3