
kibajaji kilichosheheni abiria kikikata boda leo maeneo ya chuo cha posta kijitonyama. husaidia sana wenye haraka wakati wa foleni kwani sio lazima vitembee barabarani kama magari

stendi isiyo rasmi ya vibajaji karibu na chuo cha posta kijitonyama. idadi ya vibajaji jijini dar inakuwa kwa kasi toka viliporuhusiwa rasmi kufanya shughuli jijini, ingawa bado mstakabali wake wa kuwa na leseni za biashara unafanyiwa kazi na huenda ukaanza hivi karibuni, levo ya ujuzi wa madereva wake bado kushughulikiwa
Michuzi, unaposema vi Bajaj ni vizuri sana kwa sababu vinaweza kukwepa traffic, una hakika kwamba vinaruhusiwa kupita popote pale ikiwemo pembeni ya barabara kukwepa traffic?
ReplyDeleteUnajua kwamba gari, kwa mfano, likila short cut kwenye kituo cha mafuta kilichoko kwenye kona ili kukwepa taa na foleni hapo litakuwa limevunja sheria? Vibajaji ndio unadhani havina sheria ya kuvizuia kukwepa foleni, taa, na taratibu nyingine za barabarani?
(Anyhow, hii topic ni deep sana kwa blog ya Michuzi, nimeileta tu kwa sababu Michuzi unaweza kuandika kitu hapa kikapotosha umma halafu watu wakavunja taratibu na kusababisha hatari na maafa barabarani.)
serekali ichukuwe hatuwa ya kuzuwiya kuendeshwa hizi taka taka kabla mtu mwingine hajatolewa roho kwa ajali zinazo sababisha
ReplyDeleteNazipenada sana Bajaji: zinasevu taim na hela.
ReplyDeleteNazichukia sana bajaji: Madereva wake, sidhani kama wana leseni hivyo risk yake kubwa sana!hasa ukigongwa na gari mwenye chansi ya kuumia sana ni abiria wa bajaji
Michuzi wachak uweka stori ya vibajaji subiri kesi iishe naona kama unataka kuwaharibia watu wa vibajaji unauliza sana mara wanapita njia ya miguu mara wapi? vibajaji oyeeeeeeeeeeeeeeeeee. ila vibajaji lazima uvae usalama wa kichwani ukipanda.
ReplyDeleteSASA TUMEKUWA KAMA WAHINDI.
ReplyDeleteTEMBEA UJIONEE WASWAHILI WALISEMA NINA MIAKA 10 HAPA UK SIJAWAI ONA HATA SIKUMOJA MAJI AU UMEME UMEKATIKA. BONGO TAMBARAREEEEEEEEEE HAH HAHA HAHAH AHAHA.
ReplyDeleteEeeh bwana weee........
ReplyDeleteUnajua kiukweli ni kuwa vibajaj kama vibajaj vyenyewe vinaonewa na hizi sifa ambazo zinakandamizwa kwake kila kukicha.
Kwa nionavyo mimi tatizo sio Vibajaj, tusitake kukimbia ukweli, tatizo kubwa hapa ni madereva. Nasema tatizo ni madereva nikiwa nawajumuisha madereva wote wa hapa Bongo kwa maana ukweli wa mambo ni kuwa madereva wetu wote ni wazembe, Mwenye Bajaj anazarau sana sheria za barabarani kwa kuwa tayari tumeshajenga kuwa vibajaj ni kwa ajili ya kushort cut move zote za barabarani na kwa wale wenye magari ndio wana ile mentality ya kuwa mkubwa mpishe na hapo ndipo mwanzo wa tatizo unapokuja. Tukiwa sawa kwenye sheria za barabarani basi hizi ajalii za kizembe ambazo tunashuhudia kila leo itakuwa ni historia.