mojawapo ya nyaraka ambazo mawakili wa mengi na IPPedia wamezisoma leo
wakili Michael Ngalo wa Ngalo & Company Advocates akisoma baadhi ya vielelezo vya mteja wake, Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi, kudai kwamba tuhuma zote alizomwagiwa na Mbunge wa Igunga Mh. Rostam Aziz (kama inavyoonesha kwenye posti ya hapo chini) si kweli katika mkutano wa waandishi wa habari uliomalizika sasa hivi hoteli ya movenpik, Dar. Shoto ni mwanasheria wa makampuni ya IPP, Mh Agapirus Nguma ambaye pamoja na Mh. Ngalo walimwakilisha Mengi kwenye mkutano huo.

taarifa kamili inatayarishwa na itatolewa punde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 72 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2009

    Hapa ni patamu hili soo litawapa waTZ muongozo safi jinsi ya kupiga kura mwaka kesho!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2009

    SAFI SANA.WATATAJANA TU NA NDIO TANZANIA ITAJIKOMBOA.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2009

    Usitubanie Michuzi weka paper yote kama ulivyoweka ya Rostam Aziz ili tujue ukweli lasivyo tutashuku harufu ya ufisadi mana tayari nina wasiwasi na kigugumizi chako! na usiibanie hii

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2009

    Rostam ndiye anayepokea Cheki za Dowans kila mwezi Hazina...mwizi mkubwa

    ReplyDelete
  5. ujinga wetuMay 04, 2009

    kweli sisi wajinga kweli mengi na rostam ndio wanaowakilisha serikali kwa kutaja mafisadi serikali mkoo wapi jamani mnawafanya wananchi wajinga namna hii aibu tupu .hivi hatuna kazi zaidi kuzungumza maendeleo na kukaa kusikiliza mambo ya mengi na rostam kweli serikali inavuta mnada tuu .mtu kama mengi yeye mfanyabiasha inakuhusu nini mambo ya mafisadi wakati wewe mfanyabiasha huko ni kwishiwa kiuchumi na rostam kama kweli msafi asingemzungumzia mengi angenyamaza ,sasa sisi hatuna kazi haa mengi haa rosatm kweli tuna akili.serikali iko wapi iseme ipo kwa mengi au rostam au kwa wananchi nini huu ujinga wakutangaza habazi huyu yupo hivi badili ya kutafuta maaendelo ,hata kama rostam kaiba kweli wewe mengi unafikiri kutakuwa maendeleo kwa wananchi .

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2009

    Kuuzunguka mbuyu si kazi, kazi kuukumbatia...nacheka kimaisha plus eheheheeeee

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2009

    WEWE MICHUZI, ROSTAM, MENGI, MANJI WOTE HAMNA NYIMBO BALI KUBISHANA KAMA WATOTO WADOGO.
    MICHUZI WEWE NI M'BEYA WA KIUME UNAECHUKUA MANENO HUKU NA KUPELEKA KULE, NA KUYATOA KULE KUPELEKA HUKU.
    KAMA KWELI UNA UCHUNGU NA NCHI YAKO NA SIYO HAO MAGABACHOLI AU WANAOJIITA MAMILIONEA, UNGEFATILIA HABARI ZA WALALAHOI WA MBAGALA NA KITU GANI KIFANYIKE ILI WAWEZE KUSAIDIWA.
    SIWAPIGII DEBE WAHANGA WA MABOMU WASAIDIWE, LAKINI HAYA NI MAAFA YA KITAIFA YANAYOHITAJI SI MSAADA WA SERIKALI TU, BALI HATA WANANCHI WAJITOLEE WALICHONACHO KUWASAIDIA WAATHIRIKA.
    WALIO NJE YA NCHI WANGEOMBWA KUKUSANYA HATA NGUO ZA MITUMBA, VYAKULA VYA MAKOPO NA VITU MUHIMU NA VINGEPOKELEWA BILA KULIPIWA USHURU.
    LAZIMA TUAMKE SASA NA SIYO KUWAKUMBATIA HAO WASIOWAJALI WANANCHI WANAOPIGA KURA NA KUWAWEKA MADARAKANI.
    KAMA KWELI NI MFUATILIAJI WA HABARI, UNGEFUATILIA HIYO YA MBAGALA NA KUTULETEA PICHA ZA MAAFA AMBAZO NINA IMANI WENGI ZINGEWAGUSA NA KUTOA WALICHONACHO.
    MAITI NA MAJERUJUI WANABEBWA KWENYE MIKOKOTENI KUPELEKWA HOSPITALI WAKATI TBL INATOA MABASI KWA SIMBA NA YANGA! MSAADA SI UNGELENGA KWENYE HUDUMA ZA JAMII BADALA YAKE KWENYE "ULAJI".
    ANYWAY, NADHANI HALIJAKUGUSA. KADHALIKA MIE HALIJANIGUSA HIVYO LAKINI KWA JINSI TUNAVYOJUMUISHWA HUKU UGHAIBUNI ITOKEAPO MAAFA, NASIKIA UCHUNGU JINSI GANI VYOMBO VYETU YA HABARI VILIVYOWEKWA "MFUKONI" KUWAHABARISHA WANANCHI MAAFA KAMA HAYO YAFIKAPO.
    CIAO

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2009

    The saga continues... Kheri ya fisadi nyangumi kidogo yeye sio mwizi sana lakini fisafi papa ni jambazi haswa. Mingu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2009

    i guess suala hapa ni kujua nani ni fisadi nyangumi nani ni papa,ila kwa ujumla wote mafisadi tu

    ReplyDelete
  10. southamptonMay 04, 2009

    saa ya UKOMBOZI ni sasa

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2009

    Du..!! kwa mwendo huu hatufiki mbali, hii inaonyesha kwamba vyombo vya habari siku hizi vinatumika kama kanga uswahilini, kusemana,kusengenyana, kutambiana,kupigana vijembe. Wakati mwingine nyimbo za taarabu hutumika hivi pia. Hawa jamaa wana mambo yao binafsi sasa wanatafuta hisani ya wananchi, kumbe wote wala watu, hakuna mwema.

    Mdau
    Norway

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2009

    HUU MTINDO WA WANASIASA KUWAHUSISHA WATANZANIA KWENYE HOJA ZAO BINAFSI LAZIMA UKOME. UKOME KABISAAA.
    MENGI KUDAI "WATANZANIA" WAMECHOSHWA, ENOUGH IS ENOUGH, NI WEWE MWENYEWE MENGI NA FAMILIA YAKO.
    NA WEWE AZIZ KAMA ULIVYODAI HIVYO KWENYE MADA YAKO, NA WEWE PIA NI WEWE NA FAMILIA YAKO. WATANZANIA WAMECHOKA NA NYIE WOTE, SI MENGI, SI KIKWETE, AZIZ, VIJISENTI, LOWASSA MPO WENGI TUUU.
    MMEZIMANA HELA SASA MNAANZA KUUMBUANA. KAENI KIMYA MSIZIDI KUTUCHIA MACHUNGU YASIYO NA MPANGO. SHWINE NYIE.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2009

    Mengi wewe mtumzima yani mpaka hapo nimekuvunjia heshima huo ni Utoto sasa unauanzisha, Jaribuni kila mtu kufanya biashara zenu. wacheni kupondana sasa enough is enough maana yake ni nini? Kweli Mengi maji ya shingo sasa, anatumia nguvu kupitia Vyombo vyake vya habari kisheria haitakiwi kabisa. Mengi unafanya mazuri mengi kwa wanadamu wa Tanzania ila sasa utaanza kujivunjia heshima wachak ubishana na VIJANA hao.

    Hii Beef inaonekana kila mtu anajipendekeza kwa watu wa Serikalini hapo.

    yetu macho tunasubiri mwisho wake ila mie nawaombea waache wafanye yao kwa njia nzuri na inayotakiwa.

    Mengi tafuta mke naona Pesa zinakuumizakichwa. Mwaipopo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2009

    Shida yangu kubwa ni kwa waziri Simba
    Iweje waziri ambaye anabeba dhamana ya wananchi anadhubutu kutumia madaraka yake kupendelea kikundi fulani kwa maslahi ya kikundi hicho ambacho kina uwalakini?

    Je ni haki kwa waziri tena anaye simamia utawala bora kuthubutu kunena eti, SO and so amechemsha, only kwa kuthubutu kuwataja wezi?

    nilishangazwa hasa pale anapothubutu kunena eti vyombo vya Mengi (IPP media etc) viondoke kwenye mkutano ili abaki na vyombo vya akina Rostam ambao wanakesi ya kujibu? Ingelikuwa ni nchi nyingine mbona wao wakisha tajwa tu hata fununu inawalazimu kujiuzulu toka madarakani. Rostam amefanya nini?
    Akina SImba wanamtetea mtuhumiwa kuwa ni mtu safi. Je waipatikana kwamba sio wa safi, Sofia naye atakuwa msafi? JE ATAJIUZULU? KAMA SIVYO (TUMEONA KWA AKINA WAZIRI MASHA NA WENGINEO= TANZANIA HAKUNA KUJIUZULU KWA SABABU HAKUNA UTAWALA BORA ANYWAYS NA HIVYO SIMBA ANASIMAMIA WIZARA YA UTAWALA WA KIBaBE KAMA ILIVYOJIONYESHA KWENYE MATAMSHI YAKE)

    TANZANIA TUTAFIKA WAPI?

    MBAYA ZAIDI

    BWana Michuzi na wewe angalia kama utaendelea kupost vitu vya wazi kama hivi kwa manufaa yetu, basi utaona akina Simba wakikuandama na kukufungia Blog yako. Ndio utawala wa kibabe na sio utawala bora huo. Ndio stail ya Tanzania hiyo

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2009

    Rostam amlipua Mengi, amwita nyangumi wa ufisadi

    Ramadhan Semtawa na Salim Said

    MFANYABIASHARA wa jijini Dar es salaam, Reginald Mengi aliwabatiza wafayabiashara wenzake watano jina la "mapapa wa ufisadi", na sasa mmoja wa waliotuhumiwa amejibu mapigo kwa kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi".


    Rostam Aziz, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara watano waliotuhumiwa na Mengi kuwa mapapa wa ufisadi, jana alitoa mlolongo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, na kueleza kuwa atawasilisha vielelezo kwa vyombo husika ndani ya saa 48 ili Mengi aanze kuchunguzwa.


    Mapigo ya Rostam, ambayo yanazidi kupandisha joto la vita hiyo ya maneno, yametokana na tuhuma nzito ambazo Mengi alizitoa Aprili 23 wakati alipotaja wafanyabiashara watano akitaka wadhibitiwe mapema, akiwemo mbunge huyo wa Igunga.


    Tofauti na Mengi ambaye hakutoa vielelezo na kusema yuko tayari kupandishwa kizimbani ili ukweli udhihirike, Rostam aliorodhesha tuhuma nyingi na kuahidi kuzikabidhi kwenye vyombo vya serikali ili hatua zichukuliwe.


    Huku akimtaja Mengi kwa majina yote matatu kila wakati, Rostam, aliwaambia waandishi jana akisema: "... nataka niweke wazi kwamba tuhuma zote zilizotolewa na Mengi dhidi yangu ni za uongo na ni upuuzi mtupu.


    Tuhuma hizo ni mwendelezo wa wimbo ule ule ambao amekuwa akiuimba kwa muda mrefu sasa na tayari nilikwishazitolea kauli huko nyuma.


    "... nimeamua kuitisha mkutano huu ili kuwaeleza, na kupitia kwenu kuwaelimisha Watanzania, wamjue Reginald Abraham Mengi katika sura yake halisi na dhamira yake chafu na ovu, na kumtambua kwamba mtu huyu ni nyangumi wa ufisadi katika nchi hii," alisema Rostam katika moja ya aya zake za utangulizi. Nyangumi ni samaki wa baharini aliye mkubwa kuliko papa.


    Rostam alianza kwa kuorodhesha matukio 10 ya ugomvi ambayo anadai Mengi aliuanzisha dhidi ya watu mbalimbali, kuanzia maaskofu hadi kikundi cha uchekeshaji, wakati kwa mujibu wa Rostam maslahi ya Mengi ya kibiashara yalipoingiliwa na baadaye kuyageuza kuwa ni ugomvi wa nchi nzima.


    "Sasa ameanzisha ugomvi na mimi baada ya kuona kwamba mimi nimekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, anataka kuufanya ugomvi wa nchi nzima," anaeleza Rostam.


    Akiorodhesha tuhuma za ufisadi dhidi ya Mengi, Rostam alidai mwenyekiti huyo wa IPP alianza kuifilisi nchi kwa kushiriki kwenye vitendo vilivyochangia kuifilisi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kusababishwa iuzwe "kwa bei poa".


    Alidai kuwa Mengi, akitumia kampuni yake ya Anche Mwedu Ltd katika miaka ya themanini, alichukua mkopo wa fedha NBC na amegoma kulipa hadi leo, huku akilazimisha suala hilo lifikishwe mahakamani.


    Rostam alidai kuwa mkopo wa kwanza uliotolewa kupitia hati ya maandishi ya makubaliano, ulifikia jumla ya Sh3.2 bilioni na kwamba hadi Januari mwaka 1996 ulifikia riba ya Sh 1.7 bilioni.


    Alidai mkopo wa pili chini ya kampuni hiyo ulikuwa wa mpango wa Loan Agreements na ulihusu jumla ya Sh386,746,631.06 hadi kufikia Januari 1996.


    Akiongeza kudai kuwa mkopo wa tatu ulikuwa chini ya utaratibu wa udhamini wa serikali (government guarantee) ambao ulikuwa wa jumla ya Sh1,803,137,210 hadi kufikia Januari 1996.


    Rostam alidai kupitia utaratibu mwingine, Mengi alichukua mkopo mwingine ambao ulihusu jumla ya Sh417.6 milioni hadi kufikia Januari 1996.


    "Jumla ya fedha zote za NBC ambazo amekuwa akidaiwa Mengi kupitia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML) hadi kufikia Januari 1996 zilikuwa ni Sh 5.8 bilioni, fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na riba zinafika takriban Sh28 bilioni," alidai Rostam huku akitaka akaunti za benki ambazo mikopo hiyo ilipitia.


    "Hivi ndivyo Mengi alivyochangia kuifilisi NBC, benki ya wananchi masikini wa Tanzania. Fedha hizi zilizochukuliwa na Mengi Sh28 bilioni zinaweza kujenga shule za sekondari 100 ambazo zingeweza kuwanufaisha watoto wa kimaskini wa Tanzania."


    Rostam pia alidai kuwa Mengi aliteketeza Sh2.5 bilioni kwa kutumia kampuni ya uwekezaji ya wazalendo ya NICO, kwa kununua hisa za kiwanda cha Interchem Pharma Ltd kinachomilikiwa na familia yake ambacho Rostam alidai kuwa Mengi alijua kuwa kingekufa.


    "Huku akijua hali mbaya ya kiwanda hicho alitumia nafasi yake kuziteketeza Sh2.5 bilioni fedha za Watanzania masikini wasiopungua 22,000 wenye hisa NICO kwa kuifanya inunue asilimia 51 ya hisa. Kiwanda hicho sasa kimewekwa kwenye orodha ya kufilisiwa baada ya kushindwa kujiendesha chini ya mwaka mmoja tokea Mengi kuizamisha NICO," alisema.


    Rostam, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, pia alidai Mengi kwa kutumia mpango wa Mfuko wa Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (Commodity Import Support-CIS), alichukua fedha nyingi kupitia msaada wa nchi wafadhili, lakini hadi jana alikuwa hajazilipa.


    Rostam alikiri kwamba wafanyabiashara wengi akiwemo yeye walikopa, lakini wamelipa na wanaendelea kulipa hadi sasa na kuongeza kwamba Mengi "anayejidai ana uchungu na Watanzania amekuwa akiwaongezea umasikini kwa kuchota fedha hizo baadaye kuruka na kukataa kuzilipa".


    Rostam pia alitoa mchanganuo huo wa fedha za CIS ambazo alidai Mengi alizipata na kutaja nchi zilizotoa, akianza na Norway ambayo alidai mwaka 1988 hadi 1989 iliisaidia kampuni ya IPP kupitia kampuni ya Anche Mwedu kupata Krona 6milioni, na baadaye kupitia kampuni hiyo hiyo ilipata Krona 4 milioni.


    Alidai mwaka 1991/92, Japan ilisaidia Bonite Bottlers kuchukua Yen 160 milioni na baadaye ikasaidia Medicare kupata Yen 115 milioni na Canada mwaka 1988/89 ikasaidia Anche Mwedu dola za nchi hiyo 0.5milioni.


    Pia alidai mwaka 1988/89 Italia ilisaidia Anche Mwedu kupata Lira 1.7milioni, Japan 1997 ilisaidia Anche Mwedu Yen 20milioni na Japan tena 1994 ilisaidia Bonite Bottlers kupata Yen nyingine 160 milioni.


    Pia alidai Tume ya Uchumi ya Ulaya (European Economic Commission-EEC), katika kipindi cha mwaka 1988/89 ilisaidia Bonite Bottlers kupata EEU 0.5199.


    "Fedha hizi zilizo katika sarafu tofauti za kigeni zikibadilishwa kwa shilingi za Tanzania na riba kwa miaka yote tokea zilipochukuliwa zinafikia mabilioni ya shilingi," alisema Rostam. "... badala ya kurejesha fedha hizi... Mengi alizitumia kujitajirisha."


    Pia alidai kuwa Mengi aliingia ubia na serikali katika umiliki wa kiwanda cha Tanpack Industries Ltd, lakini bila ya kumjulisha mbia wake (serikali) alitumia dhamana ya kiwanda kukopa Sh600 kutoka benki ya NBC na "kuzitumia kwa njia anazozijua yeye".


    "Benki hiyo ilipochachamaa kutaka ilipwe fedha zake, Mengi alitaka Tanpack ilipe lakini serikali ikakataa kulitambua deni hilo... Matokeo ya ufisadi huo wa Mengi, Tanpack ikafilisiwa na kufa," alidai Rostam.


    Miongoni mwa matukio ambayo Rostam alidai Mengi alikorofishana na watu mbalimbali ni pamoja na zabuni ya ubinafsishaji hoteli ya Kilimanjaro (sasa Kempiski).


    "Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora Mheshimiwa Wilson Masilingi baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya kuwa ugomvi wa nchi nzima," alidai Rostam.


    "Katika kudhihirisha jinsi alivyo na chuki na visasi kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata kushiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo."


    Kuhusu kutajwa kwenye ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), Dowans na tuhuma nyingine, Rostam alisema "hizo zote nimekwishazitolea maelezo... ni porojo tu hakuna hata moja ninayohusika nayo".


    Ni vema Watanzania wakafahamu kwamba kila anapokabiliwa na matatizo au anapotenda maovu, kimbilio lake la haraka la kujifichia limekuwa ni kusaka huruma kwa wananchi kwa kutaka aonekane ni sehemu yao na kwamba anaonewa kwa kuwatetea wao. Ukweli ni kwamba amekuwa akifanya hivyo ili kutafuta hifadhi na kinga akijua ana madhambi mengi."

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2009

    MENGI NAYE NI FISADI MKUBWA ASITUMIE KIVULI CHETU MASKINI KATIKA KUJIINEMESHA NA KUJILINDA.

    KILA KUKICHA ANAZIDI KUTAJIRIKA WAKATI SISI KILA KUKICHA TUNAZIDI KUA MASKINI.
    MENGI NA WAHINDI WAKE WOTE WEZI WAKUBWA

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2009

    HUYU MENGI ANATUDHARIRISHA MASKINI,AMESHAONA UMASKINI WETU NDIO NJIA YA KUJIPROTECT.
    BONGO KWELI YA MAFISADI KILA KITU NI DILI UKIMWI DILI KWA MAFISADI HATA UMASKINI NAO NI DILI KWA MAFISADI

    ReplyDelete
  18. AFANDE MIDAKOMay 04, 2009

    furaha yangu mnyonge ni kucomment bloguni. kabwela mimi sijui lolote kuhusu nchi inavyokwenda zaidi ya kujua mvua na jua linavyowaka, pharmacy na hospital inayoongoza kwa kutoa matibabu kwa bei nafuu

    Kaka lakini naona kama nuru inakuja coz hakuna kiongozi wa kumaliza ufisadi bongo.! MAFISADI WATAMALIZANA WENYEWE KAMA MAFIA GROUP WALIVYOJIMALIZA au drug dealers wanavyojimaliza wenyewe MEXICO wataisaidia sirikali

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 04, 2009

    Mengi achana na siasa we fanya biashara, siasa ni ngumu na itakuharibia!

    Kashfa zipo nyingi mno!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 04, 2009

    Mengi anacheza na serikali, na wanasiasa. Kuna uwezekano amekosa maslahi fulani fulani kutoka serikalini ambayo kwa kawaida huwa anayapata; Mzee huyu hakubali kushindwa wakati kupanda na kushuka ndio maisha. Serikali inamjua ila yeye ameghafirika kidogo kuhusu hilo. Kuna uwezekano kuwa ana washauri wabovu ambao watampeleka pabaya. Jihadharini sana na hawa watu hatari kwa Taifa changa kama Tanzania!

    Mdau Boston, US

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 04, 2009

    Hao wote ni mafisadi papa na nyangumi,wote wanatumia media zao kujisafisha but it's senseless,hebu wasitupotezee muda apa,tuna mambo mengi ya kufanya na sio kujibizana.

    Potz.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 04, 2009

    Watanzani tunashangilia, tunashangaa kama ni Movie inaendelea vile. Nchi imeliwa na Mi-richmond, Mi-Dowans, Mi-Kagoda, Mi-EPA na ghasia chungu nzima, lakini tunaelendelea kudunda tu na ufukara wetu!

    ReplyDelete
  23. NautiakasiMay 04, 2009

    Picha ndo limeanza..!
    Michuzi niletee popcon na coca cola ya baridi!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 04, 2009

    Tumechoka na malumbano.....si wafungue kesi mahakamani ili tujue mkweli ni yupi? Kuna mambo mengine ya maana ya kusikiliza na si upuuzi wa hawa wafanyabiashara! Kutuibia watuibie na bado waendelee kutufanya hamnazo. Serikali inapata kigugumizi kuwachukulia hatua ...labda 'watawala' wetu wamenufaika na uzandiki wa 'nyangumi' na 'papa' hawa.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 04, 2009

    mzee wa blog tunashukuru kwa kutufahamisha yanayotendeka Tanzania ni wewe pekee unaetupatia habari sahihi kwa sasa,napenda kuungana na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP kwa ushujaa wake wa kusema ukweli hadharani kweli haya mambo anayo yataja bwana Mengi ni yamsingi kabisa tuache mambo ya ukabila,hawa wahindi watatutawala mpaka lini?umefika wakati wa wao kuturejeshea mali zetu Watanzania kwa nguvu,kwa nini tutawaliwe na wahindi?JK baba uko wapi?Tunasubiri tamko lako, jaribu kuwa na msimamo kama walivyokuwa Baba wa Taifa na Sokoine,pia unapoteza umaarufu ulioupata mwanzoni mwa utawala wako.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 04, 2009

    KAMUA BABA MENGI KAMUA MPAKA HAO AKINA SUBASHI AMBAO WAMEONA NI VYEMA KUIFILISI NCHI YETU WAAMUE WENYEWE KUFUNGASHA VORAGO WAENDE KWAO, WE ARE TIRED WITH THEM,, NA KAMA MTANIITA MBAGUZI NIITENI TU LAKINI HAWA WATU SI WAZURI KWA NCHI HII ONDOKENI TUMEWACHOKA,,,, NA HAO WATANZANIA MNAOWANUNUA WAJE WAWASAFISHE KWENYE VYOMBO VYA HABARI KWELI WAMEISHIWA, YAANI MNADIRIKI KUUZA UTU WENU KWA SABABU YA VIJISENTI??? SHAME ON U ALL
    TUPO NYUMA YAKO MZEE MENI NA OLE WENU MZEE HUYU ADHURIKE KWA NAMNA YOYOTE ILE MTATUTAMBUA KAMA HATA SISI TUNAWEZA KUWARICHMOND VILE VILE.....

    MAFISADI KWISHNEY

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 04, 2009

    mmmmh!Sie twasikiliza tu wakianikana hadharani. Siku zote uovu wowote huwa una mwisho. Kwa nini sisi binadamu huwa ni wepesi kusahau kuna Mungu na hamna la siri mbele zake?!

    ReplyDelete
  28. Mchungu Wa NchiMay 04, 2009

    Ukiambiwa mbele ya watu wewe ni kikojozi huwezi kujitetea kwa kusema mbona hata wewe kikojozi? Mi nimesema wewe kikojozi dawa ni kutoa godoro nje na kusema angalieni mbona halina mkojo? Anachofanya mtukanwaji ni kuonesha naye anaweza kutukana, huu ni utamaduni duni sana na ni wazi una ukweli unauficha. Rostitamu za Ndizi jitetee huibi au hujaiba na si kusema hata Mambo Mengi naye mwizi, sawa Mengi kuwa Mwizi au fisadi hakuoneshi au hakuthibitishi wewe si fisadi. Mnakuwa kama mnacheza rede, endelea tu ila fahamu penye ukweli uongo utajitenga...Big Up Mengi! Big up sana!

    ReplyDelete
  29. SOMA HILI SHAIRI
    WATANZANIA MENGI MTAYASIKIA
    MKAE MKIJUA HILO SIO CHANGA
    SIKU INAKUJA KUFA NAO LAZIMA
    KAMA WEWE MUOGA KATU HUTO PONA
    WATU WAKICHOKA LIWALO LITAKUWA
    WAKATI WA KUAMKA NDUGU JAMAA SIKIA
    WATANZANIA MENGI MTAYASIKIA

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 04, 2009

    hawa wote ni wafujaji nguvu za wananchi mbona kila mmoja hajibu tuhuma anazopoewa.Mengi umesema kweli Rostam ana husika na hizo kampuni Dowans,Richmond na pagoda.na kwa upande wako Mengi tuhuma ulizopewa ni za kweli kabisa tabia hizo unazo za udikteta na utapeli.Sasa Serikali ni wakati wa kuammka ushahidu wote ukowazi vielezo wamevitaja wote ni wakuburuzwa mahakamani.Watanzania tumechoka kufanywa wajinga

    ReplyDelete
  31. Mgogo-DodomaMay 04, 2009

    Mengi na mawakili wake wote Fix tupu. Hamna lolote, jibuni majibu yaliandikwa na Rostam na sio kusema nani anafanyi ni sokoni. Nyiyi wenyewe(Mengi) ndio mmeaanzisha chokochoko na sasa linawashinda mnaanza kulamikia eti funika bovu. Mlitegemea kwa kuwa watu TZ wanalamikia mafisadi, mkafikiri mkitumia wakati huu na njia hizi za kusema kwamba ni waarabu au wahindi fulani basi wananchi watakubaliana na nyie. Uongo mtupu. Nyinyi ngozi nyeusi wenzetu ndio wezi wetu na wala sio hao WATZ- wahindi wala waarabu wala wasomali.Rostam sio Waziri, sio Kamishina TRA, sio Mkuregenzi wa Tanesco, sio Waziri mkuu na sio Rais, iweje aamke tu leo na kutuibia sisi WATZ ngozi nyeusi. Sisi WATZ weusi hasa Wa-Chaga kama wewe mengi ndio umewafuata-wahindi na kuwaambia kwamba mnawajua watu serikalini na mnaweza kuiba fedha na mkawatumia wao na wewe ukiwemo.
    Angalia vyama vyote vya siasa vya upinzani- wamejaa watu kutoka MOSHI tu, wao tu nchi nzima eti ndo wanaona nchi haifai kiungozi, haifai kiutawala , haifai kiuzalendo. mhh wachagga tuuuuuuuu.
    sasa mimi naanzisha kampeni ya kusema wachaga ndio wezi wakubwa TZ, maana wana maduka kila pembe ya nchi ya TZ, kama sio kuwaabia makabila mengine wanafanya nini huko mikoani. Wakiona Wasukuma wameanza kuja juu kibiashara wanasema ohh wanaonewa, wakiona wabena wameanza kuja juu kibiashara wanasema ohh tumeonewa. wakiona wahaya wanakuja juu kibiashara wanasema ohh wamecheza faulo. Wao kila kitu wanataka kuwa wao tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
    Mimi nimewastukia kweli hawana lolote wachaga, walianza ugimvi na wapemba, kibiashara, wakagundua wapemba wachawi wa popo bawa waka- waacha. sasa wameibukia wahindi eti ndio wezi. Mimi mchaga huwa simpendi kwa sababu anatabia za kujisikia fulani na kugombanisha watu ki-aina sana. Wanafikiri wao "fedha" ni zao tu na wala sio za mtu mwingine TZ.
    Mengi tapeli mkubwa ameua mabenki TZ.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 04, 2009

    I second you Mengi. t is about timt. Enough is enough. Asilete ujinga wa kujidai kusue for one shilling hapa. Ajibu yote hayo na aonyeshe ni wapi analipa kodi.

    Na sio huyo tu ....huo ni mwanzo.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 04, 2009

    hawa wote wezi 2 ila mengi amezidiwa kete katika wizi ndio anapiga kelele unacheza na asia kazi yao biashara 2 na wizi sasa babu yetu mengi wewe funga mdomo 2 unatueleza jinsi mnavyotuibia mbona wewe ipp imejaa wachaga 2.MICHUZI UKIBANIA HII KIMPANGO WAKO

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 04, 2009

    Naomba nichangie haya yafuatayo maana naamini we si mwana Mtandao!

    Huyu Prof. Mapumba inabidi anyamaze kama siasa imemshinda ! hii inaonyesha siasa zetu zinaelekea wapi! tukichunguza vizuri CUF itakuwa imehongwa au huyu Mapumba anataka kujipatia umaarufu usio na mana! suala la ubaguzi sijui linakuja vipi hapa? ina maana kama watuhumiwa ni mafisadi kweli waachwe kushtumiwa kwa vile ni ngozi tofauti? hii hainiingii akilini ni vp ubaguzi unaingia hapa sijasikia mtu akitukanwa yani akiambiwa we si mweusi au we hii nchi si yako na pia huku kusema mafisadi wako wengi (Prof. Mapumba) sielewi based on that anything can be solved! inanitia mashaka kuhusu elimu ya huyu Prof. Mapumba maana someone (Bw. Mengi) tried to be specific hapa ni suala la intended accussed na by the accusor na kutokana na evidence alizo nazo Bw. Mengi ameamua kuwa-target na pia wote ni wafanyabiashara zinazoingiliana inawezekana ufisadi wa Bw. Rostam+4 unadhoofisha biashara halali za Bw. Mengi (as the way he claims) kwa hiyo ana haki ya kutoa shutma mana PCCB+Bunge wameshindwa kazi! watu wanasema eti Bw. Mengi ana wivu wa kwanini, thats bullocks! katika dunia hii hakuna business inayoweza kuvumilia ukwepaji wa kodi wa business nyingine hasa kama zinafanana kwa vile thats is not a fair competition that's to f**k up another! vilevile katika hao wengi Bw. Mengi ameamua kuchagua hao 10 na katika hao ameamua kuchagua watano kwa kutumia ranks (most grafters)! that was his choice using graft severeness criteria kama nilimuelewa vizuri na si ubaguzi! kwa hiyo basi ningependa kuona Bw. Rostam akienda mahakamani kwa vile anadai ametuhumiwa visivyo! na sio kulia lia juu ya suala la ubaguzi! hapo ni vipi jamani ! inamaana tuwaogope kuwagusa wa-Tanznia wenye asili ya Asia kwa vile tu ya pazia/kivuli la ubaguzi? nchi haiendi hivi jamani! accountability and good leadership does not spare that!

    Na pia kuhusu suala la wafanyakazi wa Mengi jamani kama kuna aliyewahi kufukuzwa isivyo halali basi amekosea kutokwenda mahakamani na sio leo hii politician com businessman aanze kumsemea huyo aliyefukuzwa thats to distort the main issue here! there is no base here that's cheap politics (mambo ya mitaani). Lets face it Tanzanians are tired of this tit for tat politics good governance does not say that Mr. politician!

    Na suala la eti Mengi anamuawakilisha nani kuongelea suala la ufisadi! i actually laughed cause he does not need to be sb cause constitution allows that by the way he is a chairman of EABC na pia ni chairman wa CTI plus Media association na so many bodies including Nepad membership! all these bodies advocate fairness in business and not graft, pls get that!

    Kuhusu swala la Ze Comedy nathani kuna swala la copy rights huwezi kuchukua kazi ya mtu na kuhama toka mwajiri wako kwenda kwenye mwajiri pinzani kijingajinga namna hile! ndo mana baada ya wana Ze Comedy kwenda mahakamani waliamua kubadili jina na kuridhia kutotumia character names za hapo awali! sasa sioni hili swala linakuja vp?
    Swala la Masilingi, Mramba na wengineo ukweli unajulikana naomba watu waje na appealing accusations na sio eti huyu ana chuki binafsi that doesnt hold water thats a fighter and not a heater! For instance suala la Mramba na Bingo ile ilikuwa dirty trick ya Bw. Manji ili apate ile biashara that's will never be tolerable anywhere may be by then under Mr. Makapa regime!

    Mdau
    Mchambuzi

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 04, 2009

    Imeshakuwa mchezo wa kuigiza sasa.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 04, 2009

    Mkuu wa Nanihii
    Unapowaona hawa majamaa wakitoana jasho kwenye public namna hii ndo unapata kuijua Tanzania vizuri. This is one of the Smartest move in the history of Our country's Intelligency. Kwa jinsi hii ninawapa bravo kuwa sasa tumeanza kufanya kaza smart sio umbeya.
    Ushauri kwa wazee wa Internal Affairs za nchi waacheni ili waendelee kukusanya na zingine ambazo ninyi hamkua nazo.
    Good job Othman, you are doing a very Smart task, It takes a smart man to notice a smart move.

    Long Live TANZANIA

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 04, 2009

    rostam aziz,manji,lowassa na mafisadi wote bongo wanaifirisi nchi na watanzania kiujumla kwangu mie this is very personal,aiwezekani mtu ukaiba kijinga kama ao wanavyofanya alafu bado wana tesa apo bongo bila kuchukuliwa hatua yoyote,huko UK ,ceo wa RBS ambayo ni benki huko scotland kakimbilia south africa kwa usalama wake wananchi wameshambulia makazi yake just becouse of his poor laedership RBS required billion of tax payers money to run,uyu akuiba hela na kuna uwezekano akarudisha pension yake ya million moja dollars kwa mwaka,bongo we are so passive and that is the different btn us and europeans,asians,americans,arabs.watanzania tuamke we need to be a little patriotic.awa mafisadi wote wanadeserve adhabu toka kwa wananchi wa Tanzania

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 04, 2009

    Issa Leo nimekukubali...
    nimemiss kuona majibu ya mengi live ktk TV nacheki site yako nakuta mchizi umeshanyaka data na umezirusha hewani..
    Big up sanaaaaaaa

    ReplyDelete
  39. This is a very poor defense on Mr Mengi side and unharmful counter attack due to lack of concrete proof on charges.It looks like mawakili wa Mengi hawajafanya homework ya kutosha kuhusu Mr Rostam Azizi while Mr Rostam Azizi did an excellent homework on Mr Mengi.Anyway nasubiri maamuzi baada ya dakika tisini za mpambano.

    USA1

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 05, 2009

    Hapa ndio inaonesha Mengi hajasoma kabisa yani anauliza je AZIZ kafanya nini kwenye kusaidia Misaada kwa jamii? hahaha Mengi pole misaada haitangaziwi basi kama hujui, Mengi anasaidia kwa njia yak uonesha serikali ili asamehewe mambo yake tu.

    Mengi umejishusha hazi kweli Mengi unapenda kweli kutumia TV zako kuharibu biashara za wengine na hupendi kuona watu wanaendelea pole. From James Sabuni.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 05, 2009

    HAHAHAHAHAHA aliyesema Picha la Movie ndio linaanza nakupa Hongera Tambara la USwazi linaanza. Habari Ndio Hiyo Muuza Njugu Pitisha hapa.

    Boxing hii Baba EMu-JI-Emu(MGM) Mpaka sasa naona Mengi Round ya 3 Mengi kashapigwa Round 2 ila inaonesha Tatarudi labda yetu macho mpaka ikifika Round Ya 12 Tutasikia Mengi kaafilisika Rostam Aziz kastahafu. wanaanza wenyewe kwa wenyewe Michuzi tunasubiri picha ya Kipanya inasemaje?
    Round 3

    Mengi 1 Kuitwa NYangumi
    Aziz 2 Fisadi Papa,na Simzawa(Ubaguzi)

    mapigo yataendelea Muuza Mayai Lete Yai hapa na Soda Ya Coka Chupa Ndogo manake muuza karanga anachelewa. Pazi.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 05, 2009

    HONGERA MICHUZI UKO FAIR SANA KULE JAMII FORUMS WACHAGA WA CHADEMA WAKISHIRIKIANA NA MAMLUKI WAO KAMA BENSON MWAKYANJALA-MWANAKIJIJI WANAZUIA MAONI YA KUMSEMA VIBAYA MENGI KWA VILE NDIO M

    MWANAKIJIJI ANASEMA KUWA MENGI KAIPOTEZA BILIONI 28 WAKATI ROSTAM AMEPOTEZA BILLIONI 40.

    AMESHINDWA KUELEWA KUWA MENGI ALIIBA PESA ZA UKIMWI TOKA MAREKANI BILLIONI 47 KUPITIA CRDB.ACHILIA MBALI MZUNGU ALIYEIBIWA POUNDS MILIONI TATU AKIWA KAMA MUWEKEZAJI KWENYE FAMILIA YA MENGI.

    MICHUZI UMEKOMAA HUKO JAMII FORUMS-JAMBO NI KUSIFIA CHADEMA NA WACHAGGA TU.TEMA MENGI MAANDISHI YAKE YAMENUKULIWA JAMII FORUMS KAMA HIYO ENOUGH IS ENOUGH IKO JF MUDA MREFU.

    MENGI NI TAPELI NA JAMBAZI KUBWA NDIO MAANA NYERERE HAKUWAHI KUMKARIBISHA NYUMBANI-MSASANI ALIJUA KUWA NI TAPELI.

    HATA KUUUNGUA BENKI KUU WALIOHUSIKA NI WATU WA KILIMANJARO TU.

    WACHAGGA ACHENI WIVU WA KIBIASHARA.
    ROSTAM KAFANYA MENGI JIMBONI KWAKE IGUNGA KILA NYUMBA IMEPEWA CHAKULA NA ROSTAM KIPINDI CHA NJAA, ACHA SHULE, HOSPITAL NA ZAHANATI.ROSTAM HANA MPINZANI JIMBONI KWAKE KWA KAZI NZURI ALIYOIFANYA.ROSTAM NI MSOMI WA OXFORD.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 05, 2009

    Pamoja na Rostam kutajwatajwa bila ya kufikishwa mahakamani, lakini wengi wetu hatukujua kama na Mengi naye ni mchezaji wa deal chafu. Iweje apewe kiwanja halafu anakwenda kukiuza kwa watu ambao anawalalamikia?

    Kubwa zaidi kwani Mengi siku zote anaonewa yeye tu?

    Mwisho, ninaishauri serikali isimamishe hii mijadala kwani ina harufu ya kutawanya chuki miongoni mwa jammi ya Tanzania. Ikibidi Mengi afute kauli yake kwamba watanzania tumechoka, mimi sijamtuma, hayo mamlaka ya kuwasemea watanzania ameyapata wapi?

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 05, 2009

    hivi wewe madau hapo juu bado unapoeza muda kwenda JF? Kule wau wanatetea baba zao na watu wanaowadhiri. Ok! rostam amepoeza billion 40 ambazo amezipata baada ya kutoa service, mengi alichukua hizo hela kwa ajiri ya tumbo lake na kusababisha benki nzima ife. huyo mwanakijiji kila siku anaambiwa arudi shule anabisha ona sasa hajui kabisa kuwa billion 28 za wakati ule ni sawa na billion 500 za leo?

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 05, 2009

    Mengi ana udini na ubaguzi wa rangi. Mbona ameshindwa kuwataja mafisadi wa dini yake?

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 05, 2009

    Naomba serekali iingilie kati mara moja na kuwapeleka kwenye sheria watu hao wanao tumia vyombo vya habari kwa faidi zao. Hii italeta matatizo sana kwenye jamii tumechoka na kusikia hizo tuhuma kwenye vyombo vya habari mahakama na sheria vifate mkondo wake.
    Tunataka kusikia maendeleo na mikakati ya serekali ya awamu ya nne inafanya nini na sio fitina kwenye vyombo vya habari!
    Hii serekali imekuwa ni ya marumbano tuuu, hakuna kinachofanyika kunyoshea na vidolee tuu! Sasa hii sio demokrasia tunayo taka watanzania hizi ni chuki binasfi ambazo hanae pata madhara ni maskini wa chini.

    Serekali tunatumia nguvu nyingi na muda mwingi na gharama nyingikunyosheana vidole badala ya kufocus na maendeleo ya nchi.
    Tanzania hatuna Ubaguzi, Watu wenye asilia ya asian ni wenzetu ,
    Tunaomba serekali ingilie mara moja na kusimamisha utumizi wa vyombo vya habari kwa faida binafsi na chuki kwa jamii.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 05, 2009

    Waziri wa utawala bora. Kweli nchi yetu kichekesho, huyu mama ndiye ovyo kabisa sijui ilikuwaja akapewa huo uwaziri maana yeye ni zero na ndio hao wanaojifanya wanawatukuza hawa wapubavu kutoka nje yanchi.

    Rais lazima hakubali kuwa kumfanya huyu mama waziri ni pumba tu.

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 05, 2009

    Waziri wa utawala bora. Kweli nchi yetu kichekesho, huyu mama ndiye ovyo kabisa sijui ilikuwaja akapewa huo uwaziri maana yeye ni zero na ndio hao wanaojifanya wanawatukuza hawa wapubavu kutoka nje yanchi.

    Rais lazima hakubali kuwa kumfanya huyu mama waziri ni pumba tu.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 05, 2009

    Mengi tunataka ushahidi na siyo kutuuliza sisi maswali. Kama uliamua kuingia kwenye game hiyo basi piga bao na siyo kupiga chenga kufunga hufungi

    Eleza kuwa Rostam hana kamapuni yeyote na ushahidi wangu ni huu hapa

    Eleza kuwa Rostam ana mahusiano na Kagoda ushahidi wangu huu hapa.

    Eleza Rostam ana mahusiano na Dowans ushahidi wangu huu hapa

    Eleza Rostam ana mahusiano na Richmond ushahidi huu hapa.

    Lakini mambo ya kurudia kutuuliza sisi maswali haitusaidii kwani hata waandishi wa habari waliuliza pia na wakajibiwa

    Tueletee ushahidi tu na si maneno matupu.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 05, 2009

    Mh Balozi na DC wa nanihii,
    Inaelekea Bosi wako amekaribishwa kwenye Mkoa wa Dar kwa mabomu Mbagala na ya kina Mengi na Rostam.
    Mpe pole, sasa hivi ataanza kutoka mvi kama kandoro na Makamba waliingia U-RC wakiwa na nywele nyeusi lakini wametoka na mvi.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 05, 2009

    haya mani mengi sizani kama yametolewa na watanzania wazawa. Nafili mengi yametolewa na wahindi maana wanachokifanya ni kutufunga macho tu. Mengi kaiba lakini ni mali za nchi yake lakini wahindi kazi yao nikumaliza taifa kisha wakakimbia maana wao hapo sio kwa. Huyo aliyesema eti Rostam ametoa misaada huko kigoma, wewe kama ukifanya maesabu kwenye hizo pesa alizoiba kutoka benki kuu unafikili na asilimia ngapi katumia katika hiyo misaada unayoisema. Msitake kuwafanya watanzania ni wapumbavu kiasi hicho

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 05, 2009

    Mengi kama kazila potelea mbali maana ni pesa za nchi yake kuliko hii mijamaa na rahoo zao mbaya.

    Siku nikiwa rais hii mijamaa yote nairudisha kwao pumbavu zao

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 05, 2009

    WATANZANIA NIKIANGALIA HAYA MAONI YOTE YA KEJERE NA HAPA HATUWEZA KUENDELEA HATA SIKU MOJA.
    KWA KIFUPI MAHAKAMA, BUNGE, SERIKALI NA WANACHI TUMEJAA RUSHWA TUPU HAPA HIVYO HAKI VIGUMU KUPATIKANA HAKI ILIKUWA WAKATI WA BABA WA TAIFA NA WAZIRI MKUU MAREHEMU SOKOINE.

    LEO TUMEJAA NA TAMAA ZA DUNIA WATANZANIA TUNANUNULIWA KWA VITENGE HATA KUKU ANATHAMANI.

    HAPO JUU JAMAA ANATUKANA WACHANGA HUU SIO UUNGWANA KUTUKANA KABILA YOTE.
    HII INAONYESHA HUNA KABILA NA HATA ELIMU.
    TANZANIA HATUNA MAMBO YA UKABILA NA KAMA UNATAKA KUTUKANA KABILA BASI JITOKEZE KWENYE MIKUTANO ILI TUFANYE DEBATE.

    IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 05, 2009

    Mimi hawa wahindi wananiudhi sana wao ndio wanaubaguzi wa rangi..Wanafisadi nchi then hawana upendo na Watanzania...Wanawaonaga kama watu weusi ni kinyesi kwao...Wana dharau sana...Mengi kamua baba....Watoe mafisadi wote si hao tuu Mabomu yalipuliwe yote hayooo

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 05, 2009

    LOL @ Anon wa Tarehe May 04, 2009 6:55 PM Michuzi niletee popcorn na coca cola picha ndo limeanza! LOL

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 05, 2009

    Nafikili mzee mengi ana washauri wabaya watampeleka kubaya. mtu mzima kila siku kusemezana na watu ni aibu kubwa.
    wanasiasa si watu wa kubishana nao kila mara wao wana njia nyingi na wanaungana mkono. utajimaliza mwenyewe, achana nao fanya biashara zako. acha kuwachokoza na vyombo vyako vya habari. jua kuwa mpanda ngazi hushuka!!!!

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 05, 2009

    HIVI WATANZANIA WENZANGU KWANINI TUSIUNGANE TUMBOMOE UYU ROSTAM AZIZI FISADI KIWEMBE ARUDI KWAO MUMBAI AKAFILISI VIZURI ATOKE KWETU

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 05, 2009

    Jana tumeona jinsi wanasheria wa bwana Mengi walivyojibu tuhuma za Rosti-tamu nafikiri kila mtu aliyeangalia TV jana kajionea mwenyewe kwani ametoa ushahidi kwa vielelezo na kuviweka wazi kwa wanahabari kuviona.
    Ukweli unabaki palepale kwamba Rosti- tamu alitakiwa kujibu tuhuma na ndipo atoe tuhuma za bwana Mengi lakini hakufanya hivyo hii inaonyesha kashindwa kudhibitisha tuhuma dhidi yake.
    Hawa watu ni hatari sana ni lazima tuwaogope kama UKOMA kwani hawana nia nzuri na nchi yetu.Watanzania wanaowatetea watu hawa hawajui watendalo na Mungu awasaidie kwani ndugu zao ni masikini wa kutupa huko vijijini.
    Nina uhakika kuna siku ukweli UTAPATIKANA.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 05, 2009

    Mengi punguza malumbano tumechoka sasa kusikia maovu yenu kila siku, sasa tufanye kazi. wakati wa maneno umepita.lipa kodi fanya biashara zako.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 05, 2009

    HAYA WAFANYA BIASHARA WAKICHAGA WALIOPATA MITAJI KWA UJAMBAZI NA KUTOA KAFARA, NA KILA MWEZI WA 12 KWENDA MOSHI KUNYWA DAMU ZA MBUZI NA KUONGEA KWENYE MAKABURI. MCHAGA HANA UJANJA WOWOTE ISIPOKUWA NI KUTUMIA NGUVU ZA GIZA. WAKIPATA HELA WANAANZA DHARAU KWA MAKABILA MENGINE WAKATI WAO WANAKUNYA DAMU KAMA VAMPIRES. MATAJIRI WOTE WAKICHAGA UKIANGALIA WALIIBA, HAWANA AKILI YA KUTENGENEZA HELA HALALI. WAENDE ZAO NA UKABILA WAO. SISI MAKABILA MENGINE HATUWAUNGI MKONO KWENYE HILI KWASABABU TUNAWAJUWA DHARAU ZAO WAKIPATA HELA ZA WIZI.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 05, 2009

    SASA MLITAKA WAZIRI WA UTAWALA BORA ACHEKEE TABIA YA MENGI KUTUMIA VYOMBO VYAKE KUKANDAMIZA WENGINE?
    WAZIRI HAKUTETEA UFISADI ILA ALIKUA ANATAKA SHERIA IFUATWE NA SIO KUVUNJA SHERIA.
    TUMEONA MADHARA YA VYOMBO VYA HABARI RWANDA NA BURUNDI.

    TUSIWATETEE MAFISADI KWA AJILI YA UKABILA

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 05, 2009

    Jamani mengi mbona hajajibu tuhuma alizorushiwa? Kwani alitakiwa aseme naye kama anayo akaunti nje hajasema, kama alipewa kiwanja na mwinyi akamuuzia muhindi hajajibu, kufunga makampuni kwa kukwepa kodi hajajibu. Ajibu hoja siyo kusema habari za miaka.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 05, 2009

    YOTE MAJIZI MAKUBWA HAYA.HAYANA HATA SONI YANATUMIA PESA ZETU KUTAKA TUYASHABIKIE ENHE?TUMENG'AMUA STATE MACHINERY FANYENI KAZI YENU AU NANYI MMESHA............................!

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 05, 2009

    Mengi kaiba hajaiba lakini mimi naona poa zichuliwe na menngi kulikoo hii mijamaa isiyotupenda na inadiriki hata kututukana mbele zetu kama hilo hapo linamtukana ndugu yenu wa damu nyie mnampongeza.

    Sababu kubwa ya kumfanya mengi achukue pesa ni zifuatazo

    1. Amegundua pesa zetu zinachukuliwa na majambazi kutuko nje yanchi sasa anajitahidi kuzichukua zilizopo hili zisichuliwe na hiyo mijitu yenye rohoo za kwanini kwa watanzani

    2. Mengi amegundua kuwa watanzania wengi ni wapuuzi na ndio maana anajaribu kuwaifadhia pesa zao hili zisiamishwe india.

    3.Watu waliotajwa kuwa wamegombana na mengi ni kwasababu mengi haamini kuona hao wanajiita mawaziri wanawanyenyeke wahindi na waharabu wakati yeye akishuhudi upuuzi wao.

    Mwisho

    Tafadhari sana Mh. Mzee Mengi naomba usisite kwenda kuzichukua na zile zilizobaki kabra hii mijizi haijazifikia.

    Nakushukuru sana Mtanzania mwenzangu kwa kazi unayolifanyia taifa letu ingwa wapuuzi wachache wanajaribu kukukatisha tamaa kawa wale wanaomkatisha tamaa raisi wetu mpendwa DR. Jakaya Kikwete

    Tafadhari usisaau kuchukua zote zilizobakia maana walipewa majuku ya kuzisimamia ni wapuuzi wakubwa, vibaraka wa wahindi!!!!!

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 05, 2009

    KWELI MAFISADI WANA POWER.
    KULIKUA NA LINK YA VIDEO KWENYE GLOBU YETU HII YA JAMII MARA IMETOLEWA....KWELI ITACHUKUA MUDA SANA WABONGO KUAMKA...
    MUNGU ATUSAIDIE...

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 06, 2009

    HIVI INAKUAJE MAFISADI WOTE WANA ASILIA MOJA... KWANI WATANZANIA ASILIA TUTAAMKA LINI?????&$/\
    BORA WAZUNGU WAJE KUTAWALA TENA KWANI WATAJENGA NA SHULE,HOSPITAL N.K. SIO HAWA MAFISADI WAHAMISHA HELA NJE.. KILA SIKU...
    MICHUZI USIKUBALI MAFISADI WAKU-INFLUENCE KWENYE GLOBU YAKO MAKINI...

    ReplyDelete
  67. AnonymousMay 06, 2009

    Hawa wangepigana risasi mchezo uishe. Wote waongo, wanazikana katika biashara wanatafuta cover.Bali Mengi ujiandae, ukirogwa na mhindi lazima ukatibiwe India, na ukicharazwa na mwarabu, lazima upate tiba ya mwarabu-Dubai. Umejiamini mno, utachemsha. Wadau, msiwachukie wahindi na waarabu, wanasimamisha mambo mengi ya biashara na uchumi. Wategemea mchaga atakupigania katika kupiga vita umaskini? Hata siku moja, mchaga ni chapa mbaya, ina tamaa na wizi huwa ndio alternative. Mlahabwa, UK

    ReplyDelete
  68. MKO WAPI PETER NALITOLELA, JOHN MASHAKA NA US BLOGGER? WATU TUNATAKA KUSIKIA MAONI YENU.............!

    KUNA WATU WAWILI NIMESHANGAA COMMENT ZOTE HIZI KALIBU 70 SIJAONA MASWAHIBA WAWILI HAPA WAKITOA COMMENT ZAO SIJUI NI KWA NINI WAMEKAA KIMYA SI KAWAIDA YAO NA HAO NI PETER NALITOLELA NA JOHN MASHAKA? SIJUI WAMEKATIWA MTANDAO MAANA WAO NI MAHODALI WA KUJIBU COMMENTS KAMA HIZI PIA SIJAMSIKIA US BLOGGER...

    ReplyDelete
  69. AnonymousMay 06, 2009

    Huyu Rostam Aziz sijui nianzie wapi? Kuanzia hapa Nzega hadi jimboni kwake Igunga Rostam kaua sana tembo na chui ajili kusafirisha meno ya tembo na ngozi za chui
    kaka Michuzi usinibanie comment yangu la sivyo Mungu atakuhukumu.

    ReplyDelete
  70. AnonymousMay 07, 2009

    RUSHWA MBAYA SANA. RUSHWA UNAKUWA MTUMWA NA UNATUMIKA KAMA M'MBWA.
    PAMOJA NA KUDAI ETI NATAKA KUWEKA WAZI KILA MTU AONE, HAPA KUNA MKONO UMEINGIA KWENYE BLOG HII ILI HAYA MAMBO YATOLEWE.
    JAMAA ANAPITA AKIJIDAI ANATEMBELEWA NA WATI LAKINI MOJA KWA SIKU AMBAYO NI ZAIDI YA MAGAZETI MATATU AU MANNE BONGO, INAMSAIDIA KUTIA MKONO KINYWANI KWA MADAI WATU WENGI HUPITA NA KUSOMA BLOG YAKE.
    NA KWA VILE MTOA RUSHWA HUWA PUMBAVU, HAANGALII KATI YA HAO LAKI MOJA, NI WANGAPI WALIOPITA NA KUTOA HOJA ZAO! KWA HIYO KATI YA LAKI MOJA, NI WATU 50 TU AU WATANO WAMETUPIA MACHO HOJA HIZO,
    WENGI HUMU HUPITA KUANGALIA PICHA NA SIYO KUSOMA HOTUBA ZA KUTANGAZA MISHARA HEWA KILA MWAKA WAKATI KINACHONGEZWA HAKUNA.

    RUSHWA, MBAYA SANA. ADHABU YAKE INGEKUWA KUNYONGWA KWA KUPIGWA SHABA HADHARANI AU KITAZI DAMN IT.

    ReplyDelete
  71. AnonymousMay 07, 2009

    UKWELI NI KWAMBA MENGI UPO JUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  72. AnonymousMay 08, 2009

    Huyo wa kushoto sio Joachim Chissano?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...