
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagara, Kanali Issa Njiku, ( wapili kutoka kushoto) aliyenusurika katika ajali iliyotokea Mei , 4, mwaka huu eneo la Chamale, Kijiji cha Magubike, Wilayani Kilosa, katika Barabara kuu ya Dodoma - Morogoro, wakanza kushoto ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Ukerewe, Mkoani Mara, Queen Mlozi.
Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera, Kanali, Issa Njiku, na watu wengine wawi akiwemo Dereva wake wamenusurika kifo baada gari lenye namba za usajili STK 2896 aina ya Toyota Land Cruser , kuacha njia na kupinduka eneo la Chamale, Kijiji cha Magubike, Wilayani Kilosa, kwenye Barabara kuu ya Dodoma- Morogoro.
Kanali Njiku alikuwa akitokea Mkoani Kagera katika Wilaya hiyo , kwenda Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya awali ya siku nne kwa Wakuu wa Wilaya wapya waliteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kiwete.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema, ajali hiyo ilitokea juzi ( Mei 4) mwaka huu eneo ambalo, Aprili 24, mwaka huu ilitokea ajali mbaya ya Basi RS Investiment, ambalo lilikuwa likitokea Mkoani Kagara na kusababisha vifo vya watu watatu,akiwemo Bunge wa zamani wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Phares Kabuye kupitia Chama cha TLP.
Eneo hilo mbali na kutokea kwa ajali hiyo, pia ajali nyingine mbili zaidi zilitokea ndani ya mbili ambapo Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Morogoro, Mwenyekiti wake Mhandisi Petro Kingu na Katibu wake Mary Chatanda na wengine wawili na Dereva wao walinusurika vifo.
Mbali na ajali hizo mbili, Mashabiki kadhaa wa timu ya soka ya Simba wa Jijini Dar es Salaam, walipata ajali katika eneo hilo wakati wakirejea kutoka Dodoma kuishanagilia timu yao na kusababisha watu 12 kujeruhiwa huku wengine wanne kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Akizungumzia na Gazeti hili kujhusiana na ajali hiyo jana mjini hapa, Kanali Njiku, alisema walipatwa na mkasa huyo majira ya saa 7: 30 mchana wa Mei 4, mwaka huu eneo la Magubike ambalo ziliwahi kutokea ajali tatu ndani ya wiki moja ya Mwisho wa mwezi wa nne , mwaka huu.
“ tumepata ajali mbaya sana , lakini tuna mshukuru mungu wote watatu tuliokuwemo kwenye g ari tumenusurika na tumetoka salama baada ya kubilingika mara tatu…” alisema Kanali Njiku na kuongeza kuwa.
“ nilifunga mkanda na ulinibana …lakini naumenisaidia , nilipotoja nje kujichunguza nikajiona nipo salama na neno langu kubwa nikamshukuru mungu” alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Misenyi
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, kwamba siku hiyo mvua ilikuwa ikinyesha katika maeneo hayo na mara aliona gari yao inaanza kuyumba Barabarani na kutahamaki walishitukia wakupinduka mara tatu.
Hata hivyo alisema kipande cha lami iliyowekwa eneo hilo la Barabara kimeonekana ni cha kiwango cha chini kuwa laini hali inayosababisha kutokea kwa ajali za mara kwa mara kufuatia utelezi nyakati za mvua na pia nyakazi za jua kali.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, kwamba, Askari wa Usalama Barabarani wa Kituo Kidogo cha Polisi Dumila, Wilayani Kilosa, wamedai kuwa eneo hilo ni maarufu kwa kutokea kwa ajali za magari.
Alisema kuwa , kwa mujibu wa Askari hao, zaidi ya magari matano hupata ajali kwa siku nyakati za mvua na zaidi ya mbili pia kwa siku.nyakati za jua kali hali mbayo inatishia maisha ya watu na mali zao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengeye, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo hilo na kwamba hakuna mtu aliyefariki Dunia.
Hivi karibuni baada ya kutokea kwa ajali ya Basi Dodo la Mashabiki wa Simba, Mwenyekiti wa timu hiyo, Hassan Dalali aliiomba Wizara ya Miundombunu kuifanyia ukaguzi Barabara kuu ya Dodoma - Morogoro inayopitia cha Magubike, Wilayani Kilosa ili kupunguza ajali za mara kwa mara.


hivi unajuaje kwamba umenusurika kifo?
ReplyDeleteUK a.k.a Ukerewe haipo Mara ni Mwanza!
ReplyDeleteMh hilo eneo la ajali lazima lina kitu.
ReplyDeleteTanzanians it is time now we need to pray hard, if u are not a believer better be one and learn to pray, otherwise the spirit of darkness gonna finish many, (sory to say but it is true) Omba kabla hujasarifiri,hujaanza siku yako specificaly, tumia damu ya Yesu kuondoa kila aina ya matambiko yaliyofanywa barabarani and your journey or lets say life will be safe and healthier.
Wakati ndo huu.
Kikwete tafadhali ingilia kati hii issue ya usalama barabarani viongozi uliowateua kwa hii kazi ni wazi hawafani kazi yao maradufu. Kila siku maisha ya watanzania wakakamavu achana na viongozi wa taifa yanapotea au watu wanakuwa walemavu etc...this is the serious issue than who is eating what (Walaji)...
ReplyDeleteMwandishi wa hapo juu, wilaya ya Ukerewe iko mkoani Mwanza na si Mara.
ReplyDeleteJamani; Mkuu huyo ameshasema kwamba lami iliyowekwa kwenye sehemu hiyo ni dhaifu. kwa kuongezea askari wa usalama wa barabarani eneo hilo wanasema eneo hilo ni maarufu kwa ajali. Hivi jamani sisi wananchi nani atatutetea?
ReplyDeleteHilo la ajali za mara kwa mara limedhihirishwa wazi na huyo mkuu wa wilaya na polisi kwa kuthibitisha wazi kwamba ajali hizo zionatokea zaidi wakati wa MVUA na JUA KALI. Hii ni wazi inaonyesha udhaifu wa barabara katika matengenezo. Hivyo basi vyombo husika vichukue tahadfhari ya haraka kwani sasa imekuwa too much.
Au nani alipewa hiyo tenda ambaye anajaribu kutetewa kwa wahusika kulinyamazia?.
Ni mimi Mkereketwa wa nchi.
Wakerewe mababu zao wako Mara,
ReplyDeleteMwanza wameenda tu kwa sababu walichoka kuwa chini ya Wakurya wa Msoma.
Hata kama utaihamisha Ukerewe kuwa mkoa wa Mbeya bado watakuwa ni wajukuu wa mara tu....... yego!kutiki......tehe tehe tehe watani
Wahusika wakuu ni Askari wa usalama barabarani. Siyo sahihi kusema eti eneo hilo linasababisha ajali mara kwa mara. Ila ni kudhibiti eneo hilo:-
ReplyDelete1.Kuweka alama za kuonya-Danger n.k
2.Kiwango cha kasi kiwe 20km
Haitatokea tena ajali eneo hilo isipokuwa madereva wanaojua kuwasha gari tu na sio wanaojua kuendesha gari (wanajua sheria).KINGUTI/UBALOZI MAPUTO
JAMANI VIONGOZI WA NCHI HII ACHENI KUCHEZEA MAISHA YENU. HIVI KIPI NI RAHISI NA NAFUU,KUPANDA PRECISON AIR AU KUMUVUZISHA GARI ALL THE WAY TOKA MISENYI MPAKA DAR? HUYO DEREVA LAZIMA ALIKUWA AMECHOKA NA NDIO MAANA HAKUWEZA KUONA UBOVU WA BARABARA. HII YOTE NIKUTAKA AKIFIKA DAR APATE GARI YA KUTANULIA MITAANI.USALAMA KWANZA JAMANI
ReplyDelete