Bro Michu,
kwa mara nyingine tena kwa hisani yako Naomba niweke ombi langu katika blog yako ili wadau waweze kunisaidia,wadau kama mtanikumbuka mimi na itwa Majuto niliwaomba wadau wa pande zote waweze kunipatia data za box huko ughaibuni wiki chache zilizopita. ninawashukuru wote walionisaidia kwa mawazo yao mazuri na hata walionitusi niwashukuru pia.
Leo ombi langu kwenu wadau ki kwamba tayari nipo ughaibuni leo ninasiku ya nne nipo hapa uswidi katika sehemu iitwayo Sodertalje si mbali sana kutoka Stockholm kwa wale wanaofahamu.
Sasa wadau ombi langu ni jinsi gani nitaweza kuanza kupiga box au nisonge mji gani ni rahisi kupata kupiga box wadau naombeni msaada wenu katika hili hasa wadau wazoefu wa box na hata wamashambani mimi nipo kikazi zaidi sichagui kibarua chochote nitafanya.
Kama nitapatiwa na mchanganuo wa kiasi gani wastani kwa saa itakuwa vema sana, natanguliza shukrani nyingi sana kwenu wadau bila kumsahau bro Michu.
MDAU mpya wa box
sodertalje
Majuto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2009

    Nimeishi Sweden, nchi moja kame mno kupata hela....Si unajua wajamaa hao.
    Lakini, utatakiwa upate kibali cha kufanyia kazi ili uweze kukatwa kodi, na utalipwa labda shilingi elfu 60 za kitanzania kwa saa.
    Ukweli ni kwamba Sweden siyo nchi ya kutengeneza hela, lakini usikate tamaa.
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2009

    kaza msuli na upate kibali ufanye kazi, ila kama alivyosema mdau hiyo ni nchi kame kutengeneza hela, ila utapata kidogo, kuna ndugu yangu alikuwa huko anasoma na mara baada yakumaliza nilimwalika akaja UK akatengeneza hela kwa kama mwaka mmoja kisha akaenda Bongo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2009

    kaaaazi kweli-kweli na hii UZUSHI wa michu umu bloguni,,,

    ivi uko hakuna mitandao acheki iyo kitu anayotaka??

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2009

    huyo mdau wa kwanza anaota nin au alikuwa sweden gan yaan kama usd50 kwa saaa ni box au professional hapa uk kwenyewe nchi bwerere kumek huwez pata hiyo minmum kwa uk ni kama usd12 kwa saa na max ni 24 yaan boxxxxxxxxxxxx

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2009

    Pamoja na jamaa hapo juu walivjo kushauri,Mimi naongezea kuwa achana na tabia ya kutegemea kutoka haraka,ila kama ni bahati yako unaweza kupata vibali na siku hiyohiyo ukapata muelekeo.Uko ktk ulimwengu wa vibali wala usije uka puuzia jambo lolote.Kama kawaida kwa sasa utasema kazi yoyote hapo baadae utaanza kuchagua kwani ndio zenu wabongo.Jambo ya muhimu usije ukavunja sheria yoyote kwani utajiharibia kila kitu.Dazd@windoslive.com

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2009

    NYIE MA ANO´N WOTE ACHENI KUCHEMKA SWEEDEN PESA IPO LABDA MTU UWE UMELAZA DAMU.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2009

    wanadu huyo ni michuzi anatafuta mchongo wa box mbele anaona aibu kuweka mambo wazi

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2009

    Huyu Majuto kaingia hapa!! nimesoma habari zake juzijuzi alipokuwa anomba ushauri kupitia blog hii. Sasa bw. Majuto tuliza kichwa uangalie maisha, na haya mambo ya kutafuta ushauri humu kwenye blog achana nayo kabisa. Humu hutapata ushauri wowote tena Michu angekuwa hapitii hizi comments ungeambulia matusi tu, nina hakika zimetumwa nyingi tu za kukutusi ila Michu amekuokoa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2009

    we tafuta jimama likuwowe hilo ndo dili...

    ReplyDelete
  10. USIJALI NDUGI YANGU MIMI NILIKUWA SWEDEN NA NIKAZICHANGA SANA ACHANA NA HAO JAMAA SIKILIZA
    NENDA MJI KAMA VEMLAND MAENEO YA KASTAD.OREBRO.ALVIKA.TROLHATANI AU KIRUNA JAPO SI PAZURI KWA KUWA UMETINGWA HAPO SWIDI LAKINI FATA HUU USHAULI PIA WAEPUKE SANA AU KUWA MAKINI NA WABONGO WA UKO WAONGO MAJUNGU KULEWA HAYO NDIO WANAYO YAWEZA.EPUKA MIJI KAMA MALME,GOTBAGI,HATA STOCKHOLM,KUMBUKA HUU NI USHAURI WEWE NDIE UNAJUA KUSUKA AU KUNYOA NI WEWE NDIE UTAKAE JUA ULIPOTOKA NA ULIPO
    KILA LA KHERI INSHALLAH KAZA BUTI,KIMBE JOHASSON

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2009

    Mwenzako anauliza napewa ushauri sasa wewe kama unaushauri wa sehemu hiyo pesa na vibali vinapatikana kirahisi si mumshauri mwenzenu? Wew unasema wenzako labda wamelaza damu wafundishe basi jinsi ya kuchangamka na wapi pa kuchangamka....kaaa!
    Siko Sweden lakini ningekuwa nisingesita kukupa ushauri mbongo mwenzetu ndiyo kuendelezana hivyo jamani....an in turn na nchi yetu tunaiendeleza.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2009

    nadhani mdau namba 1 umekosea, itakuwa ni sh 6000 kwa lisaa. minipo sweden ila huko uliko sipajui. njoo gothenburg nahisi mabox ni mengi japo mimi sipigi box. umekuja kwa visa gani? km umekuja kidili unatakiwa kujiandaa ukajilipue mkimbizi, sema nimeolewa naogopa kukukaribisha kwangu, shemejio hasijesema nimeibua. Mungu akusaidie

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 06, 2009

    Sasa ndo utathibitisha ubinafsi wa Wabongo wa Uswidi! Yangu macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...