wadau wakiwa tayari na nondozzz zao
picha ya pamoja ya nondozzz ya tasam
wadau kibao chuo kikuu cha university of  mysore huko india majuzi wamevuta nondozzz zao. hongera sana wadau wa mysore ambao wengi wengi ni wadau damu wa globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2009

    Hogereni sana. Ila da mpo wengi wabongo! Utafikiri ni tawi la Tumaini University India

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2009

    Ni hatua kubwa tumeifikia, kila la kheri kwa Graduates wote, God Bless.

    ReplyDelete
  3. GraduateMay 09, 2009

    God bless all the graduates, ni hatua kubwa na ngumu tuliyoipita. Hongereni sana vijana, tupo pamoja.

    ReplyDelete
  4. Al MusomaMay 09, 2009

    Sikujua kama India pia kumejaa waswazi kama wahindi walivyojaa uswazi...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2009

    Inamaana hiki chuo ni cha mablaki watupu? au hiyo picha imepigwa maalum kwajili ya waswazi peke yao?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2009

    Karibuni nyumbani na ubabaishaji wa wahindi!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2009

    kwanza hongera kwa wote waliomaliza masomo yao. pili nilingelipenda kuuliza ni kitu gani kinachowavuta watanzania wengi kwenda kusoma india miaka ya hivi karibuni? je ni kwa sababu ya kiwango cha elimu au unafuu wa tuition fee au urahisi wa kupata nondoz? nielimisheni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2009

    Big up sis and broz, ila how come mpo wengi namna hiyo??? yaani kama mpo UDSM vile!? na nina swali la kizushi kwenye class zenu mlikuwa nyie tuu au kulikuwa na wanafunzi wa kihindi na nchi nyingine? coz kama mlikuwa nyie tuu mhhhh, na kama kulikuwa na wengine why hamkutake nao hizo pics?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 09, 2009

    duh!hicho chuo kimejee wabongo kama patric lumumba people's friendiship university cha moscow! na wabongo wakijirundika sehemu moja vituko huwa havikawii kuanza!! lakini hongereni kwa kuvuta nondo zenu, maisha ya usomaji sio mchezo!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 09, 2009

    nakwambia mysore ni kijiji cha watanzania......tuko kibaoooo

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 09, 2009

    Congratulations to all of you...at least nyie huwa shule mnamaliza na kurudi kwenu...abongo wa US,Europe and some other countries shule hawamalizi wanabaki kung'ang'ania nchi za watu halafu eti mtu mwenye familia anafanya kazi za dola kumi...jamani someni mrudi nyumbani...ushauri wa bure maana wengine mnaona sifa kuwa nchi za watu lakini hamna lolote la maana mnalofanya
    misupuu usinibanie

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 09, 2009

    Hongereni sana, mi nawashauri mjipange mrudi home kujenga taifa, mkianza kusema ''ngoja tusuburi tuone ustaarabu'' kama ndugu zetu wa Ulaya na Marekani, mnaweza kuishia kubeba boksi udosini! Duh! afadhali boksi la ulaya kuliko udosini!
    Mdau,
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 09, 2009

    Kisomo kitu bora kabisa ndugu wahitimu. Piganeni mpate na nondoz za juu zaidi

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 10, 2009

    Nyie mnaosema wasibakie nje ya nchi, iwe ni kwasababu mnataka watoe maarifa yao nyumbani TZ. Lakini kama mtu akirudi TZ anaanza kuhangaika tu kutafuta kazi, kwanini asibakie huko India?


    Afu wewe uliyekandia kazi za US na Ulaya, unasema kazi za $ 10, una maana gani? Kama nalipwa $10 kwa saa, na nina saa 10 kwa siku, shida gani ipo hapo. Hakuna mbongo hata mmoja anayepokea $ 10 kwa siku, huo ungekuwa uzushi. Mie najuwa wanaolipwa hata $ 20, 30 kwa saa.

    Mimi kwa mfano, natangeneza $ 100 minimum kwa siku hapa. Huwa naona si hela nyingi sana na wala si ndogo pia. Sasa, niambie, Bongo nani atanilipa hela hiyo? Acha majugu kwa kufuata tu upepo wa watu kukandia kazi nje.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 10, 2009

    Wewe anonymous wa 12:44am unasema unatengeneza $100 kwa siku na unaridhika na maisha? Basi utakuwa huna morgage au gari la uhakika! Je unalipa kodi pia?
    Mie niko Canada na nalipwa $45 kwa saa (napata $315 kwa siku kwa kufanya kazi masaa 7) lakini narudi nyumbani kwani hapa hela hizo hazitoshi kitu...ni kulipa madeni tu! In Tanzania I will have a more relaxed life and less stress; after all sitakua nacha kulipa morgage tena. Nyumbani ni nyumbani tu. (mjijenge kwanza kabla hajafikiria kurudi Bongo)

    J.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2009

    Mdau unaelipwa dola 45 kwa saa unatudanganya, kwani kwa malipo hayo ni kama unapata zaidi ya milion kumi na mbili za kibongo mwezi halafu unatuambia hazikutoshi sababu unakatwa kodi achakudanganya watu sisi wote tupo uhaibuni ndani ya milioni kumi nambili hata uwe unakatwa kodi na malipo kadhaa bado utabakiwa nafedha nyingi sana ukulinganisha na mishahara ya bongo.kama umeamua kurudi nyumbani werudi tu siyo useme sababu ya mshahara kidogo, mimi nipo uswidi napata dola 100 kwa siku na nimeweza kuishi bila tatizo na kiasi naweza kutuma nyumbani, wadau wengine naombeni mtoe mchanganuo ili huyu jamaa siku nyingine asendelee kudanganya Mdau SWEDEN.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2009

    ZAIN, ZANTEL, TTCL, TIGO, VODA zinawasubiri wasomi wetu

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 11, 2009

    WEWE MTU WA CANADA, KWANINI UWE NA MORGAGE? NI UCHAGUZI WAKO TU. UNAWEZA KUISHI KWENYE APARTMENT ZA KODI NAFUU. PIA KURUDI BONGO SABABU HAKUNA KODI NYINGI NI KUENDELEZA TU UMASIKINI, MAANA TZ HAMNA KODI NYINGI NA NDIVYO WANANCHI WETU WANAENDELEA KUWA MASIKINI.

    HALAFU DOLA ZA CANADA NA USA ZIKO TOFAUTI. HUWEZI KULINGANISHA DOLA YA USA NA CANADA. NA PIA INATEGEMEA UNAISHI KWENYE MJI WA KIWANGO GANI CHA MAISHA. KUNA MIJI AGHALI NA ILE YA RAHISI. HATA HAPA USA KUNA WANAOLIPWA ZAIDI YA HIYO $ 45 UNAYOLIPWA KWA SAA WEWE.

    HUJAJIBU SWALI LANGU PIA. UKIMALIZA CHUO NJE NANI ANAYEKUAHIDI KAZI MARA TU UMALIZAPO CHUO NJE? KAMA UNAELEWA MJADALA UMEANZAJE, NI KUWA WANAFUNZI WA INDIA WASIZAMIE HUKO. SIYO TU SWALA LA KURUDI AU KUBAKI. NADHANI ISSUE KUBWA NI OPPORTUNITY.

    J.K. - USA

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 11, 2009

    Wewe ndugu yangu wa canada unayedai kuwa unatengeneza $45/h unanisikitisha sana na sijui nani anaweza kukulipa hiyo $45 kwa saa kama hata spelling za Mortgage unakosea na kuandika morgage. naomba urudi shule tena. Otherwise malipo ya majuu ni zaidi kuliko nyumbani na kama unampangilio mzuri wa pesa unaweza hata kusomesha ndugu au jamaa wa tatu kwa mpigo kwenye vyuo vyetu vikuu vya TZ. Kalenga Boy

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 11, 2009

    Nyie msioamini kuwa kipato changu ni $45 kwa saa na fedha hizo hazitoshi huku Canada basi sijui uelewa wenu na kiwango chenu cha elimu; kwani S100 kwa siku ni dola 10 na senti hivi kwa saa ambayo ndiyo malipo ya kiwango cha chini hata huko Marekani na Canada pia.
    Dollar ya Canada ilikuwa sawa na ya US mwaka jana na sasa hivi ni Centi 90 hivi za US ndiyo $1 ya Canada hivyo ziko karibu sana na CAD$ inapanda kila siku.
    Naishi kwenye mji mkubwa wa nchi hii wenye standard za juu za maisha na Canada ina kodi kubwa ukiwa na mshahara mkubwa.
    Wewe unayesema hutaki kununua nyumba nakuwa na Morgage eti kwa vile kuna apartments za kupanga siwezi kubishana na wewe kwani how you view life is different from me as I believe we are different in our standards. When you buy a house/apartment its an investiment and here it appreciates ... eventually you are making money rather than just renting which all $$$ is going down the drain....

    Point ya opportunity sikuizungumzia kwani point yangu ilikuwa ni kumwonyesha huyo wa $100 kwa siku kuwa "Its not a big deal...that money is peanuts"
    Uamuzi wa watu kurudi Tanzania au kwenda kwingine ni 'Individual decisions' Still wanaweza kufanikiwa hata wakirudi Tanzania na kutafuta ajira nzuri au waende popote kwingineko...hayo ni maamuzi ya mtu binafsi.....After all I graduated from a University closer to where they are.

    J.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 11, 2009

    WE MDAU WA CANADA ACHA UONGO,AU ULIENGA KUCHUKUA DIGRII YA UONGO ILI UKAIFANYIE KAZI BONGO. MDAU WA BOX WAMILELE HADI KUFA.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 11, 2009

    choli nehieee!!

    jaman ni group photo ya wabongo tu,si pozi za picha yao lakini??

    hongereni kumaliza sehemu ya malengo yenu

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 11, 2009

    WILLBARD MKOBA TUWASILIANE EMAIL YANGU NI humudi5@gamil.com

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 11, 2009

    Hongereni sana brothers and sisters, Karibuni tena nyumbani.
    Nakuona Enock Chenya picha hapo juu wewe wa katikati. Hongera sana my brother....hope to see u here...

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 11, 2009

    Mdau wa canada acha kuwadanganya wenzio,usidhani ni wote wawajui au hawajafika huko canada. mimi nipo swedeni na nilikuwa hukohuko canada na hapa nalipwa 100 kwa siku na life inakwenda kama ilivyopangwa,nilicho jifunza kwako wewe lazima utakuwa muhaya kwasababu mnapenda sasa sifa za kijinga na kujikweza
    Mdau wa box KIRUNA SWEDEN

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 11, 2009

    hongera hongera sana... rudini kupambana na mafisadi basi wanaofikiria sisi kichwani ni bwelele!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 11, 2009

    hey guys that was a tanzania students assosiation graduation that was held by the students themselves another is to be held by the international students in june.and mysore university has alot of students so we all cant be in the same pics..infact u shud congratulate them for being united to have carried out such a big event on their own.big up guyz rudini bongo mkabanane na waosha vinywa.dont stop there go for masters.
    mdau hapo juu wa 2:39 pm kama unaona degree kupata india ni rahisi huku hamna degree za chupi kupata kama vipi njoo nawe upate usiishie na form 4 or six.tuition fee is very cheap if u can afford it.

    ReplyDelete
  28. Kichwa KigumuMay 12, 2009

    Hongera kwa waliomaliza elimu hapo India. Pia hongera kwa yeyote anayemaliza degree yake popote mwaka huu, iwe TZ-vyuo vyote ,Uganda,Kenya South Africa, UK , Canada, US , Sweden na kokote kule duniani, Hongera zenu.
    Kama una degree hongera , na kama huna kwa sasa ila bado unasoma hongera pia, na kama huna degree, husomi na uko nje unafanya kazi hongera pia kwani ndo chaguo lako na kila mtu anaheshimu hilo.
    Ila huyu aliendika hapo juu kwamba walio UK , Canada au USA wanaishia kufanya kazi za dola kumi kwa saa na hawarudi nyumbani naona ana-matatizo sana na walio nje hasa Uk, Canada na US.
    Kama sehemu hujafika au ulifika zamani ukaondoka usilaumu kushindwa kwako maisha na kuwaona waliobaki kwamba hawana akili.Mambo yanabadilika kila siku na dunia inabadilika. Wewe leo US imemchagua mtu mweusi kwa mara ya kwanza zaidi ya mika 500 iliyopita wewe unawambia watu eti warudi nyumbani. Siku hizi nyumbani ni nchi au pale unapopta mkate wa kila siku.Watu wamekuja kusoma huku nje sasa wana-watoto na watoto wao kwao ni huku na wala sio TZ. Wewe binafsi bila baba yako kuja Dar kufanya kazi kutoka kijijini kwenu Kandote(Kigoma), usingezaliwa Dar, hivyo basi wewe rudi Kandote-kigoma ukasaidie kijiji cha babu yako na baba yako, maana una uchungu sana na walio nje.
    Kwa taarifa yako -Hujui data za watu wangapi kwa-ujumla wanamaliza degree zao kila mwaka UK na USA na picha zao hutaziona sehemu yoyote.
    Kwa taarifa yako WATZ wanaomaliza vyuo USA tu kwa kiwango cha degree ya Associate na bachelor ya kwanza kila mwaka hapo USA,(May na December kwa jumala) katika majimbo (states)50 yote ni takribani ya wanafunzi 430(mia nne thelathini)kila mwaka . Na WATZ wanaomaliza kwa kiwango cha Masters hapo USA tu kila mwaka ni 90(tisini)
    Pia kwa kila mwaka WATZ kwa ujumla wanaoishi marekani tu (pekee yao tu)yaani (USA) kwa data za kutuma fedha nyumbani TZ, mwaka jana pekee (2008) walituma USD 100,000,000.00 (dola za kimarekani millioni mia moja).
    Kwa ujumla unatakiwa kushukuru sana sana tena sana hao unaosema wanabeba maboksi hapa US na ambao wameacha familia zao TZ. Maana wanazidi kuwatumia fedha angalau kiasi cha kufikia millioni mia moja dola za kimarekani, ndugu zao TZ.
    Huo ni mchango mkubwa sana tena sana katika uchumi wa TZ kwa kila mwaka. Sasa wewe ulitaka warudi TZ halafu walete mchango upi, ambao wewe unautaka hapo utakaoweza kuleta hizo fedha zote kila mwaka.
    Wakenya tu walio nje tena ndo wanaofanya hizo kazi unazosema zaidi ya waTZ na kwao wasomi wa kumwaga mpaka wanakuja TZ kutafuta kazi wanatuma 400 million USD kila mwaka. Wa-Nigreria 2008 walioko hapo USA pekee walituma US-Dollar million 900. Na Wa-Mexico wanaongoza kwa hizo kazi unazozikandia wewe hapo USA, mwaka jana tu 2008 walituma USD billioni 3. Na kwa sasa ndio wanategemewa na nchi yao kama kii-ngizio cha kipato kikuu cha tatu kwa uchumi baada ya mafuta,na utalii au Viwanda
    Iko hivi watarudi waliomaliza sehemu ambazo hawatumi fedha nyumbani bali wanatumiwa fedha za kusoma kutoka nyumbani.
    Kua uelewe kila mtu anjenga nchi kwa mtindo wake, wewe unataka hawa jamaa waliosoma the first world country inayoshikilia Economy takribani 2/3 ya dunia warudi nyumbani kuabika kwa kuona watu wanaiba fedha kila siku bila ethics , moral wala huruma kwa wananchi wenzao walio vijijini wasio na maji, madawa, shule wala elimu bora.
    Kwa taarifa waliomaliza hapa USA , wanajifunza shida, na wanajikamua katika shida kila siku inavyokucha na wengine weshaanza kula sukari walioisomea siku nyingi zilizopita.
    Kuna states hapa USA, WATZ karibu 3/4 wanaoishi hapo wana degree zao, pia kuna states watu wanapenda kufanya kazi na wote- at the end wanamalengo kwamba mafanikio yako njiani. Tusianze kudharauliana sasa. Maana tukianza hivyo tutaona mara msomi chuo kikuu Dar anamdharau Tumaini, na mara Msomi Makerere atamdharua UDSM, na mara msomi CapeTown atamdharau Makerere na mara India atamdharau Cape , then China atamdharau msomi India, Then Russia atamdharau msomi China, then Sweden atamdharau msomi Russia, then Canada atamdharau Msomi aliyesoma Sweden, then UK atamdharau msomi Canada, na hapo ndipo US atamdharau msomi UK na wasomi wengine popote.
    wasomi tuache hizo na wasiosoma pia tuache hizo, wote ni WATZ na mafanikio ya aliye nje au aliye ndani awe amesoma au la , kama haku-fisadi basi Hongera kwake mara elfu mbili.
    Naomba uache dharau kwa walio nje, wewe endeleza mambo yako hapo ulipo na shukuru kila kitu kinakwenda.Hao wezi unaowasifia hapo TZ ndio wakuwaambia waache wizi huo kwa kuwa wanaliangusha taifa na kuongeza umaskini kwa wananchi.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 12, 2009

    Hongereni ndugu, turudi nyumbani sasa tukafanye mambo ya maana ,kutumia elimu tuliopata na kuweza kuleta maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 12, 2009

    Asante Kichwa Kigumu 1:02am kwa maelezo yako yanayojitosheleza....asante pia kwa hizo figures za maendeleo tunayoyatoa nyumbani kwa kutuma fedha...$100M ni nyingi sana na ni mchango mkubwa sana. Je unaweza kutupa link au other details as to how those figures were found?

    Nyie mnaonikandia kuwa $45 ni uongo na degree za uongo toka India n.k. muelewe kuwa ninakofanya kazi kama Engineer kuna wanaolipwa zaidi sana ya hiyo $45 kwa saa!
    Pili mimi sio Mhaya and if I was one I would have been proud of my heritage but I am not....and to shock you more; I am a lady.

    J.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 12, 2009

    Kiruna wa Sweden kweli wewe mpumbavu sana. Mmi huyo jamaa J, wa Canada ninamkubalia kwa kupata CD 45 kwa saa. Kuna WA-TZ wanne wamesoma MSN-masters of science in Nursing niko nao hapa Arizona, US na sasa ni ma-physician assistant wanapata USD 40 kwa saa, wengine watatu wamesoma MPT-Master ya physical therapy wanapata USD 50,na ni ma-physical therapy na mwingine mmoja amesoma Master ya anasthesia huyu anapata USD 70 hadi USD 100 kwa saa inategemea akiwa stationed hospital au travelling. Pia tuma ma-engineer wawili hapa Tucson, Arizona, wako na Federal roads rehabilitation wanapata USD 50 kwa saa moja.
    Sasa wewe Kiruna wa Sweden kama ulikimbia umande huko Canada ukaenda Sweden shauri yako binafsi.
    Iko siku utakuja kuwa OK kama ukienda chuo na kumaliza kinachotakiwa, na kama hutaenda ila unapiga mzigo wako kama ulivyosema sawa tu , maana maisha popte. Ila kubisha kitoto eti J , wa Canada hapati CD 40 kwa saa , basi inaonekana hujawaona WATZ au watu kama hao huko Sweden, na hutawaona maana hawatajichanga humu katika bogu ya jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...