Mgeni rasmi Katibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi Omary Khama (kushoto)akizungumza na Mwenyekiti wa shirika la RSM Ashvir, Brian Eaton (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa RSM Ashvir Jean Stephens, katika uzinduzi wa kampuni hiyo inayojihusisha na ukaguzi wa mahesabu. Uzinduzi huo ulifanyika usiku kuamkia leo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.
Mgeni rasmi Katibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi Omary Khama,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampumi ya mahesabu RSM Ashvir usiku kuamkia leo katika Hotel ya Kempnski.

Mwenyekiti wa Shirika la RSM Ashvir Brian Eaton akishikana mkono na mfanyakazi wa shirika hilo Steven Matojo kabla ya kupokea zawadi yake, hiyo ilikuwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza ubora na ufanisi wa kampuni hiyo duniani kote.

'KAMPUNI ZA UKAGUZI WA KODI ZA KIMATAIFA KUONGEZA UFANISI NCHINI'

SERIKALI imesema kuongezeka kwa kampuni za ukaguzi wa fedha za kimataifa nchini kutaongeza uwazi na usawa katika kuripoti masuala ya kifedha na yanayohusiana na ufanyaji biashara.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na katibu wa waziri, Omari Khama wakati wa uzinduzi Kampuni ya ukaguzi, uhasibu na mambo ya kodi ya RSM Ashvir Intenational.
Akifafanua Mkullo alisema uwepo wa kampuni nyingi za kimataifa pia unaongeza idadi ya wawekezaji nchini ambao wanalisaidia taifa kukuza kiwango cha uchumi na pato lake na kuiletea maendeleo Afrika kiujumla.
“Uzinduliwaji huu rasmi wa kampuni ya RSM Ashvir International umefuatia taarifa za kuwepo kwa mazingira salama ya kiuwekezaji katika sekta za fedha iliyotolewa kwa wadau wote suala ambalo limechagiwa kwa kuzingatiwa kwa sheria nchini,” alisema Mkullo.
Mbali na hayo alieleza kuwa suala la utawala bora na ripoti safi ukizingatiwa kwenye sekta ya ukaguzi ndio suluhisho katika kuleta maendeleo na upatikanaji wa soko la mitaji jambo linalowasaidia na kuwafanya wawekezaji kuongeza morali wa kuongeza mitaji yao.
“Kama mnavyojua bila kuwepo kwa utawala bora hata kama kampuni za ukaguzi za kimataifa zenye viwango bora zikiongezeka hazitafanya kazi kwa uwazi, ukweli na usawa. Hivyo ni matarajio yangu uhasibu utakabiliana na changamoto ili kuwe na viwango vya utawala kukuza mapato na uchumi,” alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kampuni hiyo Azim Virjee alisema kuwa ukosefu wa utawala bora usimamiwaji wa sheria ni changamoto ambayo imekuwa ikiziathiri kampuni nyingi za ukaguzi wa fedha kama ilivyo kwa RSM Ashvir International.
Virjee alifafanua kuwa ili kuifanya sekta hiyo kufanya kazi ipasavyo wadau hawana dudi kuiwezesha sekta hiyo ili iwe inayofanya kazi zake kwa vitendo zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo mwenyekiti huyo ameomba ushirikiano wa hali na mali kwa serikali katika kufikia malengo.
Mbali na hayo alitoa wito kwa kampuni zingine za ukaguzi, uhasibu na mambo ya kodi kutoa huduma bora kwa jamii wanayoihudumia jambo alilosema litawaongezea wateja, kuinuia uchumi na kusaidia kuongeza mapato ya taasisi hizo.
Kampuni hiyo iliyozinduliwa rasmi jana jijini hapa ilianza rasmi kufanya shughuli zake nchini mwaka 2007.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2009

    Omari khama kumbuka ulikotoka.umebadilika ndugu yetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2009

    Khamah Omari jitambue kama alivyosema mdau wa juu hapo.kuwa mtu wa vitendo zaidi na si maneno mengi leo upo hapo kesho haupo.
    inakuwaje mtoto wa mjini unashindwa kujitambua?waliokufikisha hapo kama wasingejitambua ungekuwa huko?

    mdau Juma Ali tulikuwa wote kariakoo tukila mihogo kwa marehemu Panju.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2009

    Omari khama naamini ujumbe umekufikia.waswahili husema cheo ni dhamana.jaribu kuwasikiliza watu wako yaani uliokuwa nao huko chini.si vyema watu waanze kukulalamikia.jitahidi kuwa mtu wa jamii kama ulivyokuwa zamani.mie pia nimesikia vilio vya watu wakilia na wewe.

    kuwasikiliza watu kutakupa barka na dhawabu.kuna watu wamekufa lakini wanatajwa kwa wema wao.

    kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema wake huo ni wimbo wa marijani rajabu.wewe ni mtoto wa kigogo hata ujiweke vipi sio mtu wa mikocheni wala masaki.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2009

    Ah! Jamani mbona Khama yupo peace tu, hana uwezo wa kufanya maajabu pale alipo ni msaidizi wa waziri tu. Yupo busy mno, nadhani hamjui majukumu yake. Mie namkumbuka sana Khama enzi hizo akipiga shotokhan/judo pale Mzumbe. Mwacheni agange. Na nyie mkipata title hizo mtakuwa hivyohivyo. Kama ulikula nae mihogo ndo kakuacha hivyo, ameenda shule na sasa anakula matunda. Nendeni shule na nyie kulaleki zenu sio mnaleta story za mihogo, so what...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    kuwa msaidizi wa waziri ndio title ya kuwa na kauli mbaya kwa wenzako?Advanded diploma ya mzumbe ndio shule?wenye Phd itakuwa nini?kina Professor Malima hakuwa na maringo pamoja na uprofessor wake tena toka marekani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2009

    Samahani kumbe hujui unaloandika, ndo maana! Advanced diploma ni nini wandugu kama sio taaluma? Halafu kumbe wewe anony hapo juu umepitwa na wakati hana advanced tu ameongeza shule mshikaji wako. Na inaelekea una hasira sana na maisha tena huenda wewe ndo ulinyimwa mhogo. Umeachwa ndg.yangu na Omary Khama. POLEEE WE!! Professor Malima umemjua wapi wewe? Mtu ashavuta longtime unamzungumzia leo? Enzi hizo za professor Malima mwenzako Omary anakwenda shule. Oh kalaga bao...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2009

    msomi atatoka mzumbe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...