sebastian mwamba na mary gwera wakiwa na pozi la mahaba baada ya kumeremeta hivi karibuni. babu harusi ni mdau wa vodacom tanzania na bibi harusi ni paparazi daily news

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mkuu wa Nanihii nadhani umetumia neno BABU HARUSI ili kuleta usawa ktk lugha kwani siku zote huwa tunatumia neno BIBI HARUSI kwa upande wa pili,lakini nadhani umesahau kidogo maana ya neno lugha kuwa ni sauti za NASIBU.Hii ina maana maneno ya lugha yoyote huwa yanatokea tu,ukitaka kuanza kutafuta usawa ktk lugha utapata shida sana maana maneno kama hayo yako mengi.Nakushauli Michuzi uendelee tu kutumia neno BWANA HARUSI ndilo neno sahihi na sio BABU HARUSI;waswahili tunasema `kuchamba kwingi ni kuondoka na mavi` jiepushe na upotofu wa lugha hata kama watu wanataka USAWA.Ni hoja binafsi naomba kuwasilisha.
    THE KOP
    ST-JEAN
    CANADA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2009

    Nimeipenda hiyo "Babu Harusi", kali kuliko. Na inabidi hata kwenye hafla za kiserikali wakiwa wanahutubia waseme "Mabibi na Mababu", sio "mabibi na mabwana".

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2009

    Hongera sana Seba kwa kutuletea wifi mzuri,upendo wenu uwe hivyo hivyo siku zote za maisha yenu!! Mmependeza sanaaaaa!!! by Alice-Siwangu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2009

    MLIPENDEZA SANA. HONGERENI. MTOTO WENU ATAKUWA BOMBA ILE MBAYA

    ReplyDelete
  5. Wamependeza sana,ila ungetuwekea picha zaidi hata mbili tatu eeh!!!hongereni.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2009

    Bi harusi ni Queen Latifa?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2009

    Hao studio wameharibu picha kwa kujaribu kuiwekea marangi ili muonekane bomba zaidi. wamekufanya uonekane kama huna kidevu bwana. Hongera sana mzee mwamba

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2009

    kwa taarifa yenu , grandmaza ni NYANYA na sio bibi, bibi ni mke kwa hiyo babu harusi ni uzushi

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2009

    we anon. hapo juu grandmaza=NYANYA, wachache tunafahamu hilo lakini linatuchanganya na Nyanya za sokoni! Bibi imetulia zaidi kwa watu wote.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2009

    hongera sana kaka Seba...sipati picha jinsi ambavyo simon,kmo,max na made walivokuwa chicha siku hiyo..hope mambo yalienda poa sana tu...Nsali

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2009

    mbona km wamezeeka ivi,i mean watu wazima ivi!! au ndo background ya picah iyo imeharibu???

    wewe uliesema wanawake wa kibongo ni mkorogo,ni mkeo,mama yako,dada zako anty zako au nini!!

    uwe na adabu

    mumependeza sana

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Mary, kwa kweli mnameremeta! Mama na Mwna tunasubiri product yenu tu! teh teh!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2009

    kwa muda mrefu sijawahi kuona picha nzuri ya arusi naomba muweke na nyingine .mmepeneza mno mnafanana. ni nzuri kuliko ebu tuwekeeni picha. you are very natural GOOD.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2009

    Hongereni picha nzuri sana ila hawa watu wanaofanya uhariri wa picha waache kulipua wanatuharibia wenye kazi zetu.

    ReplyDelete
  15. mama NadineMay 08, 2009

    waaaaaaaaaooooh mmependeza saaaaaaaaaaana,mungu awabariki mkaishi maisha marefu ,awaepushe na vishawishi,awajaalie watoto eemen!!

    ReplyDelete
  16. mama NadineMay 08, 2009

    waaaaaaaohhh Mr& Mrs Seba!!!! mmependeza saaaaaana i like it!!! mungu awalinde katika ndoa yenu eemen


    Mama Nadine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...