Mjasiliamali wa bidhaa za Asili Bibi Renalda Godwin (wa atu shoto) wa Quality Clothing akiwaonyesha kinamama bidhaa zake

Picha na habari na Pascal Mayalla wa PPR

Watanzania wametakiwa kutumia fursa nyingi za kutajirika na kupunguza umasikini, kwa kutumia fursa za matumizi sahihi ya utajiri wa asili uliomo Tanzania katika medani za kiuchumi na kisanaa.
 
Wito huo, umetolewa na Mtalaamu wa Sanaa, wa Shirika la Kimataifa la Elimu na Sayansi la Umija wa Mataifa, UNESCO, kwa nchi za Tanzania, Visiwa vya Comoro, Madagasca, Mauritius.na Visiwa vya Ushelisheli (Seychells), Bw. Tim Curtis, wakati wa Mafunzo kuhusu matumizi ya Nyuzinyuzi Asilia (Natural Fibers) kwa Wajasiliamali wa Tanzania Bara na Zanzibar katika Maadhimisho ya Mwaka wa Kimaifa wa Nyuzinyuzi Asilia yanayofikia kilele chake Jumamosi katika kijiji cha Thai, kilichopo Mtaa wa Chole jijini Dar es Salaam.
 
Bwana Curtis amesema Tanzania imejaliwa kuwa na nyuzinyuzi za uoto wa asili wa aina nyuingi ambazo zikitumiwa ipasavyo kutengeneza bidhaa mbalimbali haswa za mapambo, zina thamani sana katika soko la kimaifa na zinaweza kutumika kuleta utajiri mkubwa sana kwa Taifa.
Bwana Curtis ametolea mfano bidhaa mbalimbali za mapambo kama maua ya asili ya kukaishwa, yana bei mara 5 ya maua ya kawaida katika soko la kimataifa ambalo mahitaji bado ni makubwa kuliko upatikanaji wake.
 
 Bwana Curtis Anaeleza zaidi ....(cue in kwa TV na Redio) lugha ya Kiingereza..
 
Bwana Curtis amesema anashangazwa na umasikini wa Tanzania, huku Tanzania ikiwa imejaliwa utajiri mkubwa wa maliasili zake na kutolea mfano hata majani tuu ambayo ni nyasi tuu zilizokauka, zimezagaa kwenye misitu na kandoni mwa barabara, huku nyasi hizi zikikusanywa na kugeuzwa mapamba, ziliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.
 
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakiongozwa na Bibi Renalda Godwin wa Quality Cloth amesema, tatizo kubwa la Umasikini wa Wajasiliamali wa Tanzania ni ukosefu wa elimu ya ujasiliamali na utafutaji wa masoko ya kimataifa.
  
Bibi Renalda Godwin anaeleza zaidi (cue in TV na Redio)...
 
Bibi Renalda, ameishukuru UNESCO kwa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wajasiliamali wa Kitanzania kuhusu utajiri mkubwa wa bidhaa za asili uliopo nchini
na kuwapa mbinu za kuzifikisha kwenye masoko ya kimataifa.
 
Kwa upande wa washiriki kutoka Zanzibar, wao wamesema visiwa hivyo havipaswi kuwa masikini hata kidogo kwa kuzingatia utajiri mkubwa wa kambakamba za asili walizonazo na kutolea mfano, makumbi ya nazi ambayo kwao ni takataka ama kuni za kukolezea moto, kumbe nazo pia ni mali asili za ajabu zenye utajiri mkubwa zikitumiwa kiuchumi.
 
Maadhimisho hayo, yatahitimishwa kwa maonyesho ya bidhaa hizo za kambakamba za asili, yayakayofanyika kesho Jumamosi katika Kijiji hicho cha Thai kilichopo karibu na kituo cha Mabasi ya Dala Dala cha Shule ya Kimaifa ya Tanganyika (IST), Masaki jijini Dar
Khadija Mohamed kutoka Mwembe Tanga Zenj, Mratibu wa Mafunzo Nazeer Tajudeen (kati)  na Mkufunzi Renu Rhao
Khadija Mohamed na Khadija Fadhili wakionesha utajiri wa Zenj
Khadija Fadhili, Ali Mohamed na Mkufunzi Reni Rhao kwenye maonesho hayo yaliyofana sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2009

    michuzi baba Ally huyu dada khadija nimepotezanaye miaka 12 iliyo pita OMG asante sana michuzi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2009

    Michuzi nimekuvulia kofia!. you must be a working computer!. hiyo picha ya huyo dada Khadida, mwandishi hakusema ni wa wapi, lakini mpaka umejua ni kutoka Mwembe Tanga, Zenj, Wewe kiboko!.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2009

    Diddah she is very hard working lady.I miss you you my friend and I will see you soon.maryam U.UK

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2009

    kaka michuzi huyo dada alisoma kibosho khadija hijah alikuwa kiongozi mzuri sana salamu kwa wanakibosho U.S

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2009

    hivi ni vitu vizuri sana
    na inabidi kutiana moyo sana ktk kazi za kujiajiri km hizi kwakweli,
    akinamama wanajishughulisha sana siku izi na hawabweteki chini kusubiri mume akufanyie kitu

    i wish ningekuwepo aya maswala uwa nayapenda sana asa bidhaa zao ni imara na nzuri sio feki km bidhaa kibao za KICHINA zilizojaa bongo madukani kero tupu...

    muwe basi mnafanya maonyesho aya sehemu mbali2 sio dar na zenji tuu

    je,nyie wajasiriamali wa vitu asili uwa mna mahali mnakaa mnafanyia biashara zenu?au maduka yenu je tutawapataje wengine??mna group moja ambalo ntapata contacts zenu???MISUPUU TUSAIDIANE BASI TUPATE CONTACTS ZA GROUP LAO ILI TUPATE DETAILS ZA VITU

    unajua tunaweza kuwauza kibiasara zaidi sehemu mbalimbali duniani,tusaidiane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...