hapa ni kama wamelifanyia plunning shamba la migomba ambalo liliangamizwa lote na wakaondoka na mikungu ya ndizi.pia katika vulugu hizo askari mmoja alijeruhiwa na kunyang'anywa bunduki ambayo hadi hivi sasa haijapatikana ila wahalifu wapo rumande kuisaidia polisi pia raia mmoja aliuawa katika vurugu hizo.
Mdau wa Vunjo
bora tugawane umaskini
ReplyDeleteZimbabwe ilianza hivyohivyo
ReplyDeletekwa msingi huu hakuna atakefanya ufisadi manake wataogopa hongera sana kwa kazi murua
ReplyDeletePamoja na kwamba ni katika kisingizio cha mali ya kijiji, lakini ni kawaida ya Wameru kutokupenda kuchanganyika na Watanzania wengine. Kila mara wawo wanakuwa na migogoro hata pale ardhi ni mali ya serikali. Nakumbuka kuna wakati serikali ilitaka kujenga Kijiji cha sayansi, International Science Village. Walikogama, kuna wakati kanisa lilitaka kujenga uwanja wa ndege walikataa. Nadhani mtakuwa mnakumbuka Mgogoro wa kanisa la KKKT miaka hiyo. Mji wa Arusha umeshindwa kuwa jiji kwa sababu yao. mashamba mpaka katikati ya mji kisa hawataki maendeleo. Wataki hata uendelevu wa mji kuwa jiji
ReplyDeleteNawapongeza wanakijiji kwa msimamo waliouchukua,Ipo siku tutafika tu, Ata wakoloni walitufanya hivyihivyi badae ushindi ukapatikana.
ReplyDeleteHawa wananchi vipi ni ujinga au wivu?? kama nikunyang'anya mashamba si wangeanza za wahindi, wazungu kuliko mzalendo mwenzetu? au ndio ile kasumba afadahli mzungu tajiri kuliko mwafrika tajiri tutaacha kasumba hii lini?
ReplyDeletepale arusha kuna mashamba mengi tu wa "wazungu, Wahindi, kwanini ya mwenzetu? Jamani I hate this behaviour.
Serikali ikijisahau wananchi uikumbusha.Hongera wananchi.
ReplyDeleteMbunge Kimaro " Wanavamia shamba langu mimi mzawa la ekari 250 tu wakati kuna Mzungu jirani yangu ana ekari zaidi ya 1000 wanamwacha tu" Sasa huyu ni kiongozi wa wananchi kajaa ubinafsi na ubaguzi namna hii. Wadau mnasemaje ??
ReplyDeleteMaumivu ya kichwa huanza polepole na taratibu !!
ReplyDeleteHivi jamani Arumeru ipo Vunjo? Vunjo si ipo Moshi vijijini?
ReplyDeleteDoes peace really pay?
ReplyDeleteKila siku tunajifanya nchi yetu twajivunia amani. Kumbe amani hiyo wanaenjoy ni wachache tu na wanaoifilisi nchi.
Bongo wachache sana ndio wanaishi na wengine wanasindikiza.
Watu wananjaa hawajui kesho watakula wapi hHebu ona sasa mtu ameuawa kwa ajili ya mambo haya.
Inabidi viongozi wakomeshe hii tabia ya kuvamia mali za watu lakini pia serikali ionyehse kuwa inawachunguza hawa viongozi wanaotajirika mara tu wanapochaguliwa. Kila kiongozi aonyeshe amepataje hela yake na kuwe na limitation ya kiongozi yeyote kupokea zawadi kutoka kwa raia.
Really watu wamechoka kuona viongozi wanaishi maisha kama wako nje ya nchi na ni maisha ya nchi zilizoendelea.
Ndio jana mnamshauri Lilly arudi nyumbani. Mmmmmhhhhh sirudi ng'o kama mambo yenyewe ndio haya. Mimi sina nguvu. Nguvu zangu zinatosha kunyanyua box tu
ReplyDeleteWadau tuwapongeze wenzetu hao.Na tunawaheshimu sana sana kwa kufanya ujasiri huo.kwani tulitaka pia mwekezaji aliyechukua eneo la wahzabe nae akimbie sasa hivi tunakuja.ndugu zetu wanakosa sehemu ya kufanya shughuli zao.Ninawapa heshima vile vile jamaa zetu waliobomoa uzio pale mnazi mmoja ,sehemu ambapo tulisherekea uhuru wetu.Lakini pali uzwa kwa mhindi mmoja. lakini watu wenye uchungu wa nchi hii walibomoa na kuchukua bati.DAWA YA MAFISADI SIO SERIKALI ILA NI WANANCHI WENYEWE.TUMECHOKA SANA SANA.WANA TUCHEZEA AKILI KILA SIKU.KAMA INGEKUWA TUNALIPA PESA ILI BABA WA TAIFA ARUDI DUNIANI NINGEKUWA MTU WA KWANZA KULIPA ILI ARUDI.MZEE ALIONA MBALI SANA.ALISEMA MALI ASILI HIPO ,LAKINI MNATAKIWA MPATE AKILI KWANZA ILI MUWEZE KUITUMIA VIZURI.SASA MNAONA ETI TULIKOSEA KUSAINI KWENYE HUU MRADI WA MGODI MARA ULE MARA KULE.LAKINI HAWA NI WATU WAZIMA NA WENYE AKILI.TUMECHOKA ,BABA WA TAIFA [NYERERE RUDI HARAKA]TUNAKUOMBA.MUNGU MPE NAFASI NYINGINE HATUNA WATU WENYE KUKEMEA HAPA TANZANIA.
ReplyDeleteMkuu wa Mkoa adai vurugu za Sing’isi zimetokana na uhaba wa ardhi
ReplyDeleteNa Neema Werema Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima, amesema vurugu zilizotokea hivi karibuni katika shamba la Madira katika kijiji cha Sing’isi wilayani Arumeru, zimesababishwa na uhaba wa ardhi kwa wananchi.
Shirima aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya awali,kuhusu fujo hizo zilizotokea Juni 7 mwaka huu, na kusababisha watu kujeruhiwa na mali kuharibiwa.
Katika tukio hilo, wananchi wa Sing’isi, walivamia shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 55, linalomilikiwa na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro na kuharibu nyumba 15 za mazao.
Wananchi hao wanadai kuwa hawako tayari kuona eneo kubwa kiasi hicho linamilikiwa na mtu mmoja, wakati wao wakiwa hawana ardhi.
Akizungumzia vurugu hizo ambazo Kimaro amezihusisha na mambo ya kisiasa, Shirima alikanusha madai hayo na kwamba zimetokana na uhaba wa ardhi,kwa wananchi wa Arumeru.
Pia alisema uwekezaji wa Kimaro katika eneo hilo ni kujenga hoteli na si kulima mazao, kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti. Hata hivyo alisema hatua zilizochukuliwa na wananchi kama njia ya kugombea ardhi, ni za ukiukwaji wa sheria za nchi.
Alisema kwa sasa sekretarieti yake kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya kata na vijiji, inafanya uchunguzi kuhusu vinara wa vurugu hizo, ili sheria ichukue mkondo wake.
Tayari watu 38 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na wengine 36, wanaendelea kuhojiwa. Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa hali ya usalama katika eneo hilo, imerejea kuwa ya kawaida na kwamba watu wanaendelea na shughuli zao za maendeleo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Basilio Matei, alisema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa kinara wa vurugu hizo ni kiongozi mmoja wa Chama cha TLP, ambaye bado anasakwa.
Muosha huoshwa,kwa sisi wachagga huwa tunaneno tunasema "TONDO",huyu Kimaro ni Tondo kabisa ameingia kwenye siasa kichwa kichwa hiyo ndiyo impact yake
ReplyDelete