Uga wa Waandishi na Wasomaji
Je wewe nimwandishi? Unapenda kuanza kuandika? Wewe ni mpenzi wa Vitabu?
Basi kumbuka kwamba kila siku ya Ijumaa ya pili ya wiki, SOMA inawakutanisha wapenzi wa uandishi na usomaji vitabu kupitia, kujadili, kusahihishana, kubadilishana mawazo na kufurahia dunia ya uandishi.
Hii ni nafasi muhimu kwako kuongeza ujuzi katika fani ya uandishi, kufanyia kazi kazi zako za kiuandishi, na hata kujifunza mbinu muhumu zinazoweza kukusaidia kufanikisha ndoto yako ya kuwa mwandishi. Unashauriwa kuja na hadithi yako mwenyewe ya aina na iliyo katika hatua yoyote ile.
Hata kama huna hadithi yako iliyo tayari unakaribishwa kujumuika nasi kufurahia ulimwengu wa uandishi.
Dhima: Sanaa ya uandshi wa hadithi
Maudhui: Kujadili maudhui mbalimbali ya hadithi za kimapenzi
Mahala: Soma Mkahawa wa VitabuTarehe na
Muda: Ijumaa tarehe 12 Juni 2009,
Saa 11:30 hadi 02:00 Jioni
Karibu soma,
kiota cha ujuzi,
utamaduni na burudani
Ijumaa ya pili ya mwezi????
ReplyDeleteIjumaa ya Pili ya Kila Mwezi. Ijumaa ya kwanza ya kila mwezi kunakuwa na UGA WA RIKA TATU, Ijumaa ya pili ni UGA WA WAANDISHI NA WASOMAJI, Ijumaa Ya Tatu ya kila Mwezi ni UGA WA WASHAIRI na vikolombwezo vingine, Ijumaa ya nne ya kila Mwezi ni UGA WA KUTANA NA MWANDISHI...mwezi uliopita alikuwepo Freddy Macha...mwezi huu mtatangaziwa siku za karibuni
ReplyDeleteUGA (FORUM)
Mkahawa wa Vitabu Soma upo Mlingotini Circle, Regent Estate karibu na ARR Health Center ya baada mataa ya barabarani Moroko ukielekea victoria, Dar Es Salaam, Tanzania
kwa taarifa zaidi:
info.soma@infinet.co.tz
coordinator.gmail.com
nimeipenda hii na ningependa kushiriki lakini bahati mbaya niko mbali.
ReplyDelete