Wadau wanaouliza wapo wapi wale wanamziki waliokuwa wanawika na bendi ya The Tatu Nane? Swali hili limeulizwa na baadhi ya wadau wa blog ya jamii kupitia kwa mkuu wa wilaya ya naniino, mheshimiwa balozi michuzi.
kwa jibu la haraka ili kutuliza kiu ya mdau aliyeuliza, huyo hapo (pichani) ni Seifu Rengwe ambaye ni moja wa wanamziki waliokuwa wanatamba na TATU NANE bendi ambayo enzi zile iliutangaza utamaduni wa Tanzania katika kila kona duniani.
Seifu Rengwe bado anaendeleza libeneke huko Ujerumani, kama anavyoonekana picha akiwikisha jogoo kuwa kumekucha na Trampet yake!
Swali la kwa nini wasikae pamoja na kuliunda upya The Tatu Nane Band naomba mtupe muda kidogo, sie tunawatafuta wanamziki waliokuwa Tatu Nane ili watoe jibu maana hata nasi tumewamiss katika anga.
Ila tunajua kwamba mpiga bezi wao Teddy Mubaraka yupo Dar na bendi ya Wahapahapa na Madi Tumbo (muimbaji na gitaa la kwanza) pamoja na Omari Naliene (mpuliza filimbi kwa pua) sasa ni marehemu. waliobaki Charles Muhuto (drums) na Omari Abdalla Dullah (ngoma na kuimba pia alipigia bezi msondo ngoma) tutaendelea kuwasaka...
Wadau Ujerumani
Charles Mhuto yuko marekani.
ReplyDeleteHello brother Michuzi.
ReplyDeleteKwanza kabisa naomba nikuambie kwamba nimepokea taarifa hii kwa mshtuko wa hali a juu.Kwa sababu moja ya watu waliokua wananichanganya kwenye TATU NANE ni yule mzawa aliyekuwa akiimba,kucheza na kupuliza filimbi kwa pua.Ooooooh,yaani ulivyonambia alifariki......oooooh.MAY GOD REST HIS SOUL IN ETERNAL PEACE!!Ooooooh!!
Hhhhhhhhhhhh!!Nimekosa raha kabisa kwa kweli.Na mimi ndyo nilipost lile swali kuuliza hawa jamaa wapo wpi na kwa nini wasikae tena pamoja.
Kukosekana kwa yule jamaa kutaonyesha pengo lake waziwazi kwa kweli,unless anapatikana mtu wa aina yake wa ku-replace.
Ni mimi nduguyenu,
Mkulima-Kijijini Gezaulole.
yeah,nimesikia Charles Mhuto yuko Marekani, Dullah yuo Denmark na Teddy yuko Bongo,Seif yuko Germany na hao wawili wamefariki...Mi nafikiri hawa jamaa wafikirie kufanya Reunion na wapige tour kwenye nchi mbali mbali ulaya na America alaf wakamalizie nyumbani...Kuna band moja Ya west Africa inaitwa Osibisa iliweza kufanya kitu cha namna iyo huko nyuma..Mi nafikiri wapatikane mapromota wa kuendeleza hili swala na hakika inawezekana....Mswahili
ReplyDeleteHallo wandugu
ReplyDeletehapa anazungumza ni seif rengwe original toka Ujerumani.
Hakika masuala yenu yatapata majibu hivi karibuni,kwa habari tu ni kwamba mimi nipo ujerumani na kama mnataka kuona kile nichafonya basi tafadhalini myspace.com/rengweseifproject
au www.six-nation-music.net
mavituz yangu yamekuwa hayana mpaka kwani toka madogoli,raggae,jazz na sound zooote.
cherles yuko USA.Dulla Kopenhagen
basi tusubiri tu ndo tunapika.
wasaalam