jana nimepita uwanja wa ndege wa kimataifa wa zenji na kukuta mkanda wa kusogezea mizigo ya abiria umeharibika na inabidi mizigo hiyo ibebwe kwa mikono na wafanyakazi hodari wa hapo uwanjani. raha ni yake ni tangazo la 'welcome to zanzibar' ambalo wageni toka sehemu mbalimbali dunia hukumbana nalo hapo kwenye sehemu ya mizigo... raha zaidi ni pale baada ya kuuliza kulikoni nikaambiwa ah, ndo hivo tena yakhe. mashini ina miezi sasa haifanyi kazi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2009

    alokwambia international airport nani, haina hadhi yyt ya kuitwa ivo, kidumu chama cha mapinduzi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2009

    Michuzi na wewe unautani mbaya..U just made my day.Kiwanja kuna stress bila kumchungulia michuzi..unaweza kupitisha siku bila kucheka

    ReplyDelete
  3. Ralph NahatoJune 19, 2009

    Hiyo ndiyo bongo....home sweet home!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2009

    NAFIKIRI ZANZIBAR NI MOJA KATI YA VIWANJA VICHAFU NA HAKIPO KATIKA HADHI YA KUITWA CHA KIMATAIFA,LICHA YA WATALII NA NDEGE KIBAO ZIKIRUKA DIRECT TOKA LONDON,MILAN,ROME,MADRID ZOTE HIZO ZIKILETA WATALII LAKINI UWANJA NI KICHEKESHO CHA KARNE.IKUMBUKWE UTALII NDIYO INAONGOZA KWA KUINGIZA FEDHA ZA KIGENI HIVI SASA.LAKINI WATAWALA SIJUI HAWAJUI AU HAWAJIFUNZI KWA WATANI WETU KENYA NINI WAMEFANYA MOMBASA AIRPORT

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2009

    Tena hapo sio kama mashine imeharibika jana au mwezi uliopita. Hapo hakujawahi kuwa na mashine ya aina yoyote. Sasa ukitoka nje kidogo tu hapo, kama ni jua litakupiga na mvua itakunyeshea wakati wa kucheck in. Yaani Airport ya Zanzibar ni aibu tena ya miaka mingi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2009

    hii arport yetu zenji ni aibu sana,inatia hela nyingi sana ila zote zinaishia kwa watu hasa wa migration na maofisa wengine wa serikali,utakuta watoto wadogo walioanza kazi juzi tu pale wa uhamiaji sasa anakwambia ana dola zaidi ya alfu arubaini ameeka ndani,tena walivo wajinga wanatuhadithia sisi mitaani,tourist seasons ndio balaa.....sasa unazani huo uwanja unaingiza nn na utatengenezwa vp kwa hali hiyo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2009

    Yani misupu hii airpot ina watu wavivu sijawahi ona duniani safiri na precision ujionee kila ukitua hapo mida ya usku duty free yao ishafungwa asubuhi sana hawajafungua jamani mbona aibu tunalala mno kwa nini wahusika wasipange shift kutokana na flights?hata dar airpot uozo tu flight za asubuhi mtu unataka nunua kitu duty free haijafunguliwa saa kumina moja na nusu jamani?hebu tuache uvivu tufanye kazi natumai wahusika watapata kujifunza kia wanawashinda hebu na tuamke jamani nchi inatia hasira hii basi tu ...asante michu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2009

    sirikali ya mheshmiwa karume ina mpango wa kuufanyia ukarabati uwanja wa ndege wa Zanzibar! tehtehteh....hahahahah.....hehehehe hii ndio zanzibar. labda wakipewa uhuru wao na Tanganyika ndio watawezakufanya hayo marekebisho.. huhuhuhu!!!!

    ReplyDelete
  9. Makame UsiJune 20, 2009

    Yakhe, mwashambulia uwanja wetu utadhan viwanja vya ndege vya bara ni vya kimataifa! Mnayoita JKNIA ina hadhi gani ya kuitwa 'international'? KIA ina hadhi gani ya kuitwa international? Nendeni Jomo Kenyatta International Airport ndo mtajua nini maana ya international. Kama ni uozo si unguja tu hata bara upo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2009

    serekali ya zanzibar imehamishiwa Mrima sasa ikiwa sisi hapa zanzibar tuwe na int airport Tanganyika wao wawe na nini ?wache wajikusanyie mafedha yao wale tu huo uwanja wa mtu bifsi kwa sasa aliyekwenda kenda utu na imani zimetutoka baadhi yetu pesa ndio mungu wetu kwa sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...