Heshima kwako Mkuu wa Wilaya ya naniiii....
Hongera kwa libeneke na karibu Durban!

Aisee wahandisi wenzangu hapo Dar basi fanyeni kama Durban beach kidogo(attached pic)mambo yawe tambarare au kama mnavyosema bongo mambo yawe mswano hapo Coco Beach na watu wapumzike safi!

JAMANI! HIVI TUNASHINDWA NINI KUWA KAMA WENZETU???
WAO WANAWEZA, SIE TUSHINDWE TUNA NINI....

Nawasilisha Mkuu.
Ahsante
Mdau
Durban.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    Tunasubiri msaada wa wawekezaji

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2009

    mi naona ni bora uishi kwa amani kuliko maisha ya mashaka mashaka ya kupigwa shaba kwenye mandhari nzuri....nawakilisha amani ni bora kuliko maghorofa ya almasi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    tatizo lenu sijui mnaichukuliaje bongo huku kuna beach nzuri sana nyingine zaidi ya hizo mfano kigamboni yote ile wazungu wenyewe wakija wanazima fegi ila coco ni maarufu kwa sababu ni ya bure yaani public no kiingilia there ni karibu natown na daladala zinashusha hadi pale mlangoni ndio maana iko maarufu kihivyo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2009

    Hii Beach safi sana ina Green flag kwa wanaojua manayake wananielewa mie nikija hapo Durubeni huwa napenda kwenda beach ya Umhlanga Rocks kule powa zaidi beach lake limejengwa na limetulia huwa na drive toka stanger through N2 to cape stad mkeka tu 20hrs driving aah when i drove in dat road remind me Route 66

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2009

    We anonymous wa 10:59am ya kizungu. Bora utumie lugha ya taifa hicho kiingereza chako kinaniacha hoi.

    ReplyDelete
  6. asalam aleikum ,shida ya Tanzania na halmashauri zake zimejaa ubabaishaji na u mimi mwingi sana mtu akitaka kupaendeleza na wao waongozi wanataka waendelezwe pia kwa maana ya rushwa ili waweze kupitisha documents yaani ni hovyo sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2009

    TANZANIA HAINA AKILI, KUNA NCHI HAPA DUNIANI ZINATEGEMEA UTALII TU NA MAMBO YAO MSWANO, TANZANIA HAIJUWI HILO, SISI NI MZUZU. VIONGOZI HAWAJALI WAO SI WANA KAZI WANAKULA KUKU KWA MRIJA KAMA KUMSUKUMA TEMBO KWA UBUWA KWAO, TULIOPAKI TUNASUKUMA MAWE KWA MIKINO WAPI NA WAPI! MUNGU AWAREHEMU NA PEPONI AWAFIKISHE. Just few days ago I was warcthing MARAKESHI on BBC, it is a town in MOROCCO, I guess it is a second towm after CASABLANCA, ni jangwani tu lakini pamebadilishwa pakatoka kama Ulaya hivi, shughuli yao kubwa ni utalii tu, watu wako busy kufua dollars and pounds wanatengeneza pesa si mchezo, sasa watu wako jangwani wanaweza what abou us mwajemeni, this is 21st century tuachane na mawazo mgando, tunatakiwa tutengeneza ajira kwa vijana jamani

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2009

    12.02 anony vp mbona mshamba huelewi nini hapo kizungu ndo nini lugha ya taifa ndo nini unajuaje kama yeye lugha ya taifa lake chingereza eti kizungu sio kizungu kingereza au mayai hayapandi sio na wewe pia umekosea sio wazungu wote wanaongea kingereza bye

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2009

    wajameni inabidi kweli tubadilike tuendane na karne ya 21 hapo mahala panapendeza kweli na kwa kuwa nasi tunazo beach nzuri ... City fathers basi kaeni chini mtengeneze mandari zilizoenda shule! sio kila kitu mpaka mwekezaji jamani ahhh! punguzeni mawazo mgando. mahela kila kona tunalipia hata ukitaka kwenda chooni sasa tatizo nini? nje mnasafiri mnaona - wenzetu mnasoma nini kwenye safari zenu za kikazi?! mtembee na kusoma msome basiiii!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2009

    ...wafadhili waje...

    yani ukiwaza saaana kuhusu viongozi wengi tulionao...matope

    kila mtu anabidii atoke kivyake mana ajua mda wowote hana kazi

    ovyo sana na shenzy sana

    (nna hasira sana)

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2009

    Mdau wa pili kwani huwezi kuwa na fukwe nzuri na amani kwa pamoja?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...