
Unganishwa kwa bei nafuu zaidi!!Leo - Jumatatu, Julai 20, 2009; Vodacom Tanzania imezindua huduma MPYA ya Internet ijulikanayo kama
INTERNET BOMBA
kwa wateja wake wa Malipo ya Kabla waliopo nchini Tanzania.
Huduma hii ya Internet Bomba inawaruhusu wateja wa Malipo ya Kabla kununua Internet kupitia maombi ya SMS kwenda 123 na waunganishwe kwa bei nafuu kabisa!!Kununua, kwanza wateja wanatakiwa kuhakikisha wana salio la kutosha, na kisha tuma SMS yenye neno
aidha BOMBA30 kwa Tsh 60,000 au BOMBA90 kwa Tsh 162,000 kwenda 123 na utaweza kutumia Internet kwa siku 30 au 90.
*Bei zilizoorodheshwa hapo juu ni pamoja na Kodi (VAT & Excise)
ANGALIZO:
Huduma hii MPYA ya INTERNET BOMBAinaweza kupatikana ukitumia kifaa cha Internet cha USB Modem au Data card iliyounganishwa na Internet ya Vodacom Internet kwenye laptop au kompyuta ya mezani kwa hadi spidi ya 32KB kwa sekunde!!
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii,
piga BURE :0763 300004 (Swahili)
au
0763 300005 (Kiingereza)
*Vigezo na Masharti kuzingatiwa
Nimefurahi sana kusikia kuwa sasa mtu anaweza kupata Internet kwa kupitia mtandao huo wa voda, lakini kitu kimoja naona hiyo bei imekuwa kubwa mno kiasi kwamba kwa mtu wa kawaida ni ngumu sana kufahulu, ningeomba sana kama wanaweza kupunguza hiyo bei kusudi wote waweze kumudu hiyo bei, kwa vile tunapenda na tunatamani sana kutumia huo mtandao kwa vile utarahisisha mawasilino popote hata kijijini.
ReplyDeleteNilikuwa sijajua yaani Tanzania internet speed bado sana... speed ya 34KBs ni below hata dial up kwa hapa usa.
ReplyDeleteMkonga utaanza lini maana naona kweli unaitajika.
Shilingi 162,000 kwa mwezi, Mhh, kula yenyewe ya kubahatisha, asubuhi andazi na chai ya rangi,mchana, unashindia harufu na karanga za sh 50. Mhhh, nafikiri hii imekaa vizuri, kwa wenye uwezojimwageni
ReplyDeleteaisee internet bongo ni gali sana, bora hiyo fibre optic cabel ianze kufanya kazi,mimi hapa kwangu ugaibuni kidogo, nalipa internet dola 15 kwa mwezi, ni 100Mb per second.na ni Unlimited, kwa mwezi, sijui nikirudi bongo itakuwaje? yani 34KB kwa sekunde? sh 60,000. ni very very expensive na net ipo slow.ok ndio mabo! sijui nani atatukomboa!
ReplyDeletebado gharama za huduma ya internet kwa tanzania zikojuu sana, labda ingekuwa 15,000 per month tena matumizi bila limitation zozote hapo kidogo ingekuwa reasonable. maana kwa bei hiyo ya 60,000 sidhani ni watu wa kipato gani wanaimudu kama si wachache tu kati umma wa tanzania. anyway hii ni biashara huria ukiweza unajiunga huwezi unakaa pembeni.
ReplyDeleteThis offer is still expensive in comparison to UK internet providers such as carphone warehouse,BT internet etc
ReplyDeleteI could think of the nature of competative environment where most companies want to increase their market share by undercutting competitors by achieving low cost for their margins but in case of vodacom,may be the environment is not as competative and this make them decide which ever promotional price they can set.
I would wish to know how they come up with this pricing strategy.
one other thing is,I give credit to vodacom for their corporate social responsibilities as time and time again we see them engage with communities,schools etcgiving them desks,books.by doing so they ensure their place as corporate citizen where so long as it is separate entity,it has to claim its existance in a society.
From the above,I would prefer Vodacom to reconsider prising accordingly so as to increase their internet market share as their telephone.
wewe unasemaje?
Mdau UK.
Kubwa kubwa sana hiyo pesa kwa mwezi nyie Voda! ebo! mwataka kutukamua hadi tone la mwisho? hamtampata m2 kwa mtaji huo! Bora Zantel wapo chini kuliko nyie. kula yenyewe tabu bado tu nyodo! Ebo!!!
ReplyDeleteMangi wa K'koo
Duh! 32KBps ni speed ndogo sana! Yaani hapa nalipa around TShs 16,000 kwa mwezi na speed ni 54MBps kwa unlimited access. Yaani huwa nikiwaza suala zima la infrastructure Bongo huwa hata napata uvivu kurudi nyumbani! Anyway home ni home.
ReplyDeleteserikali yetu ni lazma iwe na strategy khs ICT policy wenzetu huku serikali zao zimeondoa kodi zote kwa internet providers & broadband hardware na zinaruhusu ushindani wa makampuni kotoka nchi yoyote kwa masharti mepesi na serikali ndo inapanga bei ya huduma
ReplyDeleteserikali ya JK ni lazma ieleze ni lini free wireless internet itapatikana kama serikali za wenzetu hapa hakuna hali ngumu ya uchumi,compuer is nothing without internet. tutajaza vipi hizo form za TRA & BANDARI online kwa bei hizo kama we sio mla rushwa?
yaani hapa nalipa £25 hiyo ni sim ya landline na broadband pamoja nyumbani kwangu, upumbavu wa nyumbani ndio huo kitu kinakuwa bei halafu wanatumiaji wanakuwa ni wachache then mnakuwa hamna biashara,naona hiyo ni kwa ajili ya wenyewe tu wenye uhakika wa kula ya asubuhi mchana na usiku,na nyumba sio ya kupanga, kwa wale wanaohangaika na jua lamchana kutafuta kula haiwafai
ReplyDeleteBongo tambarare saaaaana
ReplyDeleteKumbe speed ndio hiyo na bei ndio hiyo mweee
Ukikaa intenet cafe utasoma post moja tu ya michuzi mara muda umeisha kwa speed hiyo?????
Maneno meeengi lakini ikija kwney mambo ya ukweli watu kimya....Hebu tauambiane ukweli. NI wangapi wataaford kuwa na internet kama bei zenyewe ndio hizo. Nadhani bado bongo kuwa a internet ni luxury na sio necessity.
Mimi hapa nalipwa vizuri lakini kama internet ingekua ni bei hiyo ...mbona ningekata tu nitumie ya kazini. Nyumbani yenyewew watu hatukai na kama nikuitumia ni mara moja au mbili kwa week sasa hiyo bei si kuwaua wabongo tu. Najua mwenye nayo bongo naye ni hivyo hivyo watoto shuleni na wazazi kazini. Sana sasa ni usiku tu sasa that much money jamani?
Ndio maana wageni wakija huku hawabanduki kwenye internet na TV...manake huku TV channels zipo mpaka 1000 ni macho yako na internet speed ndio husemi.
They need to do something first about the price. Too much money
Nadhani bei ni kubwa kwa sababu wana wateja wachache ukilinganisha na huko UK na USA ambako almost kila shirika/ofisi ina internet, na watu wengi sana wana internet.
ReplyDeleteKwa hiyo wateja wanafidia gharama zote, ingawa pia nahisi bado ni kubwa kiasi.
Hivi inakuwaje kama mtu akilipia wireless vodavone akaenda kuitumia bongo
hii speed ndogo sana na bei kubwa kupitiliza
ReplyDeleteTatizo sio bei inayonipa uvivu ni hiyo speed tu yaaani nikichefuchefu kwa hapo dsm afadhali wao wanapata mpaka 7mbps coz wako powered na 3g lakini huku kwetu porini kwenye mahitaji zaidi tunaambulia 54kbps
ReplyDelete