Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    Kama CCM wana matawi hadi Uingereza je itakua vibaya kwa CUF ama Chadema kuwa na matawi kama haya nje ya nchi?? Wadau Tuchangie.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2009

    Sielewi ni faida gani inayosaidia Tanzania kuwa na tawi la CCM nchi za nje? Tumieni wakati kusoma huko, wacheni siasa huku nyumbani. Sidhani kama kuma tawi la Chama chja Utawala wa Ghana huko ughaibuni. Halafu mnashangaa kwa nini Obama amekwenda Ghana na hakuchagua kuja huku kwetu.
    Hawa ni watu wa kujependekeza tu - na msimamo huu unaonyesha hakuna nafasi ya chama cho chote kingine kufanikiwa. Fanyeni Vyama watu vya Utanzania huko Ughaibuni sio wa CCM, kwa hiyo kama mimi si sapoti CCM na niko huko Reading- vipi sitakuwa Mtanzania alie na imani ni cchi yetu - na vipi kama nitahitaji msaada wa wenzangu - itabidi nionyesge kadi ya CCM kwanza?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2009

    Kumbe huu ni mkutano mkuu wa wanachama wote, nitahudhuria nina dukuduku sana na Tawi letu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2009

    Kama unataka kuanzisha tawi la CUF Uingereza watafute wenzio huko.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2009

    Wewe unayesema hatushangai mbona Obama ameenda Gana hakuja huku kwani umeambiwa ghana ni Africa nzima. Kuna nchi zisizopungua hamsini katika bara la Africa kwahiyo sio kwamba Obama alienda nchi zote za Africa lakini hakuja Tanzania. Naomba watu kabra ya kutoa maoni jipangeni na kuakikisha unachotaka kukiongelea kina maana. Rais Kikwete alikuwa rais wa kwanza Africa kukalibishwa na rais Obama, na hiyo imekaa vipi mdau wa kupayuka!!!???

    Viajama wa CCM ughaibuni jitahidini kuwashauri wabeba mabox wote warudi nyumbani watuletee utamaduni wa kisasa kama wanavyofanya wananchi wa nchi zingine waendapo ugenini

    Mungu awabariki, tunajua mtakumbana na wapuuzi wengi mmoja waoa hapo juu lakini msikate tamaa

    Mdau--Mazese kwa mfuga mbwa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 20, 2009

    We Anon Tarehe Mon Jul 20, 10:31:00 PM, Hebu kajifunze kuandika kwanza ndio uje kuandika maoni yako humu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2009

    Suala la chama kuwa na wafuasi ni la muhimu sana kwa ukuaji wa uwezo wa chama. “Chama ni watu.” Tafsiri ya msemo huu ni kwamba taasisi yoyote, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, umahili wake unategemea ridhaa ambayo wananchi au watu kwa ujumla waliyonayo kwa taasisi hiyo.
    Ishara ya kwanza kabisa ya kuwepo kwa chama ni kuwepo kwa ufuasi na ni suala ambalo liko wazi kwamba chama ambacho hakiwezi kuhawasisha watu wengi kujiunga nacho au kupoteza wanachama ni moja ya njia za chama kuporomoka.Hebu tujadili
    Mdau - Picha ya Ndege/Kibaha

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2009

    Wabongo akili mingi,kalaghabao wajameni!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2009

    Nyie mtakaa kupiga makelele wakati wenzenu wanajitengenezea ulaji, c unajua mambo ya ccm line nje nje, hao viongozi na wanachama siku wakirudi bongo wakaingia kwenye line ya kutaka kugombea unbunge kwenye maeneo yao unazania nani atawakatalia? cunajua tena unapitisha vimifuko uku uk vile vya charity vya kutoa msaada wa nguo wewe ukikusanya nyumba zako 300, uweke kwenye contena lako kama mwanafunzi aliyemaliza muda wake ukifika unalipia ushuru kidogo, ukiwapa watu kijijini kwenu na vipesa kidogo jumlisha na vi toy kwa wabongo wenzako ambavyo vimeisha muda wake , SI BUNGENI UNAINGIA, unaenda kupata maruzuku ya kumwaga na kulala kwa kwenda mbele bungeni...
    USIZANIE HAO WOTE WANAIPENDA CCM , ASILIMIA 100 KATI YAO WANAANGALIA ULAJI , Me nawajua wengi wao kwenye chama wanaishi hapa UK kama watu wa cuf , sasa nyie amshangai??? ALIYEIMBA ULE MWIMBO KWANI WAO WAWEZE WANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI HAJAKOSEA.....Kalaga bao mwanawane utabeba box hadi utoke kibiongo nukta

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2009

    kidumu chama cha mapinduzi,
    kidumu chama cha mapinduzi,
    KIDUMU!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2009

    Kidumu Kidumu Kidumu Kidumuuuu DAIMA!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2009

    Watanzania China imeendelea sababu wanaishi na itikadi zao za siasa,matamanio yao ya uchumi na utamaduni wao.Sisi tuko mbele kurushiana machafuzi.Dunia haitusubiri.CUF,CHADEMA nao wana matawi yao UK ila yanakufa kifo cha mende.
    MAPINDUZI DAIMA
    MwanaJamii

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2009

    mnaweza kuwajua CCM READING kula jamiiforums.com ukumbi wa siasa.
    kazi ipo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2009

    Najua unaweza kumzuia mtu kuwaza, kusema na kutenda ila huwezi kumzuia mtu kuota, hata kama ukamzuia kulala kwa kumnyima chakula na maisha bora, bado ataota tu hata ni mchana kweupeeeeeeeeeeee. Usithubutu Mkuu wa Wilaya ya naiiiiiiiiiiii kuzuia watu kuota, acha waote bwana, hata kama watafurahi ndotoni tuuuuuu, na njaa zinauma kutokana na kukosa maisha bora. Waache balozi wa naniib waote.
    Naota hivi!.........
    Naona kesho, jua linachomoza, watoto wanaanza kutoka nje kuendeleza michezo yao ya kitoto, toka pale walipoachia jana, watoto wa jana wanakataa, kuchezea matope ya jana, ni siku na mwaka nisioufahamu, lakini naona, naona, nasema naona. Chama cha Mapinduzi Maneno-CCM(m) kinaitwa chama cha upinzani, watu wanaanza kukikimbia, wanajiunga na chama, kisicho na jina, kilichoundwa na wakulima na wafanyakazi kwa ridhaa yao wenyewe, kuwatetea wao, watakiongoza wao wenyewe.
    Wanakusudia kuanza mapinduzi ya vitendo si ya maneno kama ya chama cha mapinduzi ya maneno. Naomba mkipe jina chama hiki kisicho na jina, hili linafaa? Chama cha Mapinduzi Vitendo-CCM(v). Nilikuwa naota tu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2009

    Naona utaota sana mwaka huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...