Severne aka Sevasha aka "Pilipili kichaa" wa
Ngoma Africa band jukwaani ! Fest Africa,mjini Tampere,Ufini
Ras Makunja na Ngoma Africa aka FFU katika
makamuzi ya hasira ndani ya Fest-Africa,
Finland. Palikuwa hapatoshi....

mpiga solo machachali wa Ngoma Africa band aka
FFU akiwa kibaruani kwake katika Fest-Afrika,Tampere,Ufini


Ras Makunja na Ngoma Africa aka FFU katika makamuzi ya hasira!ndani ya Fest-Africa,Finland.

Mwanamziki Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu na mzimu wake wa FFU wikiendi ilopita walifungua ukurasa mpya katika jukwaa la Fest-Africa,kwani waliweza kuwapa burudani ya aina washabiki wa ufini.

Washambuliaji (FFU) wa safu ya mbele waliweza kuwamdudu washabiki vizuri huku Ras Makunja akiwaongoza jukwaani washambuliaji wake wa safu ya mbele mpiga solo Chris-B,ambaye pia anaimba na Bi.Severne aka Sevasha au afande wa kike,huku mdundo mkali wa The Ngoma Africa Band ukiwasindikiza na kuweza kufanikiwa kuwayumbisha washabiki katika onesho hilo.

Kitu cha kufurahisha mziki huo wa Ngoma Africa uliweza kuwazoa washabiki na kupanda jukwaani kusakata ngoma za moto.
Mojawapo walipvutwa jukwaani "Mzee Mponda" au tumwite "Dady Mponda" ambaye alipanda jukwaani na akawashangaza maelfu ya washabiki kuwa "kuwa wazee wa Kiafrika" wanajua kucheza mziki na kutoa ushindani kwa vijana!

wasikilize ngoma afrika hapa
http://www.myspace.com/thengomaafrica





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    Ngoma Africa! au vichaa wa fanya fujo uone,wakali hawatabiliki mambo ya makubwa,hapa ufini mmeacha simulizi.
    Heshima zenu wakubwa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2009

    te!te!Ngoma Africa!!!! mwe!mwe!
    vichaa kazi mnaiweza na moto wenu ni wa kiana aina
    Bab Kubwa.
    Mdau wa Helsinki

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    hata mimi nawakubali vichaa hawa wanajua kazi yao,uwezo wao wa kulimudu jukwaa ni mkubwa mno.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2009

    kweli jinamizi la dansi limedaka wazungu,kamanda mzigo mkubwa huo lakini umeuchagua mwenyewe.miye ombi langu kiatu nimefika bei

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...