Rais Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani akisindikizwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda) ameondoka nchini mchana wa leo, Jumapili, Agosti 30, 2009, kwenda Tripoli, kuhudhuria Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Mkutano huo maalum wa AU wa siku mbili umeitishwa kujadili migogoro mbali mbali inayoendelea kulikumba Bara la Afrika ikiwamo ile ya Somalia na Darfur katika Sudan.

Mkutano huo utakuwa chini ya Mwenyekiti wa AU, Kanali Muammar Gadaffi, kiongozi wa Libya.

Katika mkutano wao uliopita wa Juni, mwaka huu, viongozi hao wa AU walikubaliana kuitisha kikao hicho maalum kujadili kwa kina migogoro ya Bara la Afrika na kuitafutia majawabu.

Mbali ya kuhudhuria mkutano huo maalum, viongozi hao wa Afrika watashiriki katika sherehe kubwa za kuadhimisha miaka 40 ya Mapinduzi ya Libya.

Sherehe hizo za kuadhimisha Mapinduzi ya Al Fateh Revolution ama First September Revolution, ni kumbukumbu za siku ambayo Gaddafi alikamata madaraka ya kuitawala Libya kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi usiku wa kuamkia Septemba Mosi, mwaka 1969.

Katika mapinduzi hayo, Gaddafi ambaye wakati huo alikuwa bado kepteni wa jeshi la nchi hiyo, alimwondoa madarakani Mfalme Idriss Al-Senussi, kwa mapinduzi ambayo hayakumwaga damu. Mfalme Idriss alikuwa nchini Uturuki kwa matibabu wakati huo.

Rais Kikwete na ujumbe wake unatarajiwa kurejea nyumbani Jumatano, Septemba 2, 2009 na atatoa hotuba yake ya mwisho wa mwezi baada ya kuwa amerejea nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. safari njema risi wetu JK

    ReplyDelete
  2. Michuzi swala muhimu watakalo zungumzia ni maswala ya mabadiliko ya tabiachi! Africa kwa mara ya kwanza itakuwa na msimamo wao katika makubaliano ya dunia yatakayo fanyika mwisho mwa mwaka huu huko Denrmark.
    ni swala muhimu sana duniani lakini alipati publicity ya kutosha.

    pk.

    ReplyDelete
  3. Jamani, nauliza swali ambalo tulijifunza kidato cha Pili ila ni miaka kibao?

    Kama Rais na makamu wake hawapo, anayekaimu uraisi ni Waziri Mkuu ama ni Spika wa Bunge?

    Msaada tutani????

    ReplyDelete
  4. hongera JK kwa kumpa nafasi Shein kwenda Geneva na wewe kuamua kwenda Tripoli.

    lakini safari ya Tripoli ungemuachia Pinda kwa kweli ingekuwa kubwa kuliko.

    ungefaa this time wewe ubaki nyumbani ujue jinsi wenzako shein na pinda wanavyojisikia wakati ukivinjari marekani na ulaya.

    vilevile ungekuwa vizuri kama ungeenda kuwapokea airport wakirudi toka safari zao.

    ReplyDelete
  5. mh, pamba ya pinda imetulia!!

    ReplyDelete
  6. Naomba kuuliza waungwana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, nchi iko chini ya nani hivi sasa? Jaji mkuu au Spika wa bunge? Sababu Rais wa nchi ndo huyo ameenda libya, makamo wake yuko Geneva!

    ReplyDelete
  7. JK and Shein wote wapo nje kwa hiyo nchi ameachiwa Pinda. JK anamwambia hapo ujue hii kazi ya Mafisadi lazima uipe kipa umbele wakati mie sipo

    ReplyDelete
  8. Jamani VASCO!
    Hana hata RAMADHAN!?!
    Khaa!

    ReplyDelete
  9. Air miles ngapi jamani?

    ReplyDelete
  10. nasikia eti kila rais wa kiafrika akienda libya, Gaddafi humpa mshiko au kitita cha dolali za kimarekani.

    ReplyDelete
  11. NINAKUTAKIA SAFARI NJEMA.

    ReplyDelete
  12. MAJAWABU YA MISUKOSUKO YA MATAIFA MENGI YA AFRICA TUNAYO SISI WAAFRICA WENYEWE.KATIKA VIKAO VYA HAO WAKUU WA NCHI NI LAZIMA PIA WAO WENYEWE WAJIANGALIE WAO WENYEWE USAFI WA KATKA NGAZI ZA VYEO WALIYONAVYO.MFANO MZURI TU LIBYA NA RAIS WAKE GADDAFI HANA SIFA YA DEMOKRASIA ILIYO BORA.NI MAMBO YALE YALE TU AMBAYO YANATAWAL NCHI NYINGINE KUTOKA NA ULAFI WA UONGOZI.
    KINGINE,NI UHURU KATIKA UCHUMI.NCHI ZA AFRICA HAZINA UHURU KATKA MASOKO NA UHURU WA KURIDHIA BEI YA VITU VYAO,YAMKINI WANAPANGIWA NA MATAIFA MAKUBWA.
    NCHI KAMA SOMALIA,CONGO SUDAN,NA KWINGINEKO NI RIDHA TU YA WATU WENYWE KUACHA VITA.TUNAJA VITA VINAFADHILIWA NA NCHI TAJIRI NA HAKUNA NCHI HATA MOJA KATKA UMOJA WA NCHI ZA AFRICA UMEKEMEA NA KUCHUKUA HATUA KALI.
    TUPO TU KIPIGA POROJO NA KUTAFUNA RESOURCES KAMA ILIVYO KWA RAIS WETU KWENDA HUKO,HIVI VITU VINGE KUWA NA MAJAWABU SIKU NYINGI.UTASHAANGA KUONA HATA RAISI MWINGINE BAADA YA JK ATAKWENDA KWENYE THE SAME THING.
    WAAAFRICA TUNAHITAJI KUBADILIKA,TUJENGE UCHUMI WETU,SARAFU YETU HAKUNA KITU KIGUMU KAITKA HII DUNIA.

    DINI,UKABILA,SIO SABABU ZA KUTUZUIA KUKAA PAMOJA,ILA TUTUMIE KAMA ZANA KATIKA NIDHAM,TAALUMA NA USHIRIKIANO.

    WHY ARICA!

    MADAU-CALIFORNIA!

    ReplyDelete
  13. Nimemind shati la Mzee Pinda!

    ReplyDelete
  14. hivi, huyu ni yule pinda mtoto wa mkulima au?

    ReplyDelete
  15. Jamani Mizengo Pinda!!....staki bwana.......kumbe UNATISHA KIASI HICHO!!!....Hilo shati ulilovaa si mchezo!!!

    ReplyDelete
  16. I can't believe tumeachwa wenyewe. Baba na mama wameondoka.....weee baba weeeeeeeeeee nyumbani hukupendi utazania una watoto wa miaka minne wanakupigia makelele

    ReplyDelete
  17. jk hicho kitita mfukoni might be about what 10m?

    ReplyDelete
  18. nakumbuka msema chochote MC mmoja alikuwa akinivunja mbavu vilivyo na line kuhusu heshima za suti, mojawapo ikiwa unapoibiwa huwezi kupayuka 'mwiziiiiiii huuuuuyooooo, kaniibiiiiiia!' bali unagumia kichinichini kwa shibe: 'muiiiiizi, muiiiiizi,kaaaamata muizi!'. hapa ningependa kuongeza 'adabu nyingine ya suti': vitu vyooote shurti viwekwe kwenye koti la suti, ndo maana lina mifuko mingi. sasa sijui hilo 'fuba' linafanya nini kwenye mfuko wa sarawili!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...