HABARI ZA ZAKO KAKA MICHUZI..
NAOMBA KUSHARE HII KITU NA WADAU WOTE WA BLOG YETU YA JAMII KUJUA KUHUSU MKUNGU HUU WA NDIZI AMBAO UNASEMEKANA KUWA NI MREFU KULIKO YOTE DUNIANI...UNAPATIKANA INDIA.
WAKO MDAU WEST.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. duuuh, kama na waona wadau wetu wa kichaga na wahaya mate yanavyowatoka!

    ReplyDelete
  2. Mdau hii picha mkundu ni huko Malaysia ni India kama unavyosema Mdau... Bofya hapa utaiona http://thumbnails.thestar.com.my/view.asp?id=4463

    ReplyDelete
  3. hautwi mkungu, unaitwa mndizi, swahili gonga gonga kidogo hee

    ReplyDelete
  4. Duh Nkikiroo??! Lakini huo mgomba ni wakichawi au wamitambiko? Mbona naona vyungu, Sinia vinaingilianaje na huo mgomba?

    Lakini huo mgomba waelekea mkungu ndio ni mrefu ila ndizi zake haziwi na afya sana ni vidogo dogo. Yaelekea unaweza ukamenya ndizi hamsini ndio zikatosha katika mlo wa mtu mmoja kwa siku kwa jinsi vilivyo vidogo.

    ReplyDelete
  5. We anon 08:25:00am hebu acha ushamba na wewe. Tangulini mkungu ukaitwa mndizi?? Hehehehe hujaenda shule!!!Ulikimbia umande.

    Mti wa ndizi unaitwa Mgomba, Kile kinachoota kimeshika ndizi na ndizi kwa ujumla kinaitwa MKUNGU wa ndizi, na ndizi ni ndizi zenyewe.

    Hakuna mndizi wala ndezi hapa.

    ReplyDelete
  6. mdau namba mbili hilo jina la mkungu ni kiboko yao jamani tuwe tunasoma meseji zetu kabla hatujazirusha kwa mkuu kweli mkungu huo umefana

    ReplyDelete
  7. Anony wa pili toka juu, chonde chonde hauitwi mkundu bali waitwa mkungu!!!

    ReplyDelete
  8. Mkungu wa ndizi nafikiri umetoakana na neno `mkonga wa tembo' kwani unaonyesha kufanana,hivyo likakokotezwa neno `mkungu wa ndizi' kama ilivyo `mkonga wa tembo'

    M3

    ReplyDelete
  9. HA HA HA MKUNDU MREFU KULIKO WOTE!
    WAINDI HAWACHELEWI KUUABUSDU ATI NI MUNGU NDIZI.

    ReplyDelete
  10. Wadau mliochangia mmenichekesha balaa. Asanteni sana kwa kuniongezea siku za kuishi maana nimecheka mpaka nikalia!

    Mdau uliyemkosoa aliyesema mndizi, mwenzio kafanya kusudi tu. We wadhani ndo hajui kweli? Basi umenifurahisha ulivyopaniki kwa kudhani kuwa kweli hajui kumbe mwenzio ndo lengo lake, alijua atampata mtu wa aina yako!

    ReplyDelete
  11. burdani imeanza hapa mkungu..mdizi..mgomba..halafu mmoja kachafua hewa humu. Haya tuendelee .....

    ReplyDelete
  12. na wewe mkilema tuondokee hapa, kujua mkungu wa ndizi kama unaitwa mkungu pia mtu mpaka uende shule? Kilema wa akili wee.

    Matangalu

    ReplyDelete
  13. mti wa ndizi unaitwa Mdizi.

    anony wa pili kutoka juu, wewe ni descendant wa mzee Mkan'ga wa magomeni? au vipi?

    mbona nakuja hapa nachafua hali hewa kabisa.

    ReplyDelete
  14. waitwa mgomba huo, acheni ujinga

    ReplyDelete
  15. Anony 12:34 hiyo ni migomigo babu umenikumbusha mbali kaka,mzee mkang'a wa magomeni,simba wakutupa vipi zuna linaendeleaje ndani ya shibamu hotel...anony 2 si mchezo mku.du wa malaysia? hahaha

    ReplyDelete
  16. Comments, burudani kabisa....

    ReplyDelete
  17. Kwa hakika huu ni feki wa kichina,wachina kwa vitu feki wapo kila mahali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...