katika kuendeleza libeneke la darasa la lugha na mambo mengine, mdau katuletea taswira hizi za nyangumu huko marekani ya kusini na kuhoji je kiumbe hiki kikubwa kuliko vyote duniani huwindwa ama huvuliwa? globu ya jamii, yenye shehena na hazina kubwa ya wadau wenye busara ina imani jibu litapatikana mara moja. wadau msaada tutani kwa swali hilo..
jamaa wakinanihii nyangumi kwa visu. inahitaji moyo lakini...
ni msosi wa miezi sita



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. duh! kwa mtindo huu nadhani anawindwa na si kuvuliwa. yani jamaa wanamrukia na mikuki utadhani wanaua simba!!!! sasa hawa jamaa waliopigwa picha wakiwa hewani wamemrukia na mikuki yao wanapotua si wanatua kwenye maji hii imekaakaa vipi hii wadau!!! sasa ukitua kwenye maji si ndo nyangumi unaye humohumo???

    ReplyDelete
  2. jkt. atakaeweza kunipa kirefu cha jkt kama nilivyomaanisha mimi atapata zawadi nono. kama uko tayari weka email address yako hapa au namba ya simu nikupigie au nikuandikie email unipe jibu na nikupe maelekezo ya kupata zawadi yako. narudia tena unatakiwa kupatia kirefu kama nilivyomaanisha mimi.
    ahsante

    ReplyDelete
  3. Dear Michuzi,
    I tried emailing you about this but can't seem to get through so I will just say it here :D
    Kusema kweli your blog is one of my favourite Tanzanian blogs lakini you need to update your layout. PLEASE! Font inaumiza macho and the lack of paragraphs makes it so hard to read. Pia sometimes unakuta unaandika na rangi nyekundu KALI na na nyeusi au blue unachanganya. Are you trying to induce a seizure? lol joking.
    Anyways to see what I am talking about check out bongocelebrity.com which is a site I came across recently. It's not as good as yours in terms of news since it's not updated frequently however the layout it great.
    thanks so much!
    xoxo Kammy.

    ReplyDelete
  4. Kuna show moja ya TV nchini USA inaitwa whales wars. Hawa jamaa wanapigania haki za Nyangumi duniani wasiuliwe. Vita vyao vikubwa ni dhidi ya meli za Kijapan ambazo zinaua kwa wingi whales duniani kwa ajili ya msosi; lakini Wajapan wanasema ni research.

    ReplyDelete
  5. duuuuuuuuuu eee banaeee

    kwa mtindo huuu hawa jamaa wanaweza hata mutusaidia kumwua shetani

    ReplyDelete
  6. Huyu nyangumi naye huwa anakula watu hivyo waachwe tu wamtie adabu. Hata hivyo inaonyesha kuwa kweli umoja ni NGUVU - Mwalimu Nyere 1958 Tabora

    ReplyDelete
  7. JKT = Jeshi la Kujenga Taifa.
    Nipe zawadi haraka....0783684684..Au kama unamaana nyingine hilo swali halihusiani na wazawa wa Tanzania

    ReplyDelete
  8. duh! hiyo picha ya tatu hao jamaa sio wale ma actor wa ile sinema ya "god must be crazy" ?? wameniacha hoi hao wanaoruka juu kwa juu mambo ya mlo hadi mbawa zinaota laivu
    mdau canada

    ReplyDelete
  9. Anawindwa (anasakwa, anatafutwa)kwanza, akiisha patikana (baada ya kumua),baadaye anavuliwa (anatolewa toka kwenye maji).

    ReplyDelete
  10. Nakubali kuwa jamaa hawa watafuta rizki lakini naona kuna ukatili wa kutisha.Huyu nyangumi masikini ni kiumbe kisichomdhuru mtu, mdau (labda atoka U) asema nyangumi anakula watu hiyo si kweli hali hata samaki
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  11. xoxo Kammy unapaswa kupata matibabu ya macho yako!! nadhani layout, font, rangi nk ni perfect hapa kwa 'Uncle'

    ReplyDelete
  12. kwanza anajengewa hoja kiki kizima, kisha ana anaviziwa viziwa kimtindo halafu ana pigwa ambush kimachale machale halafu anazimia maana huyu kufa si kirahisi hivyo. Mwisho sasa ndiyo jamaa wana mkokota huyu huwezi kumvua eti, akifikishwa ufukweni kila mtu anaanza kwa mtaji wa nguvu zake kilo mia elfu yaani hapo hamna mjadala wala hitimisho....

    ReplyDelete
  13. J~jua
    K~ali
    T~anzania,
    haya mweshimiwa thawadi yangu.

    ReplyDelete
  14. jaman huyo nyangumi hasa,
    but hakuna haki ya kumuwinda kabisa eti cjui coz anauw o wat, wewe ukimvamia maskan kwake lazima zkufanye hamna kabisa.....
    mpeni haki yake ya kuishi jaman mi rohom yuma nikiona wanavyo msulubisha hapo jamani,,, bas 2 tafanyaje zaid ya kusema DONT KIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIL IT!

    ReplyDelete
  15. HAO WAVUVI NI KWERE YAN,,, HAWAVUI VIDAA HATA KDOGO,,, WAZEE WA KAZ HASA,
    BUT HUYO JAMAA HAWINDWI HAT KIDOGO JAMAN.

    ReplyDelete
  16. Jamaani. Sasa hii ni njaaa!!!! ama nini? manake binadamu amezidi kula ovyo kila siku, na hiii minyangumi tena, hebu wawaache hao wanyama wa baharini wakae kwa amani, wapo samaki wadogo wa kila aina ambao ni wa kuliwa, kama kitoweo. Angalia kwanza jinsi wanavyoangaika, kummaliza nyangumi. wenyewe wadogo. Nyangumi mkubwa, na huyu mnyama mtaratibu, la sivyo angewamaliza wote hao

    ReplyDelete
  17. kwa wale mliojaribu kujibu swali langu kuhusu kirefu cha jkt "kama nilivyomaanisha mimi" bado hamjapatia. wewe uliyetoa namba ungepatia tu ulikuwa umekula bingo hiyo ya pound 400, yule aliyetoa jibu la pili hata angekuwa kapata ingekuwa ishu kupata zawadi sababu kumjua ingekuwa taabu. kimsingi bado hamjapatia jaribuni tena swali bado liko palepale

    ReplyDelete
  18. Anaotewa halafu anategewa tego

    ReplyDelete
  19. anonymous 1155. typical mshamba. reluctant to change. uko happy the way things are eh? If you just took a look at the website i was refering to you would see what i was talking about.
    Anyways hiyo ilikuwa suggestion to uncle michuzi to have a neater more-up-to date looking blog since he has such a large following. It might actually increase his following in my opinion. Now sijui wewe labda bado utakuwa unatumia typewriter. i wouldn't be surprised.
    peace.

    Kammy

    ReplyDelete
  20. JAMANI MAREKEBISHO HAKUNA HATA AINA MOJA YA NYANGUMI YENYE KULA WATU. NYANGUMI JAPO NDIO MNYAMA MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI CHAKULA CHAKE NI UDUVI(VERY SMALL SHRIMPS), NA SAMAKI WADOGO WADOGO WAPATIKANAO KARIBU NA BARA LA AKTIKI NA ANTAKTIKI. ELIMU MUHIMU UKIONA ELIMU NGUMU BASI JARIBU UJINGA.

    ReplyDelete
  21. Wee uliyeuliza kirefu cha JKT, Jitu Kubwa Taahira, haya fasta zawadi yangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...