Twiga aliyekuwa amewekwa katika jengo la LAP wengi wanalijua kama Millenium Tower la Kijitonyama Makumbusho ameuawa. Globu ya Jamaii imekuta 'mzoga' wa twiga huyo akiwa amelala chini na kuonekana ni uchafu badala ya mapambo. Redio mbao zinasema kuwa kafa toka wiki jana na hakuna anayeonesha kujali. Bongo tambarareeeeee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. safiii, bongo tambarare...

    ReplyDelete
  2. alikuwa na utapia mlo tu

    ReplyDelete
  3. Twiga huyo aliuwawa na majangili waliotaka kumchuna ngozi ili waisafirishe nje ya nchi, lakini zoezi hilo halikufanikiwa kutokana na kanzi nzuri ya maaskari wa jiji la Dar waliotumia mawe kuwafukuza majangiri hao.
    Mpaka muda huu askari hao kama kawaida yao wanafanya utaratibu wao wa siku zote kugawana Twiga huyo kama wanavyogawana mali za wamachinga.

    ReplyDelete
  4. Ndio ndio! Hakuna cha kujali hapo huo ndio uhalisia wetu wa Ki TZ.Ingekuwa chocho kidogo wale jamaa wa chuma chakavu mambo yangekuwa murua kwao!

    ReplyDelete
  5. Habari zilizotufikia ktk kibanda chetu cha habari ni kuwa Wizara ya Utalii na ufisadi inaunda tume ya watu 200 kuchunguza ukatili uliofanywa kwa Twiga huyu.

    ReplyDelete
  6. Enendeni twiga! nenda kacheze break dance na Michael Jackson.........neeenda twiga, nenda kacheze karate na Bruce Lee..........Neeenda twiga!!!!! Nenda kanywe chai na Samora Michelle........
    Neeeenda twiga------ neeeeenda twiga....

    ReplyDelete
  7. Kaka michuzi mimi ninashindwa kuelewa hawa watu wa baraza la sanaa wako wapi, hivi kweli twiga anawekwa marangi rangi namna hiyo?? mimi binafsi nilikosa jibu maana kuna siku nilikuwa na mwanangu akaniuliza baba mbona huyu twiga kawekwa rangi tofauti na za kwake? nikamwambia hata mi i sielewi why imekuwa hivi akasema sasa watu wengine wajifunde nini kupitia sanaa ya picha kama rangi halisi za huyu twiga zinabadilishwa? kwa kweli ilinilazimu nibadili topic haraka sana maana sikuwa na majibu ya kumpa dogo.
    Angalizo:- Ni vyema tukawa wazalendo zaidi kwani kuweka rangi zinazorandana na za twiga halisi itasaidia pia hata kwa watoto ambao hawajawahi kumuona twiga maana ikumbukwe kizazi cha sasa ni cha kushinda kwenye ma tv na kucheza game tu

    ReplyDelete
  8. Michuzii...
    mimi naona pesa hakuna za kumuweka sawa. Funds ndio tatizo.

    ReplyDelete
  9. mheshimiwa,sio LAP bali ni LAPF (Local Authorities Pensions Fund). Pia LAPF ni jina la kampuni inayomiliki jengo na sio jina mbadala ya jengo lenyewe.

    Jina kamili la jego ni LAPF Millennium Towers

    ReplyDelete
  10. Uncle Nanihii nielimishe hivi bongo tambarare maana yake ni nini?

    ReplyDelete
  11. wasije wakambandua tu hizo rangi wakaenda kuzibandika kwenye nyumba zao

    ReplyDelete
  12. Twiga wa buluuu!!!maajabu kweli,

    ReplyDelete
  13. Petro, kwa uelewa wangu ni kwamba watu wanaposema Bongo tambarare wanalinganisha na barabara ambayo haina mlima wala mtelemko ambapo kama una gari kwa mfano,unakwenda mwendo uutakao. Lakini barabara yenye mlima au mtelemko unalazimika ama kukanyaga mafuta au kukanyaga breki. Kwa maneno mengine unalazimika kwenda mwendo fulani. Kwa Bongo mambo tambarare yaani watu wanajiendea au wanafanya watakavyo!!

    ReplyDelete
  14. Wadau Ukweli kuhusu huyu twiga ni huyu hapa.

    Inasemekana watu walipewa hela kwa ajili ya kutengeneza na kupaka rangi twiga huyu walikata mbio na hela, sasa wenyewe wakajionea ujinga kuingia tena gharama nyingine kwa mtu mwingine ili kumpaka rangi halisi twiga huyu ndio wakachukua rangi zilizobaki baki wakati wa ujenzi wa jengo hilo wakamix kisha wakampaka twiga huyo na sio kwamba hawajui twiga anapaswa kuwa na rangi gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...