TUNA IMANI NA MHE. SPIKA,
KATIBU WA BUNGE – WATUMISHI WA BUNGE

Na Saidi Yakub
Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wameeleza kuwa wana imani na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye wamemuelezea kuwa ni mtu makini asiyetetereka katika kutetea hadhi ya Bunge na Taifa kwa ujumla.

Akisoma risala kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo katika sherehe ya wafanyakazi baada ya kumaliza Mkutano wa 16 wa Bunge mjini Dodoma leo, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Bwana Angumbwike Ng’wavi alisema kuwa wamesikitishwa na baadhi ya habari zinazozagaa kuwa eti Mheshimiwa Spika anawagawa watumishi wa Bunge.
"Tunafahamu kuna kundi la watu linalokereka na uhuru wa taasisi ya Bunge unavyokuwa na namna Bunge linavyofanya kazi zake kutokana na sasa Bunge kuwa mstari wa mbele kupambana na uovu uliopo katika jamii yetu. Mtu yeyote anayetetea haki na kupambana na uovu mtu huyo siku zote atakuwa na uadui kutoka kwa wale wanaonufaika na uovu huo’’ alisema Bwana Ng’wavi.

Aidha, Bwana Ng’wavi alieleleza kuwa mtu mwema kupakwa matope kwa lengo la kumkatisha tamaa siyo kitu cha kushangaza katika ulimwengu huu kwani hata vitabu vitakatifu vinaeleza kuwa Mitume wa Mungu pamoja na mema yote waliyoyatenda bado walipigwa vita na wanadamu. Wengine waliteswa na hata kuuawa.

‘’ Wafanyakazi wa Bunge tuna imani na Mheshimiwa Spika na tunapenda kutoa wito kwa Spika kuwa aendelee na ujasiri huo katika vita dhidi ya ufisadi kwani baadaye historia itaonyesha ni nani hasa alikuwa mkweli na mtetezi wa nchi hii na wananchi wake. Kuna mwanafalsa moja aliwahi kusema, kwa lugha ya Kiingereza “If want your name to continue living even after your death do something worth writing or write something worth reading” Kwa tafsiri isiyo rasmi mwanafalsafa huyu anasema ukitaka jina lako liendelee kuwa hai hata baada ya kifo chako fanya jambo linalostahili kuandikwa au andika kitu kinachostahiliki kusomwa’’ ilisema sehemu ya risala hiyo.
 
Wakizungumzia kuhusu madai kuwa Katibu wa Bunge wa sasa, hana sifa za kushikilia nafasi hiyo, Wafanyakazi hao walisema kuwa wanashangazwa na madai hayo kwa kuwa katibu wa sasa ni mtaalam aliebobea katika masuala ya Bunge na uendeshaji wake.
‘’ Bahati mbaya wanaoeneza hayo hawajafanya utafiti wa kutosha, kwani kama wangefanya utafiti wa kutosha wangegundua kuwa Dk. Thomas Kashililah ana uzoefu wa masuala ya Bunge kwa zaidi ya miaka ishirini akiwa ameshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo Ukurugenzi wa Idara nyeti ya MipangO naTeknolojia ya Mawasiliano, Ofisa wa Bajeti, Katibu Mezani, Katibu wa Kamati za Bunge na Afisa Mfawidhi wa Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es salaam’’ ilisema sehemu ya risala hiyo.

Wafanyakazi hao walisema kuwa Dkt. Kashililah ambae ni daktari wa falsafa ana sifa za kutosha na zimepita sifa za msingi anazopaswa kuwa nazo Katibu wa Bunge na wametoa wito kuwa asikatishwe tamaa na maneno hayo ya uzushi bali aendelee kuchapa kazi na kwa kushirikiana na Mhe. Spika aboreshe mazingira ya kazi na vitendea kazi.

Hivi karibuni kumekuwa na juhudi zinazofanywa na watu wasiopenda jitihada zinazofanywa na taasisi nyeti ya Bunge kwa kujaribu kuwachafua viongozi wa juu wa taasisi ya Bunge kupitia magazeti na mitandao ambapo Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge limelaani na kusema kuwa sio sahihi hata kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Habari ndo hiyo! inachoma mbaya hiyo to mafisadis!

    ReplyDelete
  2. AROBAINI YA WEZI WA JNIA INAKARIBIA SANA. BEAWARE NA BREAKING NEWS.

    ReplyDelete
  3. AROBAINI YA WEZI WA JNIA INAKARIBIA SANA. BEAWARE NA BREAKING NEWS.

    ReplyDelete
  4. bla bla tu na kulindana kwingi mnalindiana ugali wenu sio...haya tutaujua tu ukweli ipo siku

    ReplyDelete
  5. sasa ulitegemea waseme nini?
    Hata wangepiga kura ya kutokuwa na imani naye kwani wao ndio waliomuweka?
    Hizi porojo waache sawa na watu walioko sumbawanga kuwaponda wanaohoji safari za kikwete.
    Nchi hii ukiwa madarakani hata ufanye kosa vipi hakuna wa kukuhoji kwani watawala wako juu ya sheria kisa sheria zetu hazina meno kwa wakubwa. Bunge letu kwa sasa hivi haliwatetei walioliweka madarakani kwani wananchi tuna maana kwao wakati wa kampeni ndiyo maana spika naye anaongelea suala la uchaguzi hasa jimboni kwake keshaona kama kuna watu wanajitokeza naye anataka kuwa kama mfalme kwani kwenye utawala wa kifalme mtu anayetokea kumpinga mfalme kichwa ni halali ya mfale.

    Michuzi naona una kawaida ya kutupa maoni ndani ya kapu hasa pale ambapo mawazo yanayotolewa yasipikubaliana na wewe

    ReplyDelete
  6. hawa wafanyakazi wameniacha mdomo wazi waliposema

    "ana sifa za kutosha na zimepita sifa za msingi anazopaswa kuwa nazo Katibu wa Bunge"

    wao ndio wanamkatisha tamaa katibu wao.

    Je ubwabwa ukipitisha viongo unakuache?

    au chumvi ikizidi kwenye mboga ..

    nadhani kama ni maharagwe huta yala
    au sio?

    akili kumchwa!

    ReplyDelete
  7. Hili changa la macho......Ren-mich!!!

    ReplyDelete
  8. sielewi elewi tu labda kwa kuwa usiku ngoja nilale nitaisoma vizuri kesho

    ReplyDelete
  9. hiyo ni kawaida bwana. lazima wamfagilie vinginevyo hakuna ugali.

    we anon wa Aug 02, 10:29:00 PM Michuzi amewabeba hao hawabebeki sasa kaamua mambo hadharani. hatupi kitu. ila binafsi nampongeza kwa uchapakazi wake.

    mdau wa Arusha

    ReplyDelete
  10. Wana maana gani wakisema taasisi "nyeti ya bunge",hebu ninyi mnaojiita wafanyakazi wa bunge acheni ulimbukeni na ujinga,kila mtu ana umuhimu wake katika jamii siyo bunge pekee au spika/katibu wenyewe.Kila mmoja anahitaji heshima kama ambavyo wao wanavyohitaji..MLITAKIWA MUJIBU POINTI ZINAZOZUNGUMZIA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA WALIPA KODI NA SI VINGINEVYO.Sasa mbona hamjagusa huko? Ninyi wafanyakazi hamuwezi kuwa waamuzi wa sakata hilo na utetezi wenu hauhitajiki,watanzania tunataka ukweli na wala si vinginevyo jinsi ambavyo pesa za walipa kodi wa nchi hii zinavyotumika..spika anaweza kuwa anafanya kazi vizuri..ni kweli na mimi namuunga mkono lakini kama suala la matumizi mabaya ya fedha limetokea linapaswa kuchunguzwa kwani uzuri na ufanyaji wake kazi mzuri haulalishi ubadhirifu,Kama ubadhirifu upo unapaswa kushughulikiwa na ngazi zinazohusika na kama haupo basi aombwe msamaha.

    ReplyDelete
  11. spika alichaguliwa na wabunge sio hawa wafanyakazi njaa walioandika waraka huu.
    wenye kusema wana imani na spika ni wabunge,sio wao wanapalilia matumbo yao.

    wao wafanye kazi zao sio kujiingiza kwenye mambo ya bunge.

    naona kuna kundi la kujipendekeza la wafanyakazi wa Bungeni wanataka kumtapeli spika na katibu wa bunge kuwa wanatetea ili kulinda maslahi yao.

    hao ni wafanyakazi njaa,kwanza ni jina la mtu mmoja tu ndio lililojitokeza sasa hao wafanyakazi walikubaliana lini na wangapi wanalisema wana imani na spika? haiwezekani kama ilipingwa kura wote wakasema wanamtaka au wote waseme hawamtaki.

    ReplyDelete
  12. Said. Do you think about those kid in Mwakidira who doesn't have healthcare, do you think about women who are hopeless in Mwanzange? Do you think about kids who are studying without light at night ni Maweni?

    I know you said for many years, evernthough you don't know me. You was an insparation figure at Usagara, then Tambaza and BBC. But i feel something different from you now days. I knew this will come, soon after i heard about your new job. I knew you will loose touch with those who are hopeless across Tanzania.

    In the bottom of your heart Said you know how poverty is. You grow the same area i grew up. You know how those kids lost hope because Dododoma is not deliver what it promised them. I feel hopeless to hear that you too joined the torpedo of lies.

    [2:77] Do they not know that GOD knows everything they conceal, and everything they declare?

    ReplyDelete
  13. mimi kila nikikumbuka CDA Dodoma nabaki kucheka tu. Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  14. tuzidi kusali na kuomba, wanafiki Mwenyezi Mungu awabaini! ni suala la muda jipeni moyo.

    ReplyDelete
  15. Wizi mtupu...,s$##@#%****t!
    Hoja hujibiwa kwa hoja na si vinginevyo. Mshatufanya wananchi wapumbavu hatuelewi nini kinaendelea! Nyie ndio mnaotudidimiza katika lindi la ufukara. Ole wenu siku zenu madarakani zinahesabika.
    Michuzi comment yangu ibandike tafadhali.

    ReplyDelete
  16. Jamani eeehe! naomba ulinzi wa ziada hawa jamaa wamenishika baaabayaaaaa!

    ReplyDelete
  17. hizi ni hadithi za kula mbakishie baba,
    kula mbakishie baba.

    ReplyDelete
  18. shutuma za kwa spika mbona hawajajibu hata moja? wamekuja na habari za PhD ya katibu wa bunge inahusu nini?kama ana phD akafundishe university of Dodoma.

    ReplyDelete
  19. wewe yakub na wewe umeshakuwa fisadi?jamani njaa mbaya.umelipwa kiasi gani na spika?

    ReplyDelete
  20. habari ya hawa wafanyakazi hawajaipeleka gazeti lolote zaidi ya hapa na kwa mwanakijiji.

    ReplyDelete
  21. Habari hii imetoka Nipashe, Guardian na Tanzania Daima!Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...