ukumbi A
Ukumbi B
anko nanihii hakosagi kwenye minuso kama hii pahala kama hapa.
Ila wadau wamesikika kulalamika kwamba kastama kea hapa mlimani city conference centre iz not richebo kihiiiiivyo. unaambiwa jamaa wanakwambia mwisho saa sita kamili juu ya alama.
ukipitisha dakika kumi tu wanazima umeme, huku wafanyakazi wake wakiwa wamemnuna na huku wameshika kiuno mlangoni wakingoja mkitoe. ukiwauliza wanakwambia ebwaanaaaaa eeee kesho tuna kazi ingine hapa. fanyeni muondoke tuanze usafi. ukihoji zaidi utaambiwa nenda msimbazi centre uone wanavyofanya, na hakuna anayelalama.
mdau mwingine alisema tatizo sio kuheshimu muda bali kauli zisizo za kistaarabu pamoja na vitendo vya hawa jamaa, kwani kuna siku wataunguza vyombo vya mtu kwa kuzima umeme ndipo watajua nini faida ya ustaarabu.
wadau hili limekaaje?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Safi sanaaa. mkishaunguza miziki yenu ndo mtajua nini maana ya punctuality, mshaambiwa saa 6 mwisho nini hamuelewi. haa haaaa, nimelewa bwana wakati naandika ila jamaa wanaudhi hawa

    ReplyDelete
  2. Kama utaratibu mwisho saa sita, ni kitu gani ambacho hakieleweki? Wahi mapema pata maakuli na unavyotaka, muda wa kufunga ukifika nyanyuka nenda nyumbani. Hao wahudumu hawawanyanyasi nyie ndo mnawanyanyasa!Hamuwalip overtime wala hamuwapi tip, hiyo ni kazi kama kazi nyingine muziheshimu na kuwaheshimu wahudumu. Hata huku majuu muda wa kufunga ukifika umekaa tuu, wanakuambia uondoke muda umeisha na hakuna anayebishana nao, unaondoka laa sivyo utaitiwa polisi wakufundishe utaratibu.

    ReplyDelete
  3. Hivi?!! what is with that fulana? ina maana, cant you choose places that you can or can not put on that fulana michuzi! thats too much sasa, keh!

    na ole wako ubane hii comment!

    ReplyDelete
  4. Wanatakiwa wasiwazimie taa huku ukizidisha muda unalipa faini ya nusu ya gharama kamili ya ukumbi, unatakiwa kuweka deposit ukitimiza masharti yao na kutoka kabla ya muda unarudishiwa deposit na ukiwacheleweshea kufanya usafi unapewa mafagio kupangusa na kufyagia kwahiyo hiyo ndio inawafaa kuwashikisha adabu

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa Mon Sep 28, 10:53:00 PM,

    Wewe umeona hapo mahala pa maana sana nn? naona ingekuwa ni wewe ungeenda kuazima na suti kabisa.Heheh just joke usimaindi ...

    ReplyDelete
  6. sio hao tu, hapo mlimani city wafanyakazi wake ni kweli majeuri, kuna siku nilikuwa hapo na watoto na nikawanunulia ile pamba ya sukari bahati mbaya mmoja mdogo alianguka na ile pamba ilimuanguka pia, tukaiokota na kuitia kwenye dust bin, kidogo nikafatwa na mfagiaji anatukemea kwa hasira kwanini tumemwacha mtoto anachafua na akanitaka niende nikapasafishe, nikamwambia siendi kusafisha kwani nimemtuma makusudi mtoto aidondoshe ile pamba na kwani wewe kazi yako nini hapa si umewekwa kusafisha nikamwambia akawambie hao wanaouza wasiuze sababu wanunuzi wakubwa ni watoto na kama hivi mtoto kaanguka kachafua au kama huwezi ntaenda kuwambia mimi, alipoona nimesimama ngangari akawa ananiomba nisipandishe sauti basi yeye atasafisha lakini waangalieni watoto wasichafue! Basi baadae nikamkuta pale mlangoni anasafisha upande mmoja na huku upande wa pili watu wanapita na nje kulikuwa na mvua, wakawa wanaingia na matope, jamaa alikuwa anasafisha huku kanuna kakunja uso utafikiri yuko chooni anajikamua! maana anajua akitoka pale itabidi akasafishe na upande ule mwingine!
    Ukweli ni kwamba watanzania ni wavivu na mabishoo tu hiyo kazi ameikubali sababu anapata mshahara mkubwa labda lakini hataki aonekane yeye ni mfagiaji, anasubiri mshahara tu mwisho wa mwezi.
    Ma Mall ya nje wasafishaji hata hawaulizi kwanini umetupa kitu wao wanajua kazi yao wakiona uchafu wa aina yoyote ni kuuondoa, japo kuna wengine wanatupa vikaratasi kama vya chewing gum, risiti n.k kwa makusudi.

    ReplyDelete
  7. Mmmmhhhhhhh anko nanihiii hicho kifulana utafikiri hakibanduki mwilini kama ngozi! au unazo nyingi zenge rangi na size sawa! Lazima itakuwa inaprojuzi kibafyumu fulani hivi kwani lile jua la thame sio mchezo! na ile kupiga jeki kubadili tairi lazima ulivuja vimaji mmhh uwe unabadilisha wakati mwingine hasa kwenye minuso ya watu!
    Mdau USA

    ReplyDelete
  8. kwakweli mzee wa libeneke hlo halijatulia kabisaaaaaaaaaaa. pesa tutoe sisi alafu watufanyie unyama kama huo. inabid manager aambiwe mambo kama hayo yanaharibu biashara bwana kwanza hao waudumu mshahara wanaupata kutokana na wateja ngoja watu wsitishe huduma alafu tuone kama wataenda chooni

    ReplyDelete
  9. Kaka Michu, kwa kweli hiyo tisheti ina kaaazi kweli kweli! Haichagui popote inakwenda, ilikuwa safarini Arusha, kwenye mnuso hiyo hiyo!! Hayo masharti ya mganga ulioenda ni magumu!

    ReplyDelete
  10. Ukumbi unacost kiasi gani hapo? Nina mnuso karibuni....

    ReplyDelete
  11. NAAMINI TATIZO SIO WAHUDUMU NI SISI WATEJA.

    Tunalaumu tulipoangukia badala ya kuangalia tulipojikwaa.

    Usitaarabu ni kwamba fuata masharti kama mlivyoafikiana, la sivyo wafauate kabla muda hujaisha na mjadili nini kifanyike kwa muda unaotaka kuzidisha.

    ReplyDelete
  12. Michuzi Mganga wako ndio kakwambia usivue kit-shirt hicho nini, manake smhikaji kimezidi. Usikute ndio maana watu hatuishi kwenye blog yake. Pengine kinavuta kimazingara mtu kuingia humu. Yaani mimi ni lazima niingie michuzi kila siku ndio siku ikamilike, pengine ni hako ka-tshirt kanatuvuta, Hahaaaa!

    ReplyDelete
  13. sitanii wala nini hiki kifulana kimepauka sana nahisi hata huko kwenye kikwapa imekuwa ya njano EWE MUHIDIN ISSA WA MICHUZI!!!! mkuu wa libeneke tunakuomba saana hicho kifulana sasa basi tunaeelewa unaona raha kutuonyesha sisi wadau kuwa unakimaindi sana hicho kinguo lakini sasa hakileti tena maana wadhungu wanasema too much is_ _ _ _ !!!!
    miss michuzi

    ReplyDelete
  14. Mithupu ilibidi hiyo T shirt uvae na tai.
    Halafu inaeleka kana nuka maana mtazame huyo dada wa mbele yako alivyo kunja uso

    ReplyDelete
  15. Michuzi inabidi ubadilike watu wamekumaindi sana na hiyo fulana yako maaana wametafsiri kwa uvaaji huo umedharau sherehe yako has ukiangalia watu wmepiga masuti.

    ReplyDelete
  16. Michuzi inabidi uvae kulingana na mazingira hata mimi ukija kwenye sherehe yangu na T-SHIRT nitaona umedharau sherehe yangu.Jitahidi kuvaa kulingana na mazingira, hiyo T-shirt ungeivaa kwenye michezo hakuna mtu angekuuliza.Hiyo ni sehemu rasmi inabidi uwe rasmi.Ukivaa suti kwenye michezo kila mtu atakushangaa kama ilivyo kuvaa T-shirt kwenye sherehe rasmi

    ReplyDelete
  17. Kaka Michu, nakuheshimu sana ila hiyo t-shirt umeshavaa kupita kiasi tena unai-abuse. Na vipi huyo mama Michu hakupangii nguo?? Mwambie tutamsaidia kukupangia nguo ebo!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...