Habari kaka Michuzi,

Sijui utanisaidia vipi kuiweka hii na ningeshukuru kama ingefika kwa wahusika. Maeneo ya Veta leo nilikuwa naelekea nikiwa na gari aina ya Surf. Ni kweli kioo chake cha mbele kina crack na hayo matatizo mengine madogo madogo lakini gari iko kwenye good condition.

Askari alitukamata na akawa anatengeneza mazingira ya rushwa. Kwa kweli nilimsisitiza sana aangike notification na pia namba yake ya kazi. Aliponipa karatasi nikamhoji

- mbona hii ni note paper na siyo notification ya polisi yenye number na kila kitu.

- kwa nini unaniambia niache gari nikalipie Changombe polisi ndiyo nirudi kuchukua gari.

- Notification haina namba ya gari wala mhuri wala signature.

Baada ya kubishana kwa muda mrefu na kwa kuwa nilidhamiria kuona mwisho wa hii nilihakikisha nabaki na hii 'notification' (pichani) na aling'ang'ania nimpe Tsh 10,000 ambayo nilimpa ili nipate nafasi ya kuonyesha hali halisi ya hawa polisi wetu.

Tafadhali usitaje jina wala e mail yangu. Ila kama ni wahusika watataka kuwasiliana na mimi niko tayari . Kama ameandika namba ya uongo basi nitatoa picha yake niliyompiga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Nchi ya Kiswahili mwisho Naona maandishi ya Kiengereza mishoni sasa sijui kakosa la kuandika kwa kiengereza kaandika kiswahili. Pazi

    Wiiiiiiiiiizi Mtupu Ramadhani yute hii. Ungemtizama Naye Vazi la Kazini barabarani kavaa inavyotakiwa.

    ReplyDelete
  2. thats wat im talkin about..good analysis na hivi ndio watanzania sasa hivi tunatakiwa tuwe sio ukiona aksri tuuu unaanza kuchachawa..ndio maana nasema siku zote somo la Uraia na sheria mbalimbali bado linahitajika sana Tanzania kwa wananchi wote.

    Pole sana mkubwa na nimefurahi sana kuleta mfano huu maana ni mengi tunakutana nayo

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa juhudi zako. lakini hujui mpokea na mtoa rushwa wote ni maadui wa haki? Kwa vile ulikubali hatimaye kutoa rushwa, basi unapaswa kuwa mpole tu!

    ReplyDelete
  4. Haya sasa wadau, tuanzishe mpambano hadi huyu askari awajibike!!Kama kuna mtu anaweza akamfikishia kamanda kombe/Mwema/kova hii karatasi itakuwa vizuri!! mdau umefanya vizuri sana....kama pia inaweza ikapostiwa magazetini pia itakuwa bomba sana! cha msingi ni kwamba huyu askari awajibike kwa ujinga wake wa kuandika Notification kwenye plain paper!Wadau washeria tushaurini kwanini tutoe/tusitoe picha ya huyo askari ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake na sisi tuendelee na mambo mengine! hii issue isiachwe hivihivi...wamezidi sana hawa watu

    ReplyDelete
  5. Wa kulaumiwa ni wewe kwanza kwa kutembeza gari lenye kasoro mbali mbali, kwenye sheria hakuna makosa madogo madogo yote yana stahili yake, eti unasema gari lipo kwenye GOOD CONDITION mmmh! Sijui una maana gani wakati haziwaki?

    ReplyDelete
  6. Hii safi sana, Hii ndiyo tunaiita whistle blowing, wenzetu huku Ulaya wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokomeza rushwa kwa watu kuwa open, transparent. Mtu akikuomba rushwa unampa halafu unamshitaki polisi on spot, sasa kwa kuwa hawa jamaa ni faithful ukimripoti mwenzao tu wanaona kama anawapaka matope na kumshughulikia ila bongo nadhani itakuwa ni kulindana na kupeana tahadhari, kwani wanaotakiwa kuwashughulikia hawa wala rushwa barabarani ndiyo wanao watuma kuleya hesabu ili next day apangiwe tena eneo zuri.

    Nafikiri tukiwa na nia thabiti ya kutokomeza rushwa tunaweza, na wa kuanzia nao ni vigogo. Vigogo wakiisha ona wapo kwenye hatari ya kupoteza kazi zao basi watalazimika kuwawajibisha wa chini ili kulinda nafasi zao.

    Tuanzie na kuweka sheria ya kunyongwa kama china. Ila ni dhahiri kuwa huyo jamaa kaandika jina na namba za uongo. Kinachotakiwa sasa ni kutembea na Camera kama CCTV mtu akikuletea za kuleta unakuwa na mkanda.

    Rushwa haitaisha Tanzania kwani viongozi ndiyo wapaliliaji na waweka mbolea wa mdudu huyu.

    ReplyDelete
  7. tafadhali tunaomba picha ya huyo askari...Brother Michu naomba wasiliana na huyo jamaa then tubandikie picha ya huyo askari hakika atashughulikiwa tuu

    ReplyDelete
  8. tutabaki kunyanyasana wanyonge mafisadi wanapeta. akale wapi, na wewe umetoa hiyo elfu 1o badala ya 60 huoni hapo ndo jinsi mambo yanavyokuwa nanihiii bwana. achane hizo akale wapi sasa

    ReplyDelete
  9. Kwa ushamba wako;
    1. Unayo notisi unatakiwa ukalipe faini ya Shs 60000.
    2. Unakubali ulitoa rushwa hivyo unastahili kufikishwa mbele ya haki. Na naamini huna ushahidi wowote kwamba afande alipokea rushwa hiyo.
    3.Umekubali kuendesha gari ambayo haistahili kuwa barabarani.
    4. Ukumbuke bado uko barabarani na Polisi sasa wanalijua gari lako sasa wewe watakukamata tena na jasho itakutoka.
    5. Akili ni nywele nafikiri wewe una kipara.
    Mzawa

    ReplyDelete
  10. Huyo trafiki atakuwa mjinga sana kuweka namba yake hapo kwenye karatasi...

    Just curious, mwandiko ni wa kiume, je huyo trafiki ni mwanaume?

    ReplyDelete
  11. Safi sana, mdau nakupongeza, u have done ur part kuhakikisha haki na sheria zinafuatwa na umeonyesha mfano wa nini cha kufanya katika mapambano dhidi ya rushwa badala ya kukaa kulalamika. NACHONGOJEA NIKUONA WAHUSIKA WATACHUKUA HATUA GANI..NAJUA KAMANDA KOVA NA WAKUBWA WENGINE WA POLISI MSHAIONA HII MPAKA SASA...TUNAWASIKILIZIA.

    ReplyDelete
  12. kazi nzuri!nakubaliana na aliyesema somo la uraia na haki ya mwananchi linahitajika kufundishwa sana tu tangia ngazi ya shule ya msingi,na kwa walio maliza masomo ni vyema harakati za kuwaelimisha mitaani zifanywe.
    SAMAHANI KWA KUTOKA NJE YA MADA KIDOGO,ILA NINA OMBI KWA ANAYEFAHAMU NA MWENYE DATA KAMILI ZA SASA ZA VIWANGO VYA MISHAHARA (PGSS,PUT,n.k kuanzia 1.....x) anifahamishe kwa tarakimu halisi.
    yaani kaka PGSS2=80,000Tsh n.k.
    natanguliza shukrani kwa atakaye nijulisha.
    mdau

    ReplyDelete
  13. Tusiwakatishe tamaa watu jasiri kama hawa wanajitolea kwa faida ya sisi wote.Huu usumbufu wa barabarani umezidi. Tuko tayari kukamatwa kwa halali kuelezwa matatizo ya magari yetu na kwenda kulipa faini ya halali na tupewe risiti halali si ndiyo wenzangu. Ila siyo hivi kwa kweli. Je angeenda kulipa angekuwa na uhakika gani anapewa risiti ya halali?Ni vizuri kwa kweli tuwe tunawawauliza panapokuwa na mashaka

    ReplyDelete
  14. Asante sana kwa kutuma hii. Imetufungua macho sana. na watu tumeelewa ila tunaomba kweli hiyo elimu ya uraia na barabarani ilitujue haki zetu

    ReplyDelete
  15. Somo alilotoa huyo jamaa ni kwamba wote ni Wadau wa Rushwa hakika kama kweli hatuipendi rushwa kwa dhati tusingetaka mambo ya ujanja ujanja kama hayo ya kutembeza gari mbovu na kutaka sheria isifanye kazi yake!

    ReplyDelete
  16. Wewe mdau unaetaka viwango vya mishahara humu unaota nini? Kwanini usiwasiliane ofisi husika iliyo karibu nawe?

    ReplyDelete
  17. Hapo naona hakuna msaada wowote utakaopata kwani hilo ni dili la wakubwa waliopo kituoni. Huoni hapo kuna makosa zaidi ya matatu, lakini jamaa anampa dili mwenzie wa kituoni kuwa alipie matatu!
    Siajabu na huko kituoni ukilipia hizo 60,000 unapewa receipts za bandia1

    ReplyDelete
  18. 1.Huna evidence yeyote kama hiyo karatasi umepewa na police
    2.Tutathibitishaje kama kweli umetoa rushwa.
    3.Tutathibitishaje kama mwenye hiyo namber ya police ndie mwandishi wa hiyo notice
    4.Notice haina Paper head utaithibitishaje kama kweli umepewa na police
    5.kwa nini unaendesha gari ikiwa na makosa yote hayo
    6.Je umeshalipia hiyo faini? Tuwekee copy ya Risiti tafadhali...fanya uungwana kama ulivyofanya kwa hiyo notice.

    ReplyDelete
  19. Bradha pole sana na mkasa uloupata lakini "wazee" wanapojichana na EPA polisi wa kawaida wakale wapi?
    Mazingira haya ni ya kawaida kabisa bongo kwa leo na wengi wala hawaogopi.
    Ungempa huyo jamaa buku 10 mbele kwa mbele usumbufu wote usingeupata!!!!
    Njaa tu za watu hawa na nakuhakikishia kuwa hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa maana wanakula na wakubwa!!

    ReplyDelete
  20. Tunahitaji Watanzania kama hao 10,000 tuone kama kutakuwa na masuala ya rushwa.

    Pinda angalia serkali yako inavyoumbuka.

    Huyo askari atafutwe na apelekwe Chamwino Dodoma ili akafundishwe madili ya uongozi ndani ya chama.

    ReplyDelete
  21. Tunahitaji Watanzania kama hao 10,000 tuone kama kutakuwa na masuala ya rushwa.

    Pinda angalia serkali yako inavyoumbuka.

    Huyo askari atafutwe na apelekwe Chamwino Dodoma ili akafundishwe madili ya uongozi ndani ya chama.

    ReplyDelete
  22. Mie naona huyu mdau aliyeweka hiyo notisi ameula chuya.kwanza kama notisi inavyosema anatakiwa kulipa Tsh60,000 kwa hiyo bado ana jukumu la kulipa kutokana na makosa, hiyo rushwa anayodai katoa haijafanya hiyo notisi kuwa si halali, sijui ametoa rushwa kwasababu gani maana bado anatakiwa kulipia makosa ya gari yake. watu wengine bwana kwa kukurupuka.. nenda polisi ukaseme uone kama hawakukun'gan'gania kama luba kutokana na ujinga wako.

    ReplyDelete
  23. Hayo makosa yote matatu huwa hayahitaji hata siku moja faini katika nchi za wenzetu kama UK, US, na Canada.
    Bali huwa wanakupa siku saba za kuhakikisha umetengeneza hayo matatizo yote, hasa hilo la taa kutokuonyesha unaenda wapi na kuripoti kwa polisi yeyote utakayemuona barabarani ili ahakiki na kufuta katika kompyuta yake kwamaba umetengenezaau uripoti kituo cha polisi ili kuripoti kwamba umetengeneza.
    Ukishindwa kutengeneza ndani ya siku saba na ukishikwa siku yeyote basi unatakiwa kupewa faini, ambayo utapewa siku za kulipia, na sio hapo hapo, pia rekodi kuingia katika leseni. Na gari kuambiwa uliache hapo liwe towed kupelekwa kwa fundi/garage.Na wewe uombe ride ya kukupeleka unakoenda.
    Na sio huu mtindo wa TZ wa kuandikiana vikaratasi na kutozwa bei ya CD$ 50(Tshs 60,000) bila sababu za msingi.
    Huyu asakari awajibishwe na wengine waache huu mtindo wa ajabu ajabu bila kufuata sheria.

    ReplyDelete
  24. Ndio bongo tambarare,kila mtu anakula ofisini kwake.wewe kwa nini ukwenda lipia tzs.60000 ukakubali kutoa tzs 10000 kama rushwa wote ni watuhumiwa,kumbuka mtoa na mpokea rushwa wote wana kosa mbele ya haki-kwa msingi huo umeikosesha serikali mapato ya tzs 60000=.
    mdau,
    Kyela-Ipinda.

    ReplyDelete
  25. wewe anony wa sept 7 saa 4:48pm mwenzio ameuliza,inamaana anahitaji kufahamishwa ,wewe unadhani kila anayeuliza basi yuko karibu na ofisi inayoweza kumpa information anazo hitaji?ndio maana hatuendelei kwa staili hii,we toa jibu kama huwezi piga kimya anaye fahamu atajibu.

    ReplyDelete
  26. waanzania bwana kwa kujifanya wanajua mambo hawajambo,sasa wewe anoni unadhani kila kitu lazima watu waende ofisini,ndiyo maana virushwa haviishi huko tanzania maana mnataka face to face contact mnegotiate rushwa kwa kila jambo,kwani viwango vya mishahara ni siri siku hizi!acha muendelewe kuliwa na vigogo maana mmezoea vijisiri visivyo na mbele wala nyuma,vitu vidogo kama hivi vinatakiwa vinapatikana kwenye internet sio lazima ukapange foleni na kupigwa tarehe za kujulishwa viwango vya mishahara!hehehe eti nenda ofisi ya karibu! anahaki ya kuuliza maana hata mimi pia nimetafuta kwenye net sioni,ila napata vya nchi zingine tu na vya UN.

    ReplyDelete
  27. Kweli wabongo kareem hasa. Na mimi naomba viwango vya mishahara ya kampuni za simu kwani si haki yangu?

    ReplyDelete
  28. Sasa wewe unakubali kwamba ni kweli gari lako lina makosa. Umechemsha hapo. Usifikiri mwandishi wa hiyo note hana akili kama wewe. Analijua fika atendalo na nakuhakikishia mwisho wa siku lazima ile kwako. Inawezekana kabisa hiyo namba aliyoandika hapo ni yake halisi ila anajiamini kisheria humwezi kabisa. Ingekua gari halina makosa hapo sawa. Supposing hakua na hiyo headed paper mnayoidai? Amekua mjanja kamwelekeza akalipie kituoni. Sasa pale kituoni kuna kila kitu. Na wakati unaelekea kituoni anawapigia sim kuwaeleza kwamba huyo anajitia mjanja kwa hiyo treat him kwa mujibu wa sheria,maana ulishamwonesha kujua tokea mwanzo. I am so sure itakula kwako tu! Wenzio wanacheza na hizo sheria daily. Umeshabugi step hapo kwa taarifa yako. Isitoshe kiingereza chake huyo jamaa inaonesha sio kihiyo. Ni askari alieenda shule. Be so careful next time unapodeal na hawa watu. Hasa askari ambae kayaona kidogo madarasa. Ni noma mkuu, Imekula kwako hiyo!

    ReplyDelete
  29. uwanja wa fisiSeptember 08, 2009

    afadhali umemsaidia kupunguza deni la nguo za sikukuu!!

    ReplyDelete
  30. Waosha vinywa, bado hamjamsaidia mtoa mada.Jamaa kaeleza kinagaubaga yaliyomtokea yakwamba toka mwanzo askari yule alionesha mazingira ya kutaka rushwa na si kutekeleza wajibu wake pamoja na jitihada za mtoa mada kutaka kufuata sheria kwa maana ya kulipa notification lakini yule askari hakufanya hivyo na badala yake akaishia kuomba elfu 10,000 na kuipokea. Sasa kosa la mtoa mada ni nini hapo? Mlitaka ajipeleke polisi mwenyewe na kulipa notification wakati askari aliyemkamata hakuwa na lengo hilo toka awali zaidi ya kutengeneza mazingira ya kujipatia rushwa? Swali langu la msingi ni kutaka kujua kama makosa yaliyoorodheshwa yanastahili kulipa faini kwa mjibu wa sheria na kwa utaratibu gani? Kwa mtazamo wangu makosa hayo hayastahili notification ila ni makosa madogo madogo ya kuonywa na kutakiwa kuyarekebisha, askari huyo analijua hilo ndiyo maana akaishia kupokea elfu kumi.

    ReplyDelete
  31. NAKUPONGEZA KWA KUUSAIDIA UMMA KUJUA YAFUATAYO :

    1.UNAENDESHA GARI BOVU LINALOWEZA SABABISHA AJALI NA KUUA WANANCHI

    2.UMEKUBALI UMETOA RUSHWA NA NI HILI NI KOSA LA JINAI

    3.HUKUTOA TAARIFA YA KUOMBWA RUSHWA/HONGO POLISI AU TAKUKURU

    4.UNAYO NAMBA-AJIRA NA JINA LA OFISA POLISI NA NOTIFICATION/PENALTY SLIP ILIYOANDIKWA KWA MKONO WAKE(FREE HAND)

    NASIKITIKA KUWA UMEANGUSHA JITIHADA ZA MAKUSUDI ZA TAIFA ZA KUPAMBANA NA RUSHWA, WEWE NI SEHEMU YA AIBU HII NA TUNA KULAUMU.

    HAYA UNGEYATOA BAADA YA KESI KUWA INAENDESHWA NA POLISI/MAHAKAMA.

    OWINO.

    4.

    ReplyDelete
  32. jamani Watanzania tusivunjane moyo. Mngejuaje kama huwa kuna Notification za kuandikwa kutoka kwenye writing pad kama siyo kwa huyo MDAu kujitoa mhanga. Alichofanya yeye ni kutaka kupata yayo yanayojiri. Ni mara ngapi ili kupata information ya kusaidia umma inabidi utue pesa. Nia yake ilikuwa nzuri ya kurekebisha. tatizo la hilo gari amejieleza ni ubovu kidogo wa taa na kioo ambavyo vinaweza kurekebishwa. sasa je atahakikishaje kama vimerekebishwa. Mfumo kwa kweli unahitaji pia marekebisho. kama walivyo shauri waliotangulia hilo gari lingepewa muda likarekebishe matatizo kisha likaripori. kwani kupokea hongo na kumwachia haijamaliza tatizo. Wapendwa tutafute masuluhisho ya haya matatizo na siyo kuvungana moyo. Tanzania ni yetu na vijana kwa sasa tuna wajibu wa kuwatengenezea watoto wetu mazingira mazuri. Siyo watoto wanazaliwa wanakuta jina FISADI jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...