
Habari za kazi Anko Misupu
a.k.a anko Nanilii kama anavyojiita mwenyewe,
Uwanja wetu mpya wa taifa ulishakamilika muda mrefu na kufnguliwa lakini kama taswira inavyoonekana yale mabati yanawekwa na kuzungushiwa kama uzio wakati wa ujenzi mpaka leo hayajaondolewa yapo yapo tu kama yanavyoonekana yanaleta picha mbaya na kuharibu taswira ya uwanja hapo
Mdau mwanaharakati


Hayo mabati watu wanayachorea dili usiwe na wasi utaamka kesho kutwa utakuta hayapo! na mathalani ushatangaza humu sisi watu wa scrap metal tunandaa nyenzo zetu ili tukautoe uchafu ule. Huu ndo mwendo wa maisha katika shamba la bibi!
ReplyDeleteTizo la watanzania akuna anaye jiamini na kazi yake,Hapo anasubiriwa JK kutoa tamko la kuyatoa,akyamwungu vile.
ReplyDeletewanawasubiri wachina waliojenga uwanja waje wayatoe
ReplyDeleteWananchi msiwe na shaka. Mchakato unaendelea. Kila kitu kina utaratibu
ReplyDeleteTunasubiri warrant period ya uwanja iishe tutatoa, msilete ngebe zenu hapa.
ReplyDeleteBy Management
National stadium
hahahaha kaka umesahau kuwa hii ni bongo land???????????? ukute pesa ya ukuta ilishaliwa cku mingi sana. sasa wafanyaje wakati wanaendelea kusaka mahela huo ndio ukuta 4 the tym being. usiwamaindi sana kijana
ReplyDeleteTanzania ni nchi inayoongozwa kwa utawala wa sheria. faili la hayo mabati limepelekwa OFISI ya DPP Mr. Feleshi. sasa mafaili yamekuwa mengi hata mafaili ya Rada na kagoda bado yako kwa feleshi. wadanganyika kuweni na subiri.
ReplyDeleteHii imenigusa. kwa kawaida watu huingia mpirani katika muda unaopishana kabla ya mpambano na baadya ya mpambano kuanza (waliochelewa nk). Lakini watu wote hutoka kwa wakati mmoja punde mpira unapoisha.
ReplyDeletenaanisha uwepo wa mabati hayo utaleta maafa kama sio hivi karibuni basi baadaye. wakati wa kuingia hakuna msongamano na hivyo milango inayotumika inatosha. wakati wa kutoka huwa kuna msongamano wa watu usiomithilika. ukiongezea na mdundiko (yanga ikimfunga hayawani, mathalani(not vice versa)). watu watakuja kukanyagana (stampede)halafu tukatafuta mchawi kumbe wachawi sie wenyewe.
Post zako michu za leo hasa ya pancha zote kali sana.
nchi inaongozwa tu kama mifugo.
ReplyDelete