Kaka michu,Kuna habari hii tungependa

tushee na wadau wa blogu ya jamii
===================================
Yesu Mpya Aibuka nchini Urusi,
Ana Maelfu ya Wafuasi

Jamaa mmoja wa nchini Urusi amejitangaza kuwa yeye ni Yesu mtoto wa Mungu na amejipatia wafuasi wengi sana nchini humo wanaoamini kuwa yeye kweli ni Yesu.
Akifuga madevu na nywele ndefu, Yesu wa Urusi huzungukwa na wafuasi wake kila anapoenda na amefanikiwa kujikusanyia wafuasi wengi nchini humo na baadhi ya nchi za ulaya.
Yesu huyo mpya anayeitwa Sergei Torop mwenye umri wa miaka 48, awali alikuwa akifanya kazi kama trafiki polisi kabla ya kuachishwa kazi na baadae kudai kuwa mungu amemtuma kuwaokoa watu.
Torop amefanikiwa kujikusanyia wafuasi wengi zaidi ya 5,000 wakiwemo wasomi wakubwa nchini Urusi, wasanii na baadhi ya wanasiasa ambao humiminika kwenye kijiji chake cha Petropavlovka kilichopo maili 200 kutoka mji mkuu wa Urusi Moscow kwa nia ya kumuabudu.
Si ajabu ukipita kwenye kijiji hicho na kukuta watu wamepiga magoti mbele ya picha yake wakisali.
kwa habari kamili link ni hii:
http://www.nifahamishe.com/
NewsDetails.aspx?NewsId=2981654&&Cat=2
============================================
Thanks

Nifahamishe.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. hata yesu wa nazareth alipokuja kuna watu walimkataa kwa "argument" kama hiyo yako. watu walisema "wewe mtoto wa fundi seremala, kaka yake fulani na fulani; huwezi kuwa messiah".

    Watu wengi wanaosubiri ujio mwingine wa yesu, wameshatengeneza taswira ya yesu atakavyokuwa hapo atakapokuja. Na kama akija tofauti na taswira hiyo, basi ni lazima watamkataa.
    Sisemi kwamba huyu bwana wa Urusi ni yesu, lakini pia hakuna kitu chochote cha kuonyesha kwamba yeye siye Yesu.

    ReplyDelete
  2. Huyo ni feki tu...Bwana Yesu alishasema kuwa watatokea Ma-Kristo wa uongo wakidai ni Yeye siku hizi za mwisho but si Yesu original. Yesu akirudi ataonekana Duniani kote at once na ndio siku ya wateule watakaponyakuliwa live. Kasome zaidi kitabu cha Ufunuo ndio utapata picha halisi. Wasiojua maandiko ndio watakaodanganyika kirahisi.

    ReplyDelete
  3. ...siku za mwisho manabii wataongezeka danganya wengi, na wengi watapotea
    miss michuzi ukerewe

    ReplyDelete
  4. Michuzi mbona link ya habari ya huyo yesu haifunguki?
    Yesu alitabiriwa kuja na huenda ndio huyu bwana ingawa watu wengi wanaweza wakamkataa tuwekee link tafadhali tusome habari yake

    ReplyDelete
  5. tunashukuru mdau kwa habari katika biblia takatifu tayari imeandikwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu lakini msiwafuate kwani watakuwa ni manabii wa uongo hivyo tunaishi katika kizazi ambacho maandiko matakatifu tunashuhudia yanatimizwa,Yesu alisema yeye ni ALPHA NA OMEGA,MWANZO NA MWISHO,BWANA WA MABWANA,NA MFALME WA WAFALME nafikiri huyo yesu feki hajasoma haya maandiko,big up bro michuzi,mdau venezuela

    ReplyDelete
  6. HADI SASA HAPA DUNIANI KUNA YESU WENGI TU HATA USA WAPO LAKINI YESU KRISTO WA NAZARETH(MESIAH)NI MMOJA TU

    ReplyDelete
  7. UNIVERSAL VIRTUE UNIVERSITY
    DEPARTMENT MORDEN PHILOSOPHY AND NATURAL INTELGENCE.
    SECTION MORDEN THEOLOGY.

    WHO WAS, IS OR WILL BE JESUS CHRIST. JESUS CHRIST WAS YOU JESUS CHRIST IS YOU AND JESUS CHRIST WILL BE YOU. DONT WAIT FOR HIM TO COME PHYSICAL YOU ARE HIM SO WASTE NO TIME TO WAIT FOR HIM LIVE LIKE HIM JESUS IS YOU. BE GOOD ...LIKE HIM YOU WILL DO MORE MIRRACLES THAN THEY SAY HE DID.

    ReplyDelete
  8. Haya ndio matatizo ya picha za michelangelo,yesu hakuwa mzungu.ni mapropaganda yao ambayo yametufanya tuamini hivyo ili watutawale.kuna mzungu mwenye wooly hair?

    ReplyDelete
  9. kaka ahasante kwa taswira hiyo lakini siku hizi hata hapa bongo wapo wanajiita mitume, manabii watu wa miujiza kutoka kwa mungu lakini ukiuliza ni miujiza gani ametenda hana jibu wala ushahidi,kwasababu watu dini hawajui kwa undani wake wanakubali bila kuhoji maswali ya msingi watch out people.yangu macho

    ReplyDelete
  10. YESU NI ROHO NA KWELI. NA SIYO SURA NA NYWELE NDEFU. ATAKUJA KUTOKA MAWINGUNI KUWANYAKUA WATEULE. KASOMENI MAANDIKO.

    ReplyDelete
  11. Yesu atakuja kama Quran ilivyosema..ili kukana kuwa yeye alikuwa Mungu kama baadhi ya watu wanavyoamini..alisema yesu..SIKU HIYO WATU WENGI WATAKUJA KWANGU WAKILALAMA LORD, LORD..HATUKUFANYA MIUJIZA KWA JINA LAKO..KUTOWA MAPEPO KWA JINA LAKO...YESU ATAWAAMBIA ONDOKENI SIWAJUI MTOKAKO...HIYO NI BIBLIA INASEMA HIVYO...! BIBLIA INASEMA.NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU,WAKUJUWE WEWE MUNGU WA PEKEE NA WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA..KAMA WEWE UAMINI KUWA YESU NI MTUME HAUPATI UZIMA WA MILELE!!.HAPA WAZI INAONYESHA YESU ALIKUWA NI MTUME KAMA MITUME WENGINE...ILA AKAJA NABII WA UONGO AITWAE PAULO AKAWAPOTEZA WEENGI....!!TUSOME MAANDIKO !!TUSIFUATE WAZUNGU..NA MAPICHA YAO YA KUCHORA WAKIDAI YESU ALIKUWA AKIFANANA HIVI..AU HIVI..WRONG..! MUNGU MMOJA MPAKA MILELE..HANA MWANA, HAKUZAA WALA HAKUZALIWA!!KAMA HUTAKI NI WEWE TU NA CHUKI ZAKO BINAFSI..! SLAVE OF GOD!

    ReplyDelete
  12. mi naona huyu ndiye jamani na tumkubali tu, mbona amevaa viatu kama vyake?!

    ReplyDelete
  13. Kwa kauli yake ....

    "It's all very complicated," he starts quietly. "But to keep things simple, yes, I am Jesus Christ. That which was promised must come to pass. And it was promised in Israel 2,000 years ago that I would return, that I would come back to finish what was started. I am not God. And it is a mistake to see Jesus as God. But I am the living word of God the Father. Everything that God wants to say, he says through me."

    Unaweza kusoma zaidi kwenye kiunganishi kifuatacho:

    http://www.guardian.co.uk/world/2002/may/24/russia.iantraynor

    ReplyDelete
  14. hayo maandiko mnayosema si yaliandikwa na hao ndugu zake yesu (wathungu). sisi tunasubiri yesu wa afrika (mweusi tiiiii) bwana ndio tunaamini tutaokoka!!!!!

    ReplyDelete
  15. This guy lives more than 2000km and not 200mls. from Moscow, in a small village in SIBERIA. Waumini 5000 anaodai, ni % ndogo sana ya idadi ya Warusi (150 000 000 jumlisha na 15 to 20% ya migrants)na huko kijijini hao asomi wakubwa wa kirusi sijui wanatafuta nini. Kwa upande mwingine, Urusi unaweza ukakuta dereva or plumber wana PhD, na kwa matatizo yao wanaingia dini kama hizo. Russins ni Othordox na serikali yao inabagua dini karibu zote. Huyu jamaa anatafuta mlo tu.Soma hapa: http://believe-or-not.blogspot.com/2009/08/russian-man-claims-jesus-of-siberia.html

    ReplyDelete
  16. Laana tupu!

    ReplyDelete
  17. Duh...sasa huyo bwana ataenjoy mademu chungu mbovu...ahh namwonea wivu...!!!

    ReplyDelete
  18. kweli wtu mitambo. nani kasema huyo yesu ni blonde wa kizungu w/blue eyes. hata the bible itself says "his skin is as burnt brass". inasikitisha sana kuona hata sisi wabongo bado tuna picha na misalaba ya mzungu aliyevaa shuka makanisanai na majumbani mwetu.

    ReplyDelete
  19. KAKA MICHUSI LEO NI FURAHA KUBWA SANA KWANGU TANGU NIMEANZA KUTUMA MAONI KWA NANII YAKO TAKRIBAN NI MWAKA WA TATU SASA, JANA KWA MARA YA KWANZA MAONI YANGU UMEYATOA!! HIVI INAKUWAJE WAJE??

    ReplyDelete
  20. Kaka Michu,

    Hakuna jipya hapa, ni yale yale ya siku zote!! Wamezuka Yesu wengi na bado wataendelea kuzuka tu.

    Lakini tukiliangalia swala hili katika muktadha wa sasa hivi, tutagundua kwamba ujio wa akina Yesu wengi uko wazi. Kwa upande mmoja hii inatokana na ukweli kwamba siku hizi watu wengi wamejiingiza kwenye "kumpinga" Yesu wa awali lakini waking'ang'ania jina lake (Ukristo).

    Kama hilo limewezekana, hatua inayofuata ni kumkana moja kwa moja na kusema kwamba alikuwa hajatokea sasa ndiyo amekuja. Hili halitakuwa jambo la ajabu.

    Kwa upande mwingine, dini kama dini zimepoteza mwelekeo na ushawishi wa kutosha kuhusu ni ipi hasa ya kweli. Matokeo ya hili ni kuhamahama madhehebu, kuanzisha madhehebu mapya na hata kujibandika "vyeo" vyenye mamlaka za kiMungu!

    Watu wamekuwa wakijipandisha vyeo kutoka Wainjilisti kwenda Wachungaji, Maaskofu, Mitume, Manabii, n.k. Sasa tunategemea wakifika hapo mwisho watakwenda wapi? Si itabidi wengine wajiite Yesu mpya? Labda hili lina mkono wa imani kwamba dini sasa ni biashara, ni njia ya kuishi!! Wengine tumewaona wanakampeni serikali iwapangie mahubiri ili wakashirikiane nayo ufisadi!!

    Hiyo ndiyo dunia ya leo, chungu chenye mchanganyiko na mchanaytoi wa kila kitu (potpourri).

    ReplyDelete
  21. Uzushi mtupu, kufuatwa na watu wengi sio hoja, hata ibilisi ana wafuasi mamilioni. Kuwa na wafuasi hakumfanyi awe Yesu mpya. Hilo neno mpya lenyewe ni kitendawili. Yesu hakuwa trafic police. FirePower, UK

    ReplyDelete
  22. Alisema atarudi ingawaje hakusema atapoibukia, kwahiyo huwezi jua!

    ReplyDelete
  23. Lini atasulubiwa au huyu hakuambiwa hayo?

    ReplyDelete
  24. mi nawasiwasi na huyo Yesu wa Urussi, kwasababu hata biblia imeandika kwamba siku za mwisho zikikaribia watakuja manabii wengi wa uongo, watahubiri neno la Mungu na watu wengi wataamini.

    mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...