Home
Unlabelled
JK akiwajibika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
makubwa, yaani kumfunga kamba ya kiatu huyo mtoto na kigoda kimewekwa!
ReplyDeleteUdogo nao, angalia kijana alivyosimama kwa madaha na kama vile anamwambia JK, funga vizuri hiyo kamba!!
ReplyDeleteunashangaa kigoda, umri huo? ukikua utaonaona. Lakini naomba hiyo picha huyo mtoto ahifadhiwe ili ukubwani aone aliwahi kufungwa kamba za viatu na rais. ni kumbukumbu muhimu katika maisha yake
ReplyDeletendau wa kwanza unashangaa nini kwani cha ajabu kipi hapo jk hana umri wa miaka 20 ati ainame unataka apige mweleka? mie naona poa tuu angekuwa ni mwanao amefugwa kamba za viatu na raisi ungesifia kwa sana tuu tena ungeweka na picha sebuleni kwako kabisaa
ReplyDeleteSAWA KABISA RAISI WAONYESHE MFANO WAFANYAKAZI WAKO MANAKE NCHI NYENGINE TRAFIC OFFICER WANATEMBEA NA MAFAGIO NDANI YA MAGARI YAO KAMA BARABARA IMECHAFULIWA WANAWAJIBIKA SIJUI KAMA AFANDE MARWA ANAWEZA FANYA HIVO ????
ReplyDeleteUnavyomfunga huyu mtoto kamba ya kiatu. Tunaomba uwafunga kamba na watu wa TRA wanatuliza sana. Yaani yako huku Marekani yanajichana hela za kifisadi, yanatoka beach hadi nyingine. Eti yako vekesheni, kumbe ni hela za kudhulumu watu mali zao. Haya majitu yanaliza watanzania. Natamani ndege yatayopanda ianguka ikayauwe wao tu. Yanaletea wanyonge umasikini kwa ajili ya dhuluma. Mungu sikia vilio vya wanyonge wanaoletewa dhiki na umasikini. Mijitu inajigamba kwa kuiba mali za watu pale TRA. Eti yanaita hela kokoto. Mungu yaunguze kiungo kimoja badala ya kingine hadi yatokomee mwili mzima. Nina uchungu na watu wanakula mali za watu wanyonge, kuacha wanaangaika.
ReplyDeleteMdau USA
Mwenyekiti Kikwete,
ReplyDeleteUmetimiza unabii kuwa ili uwe mkubwa ni lazima utumikie kwanza.
Yesu aliwaosha miguu watu waliokuja mpokea na wanafunzi wake.
Mungu akuzidishie Afya njema. Mkoa wa MARA una imani nawe.
MAINA ANG'IELA OWINO
Hizi publicities nyingine naona kama zinakuwa stage managed! kama Mtanzania halisi ningependa kama His Excellent angekuwa anapata publicity kwenye ku-tackle ufisadi aka Usinguse na sio vitu vidogo vidogo kama hivi tena huko vijijini kwenye ziara zake? What's the motives behind this picture? Are we living in the World of Propaganda now au?
ReplyDeleteHaki ya Mungu Michuzi usipoiweka hii nitakuanika nawe ni Usinguse na unatumika kwenye kutengeneza publicity ukitusaliti maana nakujua na ninataka Mh. mwenyewe asome hii comment yangu maana naskia husoma hii blog pia!
Kitakachofuata ni kuosha Miguu wagonjwa maana ndo kazi tuliyomtuma tulipompa 84% ya kura zetu sisi kalagabaos! Huyu Mh. sasa itabidi tumuite Kikwete aka Jesus den Chalinze!
ReplyDeleteWow nice picture Jk anajitahidi sana kuwa mchanganyiko na wananchi.
ReplyDeletethats so sweet.
ReplyDeletekama macho yako hayaoni vizuri sioni kwanini unatoa maoni,kigoda kipo wapi hapo?au ndio makengeza.
ReplyDeleteanyway michuzi,nakuomba print hiyo picha ili umpe huyo mtoto hili bonge la kumbukumbu.
ASANTE SANA MHESHIMIWA MRISHO JAKAYA KIKWETE, NAJUA KABISA HII INATOKA MOYONI NA HIVI NDIVYO ULIVYO. NAONA HII ITASIADIA WALIMU WETU WA SHULE ZA CHEKECHEA NA MSINGI KUWAJALI WATOTO KULIKO KUJALI VIBOKO: HUU NI MFANO MZURI SANA. zAIDI NAONA WATU WENGI WANAUKUONA WEWE NYOTA SAFI YA UONGOZI NA MTU WA KUIGWA KWA MAMBO MBALI MBALI, MFANO KUVAA SAFI, SASA MAWASILIA NA MAOFISA WENGI DAR NA MIKOANI WANALAMBA SUTI HATA WANFUNZI VYUONI WANALAMBA SUTI ZA KWENYE MITUMBA LAKINI ZIMEREKEBISHWA VIZURI; PIA MAWAZIRI WENGI SASA HAWANA TENA MVI , HATA WAANDISHI WA HABARI KAMA MAKWAIYA WA KUHENGA! WOTE WANATUMIA MADAWA YA KUFUNIKA MVI ZAO NA MENGI. NAONA HUU NI WAKTI MZURI WA KUTOA MFANO MWINGINE HASA KIPINDI HIKI CHA KAMPEINI- SOMO LA KUCHUKIA UCHAFU ANZA NA MJI WA DAR ES SALAAM, TIA SHIME MJI UWE SAFI WAHAUSIKA KAMA HAWEZI WAFUNGE VIRAGO, UKIFIKA BAGAMOYO UKAKUTA MAKARATASI STEDI YA BUS BASI SIMAMISHA MSAFARA NA KUOMBA MFANGIO, UKIPITA MBURAHATI AU TANDALE AU TANDIKA SOKONI AU LUANGA KWA BINTI KAHENGA UKAKUTA UCHAFU SIMAMISHA GARI, MTAA WA REGENT UKIWA NA MADIBWI SIMAMISHA MSAFARA OMBA KARAHI LA MCHANGA- KWA NJIA HII HATA HUKO MIUKONI WAHUSIKA WATAPATA HABARI KUWA UNACHUKIA UCHAFU NA UNAPENDA USAFI MARA UA BAADA YA MUDA UTAONA MJI UNAWAKA KWA USAFI, KAMA WAZEE NA VIJANA WENGI HAWANA MVI HAPO DAR NA MIKOANI; WALAU LICHA YA KUTIMIA MUDA MWINGI KUWEKA DAWA ZA KUFICHA MVI NA KISHA KUTEMBEA KWENYE BARABARA ZENYE MADIMBWI YA MAJI KINYESI, TAKA TAKA BASI WATUMIA MUDA TOSHA WA KUBUNI MBINU ZA KUONDOKA KERO HILI LA AFYA-NI AIBU KABISA VIJANA WA UPANGA, MIKOCHENI NA TANDIKA KUPATWA NA UGONJWA WA UNAOTOKANA NA KULA KINYESI-YAANI KIPINDU PINDU
ReplyDeleteNi kitu kizuri hasa ni somo kwa wanaume, ambao hawajawahi kumvalisha mtoto/watoto wake hata shati, na kwa wale wazazi wasiowapa upendo watoto wao, kwa kusema eti mimi sikufanyiwa na wazazi mbona nina ishi, JIFUNZE NA UBADILIKE.
ReplyDeleteJK pole sana naona unapenda uwajibikaji ila Rais wangu, una viongozi wanaojua kula nchi. sijuiii
tulitengemea mabadiliko ila ni NNNDDDOOOTTTOOO
KUMBE MLINZI WA RAISI NAYE NI MCCM! SERIKALI IMESHINDWA KUTOA MLINZI WA RAISI?
ReplyDeleteAngekuwa mkapa hata kuinama asingeweza hata kama wangempa sofa.
ReplyDeletehahahaha....wabongo na sie...akianguka oohh kaanguka...akipewa kigoda oooh kapewa kigoda...kaaazi kwelikweli.
ReplyDeleteKwanza kabisa mimi sioni kama kuna kigoda hapo ila kwa vile tumezoea kukandia kila kitu basi mtu anakimbilia kukandia kabla hajaangalia picha vizuri. Kwa upande wa Raisi kumfungia kamba za viatu mimi kwa mtazamo wangu naona Mhe ametuonyesha kuwa yeye hata nyumbani kwake anafuatilia uvaaji wa wanae na ndio maana imekuwa rahisi kwake kunotice kuwa dogo hajafunga viatu vizuri akaamua kumrekebishia. Huu ni mfano wa kuigwa kwa wanaume ambao wanafikiri kila kitu kinafanywa na mwanamke baba pia unatakiwa uwe unarushia jicho siku moja moja kucheck je huyu dogo amechomekea vizuri? amefunga viatu vyake je yuko safi na kama sio hata wewe unaweza kumrekebisha sio kumwambia nenda kwa mamako akurekebishe vzuri au housegal. Huu ni mtazamo wangu tu.
ReplyDeleteOh,jamani this is so sweet,unatutamanisha sisi ambao hatukupata wa baba wa kutupa hayo mapenzi ure so special Man,ukweli mwenyezi mungu akuzidishie upendo ulio nao Baba yetu na akutangulie kwa yote ufanyayo Ishalla,na viogozi wengine wangejaribu kuiga mifano yako ya kuthamini kila binadam na kuwajali tungekuwa nbali sana,ila wao wanajiona kma ni akina mungu wa pili wanao takiwa kuabudiwa wasijue kwamba sisi wote ni sawa na kila kiumbe ana haki ya kuthaminiwa na mwezake ila wezetu hawajui hayo,ila at the end of the day mungu katulinganisha sie wote tunaishia futi 6 hata kma ulikuwa una nini utaviacha vyote,tujifunze kukumbuka kuna Mungu.
ReplyDeleteHe stoops to conquer
ReplyDeleteMheshimiwa JK umefanya safi sana. Yesu anatuambia ukubwa ni utumishi. Wewe baba huna makuu. Mwakani kura zangua na mke wangu tutakupa wewe JK. Wenzio sababu ya vitambi wanashindwa kujishusha kuwatumikia wadogo. Eh Mola mbariki JK Rais wetu azidi kufanikiwa katika kuiongoza nchi hii. Amen
ReplyDeletehii siyo propaganda haya ndiyo maisha halisi ya kikwete ukimvua kofia ya yeye kuwa ni mkuu wa nchi ,ana mapenzi ya kwelie kwa watu wake ni mbinafsi lakini lazima tukubali ukweli ameikuta nchi katika hali mbaya sana kimaadili hicho ndicho kinachompa shida kwa sasa.nina uhakika hata mwalimu kama angekuwa hai tanzania ya sasa angepata upinzani mkubwa sana .nakumbuka maneno ya kiongozi wa kijeshi wa guinea didas kamala kuwa ile nchi kwa sasa haiwezi kutawalika na raia maana hata yeye anapata shida sana ndani ya jeshi kwa sababu amelikuta halina nidhamu kwa hiyo hata akisema atoe nchi kwa utawala wa raia baada ya masaa 24 mwanajeshi mwingine ataibuka na kuipindua nchi..sasa hili ndilo lililopo ndani ya uongozi wa nchi kikwete amekuta viongozi hawana nidhamu na maadili ya uongozi.muheshimiwa rais tunakuunga mkono
ReplyDeleteHii inaelekea haikutarishwa, ni kwamba dogo alikuwepo na Raisi alimuona kamba imefunguka, kama kawaida ya mzazi alijipinda kumfunga, ila rangi kwenye buti ndio unaona tofauti ya maisha, JK na mjomba mwengine hapo pembeni buti zao zinangaa kwa kiwi, Dogo buti vumbi tupu!
ReplyDeleteKama ningetangulia kutoa maoni ningesema ni "PROPOGANDA zilizopitwa na wakati". lakini baada ya kusoma maoni ya hadi Oct 16 12:17:00 PM nimeansha mikono na kukubali kuwa kumbe aina hii ya PROPOGANDA bado inafanya kazi vizuri katika nchi yetu pendwa ya BONGOLAND. Kweli alituita Wabongo hakukosea!!!!!!!!
ReplyDeleteinama wee mjeshi vipi??au ulidesa nn jeshini
ReplyDeleteushachoka mara tu ata 60 hujafika jamen duh
Usituoshe vinywa, endapo kama hujawafunga MAFISADI? Tunataka usafishe mafisadi wote ndo tutaelewa kweli unajua kufunga kamba. Mijitu inadhulumu wanyonye haki yao.
ReplyDeleteMdau USA
That is good, dogo atalala atamwambia kila mtu rais alinifunga kamba za viatu vyangu vya viatu. Nakumbuka tuko wadogo tulikuwa tunaita GIDAMU. I don't know where this name came from. BWA MDOGO APATIWE PICHA KWA KUMBUKUMBU YAKE BAADAYE, as this time I guess he doesn't know anything about how huge is presidency like. ANAONA KAMA BABU YAKE TU ANAMFUNGA KAMBA ZA VIATU
ReplyDeletemsione ajabu kwa rais kikwete kufanya hivyo,mengi kayafanya ambayo ukiyaona utakubali rais ni mpole sana ana huruma sana wala hana majivuno. mungu akupe umri mrefu rais kikwete
ReplyDelete