JK akimfunga kamba za viatu Ramadhan Adam ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Iringo iliyopo mjini Musoma wakati Rais alipokwenda kufungua tawi la wakereketwa wa CCM, Kukindi cha Maisha Plus cha eneo la Kitaji,manispaa ya Musoma mjinji leo asubuhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. makubwa, yaani kumfunga kamba ya kiatu huyo mtoto na kigoda kimewekwa!

    ReplyDelete
  2. Udogo nao, angalia kijana alivyosimama kwa madaha na kama vile anamwambia JK, funga vizuri hiyo kamba!!

    ReplyDelete
  3. unashangaa kigoda, umri huo? ukikua utaonaona. Lakini naomba hiyo picha huyo mtoto ahifadhiwe ili ukubwani aone aliwahi kufungwa kamba za viatu na rais. ni kumbukumbu muhimu katika maisha yake

    ReplyDelete
  4. ndau wa kwanza unashangaa nini kwani cha ajabu kipi hapo jk hana umri wa miaka 20 ati ainame unataka apige mweleka? mie naona poa tuu angekuwa ni mwanao amefugwa kamba za viatu na raisi ungesifia kwa sana tuu tena ungeweka na picha sebuleni kwako kabisaa

    ReplyDelete
  5. SAWA KABISA RAISI WAONYESHE MFANO WAFANYAKAZI WAKO MANAKE NCHI NYENGINE TRAFIC OFFICER WANATEMBEA NA MAFAGIO NDANI YA MAGARI YAO KAMA BARABARA IMECHAFULIWA WANAWAJIBIKA SIJUI KAMA AFANDE MARWA ANAWEZA FANYA HIVO ????

    ReplyDelete
  6. Unavyomfunga huyu mtoto kamba ya kiatu. Tunaomba uwafunga kamba na watu wa TRA wanatuliza sana. Yaani yako huku Marekani yanajichana hela za kifisadi, yanatoka beach hadi nyingine. Eti yako vekesheni, kumbe ni hela za kudhulumu watu mali zao. Haya majitu yanaliza watanzania. Natamani ndege yatayopanda ianguka ikayauwe wao tu. Yanaletea wanyonge umasikini kwa ajili ya dhuluma. Mungu sikia vilio vya wanyonge wanaoletewa dhiki na umasikini. Mijitu inajigamba kwa kuiba mali za watu pale TRA. Eti yanaita hela kokoto. Mungu yaunguze kiungo kimoja badala ya kingine hadi yatokomee mwili mzima. Nina uchungu na watu wanakula mali za watu wanyonge, kuacha wanaangaika.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  7. Mwenyekiti Kikwete,
    Umetimiza unabii kuwa ili uwe mkubwa ni lazima utumikie kwanza.

    Yesu aliwaosha miguu watu waliokuja mpokea na wanafunzi wake.

    Mungu akuzidishie Afya njema. Mkoa wa MARA una imani nawe.

    MAINA ANG'IELA OWINO

    ReplyDelete
  8. Hizi publicities nyingine naona kama zinakuwa stage managed! kama Mtanzania halisi ningependa kama His Excellent angekuwa anapata publicity kwenye ku-tackle ufisadi aka Usinguse na sio vitu vidogo vidogo kama hivi tena huko vijijini kwenye ziara zake? What's the motives behind this picture? Are we living in the World of Propaganda now au?

    Haki ya Mungu Michuzi usipoiweka hii nitakuanika nawe ni Usinguse na unatumika kwenye kutengeneza publicity ukitusaliti maana nakujua na ninataka Mh. mwenyewe asome hii comment yangu maana naskia husoma hii blog pia!

    ReplyDelete
  9. Kitakachofuata ni kuosha Miguu wagonjwa maana ndo kazi tuliyomtuma tulipompa 84% ya kura zetu sisi kalagabaos! Huyu Mh. sasa itabidi tumuite Kikwete aka Jesus den Chalinze!

    ReplyDelete
  10. Wow nice picture Jk anajitahidi sana kuwa mchanganyiko na wananchi.

    ReplyDelete
  11. thats so sweet.

    ReplyDelete
  12. kama macho yako hayaoni vizuri sioni kwanini unatoa maoni,kigoda kipo wapi hapo?au ndio makengeza.
    anyway michuzi,nakuomba print hiyo picha ili umpe huyo mtoto hili bonge la kumbukumbu.

    ReplyDelete
  13. ASANTE SANA MHESHIMIWA MRISHO JAKAYA KIKWETE, NAJUA KABISA HII INATOKA MOYONI NA HIVI NDIVYO ULIVYO. NAONA HII ITASIADIA WALIMU WETU WA SHULE ZA CHEKECHEA NA MSINGI KUWAJALI WATOTO KULIKO KUJALI VIBOKO: HUU NI MFANO MZURI SANA. zAIDI NAONA WATU WENGI WANAUKUONA WEWE NYOTA SAFI YA UONGOZI NA MTU WA KUIGWA KWA MAMBO MBALI MBALI, MFANO KUVAA SAFI, SASA MAWASILIA NA MAOFISA WENGI DAR NA MIKOANI WANALAMBA SUTI HATA WANFUNZI VYUONI WANALAMBA SUTI ZA KWENYE MITUMBA LAKINI ZIMEREKEBISHWA VIZURI; PIA MAWAZIRI WENGI SASA HAWANA TENA MVI , HATA WAANDISHI WA HABARI KAMA MAKWAIYA WA KUHENGA! WOTE WANATUMIA MADAWA YA KUFUNIKA MVI ZAO NA MENGI. NAONA HUU NI WAKTI MZURI WA KUTOA MFANO MWINGINE HASA KIPINDI HIKI CHA KAMPEINI- SOMO LA KUCHUKIA UCHAFU ANZA NA MJI WA DAR ES SALAAM, TIA SHIME MJI UWE SAFI WAHAUSIKA KAMA HAWEZI WAFUNGE VIRAGO, UKIFIKA BAGAMOYO UKAKUTA MAKARATASI STEDI YA BUS BASI SIMAMISHA MSAFARA NA KUOMBA MFANGIO, UKIPITA MBURAHATI AU TANDALE AU TANDIKA SOKONI AU LUANGA KWA BINTI KAHENGA UKAKUTA UCHAFU SIMAMISHA GARI, MTAA WA REGENT UKIWA NA MADIBWI SIMAMISHA MSAFARA OMBA KARAHI LA MCHANGA- KWA NJIA HII HATA HUKO MIUKONI WAHUSIKA WATAPATA HABARI KUWA UNACHUKIA UCHAFU NA UNAPENDA USAFI MARA UA BAADA YA MUDA UTAONA MJI UNAWAKA KWA USAFI, KAMA WAZEE NA VIJANA WENGI HAWANA MVI HAPO DAR NA MIKOANI; WALAU LICHA YA KUTIMIA MUDA MWINGI KUWEKA DAWA ZA KUFICHA MVI NA KISHA KUTEMBEA KWENYE BARABARA ZENYE MADIMBWI YA MAJI KINYESI, TAKA TAKA BASI WATUMIA MUDA TOSHA WA KUBUNI MBINU ZA KUONDOKA KERO HILI LA AFYA-NI AIBU KABISA VIJANA WA UPANGA, MIKOCHENI NA TANDIKA KUPATWA NA UGONJWA WA UNAOTOKANA NA KULA KINYESI-YAANI KIPINDU PINDU

    ReplyDelete
  14. Ni kitu kizuri hasa ni somo kwa wanaume, ambao hawajawahi kumvalisha mtoto/watoto wake hata shati, na kwa wale wazazi wasiowapa upendo watoto wao, kwa kusema eti mimi sikufanyiwa na wazazi mbona nina ishi, JIFUNZE NA UBADILIKE.

    JK pole sana naona unapenda uwajibikaji ila Rais wangu, una viongozi wanaojua kula nchi. sijuiii
    tulitengemea mabadiliko ila ni NNNDDDOOOTTTOOO

    ReplyDelete
  15. KUMBE MLINZI WA RAISI NAYE NI MCCM! SERIKALI IMESHINDWA KUTOA MLINZI WA RAISI?

    ReplyDelete
  16. Angekuwa mkapa hata kuinama asingeweza hata kama wangempa sofa.

    ReplyDelete
  17. hahahaha....wabongo na sie...akianguka oohh kaanguka...akipewa kigoda oooh kapewa kigoda...kaaazi kwelikweli.

    ReplyDelete
  18. Kwanza kabisa mimi sioni kama kuna kigoda hapo ila kwa vile tumezoea kukandia kila kitu basi mtu anakimbilia kukandia kabla hajaangalia picha vizuri. Kwa upande wa Raisi kumfungia kamba za viatu mimi kwa mtazamo wangu naona Mhe ametuonyesha kuwa yeye hata nyumbani kwake anafuatilia uvaaji wa wanae na ndio maana imekuwa rahisi kwake kunotice kuwa dogo hajafunga viatu vizuri akaamua kumrekebishia. Huu ni mfano wa kuigwa kwa wanaume ambao wanafikiri kila kitu kinafanywa na mwanamke baba pia unatakiwa uwe unarushia jicho siku moja moja kucheck je huyu dogo amechomekea vizuri? amefunga viatu vyake je yuko safi na kama sio hata wewe unaweza kumrekebisha sio kumwambia nenda kwa mamako akurekebishe vzuri au housegal. Huu ni mtazamo wangu tu.

    ReplyDelete
  19. Oh,jamani this is so sweet,unatutamanisha sisi ambao hatukupata wa baba wa kutupa hayo mapenzi ure so special Man,ukweli mwenyezi mungu akuzidishie upendo ulio nao Baba yetu na akutangulie kwa yote ufanyayo Ishalla,na viogozi wengine wangejaribu kuiga mifano yako ya kuthamini kila binadam na kuwajali tungekuwa nbali sana,ila wao wanajiona kma ni akina mungu wa pili wanao takiwa kuabudiwa wasijue kwamba sisi wote ni sawa na kila kiumbe ana haki ya kuthaminiwa na mwezake ila wezetu hawajui hayo,ila at the end of the day mungu katulinganisha sie wote tunaishia futi 6 hata kma ulikuwa una nini utaviacha vyote,tujifunze kukumbuka kuna Mungu.

    ReplyDelete
  20. He stoops to conquer

    ReplyDelete
  21. Mheshimiwa JK umefanya safi sana. Yesu anatuambia ukubwa ni utumishi. Wewe baba huna makuu. Mwakani kura zangua na mke wangu tutakupa wewe JK. Wenzio sababu ya vitambi wanashindwa kujishusha kuwatumikia wadogo. Eh Mola mbariki JK Rais wetu azidi kufanikiwa katika kuiongoza nchi hii. Amen

    ReplyDelete
  22. hii siyo propaganda haya ndiyo maisha halisi ya kikwete ukimvua kofia ya yeye kuwa ni mkuu wa nchi ,ana mapenzi ya kwelie kwa watu wake ni mbinafsi lakini lazima tukubali ukweli ameikuta nchi katika hali mbaya sana kimaadili hicho ndicho kinachompa shida kwa sasa.nina uhakika hata mwalimu kama angekuwa hai tanzania ya sasa angepata upinzani mkubwa sana .nakumbuka maneno ya kiongozi wa kijeshi wa guinea didas kamala kuwa ile nchi kwa sasa haiwezi kutawalika na raia maana hata yeye anapata shida sana ndani ya jeshi kwa sababu amelikuta halina nidhamu kwa hiyo hata akisema atoe nchi kwa utawala wa raia baada ya masaa 24 mwanajeshi mwingine ataibuka na kuipindua nchi..sasa hili ndilo lililopo ndani ya uongozi wa nchi kikwete amekuta viongozi hawana nidhamu na maadili ya uongozi.muheshimiwa rais tunakuunga mkono

    ReplyDelete
  23. Hii inaelekea haikutarishwa, ni kwamba dogo alikuwepo na Raisi alimuona kamba imefunguka, kama kawaida ya mzazi alijipinda kumfunga, ila rangi kwenye buti ndio unaona tofauti ya maisha, JK na mjomba mwengine hapo pembeni buti zao zinangaa kwa kiwi, Dogo buti vumbi tupu!

    ReplyDelete
  24. Kama ningetangulia kutoa maoni ningesema ni "PROPOGANDA zilizopitwa na wakati". lakini baada ya kusoma maoni ya hadi Oct 16 12:17:00 PM nimeansha mikono na kukubali kuwa kumbe aina hii ya PROPOGANDA bado inafanya kazi vizuri katika nchi yetu pendwa ya BONGOLAND. Kweli alituita Wabongo hakukosea!!!!!!!!

    ReplyDelete
  25. inama wee mjeshi vipi??au ulidesa nn jeshini

    ushachoka mara tu ata 60 hujafika jamen duh

    ReplyDelete
  26. Usituoshe vinywa, endapo kama hujawafunga MAFISADI? Tunataka usafishe mafisadi wote ndo tutaelewa kweli unajua kufunga kamba. Mijitu inadhulumu wanyonye haki yao.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  27. That is good, dogo atalala atamwambia kila mtu rais alinifunga kamba za viatu vyangu vya viatu. Nakumbuka tuko wadogo tulikuwa tunaita GIDAMU. I don't know where this name came from. BWA MDOGO APATIWE PICHA KWA KUMBUKUMBU YAKE BAADAYE, as this time I guess he doesn't know anything about how huge is presidency like. ANAONA KAMA BABU YAKE TU ANAMFUNGA KAMBA ZA VIATU

    ReplyDelete
  28. msione ajabu kwa rais kikwete kufanya hivyo,mengi kayafanya ambayo ukiyaona utakubali rais ni mpole sana ana huruma sana wala hana majivuno. mungu akupe umri mrefu rais kikwete

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...